Eleza jinsi mbinu ya kwelikinzani imetumika kwa kurejelea riwaya ya "kidagaa kimemwozea".

      

Eleza jinsi mbinu ya kwelikinzani imetumika kwa kurejelea riwaya ya "kidagaa kimemwozea".

  

Answers


sharon
i) Bi Zuhara mke wa Mtemi haridhiki na kuolewa na kiongozi mwenye utajiri. Anawaonea gere na hata kutamani maisha ya masikini waliovaa rinda moja Januari mosi hadi Januari mosi.
ii) Kanisa ni mahali pa kuhubiri amani lakini makanisa mawili yalipigana kadamnasi sokoni juu ya uwanja wa kujengea maabadi
iii) Jina la mtemi, Nasara Bora linaashiria mtu anayetoka familia inayo heshimika au yenye ustaarabu. Mtu anayeishi maisha ya hali yajuu lakini mtemi anaishi maisha duni. Gari kachala, nyumba iliyong‘ooka mabapa ya dirisha, makochi yaliyochakaa nakadhalika.
iv) Nasaba bora ananyakua mashamba makubwa na kuwafisidi raia kwa kughushi faili, lakini hali yake kimaisha ni hali yachini. Haishi maisha ya kifahari.
v) Mashujaa kama Matuko Weye na mchezaji mashuhuri chwechwe Makwache hawadhaminiwi na jamii na wanaishi maisha ya ufukara
vi) Tunataraji maisha katika kasri yawe ya kifalme lakini hali ni duni. Panaishi panya na nzi wa buluu ambao ni wanyama wapatikanao majengo ya vitongoji duni.
vii) Mtemi anajihusisha kimapenzi na Lowela lakini anapomkuta Amani katika chumba cha mkewe anaumwa moyoni na kumtaliki papo hapo.
viii) Majisifu anarundishiwa sifa kemkem juu ya umahiri wake katika somo la Kiswahili mpaka huwakosoa watu walipofanya makosa ya Kiswahili. Kinyume na matarajio tunang‘amua kwamba hawezi kutoa mhadhara wa kuridhisha katika chuo cha mkokotoni.
ix) Tungetaraji mazishi ya kiongozi mtajika kama mtemi kuhudhuriwa na watu wengi lakini ni wachache tu waliohudhuria.
x) Kama kiongozi angepewa heshima kwa kupigwa mizinga 21 katika mazishi ya kujitoa uhai kwa njia aliyotumia Mtemi ya kujinyonga. Angeng‘atuka mamlakani au mkimbizi wa kisiasa.
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 08:32


Next: (a) What name is given to the two types of atoms.
Previous: A person of blood group B marries a woman of blood group B. Work out the possible blood group of their children.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions