Zitavuma, Zitakoma, Nitakwima, Mti-mle.

      

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Zitavuma,
Zitakoma,
Nitakwima,
Mti-mle.

Na muda nikisimama,
Nitatongoa nudhuma,
Kwa tenzi zilizo njema,
Nilisifu mti – mle.

Tazipanga tathlitha, tungo zilizo na hekima,
Za huba na thiatha, za kuburudi mitima,
Mashairi mabuthutha, musome mnaosoma.

Mti nishainukia,namea kuwa mzima,
Mizizi yadidimia, ardhini imeuma,
Nanena kitarbia, tungo zilizo adhama
Japo ni tungo za zama, mti-mle hutumia.

Zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,
Dharuba kinitikisa, mti-mle huinama,
Huyumba nikaziasa, matawi yakakingama,
Gharika ikishapisa, hurudi nikawa wima,
Na tungo za takhimisa, mti-mle huzipima.

Maswali
(1) Shairi hili ni la kimapokea. Toa sababu mbili kuunga kauli hii.
(2) Taja bahari kuu ya ushairi ambayo imetumiwa na mshairi. Fafanua.
(3) Fafanua dhamira ya mshairi.
(4) Kwa kutoa mifano bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili.
(5) Eleza jinsi mshairi ametumia idhini ya ushairi katika utungo huu.
(6) Andika ubeti wa nne kwa lugha natharia.
(7) Mshairi anamaanisha nini anaposema "zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,"
(8) Eleza toni ya shairi hili.
(9) Eleza maana ya msamiati ufuatao.
i) Nitatongoa
ii) Zitapusa.

  

Answers


sharon
(a)
i) Lina beti
ii) Lina mishororo
iii) Lina vina
iv) Lina mizani
v) Ubeti wa tatu, nne na wa tano una vipande (ukwapi, utao) za kwanza
2. Sakarani
Lina zaidi ya aina moja ya bahari za ushairi. Utenzi, tarbia, tathlitha na takhimisa Kutaja
Ufafanuzi
3. Kujinaki, au kujisifu kwa uwezo wake wa kutunga mitindo tofauti tofauti ya mashairi
4. i) Tanakuzi / kinyume/ ukinzani kama vile - Zitavuma – zitakoma
- zingaruma – zitapusa/zitakoma
ii) Jazanda – mti-mle – Bingwa wa ushairi
Gharika / Dharuba – changamoto anazopitia katika utunzi
iii) Lakabu (msimbo) - Mti – mle (amejiita mti-mle)
5. i) Inkisari - Tazipanga – Nitazipanga
-Na nena – ninanena
-Kuburudi – Kuburundisha
ii) Mazada -Nishainukia – nishainuka
iii) Lugha ya kikale –huba – mapenzi.
tongoa - sifia
iv) Lahaja m.f thiatha – badala ya siasa
Yeyote –kutaja

6. Mimi mti ninaujunzi mpana wa utunzi
Nimekita mizizi yangu barabara katika taaluma hii. Naweza kutunga mashairi aina ya tarbia ambazo ni ungo za heshima. Ingawa ni tungo za zamani, mimi, Mti - Mle huzitunga
7. Hata kukiwako na matatizo /upinzani/changamoto aina yoyote kutakuwa na mwishi wake.
i) Kuna dharau – kuwaita mashairi ni pepo ambazo zitafuma na kukoma
ii) Kuna majivuno -Anajiita mti – mle
-Kuchanganya bahari
8. i) Nitatongoa – Nitasifu/Nitaeleza
ii) Zitapusa – acha, / koma
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 08:19


Next: Outline briefly the method of ventilation used by locust and cockroach.
Previous: Explain briefly how excess protein are eliminated in the body.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions