Huyo Meya wetu ana washauri ambao huwasikiliza zaidi hata kama wanampotosha.Fafanua ukirejelea tamthilia "Mstahiki Meya".

      

Huyo Meya wetu ana washauri ambao huwasikiliza zaidi hata kama wanampotosha.Fafanua ukirejelea tamthilia "Mstahiki Meya".

  

Answers


sharon
i) Bili anamshauri Meya
ii) Bili anakubaliana na Meya anaposema ameagiza divai Ufaransa na mvinyo kutoka Urusi
iii) Bili na Meya wanakutana kajifahari wanapoponda mali bila kujuli
iv) Bili anakubaliana na Meya wasomeshe watoto wao ng‘ambo kwa vile masomo cheneo ni vivi hivi
v) Bili anaposikia Meya amempeleke mkewe kujifungulia ng‘ambo hata yeye anaona atamtuma mke wake huko wakati wake ukitimia
vi) Bili anakosa kumshauri Meya anapomgawia vipande vine vya ardhi (prime plot)
vii) Bili anamwonyesha Meya mbinu za kuufisidi mji kwa kukatiza mkataba wa mwanakandarasi ili anapolipwa fidia amgawie fungu lake.
viii) Diwani I na II wanalitetea Barasa la Meya hata wanachaguliwa kuwa ndio macho, masikio na sauti yake wanalipwa kwa sababu hii.
ix) Diwani I na II wanamshauri Meya amchukulie hatua Diwani III kwa kuwa ni mchochea
x) Bw. Usalama anasema yu tayari kuwaamrisha vijana (Askari) wa usalama wawapige waandamanaji badala ya kuwasikiliza
xi) Bw. Uhusiano mwema anahakikisha tamasha za vijana zimeandaliwa ili kudumisha uzalendo.
xii) Mhubiri (mshauri wa kiroho) hamwelekezi Meya kwa njia inayofaa mabali anauombea uongozi wake dhalimu ili apate sadaka
xiii) Bili anamshauri Meya waibe fimbo ya Meya ili wapate pesa.
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 08:24


Next: Explain how fatty acids and glycerols are absorbed in the ileum.
Previous: Oxygen is obtained on large scale by the fractional distillation of air as shown on the flow chart below.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions