Serikali kupitia Wizara ya Elimu imetoa mwongozo wa karo ambao unastahili kuzingatiwa katika shule za upili kufuatia haua ya shule mbalimbali kuongeza karo kwa viwango...

      

Serikali kupitia Wizara ya Elimu imetoa mwongozo wa karo ambao unastahili kuzingatiwa katika shule za upili kufuatia haua ya shule mbalimbali kuongeza karo kwa viwango mbalimbali. Hatua hiyo inadhamiriwa kumking mzazi dhidi ya kunyanyaswa kifedha walimu hasa ikizangiwa kuwa gharama ya maisha imepanda mara dufu.Hata hivyo, ingekuwa bora ikiwa serikali ingefanya maamzi kwa ushirikiano na walimu wakuu maana kwa hakika suala la karo linahusu matumizi ya fedha ambayo pia huja na gharama zake. Gharama hii inaokana na ununuzi wa vitabu vya Kada na vya mazoezi, karatasi za uchapishaji mitihani, kwa kuwa wanafunzi sharti wasome na waandike.Vilevile, gharama hii inatokana na ununuzi wa kemikali za kutumiwa katika maabara. Aidha kuna gharama ya kuendesha michezo na tamasha za muziki na drama. Wanafunzi wa shule za malazi hula na kulala na kwa sababu hiyo maamuzi ya kifedha lazima yafanywe.Jambo ambalo linastahili kuangaliwa kwa makini ni viwanga vya kupanda kwa gharama ya maisha. Lazima tujiulize gharama hiyo imepanda kwa kiasi gani na wapi? Kwa kweli haiwezekani kununua kilo moja ya mahindi kwa bei hiyo hiyo Kitale, Mombasa na Turkana. Vile vile ni muhimu kujiuliza ikiwa shule husika ni ya mashambani au ya mjini? Kwa hivyo sharti la kifedha ni muhimu katika kuamua karo ya shule na maeneo mbalimbali nchini.Pili, hebu tuangalie ikiwa shule inavyohusika ni ya kiwango cha kaunti ndogo, kaunti au cha kitaifa. Hili ni muhimu kwa kuwa hali ya masomo katika shule hizo hutofautiana. Tofauti kuu hutokana na miundomisingi na programu za masomo zinazoendeshwa.Kwa mfano, programu za kitahmini, kompyuta na zinazohusu ziara huhitaji fedha nyingi. Shule ambayo ina masomo kama vile muziki, sanaa na sayansikimu sharti zitoze karo ya juu kwa kuwa masomo hayo huandamana na gharama ya kununua vyombo na vyakula? Sasa mbona fedha za ziada? Wanaotetea kupunguzwa kwa karo wana punguza mchango wa motisha katika ufanifu wa masomo. Ndio, baadhi ya shule hutoza karo ya juu ili kuwamotisha walimu kwa vyakula na kwa zawadi ili kuwastahi wanapopata matokea mema. Hali hiyo huwafanya kujikakamua kazini na kutoa huduma ya hali ya juu.Fedha za ziada vile vile, hutumiwa kuwajiri walimu wa ziada ikizingatiwa kuwa serikali haijawaajiri walimu wa kutosha. Pia katika baadhi ya shule, wanafunzi huandaliwa vyakula spesheli tofauti na mseto wa maharagwe na mahindi almarufu "maram" uliozoeleka katika shule nyingi ikumbukwe kuwe lishe bora ni mojawapo ya haki za kimsingi kwa watoto ambayo sharti iheshimiwe.Kwa marefu na mafupi yake, serikali haipaswi kuweka viwango sawa vya karo kwa kila shule kwa maana hilo huenda likazua mgogoro wa kiutawala katika shule nyingi. Shinikizo za kupunguzwa kwa karo inayotozwa hasa katika shule za upili zinafaa kutetewa kimantiki wala si kihisia.Mambo huenda yangekuwa tofauti ikiwa serikali ingewajibika kwa upande wake kwa kuwaajiri walimu wa kutosha kuwaongeza walimu mshahara na kuwatambua kwa zawadi wanapofanya kazi nzuri na kuwapandisha vyeo. Hata hivyo, mgala muue na haki umpe; hatua kali zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya walimu wanaowatoza wazazi karo ya juu kupindukia ili kuendeleza maslahi yao ya kibinafsi.Naamini kuwa hatua ya Waziri wa Elimu kukutana na washikadau katika sekta ya elimu kuhusu karo na uteuzi wa wanafunzi wa kujiunga na shule za upili ni ya busara na inafaa kuta mwelekeo mzuri kuhusu masuala tata yaliyopo kwa sasa.

(a) Fafanua mambo muhimu yanayostahili kuzingatiwa katika kutathmini viwango vya karo katika shule nchini Kenya.(Maneno 65 – 70)
(b) Fupisha aya tatu za mwisho.(maneno 40 – 45)

  

Answers


sharon
(a) Mambo muhimu yanayostahili kuzingatiwa katika kutathmini viwango vya karo katika shule nchini Kenya. (Maneno 65 – 70)
- Kushirikiana na walimu wakuu.
- Gharama ya vitabu, karatasi za uchapishaji wa mitihani.
- Ununuzi wa kemikali katika maabara.
- Gharama za kuendesha michezo na tamasha za muziki.
- Gharama ya shule za malazi.
- Kupanda kwa gharama ya maisha.
- Maeneo yapatikanapo shule.
- Kiwango cha shule.
- Programu za kitathmini shuleni / mfumo wa masomo katika shule husika – gharama ya kununua vyombo vinavyohitajika katika masomo haya.
- Motisha ya walimu na wafanyakazi wengine.
- Kuwaajiri walimu wa ziada.
- Gharama ya lishe bora.
(b) Fupisha aya tatu za mwisho. (maneno 40 – 45)
- Serikali haipaswi kuweka viwango sawa vya karo kwa kile shule.
- Hili huenda likazua mgogoro wa kiutawala.
- Shinikizo la kupunguzwa karo katika shule ya upili zinafaa kutetewa kimantiki na wala si kihisia.
- Serikali ingewajibika kwa kuwaajiri walimu wa kutosha.
- Walimu wangeongezewa mshahara, kuwazidi na kuwapandisha vyeo.
- Hatua zichukuliwe dhidi ya walimu wanaowatoza wazazi karo ya juu.
- Hatua ya waziri wa Elimu kukutana na washikadau katika sekta ya elimu ni ya busara.
- Hii inafaa kutoa mwelekeo mzuri kuhusu maswala tata yaliyopo kwa sasa.
sharon kalunda answered the question on September 24, 2019 at 12:16


Next: Waziri wa uchukuzi Bwana Msafiri ametoa mwito kwa kila mwananchi kusingatia sheria za barabarani ili kumaliza visa vya ajali vilivyokithiri.
Previous: Use logarithm tables to evaluate

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions