Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Kila nikaapo hushika tama.

Kila nikaapo hushika tama
Na kuwazia hali inayonizunguka.
Huyawazia madhila
Huziwazia shida
Huiwazia dhiki

Dhiki ya ulezi
Shida ya kudhalilishwa kazini.
Madhila ya kufanyiwa dharau
Kwa sababu ya jinsia ya kike.

Hukaa na kujidadisi
Hujidadisi kujua kwa nini
Jamii haikisikii kilio changu
Wenzangu hawanishiki mikono
Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni

Hukaa na kujiuliza
I wapi raha yangu uiimwengu huu?
I wapi jamaa nzima ya wanawake?

MASWALI
(a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza
(b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
(c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata.
(d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili.
(e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili.
(f) Fafanua toni ya shairi hili.
(g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili.
(h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa.
(i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
(i) Madhila
(ii) Kudhalilishwa.

Answers


sharon
a) Huru kwa sababu haiizingatii arudhi
b) Dhamira
- Kuonyesha jinsi mwanamke anavyoonewa kwa sababu ya jinsia yake
c) Mishata ni mistari ya shairi ambayo haijakamilika mf. Hujidadisi kujua kwa nini
Hukaa na kujiuliza kueleza mifano mimli
d) Balagha mfano wapi jamaa nzima ya wanawake
Taswira mf. kushika tama
Takriri mf. kurudiwarudiwa kwa maneno wazia, jidadisi, iwapi zozote
e) Nafsi - neni ni mwanamke anayedharauliwa
f) Toni ya huzuni / majonzi / kukata tamaa
g) Maudhui
- Dhiki za ulezi
- Kudhalilishwa kazini
- Kudhalilishwa kwa sababu ya jinsia
- Usaliti - wanawake wenzake kutomuunga mkono
h) Wanawake wote hawamuungi mkono
i) Madhila - mateso / shida / maonevu
Kudhalilishwa - kudharauliwa
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 11:05

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions