Mwafulani 1: Nilikusahau lini ndiyo sasa nije kukusahau?...... Mwafulani II: …..tusikie.

      

Tamthilia "Mstahiki Meya"
Mwafulani 1: Nilikusahau lini ndiyo sasa nije kukusahau?......
Mwafulani II: …..tusikie.
(a) Eleza muktahda wa dondoo hili.
(b) Bainisha mbinu ya lugha inayojitokeza katika dondoo hili.
(c) Fafanua mambo yoyote manne yanayo zungumziwa na mwafulani wa pili kulingana na muktadha wa dondoo.
(d) Fafanua maudhui yoyote matano yanayojitokeza kulingana na muktadha wa dondoo hili.

  

Answers


sharon
a) Aliyesema maneno hayo mwafulani wa kwanza ni Meya
- Alikuwa anamwambia Bili
- Walikuwa ofisini kwa Meya alikoenda kupanga mikakati ya mapokezi la mameya
- Sauti mwafulani II sinasikika nje wakati Bili anamwambia Meya asimsaliti anapopeana kandarasi
b) Swali la Balagha.
c) Mfano haki ya kugoma. Walikuwa wanaletewa askari waliowapiga na kutishwa wangefutwa kazi
- Malipo bora. Mishahara ilikuwa ya chini iliyocheleweshwa na kutofanyiwa nyogeza za mshahara.
- Maslahi bora. Mazingira ya kufanya kazi yalikuwa mabaya mfano hawakuwa na glovu za kuosha vyoo
- Huduma za afya. Hawakuwa wanapata dawa kwa zahanati. Waliambiwa madawa yangeingia baada ya siku tatu.
- Haki ya kusikilizwa
– Walitaka kukutana na Meya hasa vingozi wao Meya alikataa kwa kusema Dairy yake ilikuwa imejaa hana nafasi au angesema hawezi kukutana na watu waliogoma
Lazima maelezo yatolewe
d) Maudhui ya ufisadi
- Bili anamwambia Meya akumbuke kandarasi mpya ilitegemea kauli ya Meya na kwamba hasimsahau anapopeana kandarasi
- Maudhui ya mgomo – Sauti ni za wafanyakazi waliogoma wakitaka maslahi yao yazingatiwe
- Maudhui ya haki – Waliogoma (sauti) wanalilia haki zao walionyimwa. Malipo bora, maslahi huduma za afya nk.
- Maudhui ya ubadhirifu – Meya kumwambia Bili hawezi kuja kumsahau
Meya alimpatia Bili vipande vya ardhi ambazo ni mali ya umma
- Maudhui ya uongozi – Uongozi ni mbaya ndio wafanyakazi wanagoma
- Maudhui ya mapendeleo – Bili anasema asisahuliwe na Meya wakati wa kupeana kandarasi
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 08:29


Next: Oxygen is obtained on large scale by the fractional distillation of air as shown on the flow chart below.
Previous: (a) What name is given to the two types of atoms.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions