Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Upo msemo usemao kuwa kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi.

      

Soma kifungu kisha ujibu maswali
Upo msemo usemao kuwa kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi. Msemo huu unaafiki kabisa ari ya watu wazima wengi ambao licha ya umri wao, wamo mbioni kutafuta elimu ili mbali na kupata nuru, wajiunge na wasomi wengine katika kuikuza na kuiendeleza jamii. Ni kwa sababu hii ndipo serikali, kwa ushirikiano na mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali, imekuwa mstari wa mbele kutoa tunu hii kwa wazee ili kukata kiu yao ya elimu.
Watu wengi wa umri wa makamo ambao labda walikosa kumaliza masomo ya kiwango fulani au walikosa kabisa kwenda shuleni kwa sababu mbalimbali, hasa za kifedha, wamekuwa wakiweka elimu kama mojawapo ya majukumu yao ya utuuzima. Hii imekuwa dhahiri hasa baada ya serikali ya Kenya kuanzisha mpango wa elimu bila malipo katika shule za msingi, kwani idadi ya watu wazima ambao wamejitokeza kunufaika na mpango huo haisemeki. Pamoja na mpango huo, wapo wale ambao walikosa kusoma au kumaliza masomo kwa sababu ya karo, na kwa sababu sasa wana mapato, wameazimia kujiendeleza ili wapate vyeti. Hii ndiyo maana si ajabu kuona hata wafungwa kwenye magereza wakifanya mitihani ya kitaifa.
Elimu ya watu wazima hutekelezwa kwa njia mbalimbali. Kunayo elimu ambayo inalenga kuwapa watu hawa ujuzi wa kujiendeleza kiuchumi. Kutokana na ufundi wanaofundishwa, ambao huwa ni kazi kama useremala, umekanika, ushoni, usonara na kadhalika, huwawezesha kujitegemea kimapato, kwa hivyo wakaweza kuwapa wanao fursa ya kufaidi kile ambacho wao walikikosa.
Kunayo pia aina ya elimu ya watu wazima ambayo inaegemea maslahi ya watu hawa, hasa mafunzo kuhusu afya na usafi, masuala ya kifamilia na mahusiano na pia suala la ulezi. Kwa kufanya hivi, watu hawa hupata motisha ya kutangamana na watu wengine na kubadilishana nao mawazo kuhusu masuala yanayoathiri maisha yao Ndiyo sababu utapata watu wa aina hii wana ujuzi mkubwa wa kila kitu kinachoendelea katika kila kona ya nchi.
Aina nyingine ya elimu kwa watu wazima ni ile ya umma, inayohusu hasa masuala ya kisiasa. Mara nyingi, utawaona wakongwe wakipishwa kwenve foleni ili kwenda kupiga kura. Hii ni kwa sababu, mbali na kuwa huenda wakawa wamestaafu kikazi, bado wana jukumu muhimu sana katika kufanya maamuzi ya kisiasa kwa ajili ya vizazi vyao. Hivyo basi, serikali hufanya kila juhudi kuhakikisha kuwa hamasisho imetolewa kwa kila mwananchi, pamoja na kutoa mafunzo ya namna ya kupiga kura ili kura zisiharibike, hasa baada ya mtu kupitia utaratibu mrefu na wenye kuchosha wa kupiga kura. Kwa hili la kisiasa, watu wazima wengi hushangaza kwa jinsi wasivyoweza kushawishika kufanya maamuzi yanayokwenda kinyume na maazimio yao.
Maswali
(a) Eleza masuala muhimu katika aya mbili za kwanza kwa maneno 60.
(b) Fafanua jinsi elimu ya watu wazima hutekelezwa ukitumia maneno 60

  

Answers


sharon
a)
- watu wazima wengi wamo mbioni kutafuta elimu licha ya umri wao
- wanataka kupata nuru ya kujiunga na wasomi wengine katika kuiendeleza jamii
- serikali na mashirika yasiyo ya serikali yanawapa elimu watu wazima
- watu wazima waliokosa kukamilisha masomo yao wanaweka elimu kama jukumu lao la utu uziina
- idadi ya watu waliojitokeza kunufaika na elimu bila malipo haisemeki
- waliokosa kusoma kwa sababu ya karo wanatumia mapato yao kujisomesha ili wapate vyeti
-hata wafungwa hujisajili kufanya mitihani ya kitaifa zote
b)
- kwa kuwapa ujuzi wa kuiiendeleza kiuchumi kupitia ufundi kama vile useremala, umakanika, ushoni na usonara
- kuegemea maslahi yao, mafunzo kuhusu afya na usafi. maswaia ya familia, mahusiano na ulezi
- kuwapa motisha ya kutangamana na watu wengine na kubadilishana mawazo nao
- elimu ya umma hasa kuhusiana na masuala ya siasa
sharon kalunda answered the question on September 25, 2019 at 05:39


Next: Find the distance between the centre A of a circle whose equation is 2x2 + 2y2 +6x +10y +7 = 0
Previous: The diagram below represents the structure of aluminium chloride.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Nyumba ya Ndolo ya vyumba viwili ilikumbwa na hali mbili tofauti usiku huo.(Solved)

    Soma taarifa inayofuata kisha uyajibu maswali
    Nyumba ya Ndolo ya vyumba viwili ilikumbwa na hali mbili tofauti usiku huo. Chumbani alimolala Ndolo mwenyewe, kimya cha kaburi kilikatizwa na misono yake. Mara mojamoja alijigeuza kitandani na kuzifanya mbavu za kitanda zilalamikie : uzito wake. Katika chumba kingine, misono ya Ndolo na milio ya chenene ilimkirihi Msela. Kuzidisha, mawazo kuhusu hali ya mamake na unyama aliotendewa babake yalimtoroshea usingizi. Akasalia kujilaza kwenye mkeka wake.Kila alipotafakari maneno ya mzee Ndolo ndivyo Msela alivyozidi kuamini kwamba matatizo ya familia yao yalisababishwa na Mzee Bonga. Lakini yote hayo akayapuuza. Kubwa kwake lilikuwa ni kumwona mama yake na kujua ni hatua gani atakayochukua licha ya uzito aliouona mbele yake kwa kutokuwa na kipato. Msela alijikuta kwenye mtihani mgumu ulioifanya mishipa ya kichwa kusimama na kichwa kumuuma.Kwa sababii ya maiimivu hayo, Msela alijisogeza na kujiegemeza kwenye ukuta. Akawa anatazama iinsi Mungu alikuwa akiufanya muujiza wake ambao alikuwa ameukosa kwa muda. Alifurahi kuliona jua likipenyeza miale yake kisha kujitokeza na kuangaza dunia. Ingawa macho yake yalifurahia mapambazuko hayo, moyo wake ulikuwa na machungu. Akili yake ilikuwa na zigo zito la kutafuta ufumbuzi ambao kwa upande wake ilikuwa ni ndoto.Msela alijiuliza mengi katika nafsi yake. Aliisaili nafsi yake kuhusu hisi za ndugu zake, kuhusu hali ya mama yao aliyesemekana kuwa mwendawazimu, na ikiwa walifahamu hilo. Alitaka kujua alikokula na alikolala mamake katika hali yake hiyo. Kila fikira iliyompitikia akilini ilitaka kupasua mishipa ya kichwa chake. 'Ina maana hawaoni au nao wamekuwa na roho ya korosho kama Mzee Bonga?' alijisaili Msela. Katika maswali yote hayo, alikosa majibu isipokuwa kuzidisha maumivu ya kichwa. Isingekuwa kwa machozi yaliyompunguzia baadhi ya machungu, labda angegeuka hayawani.Macho ya Msela yalikuwa yamevimba, tena mekundu kutokana na ukosefu wa usingizi. Mwili wake nao ulionekana kunyong'onyea kwa sababu ya mazonge ya mawazo. Alichukua kikopo kilichochoka cha maji na kunawa uso kisha akaenda kukaa juu ya jiwe. Kibaridi kilichotokana na mvua iliyokuwa ikinyesha kilimpiga lakini hakujali. Angejali vipi yeye katika mtafaruku wa hali ya mamake?
    Ingawa Mzee Ndolo alimwita ndani ili aipishe mvua, Msela alidinda. Badala yake, aliendelea kuuachilia mwili wake kuloweshwa na michonyoto ya mvua. Kila alivyofikiria maisha ya wendawazimu ndivyo moyo ulivyozidi kumuuma. Akawa yuajiuliza mama yake aliukosea nini ulimwengu hata apate adhabu ile. Halafu fumo lake la mwisho moyoni ni madhara ya mvua na baridi ile kwa mamake. Hana makao, hana mavazi mazito, hana chochote! Alipowazia makazi ya jalalani na majumba mabovu ambayo siku zote amekuwa akiwaona wendawazimu wakifaliwa kwayo, aliachama.

    Maswali
    (a) Eleza ukinzani ulio katika nyumba ya Ndolo.
    (b) Ni yapi yaliyomkosesha usingizi msela?
    (c) Kwa nini Msela hakuweza kuibadili hali yake.
    (d) Taja chanzo cha madhila ya Msela.
    (e) Muujiza wa Mungu unatoa taashira gani kwa hali ya msimulizi?
    (f) Eleza maana ya msamiati ufuatao ukirejelea taarifa.
    i) robo ya korosho
    ii) alichama
    iii) kunyong'onyea

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi yenye muundo wa: N + V + T + H + N + E + U + T.(Solved)

    Tunga sentensi yenye muundo wa:
    N + V + T + H + N + E + U + T.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya kiambishi "ku" Kulia kwake kulisababisha msongamano wa watu alikoKuwa.(Solved)

    Eleza matumizi ya kiambishi "ku"
    Kulia kwake Kulisababisha msongamano wa watu alikoKuwa.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Nomino zifuatazo zinapatikana katika ngeli zipi? i) Chumvi: ii) Nywele: iii) Mafuta:(Solved)

    Nomino zifuatazo zinapatikana katika ngeli zipi?
    i) Chumvi:
    ii) Nywele:
    iii) Mafuta:

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Ukitolea mfano mwafaka, fafanua majukumu yoyote manne ya viambishi awali.(Solved)

    Ukitolea mfano mwafaka, fafanua majukumu yoyote manne ya viambishi awali.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya mghuno katika lugha ya Kiswahili.(Solved)

    Eleza maana ya mghuno katika lugha ya Kiswahili.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Serikali kupitia Wizara ya Elimu imetoa mwongozo wa karo ambao unastahili kuzingatiwa katika shule za upili kufuatia haua ya shule mbalimbali kuongeza karo kwa viwango...(Solved)

    Serikali kupitia Wizara ya Elimu imetoa mwongozo wa karo ambao unastahili kuzingatiwa katika shule za upili kufuatia haua ya shule mbalimbali kuongeza karo kwa viwango mbalimbali. Hatua hiyo inadhamiriwa kumking mzazi dhidi ya kunyanyaswa kifedha walimu hasa ikizangiwa kuwa gharama ya maisha imepanda mara dufu.Hata hivyo, ingekuwa bora ikiwa serikali ingefanya maamzi kwa ushirikiano na walimu wakuu maana kwa hakika suala la karo linahusu matumizi ya fedha ambayo pia huja na gharama zake. Gharama hii inaokana na ununuzi wa vitabu vya Kada na vya mazoezi, karatasi za uchapishaji mitihani, kwa kuwa wanafunzi sharti wasome na waandike.Vilevile, gharama hii inatokana na ununuzi wa kemikali za kutumiwa katika maabara. Aidha kuna gharama ya kuendesha michezo na tamasha za muziki na drama. Wanafunzi wa shule za malazi hula na kulala na kwa sababu hiyo maamuzi ya kifedha lazima yafanywe.Jambo ambalo linastahili kuangaliwa kwa makini ni viwanga vya kupanda kwa gharama ya maisha. Lazima tujiulize gharama hiyo imepanda kwa kiasi gani na wapi? Kwa kweli haiwezekani kununua kilo moja ya mahindi kwa bei hiyo hiyo Kitale, Mombasa na Turkana. Vile vile ni muhimu kujiuliza ikiwa shule husika ni ya mashambani au ya mjini? Kwa hivyo sharti la kifedha ni muhimu katika kuamua karo ya shule na maeneo mbalimbali nchini.Pili, hebu tuangalie ikiwa shule inavyohusika ni ya kiwango cha kaunti ndogo, kaunti au cha kitaifa. Hili ni muhimu kwa kuwa hali ya masomo katika shule hizo hutofautiana. Tofauti kuu hutokana na miundomisingi na programu za masomo zinazoendeshwa.Kwa mfano, programu za kitahmini, kompyuta na zinazohusu ziara huhitaji fedha nyingi. Shule ambayo ina masomo kama vile muziki, sanaa na sayansikimu sharti zitoze karo ya juu kwa kuwa masomo hayo huandamana na gharama ya kununua vyombo na vyakula? Sasa mbona fedha za ziada? Wanaotetea kupunguzwa kwa karo wana punguza mchango wa motisha katika ufanifu wa masomo. Ndio, baadhi ya shule hutoza karo ya juu ili kuwamotisha walimu kwa vyakula na kwa zawadi ili kuwastahi wanapopata matokea mema. Hali hiyo huwafanya kujikakamua kazini na kutoa huduma ya hali ya juu.Fedha za ziada vile vile, hutumiwa kuwajiri walimu wa ziada ikizingatiwa kuwa serikali haijawaajiri walimu wa kutosha. Pia katika baadhi ya shule, wanafunzi huandaliwa vyakula spesheli tofauti na mseto wa maharagwe na mahindi almarufu "maram" uliozoeleka katika shule nyingi ikumbukwe kuwe lishe bora ni mojawapo ya haki za kimsingi kwa watoto ambayo sharti iheshimiwe.Kwa marefu na mafupi yake, serikali haipaswi kuweka viwango sawa vya karo kwa kila shule kwa maana hilo huenda likazua mgogoro wa kiutawala katika shule nyingi. Shinikizo za kupunguzwa kwa karo inayotozwa hasa katika shule za upili zinafaa kutetewa kimantiki wala si kihisia.Mambo huenda yangekuwa tofauti ikiwa serikali ingewajibika kwa upande wake kwa kuwaajiri walimu wa kutosha kuwaongeza walimu mshahara na kuwatambua kwa zawadi wanapofanya kazi nzuri na kuwapandisha vyeo. Hata hivyo, mgala muue na haki umpe; hatua kali zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya walimu wanaowatoza wazazi karo ya juu kupindukia ili kuendeleza maslahi yao ya kibinafsi.Naamini kuwa hatua ya Waziri wa Elimu kukutana na washikadau katika sekta ya elimu kuhusu karo na uteuzi wa wanafunzi wa kujiunga na shule za upili ni ya busara na inafaa kuta mwelekeo mzuri kuhusu masuala tata yaliyopo kwa sasa.

    (a) Fafanua mambo muhimu yanayostahili kuzingatiwa katika kutathmini viwango vya karo katika shule nchini Kenya.(Maneno 65 – 70)
    (b) Fupisha aya tatu za mwisho.(maneno 40 – 45)

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Waziri wa uchukuzi Bwana Msafiri ametoa mwito kwa kila mwananchi kusingatia sheria za barabarani ili kumaliza visa vya ajali vilivyokithiri.(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Waziri wa uchukuzi Bwana Msafiri ametoa mwito kwa kila mwananchi kusingatia sheria za barabarani ili kumaliza visa vya ajali vilivyokithiri. Alisema kuwa ongezeko la ajali za barabarani linachangiwa pakubwa na watu binafsi.Akiongea katika hafla ya kuzindua mbinu za kuhakikisha usalama barabarani, Bwana Msafiri alisema yasikitisha kuona kuwa ajali za barabarani zimeongezeka katika siku za hivi majuzi. Alielezea kuwa wizara yake imekerwa na utekelezaji wa majukumu na mapuza miongoni mwa wanaohusika na sekta ya uchukuzi.Alisema wengi wa wenye magari wamepuza masharti mengi ambayo yaliwekwa na wizara, yaliyokusudiwa kugunguza ajali. Alisema magari mengi yamekuwa kachara na kwamba mengi yameng‘olewa vidhibiti mwendo. Basi magari yanaendeshwa kwa kasi ya umeme. Hili limeongeza ajali kwa kiasi kikubwa. Mengi hayana mishipi ya usalama na wasafiri hukabiliwa na hatari wanaposafiri. Aliongeza kuwa sura ya magari hayo ni dhihirisho kuwa wenye magari wamepotoka kabisa, ―magari mengi yamerembeshwa hata kwa picha chafu, jambo linalodhihirisha utovo wa mbeko na kutofuata sheria. Mengine yanacheza muziki kwa sauti ya juu hivi kwamba hata dereva na utingo hawawezi kusikia grudumu liking‘oka. Baadhi yao yanaonyesha picha chafu chafu za video na kuufanya usafiri kuwa vyumba vya sinema chafu!‖ Alisema kutovaa sare kwa madereva na makondakta na kuwapakia abiria kupita kiasi ni kilele cha upuui wa sheria zilizowekwa.
    Wasafiri pia wanapuuza masharti yaliyowekwa kwa lengo la kuwafaa, ―alisema waziri. Alisikitika kuwa wasafiri wengi hawafungi mishipi ya usalama hata inapopatikana, aidha wanakubali kuingia magari yaliyojaa tayari, hali inayoongenzea uwezekano wa gari kupata ajali kwa kulemewa na uzito. Aliwakumbusha kuwa gali likipata ajali wakiwa wamepakiwa hivi, hawezi kugharamiwa na bima ya gari kwa vile bima yenyewe hukatiwa idadi mahususi ya wasafiri. Aliwalaumu watembeaji barabarani kwa kutozingatia sheria za kawaida. Alisema kwa mfano katika gurufu kuna mahali ambako kuna vivuko ila hawavitumii na wengine huishia kugongwa na magari.Mwisho aliwalaumu maafisa wa trafiki wanaotekeleza majukumu yao. Akitisha kuwachukulia hatua kali, alisema kuwa yaskitisha kusikia kuwa wanachukua kadhongo na kuyaachilia magari yaliyo na kasoro badala ya kuyashtaki kulingana na sheria. Aliwaongezea lawama wasafiri kwa kunyamaza wanapoyaona haya yakitendeka machoni. Alisababisha kicheko aliposema kuwa baadhi ya wasafiri huwahimiza makondakta watoe chai haraka ili waendelee na usafiri ya bila kujali hatari wanazojiingiza kwazo.
    Akionya kuwa angechukua hatua ya kuregesha utulivu, alihitimisha kwa kusema kuwa wizara yake limetoa ilani kwa watumiaji wote wa barabarani. Alitoa makataa ya siku kumi na nne ambapo yoyote asiyefuata kaida zote za barabarani atachukuliwa hatua kisheria.

    a) Fafanua sababu za mwito wa waziri wa uchukuzi Bwana Msafiri?
    b) Eleza jinsi wenye magaari wamechangia katika kukithiri kwa visa vya ajali barabarani?
    c) Fafanua mchango wa wasafiri katika kudorora kwa hali ya usalama barabarani.
    d) Eleza majukumu ya maafisa wa trafiki katika kudumisha usafiri kulingana na ufahamu.
    e) Toa visawe vya maneno yafuatayo.
    (i) Kondakta:
    (ii) Toa ilani:
    (iii) Toa makataa:

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha mofimu katika neno: Walichimba(Solved)

    Ainisha mofimu katika neno:
    Walichimba

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Huku ukitumia mifano, tofautisha sentensi ambatano na sentensi changamano.(Solved)

    Huku ukitumia mifano, tofautisha sentensi ambatano na sentensi changamano.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Geuza sentensi hii hadi usemi wa taarifa: "sitakuja shuleni kesho", mwalimu mkuu akasema,nitaenda kuhudhuria mkutano Mombasa.(Solved)

    Geuza sentensi hii hadi usemi wa taarifa:
    "sitakuja shuleni kesho", mwalimu mkuu akasema,nitaenda kuhudhuria mkutano Mombasa.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja kutofautisha "thibiti" na "dhibiti".(Solved)

    Tunga sentensi moja kutofautisha "thibiti" na "dhibiti".

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika ukubwa. Mke wa mzee huyu hupenda watoto sana.(Solved)

    Andika katika ukubwa.
    Mke wa mzee huyu hupenda watoto sana.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Changanua kwa kutumia mchoro wa matawi. Mvuvi hodari alifurahi alipofanikiwa kuvua jodari.(Solved)

    Changanua kwa kutumia mchoro wa matawi.
    Mvuvi hodari alifurahi alipofanikiwa kuvua jodari.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha Mwanafunzi ambaye amefika ametuzwa.(Solved)

    Kanusha
    Mwanafunzi ambaye amefika ametuzwa.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Andika ngeli za nomino zifuatazo. (i) Uwele (ii) Vita(Solved)

    Andika ngeli za nomino zifuatazo.
    (i) Uwele
    (ii) Vita

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Weka vitenzi hivi katika hali ya kuamrisha wingi. (i) -nywa (ii) Tubu(Solved)

    Weka vitenzi hivi katika hali ya kuamrisha wingi.
    (i) -nywa
    (ii) Tubu

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya "na" katika sentensi ifuatayo. Simba aliuawa na wawindaji haramu nasi tukawaripoti.(Solved)

    Eleza matumizi ya "na" katika sentensi ifuatayo.
    Simba aliuawa na wawindaji haramu nasi tukawaripoti.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Tumia kiwakilishi cha nafsi huru (nafsi ya pili wingi) katika sentensi.(Solved)

    Tumia kiwakilishi cha nafsi huru (nafsi ya pili wingi) katika sentensi.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi hii upya bila kubadilisha maana ukitumia "O" rejeshi. Mwanafunzi alitumwa nyumbani juzi na hajapata karo hadi leo.(Solved)

    Andika sentensi hii upya bila kubadilisha maana ukitumia "O" rejeshi.
    Mwanafunzi alitumwa nyumbani juzi na hajapata karo hadi leo.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)