"Kwa nini mnaifunga mnyororo ile doggy mgonjwa? Mbona msiiwache free".

      

Kidagaa kimemwozea
"Kwa nini mnaifunga mnyororo ile doggy mgonjwa? Mbona msiiwache free".
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Onyesha jinsi wahusika riwayani wamefungwa minyororo.
(c) Minyororo inayorejelewa katika (b) hapo juu ilifunguliwaje?

  

Answers


sharon
(a) Muktadha.
(i) Haya ni maneno ya Bob DJ.
(ii) Mzungumziwa ni Bi Zuhura.
(iii) Wakiwa katika kasri la Majununi.
(iv) Bob DJ aliliona jibwa dhaifu lililokuwa limefungwa na minyororo baada ya kumpeleka Amani kwa
Mtemi Nasaba Bora kuajiriwa kazi ya uchungaji.
(b) Wahusika walivyofungwa na minyororo.
(i) Wananchi wa Sokomoko kutoyanywa maji ya mto Kiberenge.
(ii) Majununi kupumbazwa na mapenzi ya Mitchelle.
(iii) Majisifu kutowapenda watoto wake walemavu.
(iv) Imani kutaka kujitosa katika ziwa Mawewa.
(v) Wananchi kufungwa na utawala katili wa Mtemi.
(vi) Yusufu kufungwa kifungo cha maisha kutokana na tuhuma za mauaji ya babake.
(vii) Bi Zuhura kufungwa minyororo ya kindoa na Mtemi Nasaba Bora.
(viii) Amani anapagazwa kitoto na Mtemi Nasaba Bora.
(ix) Bob D.J ananaswa kwa matibabu duni ya zahanati ya Nasaba Bora.
(c) Minyororo "ilivyofunguka".
(i) Amani na Imani wanavunja mwiko wa kutoyanywa maji ya mto Kiberenge hivyo wananchi wakaanza kuyanywa.
(ii) Majununi anaamua kutooa milele baada ya kukataliwa na Mitchelle na mapenzi yake akayaelekeza kwa ufugaji na ukulima.
(iii) Mapenzi ya imani kwa watoto walemavu wa mwalimu Majisifu yaliyokuwa ya dhati yalimfanya Majisifu kuwapenda na kuwathamini.
(iv) Imani anapopatana na Amani kando ya ziwa Mawewa anabadili nia ya kujitosa Ziwani.
(v) Kwa ushirikiano wa Amani na Madhubuti utawala adhalimu wa Mtemi Nasaba Bora unaangushwa.
(vi) Kutokana na ushahidi unaonaswa na Majisifu kwenye kanda, Yusufu anachiliwa huru
(vi) Bi. Zuhura anajitanzua kutoka kwa ndoa dhalimu baada ya kupewa talaka na Mtemi Nasaba Bora.
(vii) Bob DJ anajinasua kutoka kwa matibabu duni katika zahanati ya Nasaba Bora baada ya kutoroka na kwenda kusaka matibabu ya kienyeji.
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 10:18


Next: Mention the qualities that were required for one to be acknowledged as a King in Israel.
Previous: Study the information in the table and answer questions that follow:

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions