Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Tunga sentensi kwa kutumia kivumishi cha sifa kisichoambishika.

      

Tunga sentensi kwa kutumia kivumishi cha sifa kisichoambishika.

  

Answers


sharon
Mchezaji hodari ameumia.
sharon kalunda answered the question on September 25, 2019 at 06:40


Next: The figures below represent two phases of actively dividing cell.
Previous: The Scientific name of confused beetle is TRIBOLIUM CONFUSAM. Identify any three mistakes made in writing the name.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Unda nomino dhahania kutokana na kitenzi - abudu.(Solved)

    Unda nomino dhahania kutokana na kitenzi - abudu.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo . Jane alitengenezewa kiti na fundi kwa nyundo(Solved)

    Ainisha shamirisho katika sentensi ifuatayo .
    Jane alitengenezewa kiti na fundi kwa nyundo

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi mbili kudhihirisha maana ya vitate rika na lika.(Solved)

    Tunga sentensi mbili kudhihirisha maana ya vitate rika na lika.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha matumizi ya 'ni' Kimbieni! Huyu ni mnyama aliyeniuma mguuni.(Solved)

    Bainisha matumizi ya 'ni'
    Kimbieni! Huyu ni mnyama aliyeniuma mguuni.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha matumizi ya 'po' katika sentensi ifuatayo. Alipowasili alionyeshwa walipo.(Solved)

    Bainisha matumizi ya 'po' katika sentensi ifuatayo.
    Alipowasili alionyeshwa walipo.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi cha pekee cha kusisitiza katika ngeli ya U-U(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi cha pekee cha kusisitiza katika ngeli ya U-U

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Taja msemo mwingine wenye maana sawa na : piga maji(Solved)

    Taja msemo mwingine wenye maana sawa na :
    piga maji.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Akifisha sentensi ifuatayo: Je ni nani alingoa mti wa kiprono(Solved)

    Akifisha sentensi ifuatayo:
    Je ni nani alingoa mti wa kiprono

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Changanua kwa kutumia jedwali. Yeye alifaulu ingawa hana adabu(Solved)

    Changanua kwa kutumia jedwali.
    Yeye alifaulu ingawa hana adabu

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Nyambua kitenzi 'chwa' katika kauli ya kutendea kisha ukitungie sentensi.(Solved)

    Nyambua kitenzi 'chwa' katika kauli ya kutendea kisha ukitungie sentensi.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume cha sentensi ifuatayo . Mahindi ya mama yamekua kwa kupata mvua ya kutosha.(Solved)

    Andika kinyume cha sentensi ifuatayo .
    Mahindi ya mama yamekua kwa kupata mvua ya kutosha.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha vitenzi katika sentensi ifutayo. Wao watakuja kuwa waandishi maarufu.(Solved)

    Ainisha vitenzi katika sentensi ifutayo.
    Wao watakuja kuwa waandishi maarufu.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha mofimu katika neno lifuatalo: Milangoni(Solved)

    Ainisha mofimu katika neno lifuatalo:
    Milangoni

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Upo msemo usemao kuwa kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi.(Solved)

    Soma kifungu kisha ujibu maswali
    Upo msemo usemao kuwa kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi. Msemo huu unaafiki kabisa ari ya watu wazima wengi ambao licha ya umri wao, wamo mbioni kutafuta elimu ili mbali na kupata nuru, wajiunge na wasomi wengine katika kuikuza na kuiendeleza jamii. Ni kwa sababu hii ndipo serikali, kwa ushirikiano na mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali, imekuwa mstari wa mbele kutoa tunu hii kwa wazee ili kukata kiu yao ya elimu.
    Watu wengi wa umri wa makamo ambao labda walikosa kumaliza masomo ya kiwango fulani au walikosa kabisa kwenda shuleni kwa sababu mbalimbali, hasa za kifedha, wamekuwa wakiweka elimu kama mojawapo ya majukumu yao ya utuuzima. Hii imekuwa dhahiri hasa baada ya serikali ya Kenya kuanzisha mpango wa elimu bila malipo katika shule za msingi, kwani idadi ya watu wazima ambao wamejitokeza kunufaika na mpango huo haisemeki. Pamoja na mpango huo, wapo wale ambao walikosa kusoma au kumaliza masomo kwa sababu ya karo, na kwa sababu sasa wana mapato, wameazimia kujiendeleza ili wapate vyeti. Hii ndiyo maana si ajabu kuona hata wafungwa kwenye magereza wakifanya mitihani ya kitaifa.
    Elimu ya watu wazima hutekelezwa kwa njia mbalimbali. Kunayo elimu ambayo inalenga kuwapa watu hawa ujuzi wa kujiendeleza kiuchumi. Kutokana na ufundi wanaofundishwa, ambao huwa ni kazi kama useremala, umekanika, ushoni, usonara na kadhalika, huwawezesha kujitegemea kimapato, kwa hivyo wakaweza kuwapa wanao fursa ya kufaidi kile ambacho wao walikikosa.
    Kunayo pia aina ya elimu ya watu wazima ambayo inaegemea maslahi ya watu hawa, hasa mafunzo kuhusu afya na usafi, masuala ya kifamilia na mahusiano na pia suala la ulezi. Kwa kufanya hivi, watu hawa hupata motisha ya kutangamana na watu wengine na kubadilishana nao mawazo kuhusu masuala yanayoathiri maisha yao Ndiyo sababu utapata watu wa aina hii wana ujuzi mkubwa wa kila kitu kinachoendelea katika kila kona ya nchi.
    Aina nyingine ya elimu kwa watu wazima ni ile ya umma, inayohusu hasa masuala ya kisiasa. Mara nyingi, utawaona wakongwe wakipishwa kwenve foleni ili kwenda kupiga kura. Hii ni kwa sababu, mbali na kuwa huenda wakawa wamestaafu kikazi, bado wana jukumu muhimu sana katika kufanya maamuzi ya kisiasa kwa ajili ya vizazi vyao. Hivyo basi, serikali hufanya kila juhudi kuhakikisha kuwa hamasisho imetolewa kwa kila mwananchi, pamoja na kutoa mafunzo ya namna ya kupiga kura ili kura zisiharibike, hasa baada ya mtu kupitia utaratibu mrefu na wenye kuchosha wa kupiga kura. Kwa hili la kisiasa, watu wazima wengi hushangaza kwa jinsi wasivyoweza kushawishika kufanya maamuzi yanayokwenda kinyume na maazimio yao.
    Maswali
    (a) Eleza masuala muhimu katika aya mbili za kwanza kwa maneno 60.
    (b) Fafanua jinsi elimu ya watu wazima hutekelezwa ukitumia maneno 60

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Nyumba ya Ndolo ya vyumba viwili ilikumbwa na hali mbili tofauti usiku huo.(Solved)

    Soma taarifa inayofuata kisha uyajibu maswali
    Nyumba ya Ndolo ya vyumba viwili ilikumbwa na hali mbili tofauti usiku huo. Chumbani alimolala Ndolo mwenyewe, kimya cha kaburi kilikatizwa na misono yake. Mara mojamoja alijigeuza kitandani na kuzifanya mbavu za kitanda zilalamikie : uzito wake. Katika chumba kingine, misono ya Ndolo na milio ya chenene ilimkirihi Msela. Kuzidisha, mawazo kuhusu hali ya mamake na unyama aliotendewa babake yalimtoroshea usingizi. Akasalia kujilaza kwenye mkeka wake.Kila alipotafakari maneno ya mzee Ndolo ndivyo Msela alivyozidi kuamini kwamba matatizo ya familia yao yalisababishwa na Mzee Bonga. Lakini yote hayo akayapuuza. Kubwa kwake lilikuwa ni kumwona mama yake na kujua ni hatua gani atakayochukua licha ya uzito aliouona mbele yake kwa kutokuwa na kipato. Msela alijikuta kwenye mtihani mgumu ulioifanya mishipa ya kichwa kusimama na kichwa kumuuma.Kwa sababii ya maiimivu hayo, Msela alijisogeza na kujiegemeza kwenye ukuta. Akawa anatazama iinsi Mungu alikuwa akiufanya muujiza wake ambao alikuwa ameukosa kwa muda. Alifurahi kuliona jua likipenyeza miale yake kisha kujitokeza na kuangaza dunia. Ingawa macho yake yalifurahia mapambazuko hayo, moyo wake ulikuwa na machungu. Akili yake ilikuwa na zigo zito la kutafuta ufumbuzi ambao kwa upande wake ilikuwa ni ndoto.Msela alijiuliza mengi katika nafsi yake. Aliisaili nafsi yake kuhusu hisi za ndugu zake, kuhusu hali ya mama yao aliyesemekana kuwa mwendawazimu, na ikiwa walifahamu hilo. Alitaka kujua alikokula na alikolala mamake katika hali yake hiyo. Kila fikira iliyompitikia akilini ilitaka kupasua mishipa ya kichwa chake. 'Ina maana hawaoni au nao wamekuwa na roho ya korosho kama Mzee Bonga?' alijisaili Msela. Katika maswali yote hayo, alikosa majibu isipokuwa kuzidisha maumivu ya kichwa. Isingekuwa kwa machozi yaliyompunguzia baadhi ya machungu, labda angegeuka hayawani.Macho ya Msela yalikuwa yamevimba, tena mekundu kutokana na ukosefu wa usingizi. Mwili wake nao ulionekana kunyong'onyea kwa sababu ya mazonge ya mawazo. Alichukua kikopo kilichochoka cha maji na kunawa uso kisha akaenda kukaa juu ya jiwe. Kibaridi kilichotokana na mvua iliyokuwa ikinyesha kilimpiga lakini hakujali. Angejali vipi yeye katika mtafaruku wa hali ya mamake?
    Ingawa Mzee Ndolo alimwita ndani ili aipishe mvua, Msela alidinda. Badala yake, aliendelea kuuachilia mwili wake kuloweshwa na michonyoto ya mvua. Kila alivyofikiria maisha ya wendawazimu ndivyo moyo ulivyozidi kumuuma. Akawa yuajiuliza mama yake aliukosea nini ulimwengu hata apate adhabu ile. Halafu fumo lake la mwisho moyoni ni madhara ya mvua na baridi ile kwa mamake. Hana makao, hana mavazi mazito, hana chochote! Alipowazia makazi ya jalalani na majumba mabovu ambayo siku zote amekuwa akiwaona wendawazimu wakifaliwa kwayo, aliachama.

    Maswali
    (a) Eleza ukinzani ulio katika nyumba ya Ndolo.
    (b) Ni yapi yaliyomkosesha usingizi msela?
    (c) Kwa nini Msela hakuweza kuibadili hali yake.
    (d) Taja chanzo cha madhila ya Msela.
    (e) Muujiza wa Mungu unatoa taashira gani kwa hali ya msimulizi?
    (f) Eleza maana ya msamiati ufuatao ukirejelea taarifa.
    i) robo ya korosho
    ii) alichama
    iii) kunyong'onyea

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi yenye muundo wa: N + V + T + H + N + E + U + T.(Solved)

    Tunga sentensi yenye muundo wa:
    N + V + T + H + N + E + U + T.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya kiambishi "ku" Kulia kwake kulisababisha msongamano wa watu alikoKuwa.(Solved)

    Eleza matumizi ya kiambishi "ku"
    Kulia kwake Kulisababisha msongamano wa watu alikoKuwa.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Nomino zifuatazo zinapatikana katika ngeli zipi? i) Chumvi: ii) Nywele: iii) Mafuta:(Solved)

    Nomino zifuatazo zinapatikana katika ngeli zipi?
    i) Chumvi:
    ii) Nywele:
    iii) Mafuta:

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Ukitolea mfano mwafaka, fafanua majukumu yoyote manne ya viambishi awali.(Solved)

    Ukitolea mfano mwafaka, fafanua majukumu yoyote manne ya viambishi awali.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya mghuno katika lugha ya Kiswahili.(Solved)

    Eleza maana ya mghuno katika lugha ya Kiswahili.

    Date posted: September 24, 2019.  Answers (1)