Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

UFAHAMU Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali :- Utandawazi Kufikia miongo michache iliyopita, ujumbe ulisafirishwa kwa njia zilizochukua muda mrefu sana kufika. Kwa mfano, mtu alipotaka kupiga...

      

UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali :-

Utandawazi
Kufikia miongo michache iliyopita, ujumbe ulisafirishwa kwa njia zilizochukua muda mrefu sana kufika. Kwa mfano, mtu alipotaka kupiga simu katika nchi jirani barani Afrika, ilimbidi kupitia kwa
opareta katika nchi za Ulaya ndipo aunganishwe. Kupigia simu kutoka Gambia kwenda Senegali
ilibidi kutumia opareta wa Kule London na wa Paris, Ufaransa, na wa Senegal.

Leo hii kuna njia nyingi za mawasiliano zilizo bora, za kutegemewa na zinazofikisha ujumbe kwa
kasi sana. Ujumbe ambao ungechukua muda mrefu kuufikisha, sasa unapelekwa kwa sekunde moja.
Miongoni mwa njia hizi ni mdahilishi, simu tamba na tuama, faksi, setelaiti, mitandao ya wavuti, n.k.
Hamna eneo sasa hivi hata liwe mbali vipi lisilofikika na aina hizi za mawasiliano.

Maendeleo haya ya mawasiliano yamechangia pakubwa sana kuufanya ulimwengu kuwa kijiji
kimoja. Sasa kuna uhusiano wa karibu sana miongoni mwa mataifa duniani katika Nyanja zote za
maisha. Hall hii ndiyo inayoitwa utandawazi au utandaridhi. Utandawazi umeleta mabadiliko mengi
maishani.

Mojawapo ni utoaji na uzalishaji wa mali. Mabadiliko ya mawasiliano yameruhusu mashirika ya
kimataifa kusambaza utoaji na uzalishaji wa bidhaa zao katika maeneo mbalimbali duniani. Hali hii
imepunguza gharama za usafirishaji sana. Bidhaa zinazoundwa na kiwanda chenye hakimiliki
kilichoko kule New York masafa ya mbali, zinaweza kuzalishwa na kiwanda kilicho hapa Nairobi.
Bila shaka umesikia kuhusu madawa ya kurefusha maisha ya wahasiriwa wa UKIMWI ambayo
yanazalishwa na baadhi ya viwanda vya kutengeneza madawa humu nchini. Kiwanda chenye
hakimiliki kipo jijini London.

Viwanda ambavyo vilikuwa katika mataifa tajiri kama vile Uingereza, Ufaransa, Marekani, Ujerumani na Japani sasa vimeweza kutandaza vitandabui vyake kote duniani. Utandazaji huu
hufanywa kwa njia kadhaa. Kwanza, viwanda hivi huvinunua viwanda vilivyoko katika mataifa
yanayostawi. Vinaweza kuingia katika ubia na viwanda vya mataifa wanakotaka kuhamia.
Viwanda hivi vya mataifa yanayoendelea hupatana kuwa watasimamia utoaji na uzalishaji wa bidhaa
fulani na kukubaliana namna ya kugawa mapato.

Utandawazi katika sekta ya uzalishaji na utoaji bidhaa umeleta manufaa kadhaa katika nchi zinazoendelea. Mojawapo ya haya ni kupatikana kwa nafasi za kazi. Pili, bidhaa za nchi zinazoendelea ambazo hazingeshindana na zile za mataifa yalioendelea sasa zimepata nafasi ya kushindana. Halikadhalika, wateja wana nafasi ya kupata bidhaa watakayo bila kuvunjwa moyo.

Iwapo bidhaa anazohitaji mteja hazipatikani katika nchi, zinaweza kuagizwa moja kwa moja kutoka
kwa kiwanda kingine chenye uhusiano nacho. Uagizaji hauchukui muda kutokana na hali ya
mawasiliano inayoweza kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza wakati. Fauka ya haya,
wateja hupata uwanja mpana wa kuchagua wanachokihitaji.

Utandawazi umehimiza kustawi kwa mazingira ya mashindano katika utoaji na uzalishaji mali
viwandani. Sasa hivi hakuna nchi yenye uwezo Wa kufungia bidhaa za nchi nyingine katika mipaka
yake. Kufanya hivi ni kujitia kitanzi kiuchumi. Lazima nchi zifüngue masoko yao. Navyo viwanda
vya kimataifa huweza kuwania masoko haya. Matokeo yake ni wateja kufaidika kwa kupata uwanja
mpana wa bidhaa za kuchagua. Wateja pia hupata bidhaa za hali ya juu na kwa bei isiyo ghali
kutokana na mashindano haya. Mashindano ya kimataifa ni kama ya paka na panya na kiwanda
kisichojifunga nira vizuri, huwa kinajihatarisha. Kinaweza kujipata kimetupwa nje ya soko na
kuangamia.Manufaa mengine ya utandawazi ni kuwa watu sasa hivi wanaweza kuwasiliana kwa
urahisi na wepesi. Kwa kutumia simu, au mdahilishi, mtu anaweza kuwasiliana na mwenzake popote
alipo licha ya masafa. Zaidi ya haya, utandawazi umewawezesha watu kutoka asili mbalimbali
kuingiliana na kutangamana. Utangamano huu umeweza kuleta umoja baina ya watu kwa kutoa hisia za ubaguzi.

Hata hivyo utandawazi umetokeza kuwa na madhara. Kwanza, uchumi wa nchi nyingi umeibukia
kutawaliwa na matukio ambayo hayazihusu nchi hizo moja kwa moja. Uvamizi wa kijambazi wa
Septemba 11,2000 kule Marekani uliathiri uchumi wa nchi nyingi sana. Matukio ya vita katika
Mashariki ya kati nayo yamechangia kuzorotesha uchumi wa nchi nyingi hasa zile maskini ambzo zinategemea mafuta kutoka huko ilhali vita hivyo haviwahusu sikio wala ndewe.

Athari kubwa ya utandawazi yaonekana katika sekta ya kijamii. Tamaduni nyingi za jamii katika nchi maskini zinaendelea kuvurugwa na maadili kuporomoka kutokana na ustawi wa kimawasiliano.
Vijana wanaiga kutoka mataifa ya kimagharibi bila kuchuja. Si ajabu kuwa vijana wetu wanavaa
mavazi yasiyositiri uchi wao vizuri na yasiyostahiki kwa jina la ustaarabu. Wavulana nao huzidisha
kwa kutoga masikio na kusuka nywele usiweze kuwatofautisha na dada zao.

Maswali
(a) Utandawazi ni nini?
(b) Ni mambo yapi yanayosababisha kutokea kwa utandawazi?
(c) Mashirika ya mataifa yaliyostawi yanatumia mikakati ipi kutandaza vitandabui vyao kote
duniani?
(d) Fafanua:
(i) Manufaa matatu ya utandawazi.
(ii) Hasara tatu za utandawazi.
(e) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa.
(i) Ubia
(ii) Mashindano ya paka na panya.
(iii) Kutoga
(iv) Vitandabui

  

Answers


Kavungya
[a] Ni hali ambapo mataifa ya dunia yameweza kuwa na uhusiano wa karibu katika nyanja zote za maisha kupitia kwa maendeleo ya teknolojia, hasa ya habari.
[b] uvumbuzi wa njia nzuri za mawasiliano zinazowezesha warn kuwasiliana kwa wepesi pamoja na
haja ya warn duniani kuingiliana kwa shughuli mbaiimbali kama vile biashara, utalii, utafiti, elimu.
[c] [i] Kununua viwanda katika nehi zinazoendelea.
[ii] Kuingia katika ubia na viwanda katika nehi zinazoendelea na kuweka micataba wa kugawana usimamizi wa mapato.
[iii] Kuhamia katika mataifa yanayoendelea
d [ij Kupunguza gharama ya usafirishaji kwa wazalishaji kufanyia uzalishaji wa bidhaa karibu na soko.
[ii] Kuzalisha nafasi za kazi
[iiiJ Wateja wana nafàsi ya kupata bidhaa waitakayo.
[iv] Umehimiza kustawi kwa mazingira na mashindano katika utoaji na uzalishaji wa mali. Hili huhakikisha kuwa wanaoshindana wanatoa bidhaa za hali yajuu.
[ii] 1 .Chumi za nehi zinatawaliwa na matukio ya dunia ambayo nehi hizo hazina uhusiano.
2.Athari za kiutamaduni ambapo maadilikatika nehi maskini yanavurugwa. Vijana wan ehi hizi wan aiga upotovu wa mataifa yanayoendelea.
3. Kuangamia kwa viwanda asilia vya mataifa maskini.
[e][i] Ushirikiano katikajambo kwa madhumuni ya kuleta faida.
[iii Kufànya kwa kuviziana
[iii] Tuweze-kudhibiti uzalishaji-mali
Kavungya answered the question on September 28, 2019 at 08:17


Next: The compulsory set text: The River and The Source: By Margaret Ogola. Using atleast three characters in the novel, write an essay to show how the...
Previous: Muhtasari Sikukuu ya wafanyikazi huadhimishwa na wafanyikazi kote ulimwenguni kwa minajili ya kukumbushana na kutanabahishana umuhimu wa mshikamano na umoja katika kudai na kutetea maslahi na...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Tunga sentensi yenye kiingizi na kihusishi cha mahali.(Solved)

    Tunga sentensi yenye kiingizi na kihusishi cha mahali.

    Date posted: September 26, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi hii Nikimwona mwalimu wangu nitamjulisha habari hizo.(Solved)

    Kanusha sentensi hii
    Nikimwona mwalimu wangu nitamjulisha habari hizo.

    Date posted: September 26, 2019.  Answers (1)

  • Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano. i) twaa (kutendeka) ii) Kosa (Kutendesha) iii) Cha (Kutendwa)(Solved)

    Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano.
    i) twaa (kutendeka)
    ii) Kosa (Kutendesha)
    iii) Cha (Kutendwa)

    Date posted: September 26, 2019.  Answers (1)

  • Maneno haya yamo katika ngeli gani? i) Fagio ii) Nyigu(Solved)

    Maneno haya yamo katika ngeli gani?
    i) Fagio
    ii) Nyigu

    Date posted: September 26, 2019.  Answers (1)

  • Ngeli ni nini?(Solved)

    Ngeli ni nini?

    Date posted: September 26, 2019.  Answers (1)

  • Kiswahili ni lugha ambayo inakua na kuenea kila uchao. Imeenea kwa kasi hivi kwamba waliokuwa wameitweza wamelazimika kujifunza, kuizungumza na hata kuitumia katika maandishiLugha hii...(Solved)

    Soma taarifa ifuatavo kisha uiibu maswali
    Kiswahili ni lugha ambayo inakua na kuenea kila uchao. Imeenea kwa kasi hivi kwamba waliokuwa wameitweza wamelazimika kujifunza, kuizungumza na hata kuitumia katika maandishiLugha hii imetambuliwa kama mojawapo ya lugha za mawasiliano katika muungano wa Afrika. Magwiji wa Kiswahili wamechaguliwa kuunda msamiati mwafaka kutegemea mabadiliko ulimwenguni na kuingiza katika matumizi kupitia tarakilishi.
    Mpango huu utakapo faulu, mtu ataweza kutumia tarakilishi akiwasiliana kwa Kiswahili. Juhudi hizi heri zizidi kupongezwa na nyingine kuimarishwa Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili barani ni mojawapo wa hatua za kufanikisha juhudi hizi. Taasisi kama hiyo itatafiti historia ya lugha, mabadiliko yake na maenezi, msamiati wake na kuleta usawa wa mazungumzo kwa Kiswahili miongoni mwa mambo mengine.Kuweka lugha hii katika maandishi ni jambo litakalochangia kuimarisha lugha ya Kiswahili. Vitabu ,magazeti, na majarida yatakayolenga kiwango cha wasomaji yaandikwe na bei yake isiwe ghali mno ili wengi waweze kugharamia. Tanzu zote za lugha zizingatiwe.Lugha hii ifunzwe na kutahiniwa katika daraja zote za elimu. Lifanyapo hili, bila shaka lugha ya Kiswahili itaimarika.Uajiri wa wafanyikazi ukitambua ujuzi katika lugha hii hadhi yake itaimarika.Tafsiri ya kazi zilizoandikwa katika lugha mbalimbali zikifanywa katika Kiswahili, lugha hii itakua na kukitamizizi kwingi ulimwenguni.Watu wengi watapata hamu ya kusoma kazi asilia na ile ya tafsiri yake.Redio na magazeti ni vyombo muhimu katika kuwasiliana na kundi kubwa la watu kote duniani. Vyombo hivi vya mawasiliano kwa umma vikihimiza matumizi ya Kiswahili, bila shaka mchango mkubwa utaonekana katika kustawisha lugha hii. Vipindi maalumu matangazo na burudani vizingatie matumizi ya Kiswahili.Mashindano kati ya shule na shule,nchi na nchi ya kianzishwa na kuzingatiwa yanaweza kuimarisha Kiswahili pakubwa. Mashairi, mijadala, matokeo ya utafiti fulani, nyimbo, ngano na hadithi za kufunza umma ni njia za kuwezesha kufanyiwa mashindano kama hayo.Mikakati hii na mingine ikizingatiwa itakuwa mbolea nzuri ya kukuza lugha ya Kiswahili.

    Maswali
    i) Bila kubadilisha maana iliyokusudiwa ,fupisha aya mbili za mwanzo. (maneno 35 - 40)
    ii) Andika kwa muhtasari juhudi zinazofaa katika uimarishaji wa lugha ya Kiswahili kwa mujibu wa Makala haya. (maneno 70 -80)

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambalo una kwamiza juhudi za maendeleo.(Solved)

    Soma nakala yafuatayo kishaujibu maswali
    Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambalo una kwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoukabili mataifa yanayoendelea. Unayatosa kwenye dhiki kubwa huku mataifa ya kimagharibi yakipiga hatua kubwa kimaendeleo. Ufa uliopo baina ya mataifa yanayoendelea na yaloyaliyoendelea kama vile Marekani, nchi za Ulaya na Ujapani unapanuka kila uchao.
    Vyanzo vya umaskini huu ni anuwai ; mathalan, ufisadi, uongozi mbaya, turathi za kikoloni, uchumi kuegemea mvua isiyotabirika,idadi ya watu inayoupiku uwezo wa uchumi wa taifa linalo husika na ukosefu wa nyenzo na amali za kuwakwamua raia kutoka lindi la umaskini. Ukosefu na adimu za ajira huchangia pia katika tatizo hili.
    Jamii ya xxxxxxx mpaswa kuelewa kuwa umaskini unaoathiri nchi fulani unaathari pana sana.Uvunigu unaotokana na umaskini unaweza kuwa msingi ambako matendo ya kihalifu ili kujinasua kutoka dhiki ile. Hii inaweza kuwa mbegu ya kuatika maovu kama ugaidi na uhalifu wa kila aina.
    Mataifa ya magharibi yanapaswa kuyaburai madeni mataifa yanayoendelea kama njia mojawapo ya kupambana na umaskini. Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. Katika hali hii inakuwamuhali kwa mataifa hayo kujikwamua kutokana na pingu za umaskini. Njia nyingine ni kustahabu kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi zinazoendelea.
    Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanapaswa kuibuka na mikakati bora yakupambana na umaskini. Ni muhimu pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini. Pana dharura ya kuzalisha nafasi za ajira, kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tegemeo kuu la mataifa mengi, kuendeleza elimu na kuimarisha miundo msingi. Ipo haja pia ya mataifa haya kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huru unaotawala ulimwengu sasa hauishii kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza umasikini zaidi. Kwa ufupi, maamuzi yote ya sera za kiuchumi lazima ya zingatie uhalisi wa maisha ya raia wa mataifa hayo.

    a) Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea?
    b) Madeni yana athari gani kwa mataifa yanayoendelea?
    c) Ni mapendekezo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu utatuzi wa tatizo la umaskini?
    d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa machanga?
    e) Ukirejea kifungu, eleza maana ya:
    i) Kulitadarukia
    ii) Kuatika
    iii) Kuyaburai madeni

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • "Asanteni sana kwa kuja, sisi. . . hukabiliana na mengi."(Solved)

    Damu Nyeusi na Hadithi nyingine : Ken Walibora na Said A. Mohamed
    "Asanteni sana kwa kuja, sisi. . . hukabiliana na mengi."
    i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    ii) Fafanua matukio yaliyosababisha mkutano huu. (alama 4)
    iii) Jadili changamoto sita zinazokumba jinsia ya kike katika hadithi hii.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Matatizo yanayowakumba wanacheneo ni kielelzo cha matatizo yanayowakumba wananchi wa mataifa mengi ya ulimwengu wa tatu. Thibitisha ukerejelea "Mstahiki Meya".(Solved)

    Matatizo yanayowakumba wanacheneo ni kielelzo cha matatizo yanayowakumba wananchi wa mataifa mengi ya ulimwengu wa tatu. Thibitisha ukerejelea "Mstahiki Meya".

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Mstahiki Meva : Timothy M. Arege "Nilikusahau lini. . , ? Mtu haukati mkono unaomlisha.(Solved)

    Mstahiki Meva : Timothy M. Arege
    "Nilikusahau lini. . , ? Mtu haukati mkono unaomlisha.
    a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
    b) Taja na ueleze mbinu ya kifasihi iliyotumika katika dondoo hili.
    c) Eleza sifa nne za msemewa.
    d) Kwa kutoa mifano mitano thibithisha jinsi viongozi wa cheneo walivyoukata mkono uliokuwa ukiwalisha.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Huku ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea thibitisha kwamba vijana wana suluhu tosha kwa matatizo yanayoikumba jamii wanamoishi.(Solved)

    Huku ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea thibitisha kwamba vijana wana suluhu tosha kwa matatizo yanayoikumba jamii wanamoishi.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Kidagaa kimemwozea ; Ken Walibora . .. alisimama jadidi na kuwatazama hawa watu wawili waliosimama wima na kutetemeka kama waliopigwa na dhoruba ya theluji."(Solved)

    Kidagaa kimemwozea ; Ken Walibora
    . .. alisimama jadidi na kuwatazama hawa watu wawili waliosimama wima na kutetemeka kama waliopigwa na dhoruba ya theluji."
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Bainisha hulka ya mrejelewa.
    c) Huku ukitoa mifano mwafaka jadili mchango wa wanawake katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume. Sufuria iliyoinjikwa mekoni ni chafu.(Solved)

    Andika kinyume.
    Sufuria iliyoinjikwa mekoni ni chafu.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha aina za viwakilishi katika sentensi ifuatayo; Ule wangu niliopalilia unakua vizuri.(Solved)

    Bainisha aina za viwakilishi katika sentensi ifuatayo;
    Ule wangu niliopalilia unakua vizuri.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi kudhihirisha maana ya msemo ufuatao. enda benibeni.(Solved)

    Tunga sentensi kudhihirisha maana ya msemo ufuatao. enda benibeni.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Andika visawe vya maneno haya; i) Wajihi ii) Laazizi(Solved)

    Andika visawe vya maneno haya;
    i) Wajihi
    ii) Laazizi

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Sahihisha kwa kutumia kirejeshi cha mazoea. Kambarau ambao iliyoundwa vyema haitatizi.(Solved)

    Sahihisha kwa kutumia kirejeshi cha mazoea.
    Kambarau ambao iliyoundwa vyema haitatizi.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Tambua matumizi ya kiambishi -ji- katika sentensi ifuatayo. Jino la jitu hilo lililiwezesha kujilia chakula kingi kuliko mkimbiaji yule.(Solved)

    Tambua matumizi ya kiambishi -ji- katika sentensi ifuatayo.
    Jino la jitu hilo lililiwezesha kujilia chakula kingi kuliko mkimbiaji yule.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Andika upya sentensi ifuatayo ukianzia yambwa tendwa. Wakulima waliwakatia ngamia wote majani ya mti huo.(Solved)

    Andika upya sentensi ifuatayo ukianzia yambwa tendwa.
    Wakulima waliwakatia ngamia wote majani ya mti huo.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mistari, Wakazi waligawiwa vyandarua vya mbu lakini wanavitumai kujengea nyua.(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mistari,
    Wakazi waligawiwa vyandarua vya mbu lakini wanavitumia kujengea nyua.

    Date posted: September 25, 2019.  Answers (1)