Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambalo una kwamiza juhudi za maendeleo.

      

Soma nakala yafuatayo kishaujibu maswali
Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambalo una kwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoukabili mataifa yanayoendelea. Unayatosa kwenye dhiki kubwa huku mataifa ya kimagharibi yakipiga hatua kubwa kimaendeleo. Ufa uliopo baina ya mataifa yanayoendelea na yaloyaliyoendelea kama vile Marekani, nchi za Ulaya na Ujapani unapanuka kila uchao.
Vyanzo vya umaskini huu ni anuwai ; mathalan, ufisadi, uongozi mbaya, turathi za kikoloni, uchumi kuegemea mvua isiyotabirika,idadi ya watu inayoupiku uwezo wa uchumi wa taifa linalo husika na ukosefu wa nyenzo na amali za kuwakwamua raia kutoka lindi la umaskini. Ukosefu na adimu za ajira huchangia pia katika tatizo hili.
Jamii ya xxxxxxx mpaswa kuelewa kuwa umaskini unaoathiri nchi fulani unaathari pana sana.Uvunigu unaotokana na umaskini unaweza kuwa msingi ambako matendo ya kihalifu ili kujinasua kutoka dhiki ile. Hii inaweza kuwa mbegu ya kuatika maovu kama ugaidi na uhalifu wa kila aina.
Mataifa ya magharibi yanapaswa kuyaburai madeni mataifa yanayoendelea kama njia mojawapo ya kupambana na umaskini. Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. Katika hali hii inakuwamuhali kwa mataifa hayo kujikwamua kutokana na pingu za umaskini. Njia nyingine ni kustahabu kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi zinazoendelea.
Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanapaswa kuibuka na mikakati bora yakupambana na umaskini. Ni muhimu pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini. Pana dharura ya kuzalisha nafasi za ajira, kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tegemeo kuu la mataifa mengi, kuendeleza elimu na kuimarisha miundo msingi. Ipo haja pia ya mataifa haya kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huru unaotawala ulimwengu sasa hauishii kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza umasikini zaidi. Kwa ufupi, maamuzi yote ya sera za kiuchumi lazima ya zingatie uhalisi wa maisha ya raia wa mataifa hayo.

a) Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea?
b) Madeni yana athari gani kwa mataifa yanayoendelea?
c) Ni mapendekezo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu utatuzi wa tatizo la umaskini?
d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa machanga?
e) Ukirejea kifungu, eleza maana ya:
i) Kulitadarukia
ii) Kuatika
iii) Kuyaburai madeni

  

Answers


sharon
(a)
- Ufisadi
- Uongozi mbaya
- Turatbi za kikoloni
- Uchumi unauegamizwa kwenye kilimo
- Idadi ya watu inayopiku uwezo wa uchumi
- Okosefu wa amani kukwamua raia kuto lindi la umaskini
- Ukosefu wa elimu na nafasi za ajira
- Madeni za kigeni
(b) Kudidimiza maendeieo
Umaskini - kuzidisha
Husababisha uhalifu
(c) 1) Kuwa na sera bora zinazotambua raia wengi wa mataifa hayo ni Maskini
2) Kizalilisha nafasi za ajira (kazi)
3) Kupanua viwaada hasa vinavyohisiana na kilimo
4) Kuendeleza elimu
5) Kuimarisha miuondo msingi
6) Kuchunga mfumo wa soko huru kuwa viwanda asiliha kuzidisha Umaskini
(d) Kuua viwanda asilia
Kuendeleza umaskmi
(e) i) Kulikabili nalo, kulitatua, kulishughulikia, kulitanzua kupambana, Nalo, kuiingazia, komesha
ii) Kuzua, kupanda, kukuza, kuanzisha, kuotesha
iii) Kuondolea, kusaheha, kuyafeleli
sharon kalunda answered the question on September 25, 2019 at 13:57


Next: Highlight four reasons why a country would like to know the structure of it’s population.
Previous: Identify four circumstances under which communication may be ineffective .

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions