Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo.

      

Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
(i) Kanda la usufi
(ii) Shaka ya mambo
(iii) Mwana wa darubini
(iv) Ndoa ya Samani.

  

Answers


sharon
Ukatili unavyoijitokeza.
(i) Kanda la usufi.
(a) Chris anajitia hamnazo anapojulishwa kuhusu mimba ya Sela.
(b) Chris kuandamana na Sela kwenda kumuiba mtoto - hakujulisha wazazi wa Sela.
(c) Mzee Butali kumsomea mamake Sela kwa kutomshauri vyema msichana wake.
(d) Mzee Butali kuwafukuza Sela na mamake
(ii) Shaka ya mambo.
(a) Kamata kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasichana wawili kwa pamoja - Grace na Esther.
(b) Kamata kujifanya kumpelekea mzungu pesa zake lakini tunashuku hakuzipeleka.
(c) Grace anakataa kumbadilishia Esther zamu kama alivyokuwa amemuahidi.
(d) Kamata anakataa kupokea simu ya Esther jambo linalomfadhaisha (Esther)
(iii) Mwana wa darubini.
(a) Mwatela anamnajisi Kananda.
(b) Mwatela anamsaliti Maria kimapenzi anapojamiana na Kananda.
(c) Mwatela anapolewa anampiga mkewe.
(d) Mwatela anamuuza Kananda kama mtumwa Kongo.
(e) Mwatela anamnunulia mwanawe mwakitawa manati ya kumpiga mamake.
(f) Mwatela anamdanganya mwakitawa kwamba mamake alikufa.
(g) Mwakitawa anamgonga jiwe Kananda.
(iv) Ndoa ya Samani.
(a) Mamake Zena anakataa pesa ya msimulizi kwa kuwa ni maskini.
(b) Mmake Zena anadai Samani kutoka Arabuni.
(c) Mamake Zena anamshinikiza msimulizi kumwandalia mwanawe =arusi ya ndovu kumla mwanawe‘.
(d) Mamake Zena anamshinikiza msimulizi kuandaa fungate kwa bibi harusi nyumbani.
(e) Ghulamu fulani kuitisha fedha za ziada ili =dadake‘ Amali akubaliwe kutoka ndani ya nyumba.
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 10:13


Next: A compound of carbon, hydrogen and oxygen contains 71.12g by mass of oxygen, 2.2g hydrogen and the rest is carbon. It has relative molecular mass...
Previous: Mention the qualities that were required for one to be acknowledged as a King in Israel.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions