Matumizi ya sheng' yameshamiri sana nchini Kenya hasa miongoni mwa vijana.

      

Soma taarifa inayofuata kisha uyajibu maswali
Matumizi ya sheng' yameshamiri sana nchini Kenya hata miongoni mwa vijana. Ni kilugha ambacho kinakisiwa kuzuka katika miaka ya 60 na 70 katika makazi ya mashariki mwa jiji la Nairobi kama vile Kaloleni, Mbotela/ Bahati na kadhalika.Kwa sasa ni kilugha kilichoenea kwingi nchini Kenya na kuwa kitambulisho cha takriban vijana wengi. Wataalam mbalimbali wanabainisha nadharia mbalimbali kuhusu chanzo cha lugha hii. Kuna nadharia mbili kuu kuhusu asili ya lugha ya Sheng: kwamba kilugha hiki kiliibuka kutokana na wahuni na wakora jijini Nairobi ambao lengo lao Iilikuwa kuwasiliana kwa siri. Nadharia nyingine ni kuwa kilichipuka kutokana na vijana ambao walizua lugha ya kuwasiliana baada ya uhuru (kwa sababu walikichukia Kiswahili ambacho walikiona kama lugha ya uboi)
Dhana hizi kwa muda mrefu, zimeathiri mitazamo kuhusiana na kilugha hiki. Kwa sasa ni kilugha ambacho ,yjiasambaa katika sehemu mbalimbali za Kenya na watu wa matabaka mbalimbali wanakitumia. Kilugha hiki kimeanza kuashiria uhalisia mkubwa wa maisha ya kisasa, zaidi katika jamii ya Wakenya. Aidha, sheng imejitanzua kutoka hali ya kuwa kilugha cha maongezi pekee na sasa kinatumiwa katika baadhi ya vitabu, hata waandishi wa vitabu wameanza kukitumia. Kwa mfano, katika miaka ya 80, David Mailu katika kitabu chake 'Without Kiinua Mgongo' alitumia Sheng. Katika siku za hivi karibuni, riwaya ya 'Kidagaa Kimemwozea' iliyoandikwa na Ken Walibora kilugha cha sheng kimepewa nafasi kama kitambulisho cha vijana kupitia kwa mhusika DJ Bob.
Vilevile kumezuka vyombo vya habari kama redio, mfano idhaa ya Ghetto, redio ambayo inaendeleza mawasiliano kwa matumizi ya Sheng. Kuna vipindi vya matangazo ya kibiashara katika runinga ambayo yanaendelezwa kwa Sheng. Kwa mfano, katika 'gazeti la Taifa Leo, kuna ukumbi wa 'Mchongoano' ambao umekuwa ukiendelezwa kwa Sheng.
Nchini Kenya ambapo asilimia 60% ya idadi ni vijana, Sheng imetokea kuwatambulisha vijana. Katika enzi hii ya Teknohama. wanaomiliki vyombo vya habari na sekta nyingine za biashara wamegundua kuwa matumizi ya Sheng ndiyo njia mwafaka zaidi ya kulifikia soko kubwa la vijana kwa ajili ya kueneza matangazo ya bidhaa na huduma za kibiashara. Kwa hivyo, Sheng imekuwa daraja la kuwafikia na kuwavutia vijana.
Hata hivyo, kwa upande mwingine matumizi ya Sheng yamelaumiwa na walimu wengi katika shule za msingi na zile za upili kuwa ni sababu mojawapo kuu ya kushuka kwa matokeo ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza miongoni mwa wanafunzi. Sheng imelaumiwa kwamba inasababisha wanafunzi kutozingatia mafunzo ya kanuni za sarufi na tahajia au maendelezo. Wataalam wanadai kuwa ni msimbo ambao hauzingatii sheria za sarufi na tahajia kwa sababu zisizofahamika, kwani ingawa muundo wake wa kisarufi hushahabiana na ule wa Kiswahili, Sheng hupuuza sarufi ya Kiswahili katika matumizi yake.
Ingawa sheng imekuwa ikipigwa vita, kuna wataalam ambao wana mtazamo kwamba juhudi hizo haziwezi kufanikiwa kwani Sheng ni chombo cha mawasiliano miongoni mwa vijana na kwa hivyo ina umuhimu wake ambao hauwezi kufumbiwa macho. Wanasema kuwa ni chombo ambacho kinafumbata hisia na mshikamano wa kizazi kipya kama ilivyojitokeza katika kauli mbiu ya mgombeaji urais mwaka wa 2012,'Tunawesmake.
Katika hali ambapo kiwango cha ubora wa matokeo ya Kiswahili yalidorora katika mtihani wa kidato cha nne (KCSE) mwaka wa 2012 na kuwa asilimia 35.81 pekee yakilinganishwa na asilimia 48.82 ya mwaka 2011, Sheng imekuwa ikilaumiwa kuwa ndicho chanzo cha kudorora kwa viwango vya ubora wa matokeo. Baadhi ya hao wataalamu wanasema kwamba Sheng haipaswi kuhujumiwa. kinachohitajika kufanywa ni kuwaelimisha vijana kuhusu mipaka ya matumizi yake.

Maswali
a) Taja mada ya kifungu hiki.
b) Fafanua nadharia mbili zilizoeleza asili ya lugha ya sheng.
c) Eleza matumizi bainifu ya kilugha cha Sheng katika jamii ya sasa.
d) Taja matokeo hasi ya matumizi ya Sheng katika jamii.
e) Ni kwa nini mwandishi Walibora ameshirikisha matumizi ya Sheng katika kazi yake ya Kidagaa Kimemwozea
f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu hiki.
i) Teknohama
ii) kudorora
iii) msimbo
iv) Kuhujumiwa

  

Answers


sharon
a) Lugha ya sheng / sheng katika jamii / matumizi ya sheng / athari ya sheng katika elimu
b) i) Kilugha cha sheng kiliibuka kutokana na wahuni na wakora jijini Nairobi ambao lengo lao lilikuwa kuwasiliana kwa siri.
ii) Kilugha cha Sheng kiiichipuka kutokana na vijana ambao walizua lugha ya kuwasiliana baada ya uhuru kwa sababu walikichukia Kiswahiii ambacho walikiona kama lugha ya uboi zozote
c)
i) Maongezi / mazungumzo / mawasiliano
ii) Katika maandishi ya vitabu
iii) Kutangaza mawasiliano katika vyombo vya habari
iv) Kueneza matangazo ya bidhaa na huduma za kibiashara ili kuliflkia soko kubwa la vijana
d) Matumizi ya Sheng yamelaumiwa na walimu kwa kushuka kwa matokeo ya lugha ya Kiswahiii na Kiingereza miongoni wa wanafunzi katika mitihani
- kutozingatia mafunzo ya kanuni za sarufi na
tahajia /' maendelezo
e) Ili kukipa kilugha cha Sheng nafasi kama
kitambulishi cha vijana
f)
i) Teknohama
Teknolojia ya habari na mawasiliano
ii) Kudorora
Kuenda chini, kurudi nyuma
iii) Msimbo
Lugha ya kupanga katika kundi la watu
iv) Kuhujumiwa Kuvurugwa, kuingiliwa
sharon kalunda answered the question on September 25, 2019 at 09:13


Next: The capital A/C of Mbele Kabisa Traders showed a balance of shs 50,000 as at 1st July 2004. For the year ended June 2005 the...
Previous: Koech started a business dealing in ladies clothing ten years ago. His business has gradually been growing and making more profits. Outline four reasons that...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions