a) Kanda la usufi ni anwani mwafaka. Fafanua kwa kutolea mifano. (b) Lini angepata nafasi ya kupenya kwenye chungio…" Fafanua jinsi msemewa angepata nafasi na changamoto zake.

      

Kanda la Usufi - (R. Nyaga)
(a) Kanda la usufi ni anwani mwafaka.
Fafanua kwa kutolea mifano.
(b) Lini angepata nafasi ya kupenya kwenye chungio…"
Fafanua jinsi msemewa angepata nafasi na changamoto zake.

  

Answers


sharon
a) Mimba ya Sela kwa Masazu ilikuwa ni kanda la usufi. Masazu alimwandikia barua na kumuuliza ni kwa nini hakujikinga. Alimwambia "yajapo yapokee‘
- Wanafunzi waliokuwa wajawazito majina yao yalipoitwa, wanafunzi wenzao waliangua vicheko vya chini kwa chini. Walijua kwamba wanafunzi hao ni wajawazito. Kwa wanafunzi wale wengine ujauzito wa wanafunzi ilikuwa kanda la usufi
- Sela na wenzake wawili ingawa walielewa sababu ya kuitwa ofisini hawakujua kilichokuwa kitendeke. Hakuna aliyezungumza na mwenzake kutokana na mawazo. Wote waliinamisha nyuso zao. Kwa mwalimu mkuu ilikuwa mzigu wao ni kanda la usufi alisema ni jambo la kawaida.
- Bakali babaye Sela alimuuliza mwalimu mkuu ni kwa nini wao huwaletea watoto shuleni. Yeye hajui waalimu huwa na majukumu hasa ya kutoa ushauri, kuwasomesha kwake Butali kazi ya waalimu ni kanda la usufi haoni kazi gumu na nyingi wanazotekeleza
- Kupata mimba kwa wasichana watatu ni mzigo kwa wazazi lakini kwa Bi. Margret ni kanda la usufi aliwaambia tukio lililowaleta hapo lilikuwa nila kawaida kwao.
- Mzee Butali anaonelea kosa la Sela la kuwa mja mzito mamaye ni wa kulaumiwa na hata anawafukuza nyumbani. Kwake mzigo huo ni wake lakini kwa mkewe ni kanda la usufi
b) Ukimbizi
- Angetukanwa na kusumbuliwa pale uwanja wa ndege kuwa yeye mkimbizi mwongo mzandiki
- Mkimbizi anayejidai kwao kuna fujo na kuuliwa watu
- Kuwa anakimbia shinda.
- kuwa anataka kuingia kwa wenyewe kwa lazima kuharibu mazingira, utulivu na utamanduni wa wenyeji wake.

Ajifanye mgonjwa mahututi wa maradhi yake hayatibiki hapa pao
- Ubalozi wa uingereza unajua ujanja huo.
- Wana daktari anayepima mtu kwanza ndio aruhusiwe kwenda uingereza kwa matibabu.

Ajifanye anaenda kusoma
- Lazima apate shule itakayomkubali
- Lazima aonyeshe mtaji mkubwa wa fedha za kilipia karo na gharama ya maisha
- Matokeo yake ya kidato cha sita yalikuwa mabaya

Aseme ni mtalii
- Yeye ni maskini kinyume cha mtalii

Kuolewa
- Ni nani huyo kutoka uingereza atakuja kumuoa hakuna
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 08:53


Next: Explain why molten calcium chloride conducts electricity while silicon (IV) oxide does not.
Previous: State two ways of preventing drug abuse.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions