"Hadi sasa sijaelewa kwa nini hakujitokeza kueleza hali ilivyo........Huenda hii ni dalili za..........."

      

"Mstahiki Meya"
"Hadi sasa sijaelewa kwa nini hakujitokeza kueleza hali ilivyo........Huenda hii ni dalili za..........."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Fafanua masuala matano yanayofaa kuelezewa kuhusu hali inayorejelewa.
c) Eleza umuhimu wa anayerejelewa
d) Bainisha matumizi ya tamathali moja katika dondoo

  

Answers


sharon
a) Msemaji ni siki.
Anamwambia Waridi
Wakiwa zahanatini/ hospitalini.
Siki anamrejelea Bwana uchumi na kazi/diwani III/ Kheri kwa kutojitokeza kueleza hali ilivyo kuhusiana na dawa badala ya meya.
b)
i) Ukosefu wa dawa zahanatini.
ii) Hali ngumu ya maisha inayowakabili wanacheneo
iii) Mishahara duni kwa wafanyakazi.
iv) Kucheleweshwa kwa mishahara.
v) Mishahara ikilipwa ni nusunusu.
vi) Madiwani kutotozwa kodi
vii) Ukosefu wa maji.
viii) Upungufu wa chakula/njaa
ix) Mazingira machafu
x) Idadi ya wagonjwa kuongezeka.
xi) Ukosefu wa vifaa vya kazi kwa mfano glavu.
c)
i) Kielelezo cha uzalendo thabiti.
ii) Mfano wa viongozi wenye maono.
iii) Anawakilisha viongozi waadilifu
iv) Kielelezo cha ukombozi
v) Anasimamia ukweli katika jamii.
d) Methali- Dalili za mvua ni mawingu
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 09:22


Next: Explain ways through which the media can help promote peace and good governance in Kenya today.
Previous: Study the diagram below for the reaction between sodium carbonate and hydrochloric acid and answer the questions that follow

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions