Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,

      

Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
1. Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
Asinywe yalo na vunju,
Yakampa kigegezi,
Yakamkibua roho akaona na kinyaa,
Awali ndio awali, awali mbovu hamna.

2. Kiwa utalimatia.
Utayaramba makombo,
Utadata vitu cheche,
Kisomo chenye dhamana kikakupa kisogo,
Inajuzu ujihimu
Mwanafuu darasani,
Urauka po mapema,
Katu hutayaramba makombo,
Hutakosa kisebeho.

3. Dereva hata utingo,
Natija ni asubuhi,
Wateja utawawahi,
Wasaa kuzingatia,
Uwafikishe kazini,
Kwa wasaa ufaao,
Wasije wakateteshwa,
Na bosi wao kazini,
Nao wakakuapiza.

4. Na ewe mwanazaraa,
Mpini uukamate,
Kabla jua kuwaka sana,
Majasho kutiririsha mwilini,
Yang‘oe yote magugu,
Kutoka kwa lako konde.

5. Mhadimu mwenye ajizi,
Yakujuza ujihimu,
Ununue na maziwa,
Majogoo uyawahi mapema,
Usije ukayadata,
Chai mkandaa ukaandaa,
Wateja wakuambae mithili ya ibilisi.

Maswali
(a) Eleza nasaha yoyote inayotolewa kwa wafanyakazi wowote watatu kwenye shairi.
(b) Taja sifa zozote za kimuundo zilizotumiwa na mtunzi.
(c) Eleza toni ya mshairi.
(d) Nafsi nenewa anahimizwa kufanya nini.
(e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi.
(f) Toa mifano miwili ya uhuru wa mshairi.
(g) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa kwenye shairi.
(i) Maji maenge
(ii) Natija
(iii) Majogoo

  

Answers


sharon
(a) Nasaha;
(i) Dereva na Utingo: - Kuamka mapema ili wapeleke wasafiri kazini.
(ii) Mkulima:- Aamke mapema kwenda shambani kulima
(iii) Mhadimu: Aamke mapema ili anunue vitu muhimu vinavyohitajika katika upishi. Kwa Mfano, maziwa.
(b) Toni.
Toni ya mshairi.
-Ushauri
- Kuelekeza
- Elimsiha
- Onyo
(d) Nafsi nenewa anahimizwa.
(i) Mhadimu aamke mapema akanunue vitu vya upishi.
(ii) Mkulima aamke mapema aende shambani akalime.
(iii) Dereva na Utingo waamke mapema kuwapeleka wasafiri kazini mwao.
(e) Lugha nathari.
Dereva na utingo wakiamka asubuhi wanayo faida ya kuwapata wasafiri ambao wanatarajiwa kuwafikisha kazini kwa wakati ufaao ili wasije wakapigiwa kelele na wakubwa wao hivyo kusababisha wasafiri kuwalaani.
(f) Uhuru wa mshairi.
(i) Lahaja - Vunju
- Yalo
- Mwanafuu
(ii) Kuboronga sarufi:
Yang‘oe yote magugu - yang‘oe magugu yote.
Kutoka kwa lako konde - kutoka kwa konde lako.
Chai mkandaa ukaandaa - ukaandaa chai ya mkandaa
Mpini uukamate - uukamate mpini.
(iii) Inkisari:
yakujuza - inakujuza
kiwa - ikiwa
(iv) Ukale wa lugha.
- Vunju
- Yalo
- Mwanafuu
(g) Misamiati
(i) Maji maenge - Maji safi.
(ii) Natija - Faida
(iii) Majogoo - Alfajiri au mapema.
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 10:50


Next: Describe the works and activities of Jesus after His Baptism.
Previous:  Study the table below and answer the questions that follow.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions