Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Ningemweka hai afikishwe mahakamani kweli idhihiri na uongo ujitenge".

      

Kidagaa Kimemwozea; Ken Walibora
Ningemweka hai afikishwe mahakamani kweli idhihiri na uongo ujitenge".
(a) Eleza muktadha wa dondoo.
(b) Fafanua kwa kutolea mifano ukweli wa kauli "kweli idhihiri".
(c) Eleza hulka ya mnenaji.
(d) Vitaje vitushi vyovyote vitatu vilivyomshangaza msemaji kulingana na muktadha wa dondoo.

  

Answers


sharon
a) Maneno hayo ni uzungumzi wa nafsia wa Amani wa kimoyomoyo.
- Ilikuwa baada ya siku nyingi walipofanya mazishi ya Mtemi Nasaba
- Amani alikuwa anafikiria juu ya hatima ya mwajiri wake wa awali
- Amani alisema angekuwa mhusika wa riwaya yake angemfisha kwa mikono yake angemweka hai ili apelekwe mahakama ukweli wa vitendo vyake ujilikane. (Alama. 4)
b) Mtemi alikuwa anawanyang‘anya watu mashamba mfano Chirchir Hamadi na mamaye Imani.
- Mtemi alikuwa anatumia hati miliki bandia baada ya kupokonya watu mashamba.
- Aliamrisha watu wapigwe mfano Matuko Weye, Amani na Imani
- Aliua watu mfano Chirchir Hamadi mamaye Imani
- Alikuwa anawapiga na kuwaumiza watu mfano alivyomfanyia Amani baada ya tuhuma ya uhusiano wa kimapenzi na mkwewe Zuhura alimpiga na kwenda kumtupa kando ya mto Kiberenge akidhani amekufa
- Alikuwa akiwadhulumu watu. DJ baada ya kuumwa na mbwa wake Jimmy aliyekuwa mgonjwa alikataa kumsaidia atibiwe.
- Mtemi alikuwa mfisadi, kutoa hongo kwa Askari na asasi ya mahakama Yusufu afungwe kwa kosa la tuhuma ya mauaji ya babaye.
- Mtemi alitoa hongo mtoto wake Madhubuti apate kazi
- Mtemi na wenzake walitumia pesa za kujenga hospitali, wakaziweka mfuko na kujenga zahanati alilolipa jina lake baadaye.
- Alitembea na mabibi wa watu na wasichana wadogo wa shule. Lowela huku akidanganya bibiye huwa anasuluhisha migogoro ya mashamba baada ya kuchelewa usiku.
- Alienda kukitupa kitoto Uhuru baada ya Lowela kujifungua.
- Alimtuhumia Amani kwamba ndiye alikuwa babaye mtoto aliye mwokota nje ya kibanda chake kwa hivyo amlee.
-Aliwafuta wafanyakazi wake kazi kwa sababu ambazo hazikuwa na msingi mfano ukizingatia usafi.
c) Tabia za Auani
- Mwenye Amani
Shujaa
- Kwenda sokomoko ambako hakujui uhali alijua akijulikana na Mtemi na amtambue yeye ni nani angemuua.
Mwenye utu.
- Kumwambia Oscar asimuue Mtemi,
- Kumpatia D.J. shati.

Mwaminifu
- Aliweza kukaa kwa Nasaba Bora kwa miaka miwili
- Kutimiza ahadi ya D.J
- Hakuwa na uhusiano wowote wa mapenzi na Imani
Msiri
- Hakumweleza Imani siri zake hasa siri ya mswada

Msikivu
- Alivyosikiliza maelezo kuhusu Imani

Mlezi mwema/ amewajibika
- Kumlea vizuri Uhuru
- Kuwa mwaminifu kwa utekelezaji wa kazi

Mwanamapinduzi
- Yeye, Imani wanabadilisha imani ya wanasokomoko kuhusu maji ya mto Kiberenge.
- Aliwagawia wanasokomoko ardhi

Mkarimu
- Kumpea D.J shamba, shati
- Kumpea Matuko nyumba
- Madhubuti shamba
-Kadiria majibu ya wanafunzi
d)
1) Jina la mwajiri wake (Mtemi) lilitoweka kabisa katika mazungumzo na kumbukizi za watu wa Sokomoko.
2) Jina la Mtemi Nasaba Bora lilifutwa katika chochote kilichojulikana kwalo
3) Kati ya mazungumzo yake na Madhubuti mwanawe, jina la Mtemi halikuzuka tena hata mara moja.
4) Madhubuti alishikilia kana kwamba mapambano bado yanaendelea kunyanyoosha mambo yaliyokwenda kombo nchini.
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 08:42


Next: Below is a list of some sources of energy: Coal, Nuclear Energy, Petroleum, Hydroelectric Power, Solar Energy and Wind Energy. Classify them into: a)Non – renewable b)Renewable
Previous: What is meant by the terms: (i) Atom (ii) Mass number

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions