Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Mtu mmoja alimpa mke wake nambari yake ya simu.

      

Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.
Mtu mmoja alimpa mke wake nambari yake ya simu. Kila mara bibi akipigia mumewe simu, ilipokelewa na sauti nyororo "mteja wa nambari uliopiga hapatikani kwa sasa."Alifunga safari kumtembelea mume wake mjini na kukabiliana na huyu kisura.

MASWALI
a) Bainisha kipera cha utungo huu.
b) Onyesha sifa tano za kipera hiki.
c) Eleza manufaa tano ya kipera hiki.

  

Answers


sharon
a) Sogo / soga - Mazungumzo ya kupitisha wakati au porojo
b) i) Soga huongezwa chumvi
ii) Mara nyingine ni jambo la ukweli na wakati mwingine ni uongo
iii) Wahusika ni wa kubuniwa / hupewa majina ya watu katika jamii hiyo
iv) Muundo wa kisa kimoja
v) Wahusika wachache
vi) Hutania Za kwanza
c) i) Hupitisha wakati
ii) Huburudisha wakati watu wanapumzika
iii) Hukejeli kwa njia ya utani
iv) Huelimisha jamii
v) Huleta umoja na ushirikiano miongoni mwa watu
vi) Huonya wanajamii
vii) Kukuza lugha kwa wasimulizi
viii) Hukuza kipawa cha uzungumzaji
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 08:58


Next: The table shows some data about one human kidney. FLUID Vol....
Previous: Study the diagram below and answer the question that follows.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions