Ewe mpwa wangu, Kwetu hakuna mwoga, usiwe kama msichana.

      

Soma wimbo ufuatao kisha ujibu maswali
Ewe mpwa wangu,
Kwetu hakuna mwoga, usiwe kama msichana.
Uoga ukikufika, huenda ni wa akina mamayo,
Fahali tulichinja ili uwe mwanamume
Iwapo utatingiza kichwa
Uhamie kwa wasiokatwa
Waume wa mbari yetu
Si waoga wa kisu
Wao hukatwa kuanzia macheo hadi machweo.

Simama jicho liwe juu
Ngariba alilala jikoni
Visu ametia makali
Kabiliana na kisu kikali
Wengi wasema ni kikali
Mbuzi utampata
Na hata shamba la mahindi
Usiende kwa wasiotahiri.

MASWALI
(a) Huu ni wimbo gani? Fafanua
(b) Eleza shughuli mbili za kiuchumi zinazodokezwa na wimbo huu.
(c) Onyesha taasubi ya kiume inavyojitokeza katika wimbo huu.

  

Answers


sharon
a. Nyiso / wimbo wa tohara
Anayeimbiwa anahimiza kukabiliana na ukaliwa kisu kwa ujasiri.
b. i) Ufugaji - Akivumilia atapewa mbuzi
ii) Kilimo – Atapata shamba la mahindi
c. i) Mwimbaji anasema kuwa waoga ni wa akina mama anayeimbiwa
ii) Waume wa mbari ya mwimbaji si waoga wa kisu
iii) Anayeimbiwa anaarifiwa kuwa fahali alichinjwa ili awe mwanamume
iv) Anahimizwa asiwe mwoga kama msichana
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 09:01


Next: Briefly explain how an aquatic green plant meets light intensity and carbon – dioxide requirements.
Previous: Identify the elements present in the following compounds. i) Magnesium oxide. ii) Zinc chloride iii) Sodium sulphate. iv) Aluminium nitrate

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions