Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili

      

Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili.

  

Answers


sharon
Jazanda ya kifo cha kitoto Uhuru.
(i) Walemavu hawapati malezi yanayowastahiki kwani wanadunishwa kwa kufungwa.
(ii) Matajiri wanawalazimisha maskini kuchangia masomo ya watoto wao k.m masomo ya Madhubuti.
(iii) Yusuf, Amani, Imani na Matuko Weye wanatiwa gerezani ingawa hawana hatia kwa makosa ya kusingiziwa.
(iv) Mtemi anamdhulumu Bi. Zuhura kwa kumpatia talaka anaposhuku ana uhusiano wa kimapenzi na Amani.
(v) Amani na Imani wanatiwa mbaroni kwa zingizio la kusababisha kifo cha Uhuru.
(vi) Mtemi Nasaba Bora anaghushi faili na kunyakua mashamba ya watu kama la Chichiri Hamadi wanauliwa ili mali yao
itwaliwe.
(vii) Matuko Weye na chwechwe makweche walio mashujaa kweli wa Tomoko hawatambuliwi na wanaishi maisha ya kimaskini huku wakihangaishwa na kutiwa gerezani.
(viii) Mwalimu Majisifu anakiuka haki ya wanafunzi kusoma na kwenda kuchapa mtindi.
(ix) Haki za wagonjwa zinakiukwa kwa kutopewa matibabu na wauguzi.
(x) Raia wanatolewa hotuba kwa kiingereza kisichoeleweka badala ya Kiswahili.
(xi) Wanatomoko kulazimishwa kuhudhuria sherehe za sikukuu ya wazalendo huku wakichomwa na jua na kunyeshewa.
(xii) Gazeti la Tomoko huchapisha picha ya Mtemi Nasaba Bora kwa sababu nduguye ni mhariri.
(xiii)Mtemi Nasaba Bora hachaji mbwa wake ilihali anawataka raia kuwachanja mbwa wao.
(xiv) Mtemi Nasaba Bora anawafuta watu kazi apendavyo; kuwalipa mishahara duni hivyo kuwanyima haki zao.
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 10:22


Next: Study the information in the table and answer questions that follow:
Previous: What volume of oxygen will be required for complete combustion of 100cm3 of carbon (II) oxide. What is the volume of the product formed (All...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions