Kiswahili ni lugha ambayo inakua na kuenea kila uchao. Imeenea kwa kasi hivi kwamba waliokuwa wameitweza wamelazimika kujifunza, kuizungumza na hata kuitumia katika maandishiLugha hii...

      

Soma taarifa ifuatavo kisha uiibu maswali
Kiswahili ni lugha ambayo inakua na kuenea kila uchao. Imeenea kwa kasi hivi kwamba waliokuwa wameitweza wamelazimika kujifunza, kuizungumza na hata kuitumia katika maandishiLugha hii imetambuliwa kama mojawapo ya lugha za mawasiliano katika muungano wa Afrika. Magwiji wa Kiswahili wamechaguliwa kuunda msamiati mwafaka kutegemea mabadiliko ulimwenguni na kuingiza katika matumizi kupitia tarakilishi.
Mpango huu utakapo faulu, mtu ataweza kutumia tarakilishi akiwasiliana kwa Kiswahili. Juhudi hizi heri zizidi kupongezwa na nyingine kuimarishwa Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili barani ni mojawapo wa hatua za kufanikisha juhudi hizi. Taasisi kama hiyo itatafiti historia ya lugha, mabadiliko yake na maenezi, msamiati wake na kuleta usawa wa mazungumzo kwa Kiswahili miongoni mwa mambo mengine.Kuweka lugha hii katika maandishi ni jambo litakalochangia kuimarisha lugha ya Kiswahili. Vitabu ,magazeti, na majarida yatakayolenga kiwango cha wasomaji yaandikwe na bei yake isiwe ghali mno ili wengi waweze kugharamia. Tanzu zote za lugha zizingatiwe.Lugha hii ifunzwe na kutahiniwa katika daraja zote za elimu. Lifanyapo hili, bila shaka lugha ya Kiswahili itaimarika.Uajiri wa wafanyikazi ukitambua ujuzi katika lugha hii hadhi yake itaimarika.Tafsiri ya kazi zilizoandikwa katika lugha mbalimbali zikifanywa katika Kiswahili, lugha hii itakua na kukitamizizi kwingi ulimwenguni.Watu wengi watapata hamu ya kusoma kazi asilia na ile ya tafsiri yake.Redio na magazeti ni vyombo muhimu katika kuwasiliana na kundi kubwa la watu kote duniani. Vyombo hivi vya mawasiliano kwa umma vikihimiza matumizi ya Kiswahili, bila shaka mchango mkubwa utaonekana katika kustawisha lugha hii. Vipindi maalumu matangazo na burudani vizingatie matumizi ya Kiswahili.Mashindano kati ya shule na shule,nchi na nchi ya kianzishwa na kuzingatiwa yanaweza kuimarisha Kiswahili pakubwa. Mashairi, mijadala, matokeo ya utafiti fulani, nyimbo, ngano na hadithi za kufunza umma ni njia za kuwezesha kufanyiwa mashindano kama hayo.Mikakati hii na mingine ikizingatiwa itakuwa mbolea nzuri ya kukuza lugha ya Kiswahili.

Maswali
i) Bila kubadilisha maana iliyokusudiwa ,fupisha aya mbili za mwanzo. (maneno 35 - 40)
ii) Andika kwa muhtasari juhudi zinazofaa katika uimarishaji wa lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa Makala haya. (maneno 70 -80)

  

Answers


sharon
(a)
- Kiswahiii kimekua na kuenea kwa kasi cha kulazimisha walioitweza kujifunza, kuzungumza na kuandikia.
- Kiswahiii kimetambuiiwa kama lugha ya mawasiliano katika muungano wa Afrska.
- Magwiji wa Kiswahiii wamechaguliwa kuandaa msamiati mwafaka kutegemea mabadiliko ulimwenguni na kuingiza katika matumizi kupitia tarakiiishi. (Tuza moja ya utiririko kama zimetiririshwa kwa aya moja)
(b) Juhudi za kuimansha lugha ya Kiswahiii
- Magwijij ………….. changuliwa kuandaa msamiati mwafaka kutegemea mabadiliko uJirawenguni.
- Kuingiza msamiati katika matumizi kupitia tarakiiishi -Kubuniwa kwa taasisi ya uchunguzi wa Kiswahiii batani -Kuweka lugba hii katika maandishi.
- Tafsiri ya kazi zilizoandikwa katika lugba mbalimbali katika kiswahiii ill kukuza lugha hii.ote za elimu.
- Lugha hii ifunzwe na kutahiniwa katika daraja
- Vyombo vya habari vikitumia kiswahiii bila shaka lugha hii itastawishwa.
- Mashindano ya lugha kati ya shule na shule au nchi na nchi yakianzishwa yataimarisha kiswahiii pakubwa.
- Uajiri wa wafanyikazi kwa kutambua ujuzi katika lugha hii hadhi yake itaimarika.
sharon kalunda answered the question on September 25, 2019 at 14:07


Next: The following diagram shows demands and supply carve of commodity. State four things that will happen if the supply of the commodity is increased while demand...
Previous: Ukweli enterprises has a working capital of sh.200,000 and a current ratio of 3:1.Calculate (i)Current assets (ii)Current liabilities

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions