Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Waziri wa uchukuzi Bwana Msafiri ametoa mwito kwa kila mwananchi kusingatia sheria za barabarani ili kumaliza visa vya ajali vilivyokithiri.

      

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Waziri wa uchukuzi Bwana Msafiri ametoa mwito kwa kila mwananchi kusingatia sheria za barabarani ili kumaliza visa vya ajali vilivyokithiri. Alisema kuwa ongezeko la ajali za barabarani linachangiwa pakubwa na watu binafsi.Akiongea katika hafla ya kuzindua mbinu za kuhakikisha usalama barabarani, Bwana Msafiri alisema yasikitisha kuona kuwa ajali za barabarani zimeongezeka katika siku za hivi majuzi. Alielezea kuwa wizara yake imekerwa na utekelezaji wa majukumu na mapuza miongoni mwa wanaohusika na sekta ya uchukuzi.Alisema wengi wa wenye magari wamepuza masharti mengi ambayo yaliwekwa na wizara, yaliyokusudiwa kugunguza ajali. Alisema magari mengi yamekuwa kachara na kwamba mengi yameng‘olewa vidhibiti mwendo. Basi magari yanaendeshwa kwa kasi ya umeme. Hili limeongeza ajali kwa kiasi kikubwa. Mengi hayana mishipi ya usalama na wasafiri hukabiliwa na hatari wanaposafiri. Aliongeza kuwa sura ya magari hayo ni dhihirisho kuwa wenye magari wamepotoka kabisa, ―magari mengi yamerembeshwa hata kwa picha chafu, jambo linalodhihirisha utovo wa mbeko na kutofuata sheria. Mengine yanacheza muziki kwa sauti ya juu hivi kwamba hata dereva na utingo hawawezi kusikia grudumu liking‘oka. Baadhi yao yanaonyesha picha chafu chafu za video na kuufanya usafiri kuwa vyumba vya sinema chafu!‖ Alisema kutovaa sare kwa madereva na makondakta na kuwapakia abiria kupita kiasi ni kilele cha upuui wa sheria zilizowekwa.
Wasafiri pia wanapuuza masharti yaliyowekwa kwa lengo la kuwafaa, ―alisema waziri. Alisikitika kuwa wasafiri wengi hawafungi mishipi ya usalama hata inapopatikana, aidha wanakubali kuingia magari yaliyojaa tayari, hali inayoongenzea uwezekano wa gari kupata ajali kwa kulemewa na uzito. Aliwakumbusha kuwa gali likipata ajali wakiwa wamepakiwa hivi, hawezi kugharamiwa na bima ya gari kwa vile bima yenyewe hukatiwa idadi mahususi ya wasafiri. Aliwalaumu watembeaji barabarani kwa kutozingatia sheria za kawaida. Alisema kwa mfano katika gurufu kuna mahali ambako kuna vivuko ila hawavitumii na wengine huishia kugongwa na magari.Mwisho aliwalaumu maafisa wa trafiki wanaotekeleza majukumu yao. Akitisha kuwachukulia hatua kali, alisema kuwa yaskitisha kusikia kuwa wanachukua kadhongo na kuyaachilia magari yaliyo na kasoro badala ya kuyashtaki kulingana na sheria. Aliwaongezea lawama wasafiri kwa kunyamaza wanapoyaona haya yakitendeka machoni. Alisababisha kicheko aliposema kuwa baadhi ya wasafiri huwahimiza makondakta watoe chai haraka ili waendelee na usafiri ya bila kujali hatari wanazojiingiza kwazo.
Akionya kuwa angechukua hatua ya kuregesha utulivu, alihitimisha kwa kusema kuwa wizara yake limetoa ilani kwa watumiaji wote wa barabarani. Alitoa makataa ya siku kumi na nne ambapo yoyote asiyefuata kaida zote za barabarani atachukuliwa hatua kisheria.

a) Fafanua sababu za mwito wa waziri wa uchukuzi Bwana Msafiri?
b) Eleza jinsi wenye magaari wamechangia katika kukithiri kwa visa vya ajali barabarani?
c) Fafanua mchango wa wasafiri katika kudorora kwa hali ya usalama barabarani.
d) Eleza majukumu ya maafisa wa trafiki katika kudumisha usafiri kulingana na ufahamu.
e) Toa visawe vya maneno yafuatayo.
(i) Kondakta:
(ii) Toa ilani:
(iii) Toa makataa:

  

Answers


sharon
(a) Kumaliza visa vya ajali vilivyokithiri (wananchi kuzingatia sheria za barabarani.)
(b)
- Kupunguza masharti yaliyowekwa na wizara.
- Magari mengi yamekuwa kachara.
- Magari mengi yameng‘olewa vidhibiti mwendo.
- Magari kuendeshwa kwa kasi ya umeme.
- Magari hayana mishipi ya usalama.
- Magari kucheza mizigi kwa sauti ya juu.
- Kuwapakia abiria kupita kisai.
(c)
- Wasafiri kupuuza masharti yaliyowekwa.
- Hawafungi mishipi ya usalama.
- Wasafiri wanakubali kuingia katika magari yaliyojaa tayari.
- Watembeaji barabarani kutozingatia sheria za kawaida.
- Kutotumia vivuko wakati wa kuvuka barabara.
- Wasafiri kunyamazia makosa kwenya magari.
(d)
- Kuchukuwa kadhongo.
- Kuyaachilia magari yaliyo na kasoro.
- Kutoshtaki magari yaliyo na kasoro kulingana na sheria.
(e)
- Kondakta – utingo, tani boi
- Toa ilani – toa onyo / tangazo
- Toa makataa – toa mapatano
sharon kalunda answered the question on September 24, 2019 at 12:09


Next: Triangle ABC is such that A(-5, 1), B(-1, 1) and C(-3, 4). Triangle A'B'C'.is the image of ?ABC under transformation a)Determine the co-ordinates of ?A'B'C'. b)On...
Previous: Serikali kupitia Wizara ya Elimu imetoa mwongozo wa karo ambao unastahili kuzingatiwa katika shule za upili kufuatia haua ya shule mbalimbali kuongeza karo kwa viwango...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions