Po - wakati
Ki - Kitendo kilikuwa kikiendelea wakati kingine kilitendeka.
Kwa - jinsi au namna
Kavungya answered the question on September 28, 2019 at 08:56
- Andika katika hali ya udogo:
Mvulana yule alibeba kiti kikubwa (Solved)
Andika katika hali ya udogo:
Mvulana yule alibeba kiti kikubwa
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Taja sauti zinazotamkiwa kwenye ufizi.(Solved)
Taja sauti zinazotamkiwa kwenye ufizi.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Onyesha vishazi tegemezi na vishazi huru katika sentensi ifuatayo.
Nilimwona Agwambo nilipofika Mombasa
(Solved)
Onyesha vishazi tegemezi na vishazi huru katika sentensi ifuatayo.
Nilimwona Agwambo nilipofika Mombasa
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Eleza maana mbili katika sentensi hii.
Majambazi walimwibia Letangule gari jipya.
(Solved)
Eleza maana mbili katika sentensi hii.
Majambazi walimwibia Letangule gari jipya.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi ukitumia viunganishi hivi vya kinyume Ingawaje, ila(Solved)
Tunga sentensi ukitumia viunganishi hivi vya kinyume Ingawaje, ila
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi moja ili kudhihirisha matumizi ya viwakifishi hivi:
i)Semi koloni
ii)Mshazari(Solved)
Tunga sentensi moja ili kudhihirisha matumizi ya viwakifishi hivi:
i)Semi koloni
ii)Mshazari
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Vinyambue vitenzi vifuatavyo kulingana na maagizo.
(i) Ja ................. (tendwa)
(ii) La .................(tendesha)(Solved)
Vinyambue vitenzi vifuatavyo kulingana na maagizo.
(i) Ja ................. (tendwa)
(ii) La .................(tendesha)
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Pambanua sentensi ifuatayo kwa kutumia kielezo cha mchoro matawi.
Mwanafunzi mwenye juhudi amefuzu mtihani.
(Solved)
Pambanua sentensi ifuatayo kwa kutumia kielezo cha mchoro matawi.
Mwanafunzi mwenye juhudi amefuzu mtihani.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Fafanua kwa kutungia sentensi matumizi mawili ya neno beberu.(Solved)
Fafanua kwa kutungia sentensi matumizi mawili ya neno beberu.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Kanusha katika wingi.
Alikuarifu kuhusu yule hajala. (Solved)
Kanusha katika wingi.
Alikuarifu kuhusu yule hajala.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Andika.katika usemi halisi
Wanzare alimwambia shangazi yake kuwa angekuwa akienda kumtembelea kwake kila mwezi.(Solved)
Andika.katika usemi halisi
Wanzare alimwambia shangazi yake kuwa angekuwa akienda kumtembelea kwake kila mwezi.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Unganisha sentensi hizi kwa kutumia kirejeshi cha kati.
(i) Kalamu imeibwa
(ii) Kalamu ni yangu(Solved)
Unganisha sentensi hizi kwa kutumia kirejeshi cha kati.
(i) Kalamu imeibwa
(ii) Kalamu ni yangu
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Tambulisha ina za nomino katika sentensi ifuatayo.
Umma katika Jamhuri yetu unataka haki ya kila mja itekelezwe.(Solved)
Tambulisha ina za nomino katika sentensi ifuatayo.
Umma katika Jamhuri yetu unataka haki ya kila mja itekelezwe.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Unda nomino mbili kutokana na kitenzi arifu.(Solved)
Unda nomino mbili kutokana na kitenzi arifu.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Ainisha viambishi katika neno lifuatalo: aliyelima(Solved)
Ainisha viambishi katika neno lifuatalo: aliyelima
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Muhtasari
Sikukuu ya wafanyikazi huadhimishwa na wafanyikazi kote ulimwenguni kwa minajili ya
kukumbushana na kutanabahishana umuhimu wa mshikamano na umoja katika kudai na kutetea
maslahi na...(Solved)
Muhtasari
Sikukuu ya wafanyikazi huadhimishwa na wafanyikazi kote ulimwenguni kwa minajili ya
kukumbushana na kutanabahishana umuhimu wa mshikamano na umoja katika kudai na kutetea
maslahi na maendeleo yao. Kwa jumla wafanyakazi hukongamana kwa nia ya kutafakari kuhusu hali
yao ya baadaye.
Kwa sababu ya umuhimu wa wafanyakazi kuna kila nui ya sababu ya kuienzi sikuhii. Kwao ni siku yao ya kufanya tathmini ya jinsi wanavyotimiza wajibu wao wa kutoa kuzalisha mali pamoja na kutambua changamoto zinazowasakama kwa lengo la kubuni mbinu za kuzikabili.
Aidha siku hii hutoa jukwaa kwa wafanyakazi na viongozi wao kuwapa tuzo wenzao waliobobea katika nyanja mbali mbali za kazi zao. Yaani, ni wakati wa methali, mcheza kwao hutuzwa au la, huangaliwa kwa muktadha wa matumizi. Hata hivyo, ukweli mmoja ni kuwa sio wote waliotamba huweza kutuzwa madhali ni muhali kumtuza kila mtu. Ama thamani na manufaa ya tuzo hupatikana katika uchache wake. Jambo muhimu na Ia kukumbukwa ni kwamba kila mfanyakazi ni mchapa kazi, atuzwe asituzwe!
Jambo ambalo wafanyakazi hawapaswi kufunzwa, labda kukumbushwa tu, ni kuwa waendelee kufanya kazi kwa ari, umahiri na weledi wa hali ya juu. Mradi ni lazima watambue kuwa nafasi yao katika kuleta maendeleo ya kitaifa ni kubwa mno wala haimithilishwi na chochote.
Ni kutokana na kuelewa umuhimu mkubwa wa wafanyakazi ambapo katiba za nchi nyingi kote duniani husabili sahifa nyingi kuangazia masuala ya wafanyakazi. Baadhi ya masuala yanayofafanuliwa ni wajibu wa wafanyakazi na waajiri pamoja na haki za kila kundi ambapo wajibu wa kundi moja ni haki za kundi lingine. Hata hivyo, haiwezekani katiba za nchi kushughuulikia masuala yote ya wafanyakazi. Kwa sababu hii, stakabadhi zingine kama sheria za nchi husika ni adhimu, huduma na mikakati yao hufafanua zaidi kuhusu masuala ya waajiri na waajiriwa. Nyaraka hizi zote huandaliwa katika misingi ya maazimio ya Shirika la Wafanyakazi Duniani yaani ILO.
Haimhitaji mweledi kutambua kwamba wajibu mkubwa wa kila mwajiri ni kuhakikisha ya kuwa maslahi ya wafanyakazi yamepewa nafasi ya kwanza katika mipango yake yote. Miongoni mwa waajiri wote, serikali ndiyo mwajiri mkubwa. Hivyo basi, serikali inastahili kuwa kwenye msitari wa mbele katika kutunza na kutekeleza maslahi ya wafanyakazi wake.
Jambo linalotamausha ni kushuhudia na kusikia kuhusu visa vingi vya migomo ya wafanyakazi kote duniani wakilalamikia mazingira duni ya kutenda kazi, mishahara midogo, marupurupu madogo na machache, ukosefu wa muda wa mapumziko na kadhalika. Na shani kubwa ni kwamba aghalabu mwajiri anayesusiwa huwa ni serikali. Hofu kubwa hapa ni kwamba serikali zikikosa kujali maslahi ya wafanyakazi wao, waajiri wengine katika sekta ya kibinafsi kama mashirika, taasisi na watu binafsi, hawataona haja ya kufanya hivyo. Na katika hali kama hii basi msemo kwamba kazi isiyo kipimo, mwishowe watu huteta huwa kitulizo kikubwa kwa waajiriwa.
Wanapofikia na kufikishwa katika kiwango hiki, wafanyakazi hupandwa na jazba na kariha isiyoruhusu wala kusikiliza ama yoyote ya vitisho au ushauri ila tu utekelezaji wa matakwa yao!
Maswali
(a) Eleza umuhimu wa kuadhimishwa Sikukuu ya wafanyakazi unavyodhihirika katika aya tatu za kwanza.
Maneno 45-50
Matayarisho
Jibu
(b) Kwa kurejelea aya zilizosalia, andika hoja kuu zinazozungumziwa.
(Maneno 90— 100)
Matayarisho
Jibu
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali :-
Utandawazi
Kufikia miongo michache iliyopita, ujumbe ulisafirishwa kwa njia zilizochukua muda mrefu sana kufika. Kwa mfano, mtu alipotaka kupiga...(Solved)
UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali :-
Utandawazi
Kufikia miongo michache iliyopita, ujumbe ulisafirishwa kwa njia zilizochukua muda mrefu sana kufika. Kwa mfano, mtu alipotaka kupiga simu katika nchi jirani barani Afrika, ilimbidi kupitia kwa
opareta katika nchi za Ulaya ndipo aunganishwe. Kupigia simu kutoka Gambia kwenda Senegali
ilibidi kutumia opareta wa Kule London na wa Paris, Ufaransa, na wa Senegal.
Leo hii kuna njia nyingi za mawasiliano zilizo bora, za kutegemewa na zinazofikisha ujumbe kwa
kasi sana. Ujumbe ambao ungechukua muda mrefu kuufikisha, sasa unapelekwa kwa sekunde moja.
Miongoni mwa njia hizi ni mdahilishi, simu tamba na tuama, faksi, setelaiti, mitandao ya wavuti, n.k.
Hamna eneo sasa hivi hata liwe mbali vipi lisilofikika na aina hizi za mawasiliano.
Maendeleo haya ya mawasiliano yamechangia pakubwa sana kuufanya ulimwengu kuwa kijiji
kimoja. Sasa kuna uhusiano wa karibu sana miongoni mwa mataifa duniani katika Nyanja zote za
maisha. Hall hii ndiyo inayoitwa utandawazi au utandaridhi. Utandawazi umeleta mabadiliko mengi
maishani.
Mojawapo ni utoaji na uzalishaji wa mali. Mabadiliko ya mawasiliano yameruhusu mashirika ya
kimataifa kusambaza utoaji na uzalishaji wa bidhaa zao katika maeneo mbalimbali duniani. Hali hii
imepunguza gharama za usafirishaji sana. Bidhaa zinazoundwa na kiwanda chenye hakimiliki
kilichoko kule New York masafa ya mbali, zinaweza kuzalishwa na kiwanda kilicho hapa Nairobi.
Bila shaka umesikia kuhusu madawa ya kurefusha maisha ya wahasiriwa wa UKIMWI ambayo
yanazalishwa na baadhi ya viwanda vya kutengeneza madawa humu nchini. Kiwanda chenye
hakimiliki kipo jijini London.
Viwanda ambavyo vilikuwa katika mataifa tajiri kama vile Uingereza, Ufaransa, Marekani, Ujerumani na Japani sasa vimeweza kutandaza vitandabui vyake kote duniani. Utandazaji huu
hufanywa kwa njia kadhaa. Kwanza, viwanda hivi huvinunua viwanda vilivyoko katika mataifa
yanayostawi. Vinaweza kuingia katika ubia na viwanda vya mataifa wanakotaka kuhamia.
Viwanda hivi vya mataifa yanayoendelea hupatana kuwa watasimamia utoaji na uzalishaji wa bidhaa
fulani na kukubaliana namna ya kugawa mapato.
Utandawazi katika sekta ya uzalishaji na utoaji bidhaa umeleta manufaa kadhaa katika nchi zinazoendelea. Mojawapo ya haya ni kupatikana kwa nafasi za kazi. Pili, bidhaa za nchi zinazoendelea ambazo hazingeshindana na zile za mataifa yalioendelea sasa zimepata nafasi ya kushindana. Halikadhalika, wateja wana nafasi ya kupata bidhaa watakayo bila kuvunjwa moyo.
Iwapo bidhaa anazohitaji mteja hazipatikani katika nchi, zinaweza kuagizwa moja kwa moja kutoka
kwa kiwanda kingine chenye uhusiano nacho. Uagizaji hauchukui muda kutokana na hali ya
mawasiliano inayoweza kutegemewa na inayofikisha ujumbe bila kupoteza wakati. Fauka ya haya,
wateja hupata uwanja mpana wa kuchagua wanachokihitaji.
Utandawazi umehimiza kustawi kwa mazingira ya mashindano katika utoaji na uzalishaji mali
viwandani. Sasa hivi hakuna nchi yenye uwezo Wa kufungia bidhaa za nchi nyingine katika mipaka
yake. Kufanya hivi ni kujitia kitanzi kiuchumi. Lazima nchi zifüngue masoko yao. Navyo viwanda
vya kimataifa huweza kuwania masoko haya. Matokeo yake ni wateja kufaidika kwa kupata uwanja
mpana wa bidhaa za kuchagua. Wateja pia hupata bidhaa za hali ya juu na kwa bei isiyo ghali
kutokana na mashindano haya. Mashindano ya kimataifa ni kama ya paka na panya na kiwanda
kisichojifunga nira vizuri, huwa kinajihatarisha. Kinaweza kujipata kimetupwa nje ya soko na
kuangamia.Manufaa mengine ya utandawazi ni kuwa watu sasa hivi wanaweza kuwasiliana kwa
urahisi na wepesi. Kwa kutumia simu, au mdahilishi, mtu anaweza kuwasiliana na mwenzake popote
alipo licha ya masafa. Zaidi ya haya, utandawazi umewawezesha watu kutoka asili mbalimbali
kuingiliana na kutangamana. Utangamano huu umeweza kuleta umoja baina ya watu kwa kutoa hisia za ubaguzi.
Hata hivyo utandawazi umetokeza kuwa na madhara. Kwanza, uchumi wa nchi nyingi umeibukia
kutawaliwa na matukio ambayo hayazihusu nchi hizo moja kwa moja. Uvamizi wa kijambazi wa
Septemba 11,2000 kule Marekani uliathiri uchumi wa nchi nyingi sana. Matukio ya vita katika
Mashariki ya kati nayo yamechangia kuzorotesha uchumi wa nchi nyingi hasa zile maskini ambzo zinategemea mafuta kutoka huko ilhali vita hivyo haviwahusu sikio wala ndewe.
Athari kubwa ya utandawazi yaonekana katika sekta ya kijamii. Tamaduni nyingi za jamii katika nchi maskini zinaendelea kuvurugwa na maadili kuporomoka kutokana na ustawi wa kimawasiliano.
Vijana wanaiga kutoka mataifa ya kimagharibi bila kuchuja. Si ajabu kuwa vijana wetu wanavaa
mavazi yasiyositiri uchi wao vizuri na yasiyostahiki kwa jina la ustaarabu. Wavulana nao huzidisha
kwa kutoga masikio na kusuka nywele usiweze kuwatofautisha na dada zao.
Maswali
(a) Utandawazi ni nini?
(b) Ni mambo yapi yanayosababisha kutokea kwa utandawazi?
(c) Mashirika ya mataifa yaliyostawi yanatumia mikakati ipi kutandaza vitandabui vyao kote
duniani?
(d) Fafanua:
(i) Manufaa matatu ya utandawazi.
(ii) Hasara tatu za utandawazi.
(e) Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa.
(i) Ubia
(ii) Mashindano ya paka na panya.
(iii) Kutoga
(iv) Vitandabui
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi yenye kiingizi na kihusishi cha mahali.(Solved)
Tunga sentensi yenye kiingizi na kihusishi cha mahali.
Date posted: September 26, 2019. Answers (1)
- Kanusha sentensi hii
Nikimwona mwalimu wangu nitamjulisha habari hizo.(Solved)
Kanusha sentensi hii
Nikimwona mwalimu wangu nitamjulisha habari hizo.
Date posted: September 26, 2019. Answers (1)
- Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano.
i) twaa (kutendeka)
ii) Kosa (Kutendesha)
iii) Cha (Kutendwa)(Solved)
Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano.
i) twaa (kutendeka)
ii) Kosa (Kutendesha)
iii) Cha (Kutendwa)
Date posted: September 26, 2019. Answers (1)