Kidagaa kimemwozea ; Ken Walibora . .. alisimama jadidi na kuwatazama hawa watu wawili waliosimama wima na kutetemeka kama waliopigwa na dhoruba ya theluji."

      

Kidagaa kimemwozea ; Ken Walibora
. .. alisimama jadidi na kuwatazama hawa watu wawili waliosimama wima na kutetemeka kama waliopigwa na dhoruba ya theluji."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha hulka ya mrejelewa.
c) Huku ukitoa mifano mwafaka jadili mchango wa wanawake katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

  

Answers


sharon
a) Msemaji - mwandishi
Kuhusu - mtemi Nasibu Bora anayewatazama Amani na Bi Zuhura wakiwa chumbani mwake
Amani alikuwa ameitwa na Bi Zuhura kwenda kuangalia kilichokuwa mvunguni mwa kitanda ndipo Mtemi akawakuta
b) Sifa za mtemi (mreielewa)
i) Sherati
ii) Katili
iii) Laghai
iv) fisadi
v) Mwenye tamaa
vi) Mwenye mapuuza
vii) Mdanganyifu zozote 3x2= alama 6
c)- Ni walezi - Imani / Dora / Bi Zulwa
- Wasamehevu - Bi Zuhura / Imani
- Wavumilivu - Bi Zuhura / Imani / Dora
- Wakarimu - Bi Zuhura
- Wasema kweli - Dora
- Watetezi wa haki - Lowela / Imani /Bi Zuhura / Dora
- Wapenda anasa / wazinzi - Lowela
- Wavivu -Dora
- Matumaini - Imani
- Wanamapinduzi - Imani kushirikiana na Amani
sharon kalunda answered the question on September 25, 2019 at 12:42


Next: People hold money for various reasons. Identify the motive for holding money in each of the following cases (i)To meet hospital expenses.. (ii) To pay for...
Previous: The following relate to Ekerubo traders as at 30/09/2006. Stock 1 -10-05 7,500 Purchases 65,000 Sales 85,000 Return inwards 1,000 Mark-up 25 % General expenses 12,200 Required: Prepare a trading, profit and loss...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Andika kinyume. Sufuria iliyoinjikwa mekoni ni chafu.(Solved)

    Andika kinyume.
    Sufuria iliyoinjikwa mekoni ni chafu.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha aina za viwakilishi katika sentensi ifuatayo; Ule wangu niliopalilia unakua vizuri.(Solved)

    Bainisha aina za viwakilishi katika sentensi ifuatayo;
    Ule wangu niliopalilia unakua vizuri.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi kudhihirisha maana ya msemo ufuatao. enda benibeni.(Solved)

    Tunga sentensi kudhihirisha maana ya msemo ufuatao. enda benibeni.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Andika visawe vya maneno haya; i) Wajihi ii) Laazizi(Solved)

    Andika visawe vya maneno haya;
    i) Wajihi
    ii) Laazizi

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Sahihisha kwa kutumia kirejeshi cha mazoea. Kambarau ambao iliyoundwa vyema haitatizi.(Solved)

    Sahihisha kwa kutumia kirejeshi cha mazoea.
    Kambarau ambao iliyoundwa vyema haitatizi.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Tambua matumizi ya kiambishi -ji- katika sentensi ifuatayo. Jino la jitu hilo lililiwezesha kujilia chakula kingi kuliko mkimbiaji yule.(Solved)

    Tambua matumizi ya kiambishi -ji- katika sentensi ifuatayo.
    Jino la jitu hilo lililiwezesha kujilia chakula kingi kuliko mkimbiaji yule.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Andika upya sentensi ifuatayo ukianzia yambwa tendwa. Wakulima waliwakatia ngamia wote majani ya mti huo.(Solved)

    Andika upya sentensi ifuatayo ukianzia yambwa tendwa.
    Wakulima waliwakatia ngamia wote majani ya mti huo.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mistari, Wakazi waligawiwa vyandarua vya mbu lakini wanavitumai kujengea nyua.(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mistari,
    Wakazi waligawiwa vyandarua vya mbu lakini wanavitumia kujengea nyua.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha Ukiona vyaelea vimeundwa.(Solved)

    Kanusha
    Ukiona vyaelea vimeundwa.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Andika kifungu kifuatacho katika msemo wa taarifa; Amani alilia, "Marafiki zangu, majambazi wamenipiga na kunipora pesa zangu zote. Mali yangu sasa hali yangu nimbaya(Solved)

    Andika kifungu kifuatacho katika msemo wa taarifa;
    Amani alilia, "Marafiki zangu, majambazi wamenipiga na kunipora pesa zangu zote. Mali yangu sasa hali yangu nimbaya."

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi mbili tofauti kudhihirisha maana ya neno 'ilimradi'(Solved)

    Tunga sentensi mbili tofauti kudhihirisha maana ya neno 'ilimradi'

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha vielezi katika sentensi hii. Mwalimu wetu anayefundisha kistadi hutembea kwa maringo.(Solved)

    Ainisha vielezi katika sentensi hii.
    Mwalimu wetu anayefundisha kistadi hutembea kwa maringo.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja yenye viungo vya sarufi vifuatavyo;(Solved)

    Tunga sentensi moja yenye viungo vya sarufi vifuatavyo;
    i) Kikanushi
    ii) Kiima katika nafsi ya pili wingi.
    iii) Kiwakilishi cha wakati uliopita.
    iv) Mtendewa katika nafsi ya tatu wingi.
    v) Mzizi wa kitenzi cha silabi moja.
    vi) Mnyambuliko wa kitenzi kauli ya kutendea.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Taja sifa mbili bainifu za vokali /i/(Solved)

    Taja sifa mbili bainifu za vokali /i/

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya sauti.(Solved)

    Eleza maana ya sauti.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Ubinafsishaji wa mashirika ya umma ni nguzo kuu katika ulimwengu wa leo.(Solved)

    Soma kifungu kisha uiibu maswali
    Ubinafsishaji wa mashirika ya umma ni nguzo kuu katika ulimwengu wa leo. Kimsingi, ubinafsishaji ni hatua na harakati zinazochukuliwa kupunguza kushiriki kwa serikali katika uendeshaji wa mashirika na kuhimiza kupanuka kwa sekla ya kibinafsi.Serikali huweza kuhimiza, kutokana na uuzaji, uhawilishaji wa mali kutoka umiliki wa umma hadi kwenye umilikaji wa sekta ya kibinafsi. Aidha, serikali inaweza kuuza hisa zake kwenye mashirika ya umma. Njia nyingine ni kuchochea ugavi wa zabuni kupitia kwa mikataba ambayo inashindaniwa na mashirika au kampuni tofauti. Lengo kuu la ubinafsishaji ni kuigatuanafasi ya serikali katika utendakazi na uendeshaji wa mashirika.Uuzaji wamashirika ya kiserikali au hisa huwa chanzo cha mapato yanayoweza kutumiwa kuendesha miradi mingine, Hii ni njia ya kupunguza harija ya serikali inayotokana na uendeshaji wa mashirika yasiyoleta faida. Ubinafsishaji huzuia uwezekano wa kuingiliwa kwa mashirika na wanasiasa, huimarisha utamaduni mpya wa muundo wa mashirika na huvunja uhodhi wa kiserikali. Ubinafsishaji huweza kuatika mbegu za ujasiriamali wa raia kutamani kuanzisha amali tofauti.
    Ubinafsishaji huweza kuyaruhusu mashirika ya kimataifa kutwaa mashirika muhimu nchini, kufutwa kazi kwa wafanyikazi na kuongezeka kwa umaskini. Ubinafsishaji wa sekta zinazohusiana na elimu na afya huweza kuathiri vibaya wenye mapato ya chini.
    Ubinafsishaji haumaanishi ufanisi wa utendakazi wa makampuni na mashirika. Aidha, ikiwa haupo utaratibu mzuri wa kutathmini au kupima thamani za hisa pana uwezekano wa hisa zinazouzwa kupewa thamani ya juu au ya chini.
    Maswali
    a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi wa kifungu, andika muhtasari wa aya ya kwanza na ya pili. (Maneno 35 - 40).
    b) Dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya ya tatu na ya nne. (Maneno 45 - 50)

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Matumizi ya sheng' yameshamiri sana nchini Kenya hasa miongoni mwa vijana.(Solved)

    Soma taarifa inayofuata kisha uyajibu maswali
    Matumizi ya sheng' yameshamiri sana nchini Kenya hata miongoni mwa vijana. Ni kilugha ambacho kinakisiwa kuzuka katika miaka ya 60 na 70 katika makazi ya mashariki mwa jiji la Nairobi kama vile Kaloleni, Mbotela/ Bahati na kadhalika.Kwa sasa ni kilugha kilichoenea kwingi nchini Kenya na kuwa kitambulisho cha takriban vijana wengi. Wataalam mbalimbali wanabainisha nadharia mbalimbali kuhusu chanzo cha lugha hii. Kuna nadharia mbili kuu kuhusu asili ya lugha ya Sheng: kwamba kilugha hiki kiliibuka kutokana na wahuni na wakora jijini Nairobi ambao lengo lao Iilikuwa kuwasiliana kwa siri. Nadharia nyingine ni kuwa kilichipuka kutokana na vijana ambao walizua lugha ya kuwasiliana baada ya uhuru (kwa sababu walikichukia Kiswahili ambacho walikiona kama lugha ya uboi)
    Dhana hizi kwa muda mrefu, zimeathiri mitazamo kuhusiana na kilugha hiki. Kwa sasa ni kilugha ambacho ,yjiasambaa katika sehemu mbalimbali za Kenya na watu wa matabaka mbalimbali wanakitumia. Kilugha hiki kimeanza kuashiria uhalisia mkubwa wa maisha ya kisasa, zaidi katika jamii ya Wakenya. Aidha, sheng imejitanzua kutoka hali ya kuwa kilugha cha maongezi pekee na sasa kinatumiwa katika baadhi ya vitabu, hata waandishi wa vitabu wameanza kukitumia. Kwa mfano, katika miaka ya 80, David Mailu katika kitabu chake 'Without Kiinua Mgongo' alitumia Sheng. Katika siku za hivi karibuni, riwaya ya 'Kidagaa Kimemwozea' iliyoandikwa na Ken Walibora kilugha cha sheng kimepewa nafasi kama kitambulisho cha vijana kupitia kwa mhusika DJ Bob.
    Vilevile kumezuka vyombo vya habari kama redio, mfano idhaa ya Ghetto, redio ambayo inaendeleza mawasiliano kwa matumizi ya Sheng. Kuna vipindi vya matangazo ya kibiashara katika runinga ambayo yanaendelezwa kwa Sheng. Kwa mfano, katika 'gazeti la Taifa Leo, kuna ukumbi wa 'Mchongoano' ambao umekuwa ukiendelezwa kwa Sheng.
    Nchini Kenya ambapo asilimia 60% ya idadi ni vijana, Sheng imetokea kuwatambulisha vijana. Katika enzi hii ya Teknohama. wanaomiliki vyombo vya habari na sekta nyingine za biashara wamegundua kuwa matumizi ya Sheng ndiyo njia mwafaka zaidi ya kulifikia soko kubwa la vijana kwa ajili ya kueneza matangazo ya bidhaa na huduma za kibiashara. Kwa hivyo, Sheng imekuwa daraja la kuwafikia na kuwavutia vijana.
    Hata hivyo, kwa upande mwingine matumizi ya Sheng yamelaumiwa na walimu wengi katika shule za msingi na zile za upili kuwa ni sababu mojawapo kuu ya kushuka kwa matokeo ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza miongoni mwa wanafunzi. Sheng imelaumiwa kwamba inasababisha wanafunzi kutozingatia mafunzo ya kanuni za sarufi na tahajia au maendelezo. Wataalam wanadai kuwa ni msimbo ambao hauzingatii sheria za sarufi na tahajia kwa sababu zisizofahamika, kwani ingawa muundo wake wa kisarufi hushahabiana na ule wa Kiswahili, Sheng hupuuza sarufi ya Kiswahili katika matumizi yake.
    Ingawa sheng imekuwa ikipigwa vita, kuna wataalam ambao wana mtazamo kwamba juhudi hizo haziwezi kufanikiwa kwani Sheng ni chombo cha mawasiliano miongoni mwa vijana na kwa hivyo ina umuhimu wake ambao hauwezi kufumbiwa macho. Wanasema kuwa ni chombo ambacho kinafumbata hisia na mshikamano wa kizazi kipya kama ilivyojitokeza katika kauli mbiu ya mgombeaji urais mwaka wa 2012,'Tunawesmake.
    Katika hali ambapo kiwango cha ubora wa matokeo ya Kiswahili yalidorora katika mtihani wa kidato cha nne (KCSE) mwaka wa 2012 na kuwa asilimia 35.81 pekee yakilinganishwa na asilimia 48.82 ya mwaka 2011, Sheng imekuwa ikilaumiwa kuwa ndicho chanzo cha kudorora kwa viwango vya ubora wa matokeo. Baadhi ya hao wataalamu wanasema kwamba Sheng haipaswi kuhujumiwa. kinachohitajika kufanywa ni kuwaelimisha vijana kuhusu mipaka ya matumizi yake.

    Maswali
    a) Taja mada ya kifungu hiki.
    b) Fafanua nadharia mbili zilizoeleza asili ya lugha ya sheng.
    c) Eleza matumizi bainifu ya kilugha cha Sheng katika jamii ya sasa.
    d) Taja matokeo hasi ya matumizi ya Sheng katika jamii.
    e) Ni kwa nini mwandishi Walibora ameshirikisha matumizi ya Sheng katika kazi yake ya Kidagaa Kimemwozea
    f) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu hiki.
    i) Teknohama
    ii) kudorora
    iii) msimbo
    iv) Kuhujumiwa

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Uozo katika jamii ni maudhui yaliyoshughulikiwa pakubwa katika diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi nyingine. Kwa kurejelea hadithi zozote tano fafanua kauli hii.(Solved)

    Uozo katika jamii ni maudhui yaliyoshughulikiwa pakubwa katika diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi nyingine. Kwa kurejelea hadithi zozote tano fafanua kauli hii.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • "Ingawa walifahamu sababu ya kuitwa pale mpango uliokuwepo ulikuwa usiku wa giza."(Solved)

    Damu Nyeusi na Hadithi nyingine : Ken Walibora na Said A. Mohamed
    "Ingawa walifahamu sababu ya kuitwa pale mpango uliokuwepo ulikuwa usiku wa giza."
    (a) Fafanua muktadha wa maneno haya.
    (b) Eleza tamathali iliyotumika katika dondoo hili.
    (c) Onyesha vile wahusika mbalimbali hadithini waiivyoathiriwa na sababu ya kuitwa pale.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • "Ndoto za uhuru barani Afrika imegeuka kuwa jinamizi, jinamizi inayowafanya wazalendo kulia Kidagaa kimetuozea". Ukirejelea riwaya ya kidagaa kimemwozea eleza sababu za wazalendo kulia Kidagaa...(Solved)

    "Ndoto za uhuru barani Afrika imegeuka kuwa jinamizi, jinamizi inayowafanya wazalendo kulia Kidagaa kimetuozea". Ukirejelea riwaya ya kidagaa kimemwozea eleza sababu za wazalendo kulia Kidagaa kimetuozea.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)