Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.

      

Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.

  

Answers


sharon
Jumuiya ya "mstahiki Meya" inavyoafiki jamii ya kisasa.
(a) Haki za wafanyikazi.
(i) Hawaongezewi mishahara na iwapo wataongezewa ni asilimia ndogo.
(ii) Hawasikizwi wanapolalamika.
(iii) Wanapogoma, nguvu zaidi hutumika kuwatimua.
(iv) Hutishwa kufutwa kazi wanapodai haki zao.
(v) Hali yao ya afya haitiliwi maanani - hawana bima ya matibabu.
(vi) Elimu bora ya watoto wao hupuuzwa.
(vii) Vifaa vya kazi havipo km. glavu.
(viii) Wagomapo mishahara yao hukatwa.
(ix) Mshahara unaoongezwa huchukua muda mrefu kutekelezwa.

(b) Migomo na maandamano.
(i) Viongozi kushughulikia maslahi yao, k.m kujiongezea mishahara.
(ii) Ahadi za uongo kutoka kwa viongozi.
(iii) Hali mbaya ya kazi - hakuna vifaa vya kazi - glavu.
(iv) Vyombo vya dola kutumiwa kunyanyasa wanaogoma.

(c) Ubadhirifu wa mali ya umma.
(i) Baraza kutoa laki moja kama sadaka kwa muhubiri kila mwezi.
(ii) Viongozi (meya) kumpeleka bibi yake ng‘ambo kujifungua.
(iii) Viongozi wana pesa za burudani - Entertainment vote.
(iv) Madiwani na askari wanaongezwa mishahara kiholela bila sera maalum.
(v) Wageni kupokewa kwenye hoteli za kifahari.
(vi) Mapokezi ya wageni ni ya gharama ya juu.
(vii) Viongozi kuandaa karamu maalum kwa heshima ya wageni ilihali baraza halina pesa.

(d) Ufisadi.
(i) Mwenye kandarasi kupokonywa kandarasi eti aliyempa kandarasi hiyo, wakati wake umepita.
(ii) Bili kusema kuwa, dawa ya adui ni kummegea unachokula ili wote wafaidike.
(iii) Bili anaibia Baraza kwa kulipwa ilhali si mfanyikazi wa Baraza.
(iv) Meya ananyakua vipande vinane vya ardhi na kumgawia Bili vinne.

(e) Utegemezi.
(i) Wafadhili ndio wanatoa mwongozo wa maamuzi kwa viongozi - wanapendelea mfumo wa kugawana gharama ya
maisha.
(ii) Elimu ya cheneo ni duni hivyo viongozi wanasomeshea watoto wao ughaibuni.
(iii) Wafadhili ndio wanaamua idadi ya wafanyakazi.
(iv) Dawa kuagizwa kutoka ng‘ambo.
(v) Meya na madiwani wanatarajia wageni kifedha hata wanakopa pesa ili kulipa mishahara.

(f) Umaskini.
(i) Wananchi hawana pesa za kugharamia matibabu.
(ii) Watoto kukosa lishe bora.
(iii) Watu wengi ni maskini kwa sababu ya mshahara duni.
(iv) Kula mabaki ya kupewa mbwa.
(v) Bei ya mafuta na makaa ni ghali mno.

(g) Tamaa na ubinafsi.
(i) Madiwani hawalipi ushuru.
(ii) Watoto wa meya wanapata elimu bora, watoto wa wafanyakazi hawana elimu bora.
(iii) Meya anawaongezea mishahara askari kwani wao ni =vyombo vya kulinda ufisadi‘

(h) Utawala na uongozi mbaya;
(i) Meya na madiwani na vikaragosi wao hawako tayari kushawishiwa.
(ii) Viongozi hawajali maslahi ya umma. Meya anasema mtoto aliyekufa ni mmoja tu.
(iii) Sera za kubuni kilimo mwafaka zimekosekana watu wanakula mabaki ya chakula.
(iv) Viongozi hawaoni mbele wanajilinganisha na majirani maskini.

(i) Huduma mbovu za kiafya kwa umma.
(i) Zahanatini hamna dawa.
(ii) Wagonjwa wanaotafuta matibabu ni wengi.
(iii) Wahudumu ni jeuri kama Waridi.
(iv) Wengi wa watoto wanaougua, wanakosa lishe bora.
(v) Sera za kuboresha elimu ni duni.

(j) Utabaka.
(i) Watoto wa meya wanapata elimu bora, watoto wa wafanyakazi hawana elimu bora.
(ii) Madiwani hawalipi ushuru ilihali mama muuza ndizi analipa kodi.
(iii) Meya na madiwani wana bima za matibabu ilihali wafanyakazi hawana.
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 10:41


Next: Study the flow chart below and answer the questions that follow.
Previous: State one way of making surface tension of water stronger.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions