Mbona isiwe kweli? Wewe panga uwalete tule matunda ya jasho letu nao watoto.(Kwa kurejelea tamthilia "Mstahiki Meya")(Solved)
Mbona isiwe kweli? Wewe panga uwalete tule matunda ya jasho letu nao watoto.(Kwa kurejelea tamthilia "Mstahiki Meya")
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza mbinu mbili za uandishi katika dondoo hili.
(c) Eleza yaliyopangwa baada ya usemi huu.
Date posted: September 25, 2019. Answers (1)
Ole wangu! Ole wangu, nisikize Mola wangu,(Solved)
Ole wangu! Ole wangu, nisikize Mola wangu,
Lipokee ombi langu, wanisikize wenzangu,
Washike ujumbe wangu, uloleta Mola kwangu,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Amri kumi za Mola, mumekwisha zikiuka
Ndipo hamuwezi lala, mumekwisha vurugika,
Mumemsahau Mola, ndipo nanyi mwasumbuka,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Mwaabudu mashetani, ushirikina ni mwingi,
Munaiba hadharani, waongo nao ni wengi,
Mwajawa na taraghani, na wazimu mwingi,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora,
Mwauana ovyoovyo, mwasemana ndivyo sivyo,
Fitina nazo zilivyo, mwarogana vivyo hivyo,
Matusi ni vile sivyo, munaisha ka isivyo,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Kuna dawa za kulevya, na hata pembe haramu,
Na ukimwi nakujuvya, unaua wanadamu,
Na mimba nazo kuavya, watoto ni marehemu,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Wengine nao hudai, waoe jinisi moja,
Ati mwingine hafai, heri sawia ya mja,
Haya maoni ni hoi, tupinge kila mmoja,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Ploti mwazinyakua, na viwanja vya mipira,
Makaburi mwala pia, mabibi mwateka nyara,
Ibada zikifikia, mwafurika kwa majira
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Wengi tuwachaguao, si viongozi ni waizi,
Tamaa walio nao, yaongoza maamuzi,
Mishahara ile yao, huongezwa kila mwezi,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Usalama hatunao, wasiwasi umezidi,
Waja kiwa makazio, huogopa magaidi,
Mabomu walipuao, huruma wamekaidi,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
Beti kumi namaliza, dua yangu imetimu,
Mungu amekwisha anza, kuhukumu mwanadamu,
Wote walojipotoza.waiepuke hukumu,
Nyakati tunazoishi, ni Sodoma na Gomora.
MASWALI
(a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka.
(b) Shairi hili linaweza kuwekwa katika bahari kadhaa. Taja na ueleze bahari zozote tatu.
(c) Taja na ueleze mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika ubeti wa kwanza.
(d) Eleza sababu ya mshairi kutumia alama ya ritifaa katika ubeti wa nne
(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumika katika ubeti wa tisa mshororo wa tatu na ueleze umuhimu wake.
(f) Andika ubeti wa sita kwa lugha tutumbi.
(g) Taja mifano mitatu ya uozo anaolalamikia mwandishi.
(h) Eleza toni ya mwandishi.
Date posted: September 25, 2019. Answers (1)
Upo msemo usemao kuwa kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi.(Solved)
Soma kifungu kisha ujibu maswali
Upo msemo usemao kuwa kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa upishi. Msemo huu unaafiki kabisa ari ya watu wazima wengi ambao licha ya umri wao, wamo mbioni kutafuta elimu ili mbali na kupata nuru, wajiunge na wasomi wengine katika kuikuza na kuiendeleza jamii. Ni kwa sababu hii ndipo serikali, kwa ushirikiano na mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali, imekuwa mstari wa mbele kutoa tunu hii kwa wazee ili kukata kiu yao ya elimu.
Watu wengi wa umri wa makamo ambao labda walikosa kumaliza masomo ya kiwango fulani au walikosa kabisa kwenda shuleni kwa sababu mbalimbali, hasa za kifedha, wamekuwa wakiweka elimu kama mojawapo ya majukumu yao ya utuuzima. Hii imekuwa dhahiri hasa baada ya serikali ya Kenya kuanzisha mpango wa elimu bila malipo katika shule za msingi, kwani idadi ya watu wazima ambao wamejitokeza kunufaika na mpango huo haisemeki. Pamoja na mpango huo, wapo wale ambao walikosa kusoma au kumaliza masomo kwa sababu ya karo, na kwa sababu sasa wana mapato, wameazimia kujiendeleza ili wapate vyeti. Hii ndiyo maana si ajabu kuona hata wafungwa kwenye magereza wakifanya mitihani ya kitaifa.
Elimu ya watu wazima hutekelezwa kwa njia mbalimbali. Kunayo elimu ambayo inalenga kuwapa watu hawa ujuzi wa kujiendeleza kiuchumi. Kutokana na ufundi wanaofundishwa, ambao huwa ni kazi kama useremala, umekanika, ushoni, usonara na kadhalika, huwawezesha kujitegemea kimapato, kwa hivyo wakaweza kuwapa wanao fursa ya kufaidi kile ambacho wao walikikosa.
Kunayo pia aina ya elimu ya watu wazima ambayo inaegemea maslahi ya watu hawa, hasa mafunzo kuhusu afya na usafi, masuala ya kifamilia na mahusiano na pia suala la ulezi. Kwa kufanya hivi, watu hawa hupata motisha ya kutangamana na watu wengine na kubadilishana nao mawazo kuhusu masuala yanayoathiri maisha yao Ndiyo sababu utapata watu wa aina hii wana ujuzi mkubwa wa kila kitu kinachoendelea katika kila kona ya nchi.
Aina nyingine ya elimu kwa watu wazima ni ile ya umma, inayohusu hasa masuala ya kisiasa. Mara nyingi, utawaona wakongwe wakipishwa kwenve foleni ili kwenda kupiga kura. Hii ni kwa sababu, mbali na kuwa huenda wakawa wamestaafu kikazi, bado wana jukumu muhimu sana katika kufanya maamuzi ya kisiasa kwa ajili ya vizazi vyao. Hivyo basi, serikali hufanya kila juhudi kuhakikisha kuwa hamasisho imetolewa kwa kila mwananchi, pamoja na kutoa mafunzo ya namna ya kupiga kura ili kura zisiharibike, hasa baada ya mtu kupitia utaratibu mrefu na wenye kuchosha wa kupiga kura. Kwa hili la kisiasa, watu wazima wengi hushangaza kwa jinsi wasivyoweza kushawishika kufanya maamuzi yanayokwenda kinyume na maazimio yao.
Maswali
(a) Eleza masuala muhimu katika aya mbili za kwanza kwa maneno 60.
(b) Fafanua jinsi elimu ya watu wazima hutekelezwa ukitumia maneno 60
Date posted: September 25, 2019. Answers (1)