"...........wanaume wangewastahi wanawake kidogo,.......dunia ingekuwa pahala pema zaidi pa kuishi.

      

kidagaa kimemwozea
"...........wanaume wangewastahi wanawake kidogo,.......dunia ingekuwa pahala pema zaidi pa kuishi.
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
b) Kwa kurejelea wahusika wanne, onyesha jinsi Mtemi Nasaba Bora anavyochangia kumkandamiza mwanamke.

  

Answers


sharon
a) Mawazo yanapatikana akilini mwa Bi. Zuhurav akiwa nyumbani kwakev alikuwa akimwazia mumewe Mtemi Nasaba Bora ambaye hurudi nyumbani usiku wa manane baada ya kutafunwa na ukiwa na jakamoyo
b) Bi Zuhura.
- Anamwacha na kwenda kushiriki mapenzi na Lowela.
- Anamtusi akimwita jamvi la wageni.
- Anamtaliki kwa kumtuhumu.
- Anapuuza ushauri wa zuhura kumtibu DJ.
- Anarudi nyumbani usiku.
- Anaishi kwa upweke.
- Anasababisha utengano kati ya Zuhura na watoto wake.
- Anasababisha utengano kati ya Zuhura na watoto wake.
- Anamwuliza kwa ukali kuhusu kitoto alichomkuta Zuhura amebeba mkononi.

Lowela.
-Anahusiana kimapenzi na Lowela akiwa mdogo.
- Anamkatiza masomo.
- Anampachika mimba.
- Anamtenganisha na kitoto chake.
- Anamficha katika shamba la Baraka.
- Anamtenganisha na aila yake.

Imani
- Anamfungia Imani na Amani kwa madai wamekiua kitoto uhuru kilichokufa kwa kichomi.
- Anatuma watu /askari kuteketeza nyumba yao.
- Anamfananisha na Tamari aliyefanya uzinzi na Anoni.

Mashaka
- Anamtenga na ulimwengu wa nje.
- Anampa uchungu kwa kuchangia kuvunjika kwa uchumba wake na Benbella.
- Anamsababisha kukatiza masomo.
- Anamsababisha kuwehuka /kuwa wazimu
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 09:37


Next: Explain at least seven purposes of betrothal before marriage today
Previous: The set-up below was used to prepare a sample of oxygen gas. Study it and answer the questions that follow.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions