a) Diwani wa 111
Mwandishi amemtumia kuibua maudhui yafuatayo
- Matatizo yanayowakumba wanacheneo - kupitia mazungumzo yake na daktari Siki, Meya na madiwani k.m. uk.21 - watu wana njaa, wana uhitaji wa dawa
- Uzalendo - anatetea maslahi ya wafanyakazi ambao ni wanacheneo
- Uwajibikaji - anawajibika katika kazi yake hata anapopata pingamizi kutoka kwa Meya na madiwani
- Usaliti - anakataa kuungana mkono na viongozi wengine (Diwani 1, II na Meya) katika mipango ya kuliendeleza baraza
- Ubaguzi - anabaguliwa na Meya kikazi. Harnshughulishi katika maamuzi muhimu ya baraza
- Matumizi mabaya ya mamlaka - Meya anapomwamrisha awaongeze madiwani mishahara na kuacha kuwatoza kodi. Aiilazimika kumtii Meya hata ingawa shingo upande
- Ukoloni mamboleo uk.20 ?tumelazimishwa na kaka zetu kupunguza idadi ya wafanyakazi
- Utegemezi - uk.20 ?kaka zetu hao hawajatoa hela za mkopo
- Anaibua maudhui ya ukweli - anamwambia Meya ukweli kuhusu baraza k.m. Lina nakisi zozote.
b) Bili
- Anaibua maudhui ya ufisadi - ndiye anayeleta wazo la kuiba fimbo ya Meya
- anamshauri Meya aongee na mwanakandarasi ili ashinde kesi akiiipwa wagawane pesa
- anagawiwa vipande vya ardhi na Meya
- Msaliti
- baada ya Bili kumpa Meya ushauri mbaya na mambo kuharibika, anatoroka. Hapatikani Meya anapomtafuta
- Ubadhirifu
- Meya anampeleka hoteli ya kajifahari kujivinjari kwa kutumia mali ya umraa
- Mapuuza - anamshauri Meya kupuuza vilio vya wafanyakazi wanapomlilia awasikilize
- Tamaa - hasa ya Meya anapokubali mawazo ya Bili ya kuliibia baraza zozote.
c) Mhubiri
Anasaidia kukuza maudhui yafuatayo;
- Unafiki wa kidini (uk.41 -44)
Anajifanya kuwa mwanadini ilhaii anaitumia kujinufaisha
- anaombea baraza la Meya lidumu ilhaii linawakandamiza wananchi
- unafiki wa Meya - anapojifanya mpole
- Tamaa
Anakubali kupewa sadaka ya shilingi laki moja na mafuta ya gari kila mwezi kwa kuliombea baraza
- Ubadhirifu (uk.44)
Kupitia kwake tunaona matumizi mabaya ya mali ya umma na Meya anapoahidi kumpa sadaka kila mwisho wa mwezi na kugharamia petroli
- Usaliti
Anawasaliti wananchi wanaorntegemea kutuliza nyoyo zao anapokubali kushirikiana na Meya badala ya kumwambia ukweli kuhusu utawala wake mbaya
- Uwajibikaji (uk.42-43)
- Kupitia kwake tunapata uwajibikaji wa askari hasa wanaposikia kelele na kuchukua hatua mara moja
d) Diwani wa kwanza na wa pili Wanasaidia kukuza maudhui kama
i) Usaliti
- Wanawasaliti wananchi waliowachagua kwa kuunga mkono uongozi dhalimu wa Meya
ii) Ubarakala - wanaliwajibikia baraza (Meya) badala ya wananchi
- wao ni macho na masikio ya Meya (uk. 16)
iii) Wanakuza swala la ubinafsi ambapo wanakuwa macho na masikio ya Meya na wanafanya hivi kwa sababu wanalipwa (uk. 16)
- wanaomba wasitozwe kodi
iv) Kutowajibi.ka
- Madiwani wanawajibikia baraza badaia ya wananchi waliowachagua (uk.17)
v) Unafiki
- Madiwani wanajifanya kutumikia baraza ilhaii wanamtumikia Meya na kujali maslahi yao wenyewe
vi) Ukatili
- Wanamshauri Mey^K^^feiH hatua za kikatili dhidi ya wafanyakazi k.v. kutembeza virungu, kupeana ahadi za uongo n,k.
vii) Tamaa
- Wanaendeieza maudhui ya tamaa kwa sababu wanamtumikia Meya iii kujinufaisha
- Wanaomba nyongeza ya mishahara ilhaii wafanyakazi wanalipwa malipo duni wanaomba pesa za kununua nguo huku wananchi wakilala njaa na kufa kwa magonjwa
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 11:46
- Kila nikaapo hushika tama.(Solved)
Kila nikaapo hushika tama
Na kuwazia hali inayonizunguka.
Huyawazia madhila
Huziwazia shida
Huiwazia dhiki
Dhiki ya ulezi
Shida ya kudhalilishwa kazini.
Madhila ya kufanyiwa dharau
Kwa sababu ya jinsia ya kike.
Hukaa na kujidadisi
Hujidadisi kujua kwa nini
Jamii haikisikii kilio changu
Wenzangu hawanishiki mikono
Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni
Hukaa na kujiuliza
I wapi raha yangu uiimwengu huu?
I wapi jamaa nzima ya wanawake?
MASWALI
(a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza
(b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
(c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata.
(d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili.
(e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili.
(f) Fafanua toni ya shairi hili.
(g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili.
(h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa.
(i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
(i) Madhila
(ii) Kudhalilishwa.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,(Solved)
Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
1. Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,
Ondoka andama ndiya, nondosheya uso wako,
Ondoka wanisikiya, ziwate jeuri zako,
Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani?
2. Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri,
Haistahamilikii, uovu umekithiri,
Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri,
Sikati yako shari, enda zako wasiwasi.
3. Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha,
Viumbe na zao nyoyo, vitina kuwagotanisha,
Hiino ndio kaziyo, yenye kukufurahisha,
Ni kazi isiyokuchosha, mno umeizoeya.
4. Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani,
Ati mambo si mazuri, mambo yote tatashani,
Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini,
Nisononeke moyoni, upate kufurahika.
5. Au mara hunijiya, na kingine kisahani,
Kuhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani,
Huwa husishi nambiya, hali zao taabani,
Zingawa wakati gani? Ni zako au ni zao?
6. Na mara kuja mambiya, nitakapotoka humu,
Na kwamba yaningojea, nde maisha magumu,
Uliloni kusudiya, ni kunitiya wazimu,
Kama ndiyo yako hamu, basi unshatahayari.
(a) Eleza ujumbe uliojitokeza katika shairi hili.
(b) Fafanua muundo wa ubeti wa tatu.
(c) Eleza aina ya shairi hili.
(d) Fafanua arudhi za utunzi alizozingatia mshairi.
(e) Eleza toni ya mshairi.
(f) Andika ubeti wa tano katika lugha ya kinathari.
(g) Eleza mifano mitatu ya uhuru wa mshairi.
(h) Eleza maana ya misamiati ifuatayokama ilivyotumika katika shairi.
(i) ndiya
(ii) kisahani
(iii) nde
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
(Solved)
Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
1. Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
Asinywe yalo na vunju,
Yakampa kigegezi,
Yakamkibua roho akaona na kinyaa,
Awali ndio awali, awali mbovu hamna.
2. Kiwa utalimatia.
Utayaramba makombo,
Utadata vitu cheche,
Kisomo chenye dhamana kikakupa kisogo,
Inajuzu ujihimu
Mwanafuu darasani,
Urauka po mapema,
Katu hutayaramba makombo,
Hutakosa kisebeho.
3. Dereva hata utingo,
Natija ni asubuhi,
Wateja utawawahi,
Wasaa kuzingatia,
Uwafikishe kazini,
Kwa wasaa ufaao,
Wasije wakateteshwa,
Na bosi wao kazini,
Nao wakakuapiza.
4. Na ewe mwanazaraa,
Mpini uukamate,
Kabla jua kuwaka sana,
Majasho kutiririsha mwilini,
Yang‘oe yote magugu,
Kutoka kwa lako konde.
5. Mhadimu mwenye ajizi,
Yakujuza ujihimu,
Ununue na maziwa,
Majogoo uyawahi mapema,
Usije ukayadata,
Chai mkandaa ukaandaa,
Wateja wakuambae mithili ya ibilisi.
Maswali
(a) Eleza nasaha yoyote inayotolewa kwa wafanyakazi wowote watatu kwenye shairi.
(b) Taja sifa zozote za kimuundo zilizotumiwa na mtunzi.
(c) Eleza toni ya mshairi.
(d) Nafsi nenewa anahimizwa kufanya nini.
(e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi.
(f) Toa mifano miwili ya uhuru wa mshairi.
(g) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa kwenye shairi.
(i) Maji maenge
(ii) Natija
(iii) Majogoo
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.(Solved)
Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Huu ni ukoloni mamboleo"(Solved)
Mstahiki Meya
"Huu ni ukoloni mamboleo"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza umuhimu wa msemewa katika tamthilia hii.
(c) Jadili namna ukoloni mamboleo unavyojitokeza katika tamthilia.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili(Solved)
Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Kwa nini mnaifunga mnyororo ile doggy mgonjwa? Mbona msiiwache free".(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Kwa nini mnaifunga mnyororo ile doggy mgonjwa? Mbona msiiwache free".
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Onyesha jinsi wahusika riwayani wamefungwa minyororo.
(c) Minyororo inayorejelewa katika (b) hapo juu ilifunguliwaje?
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo. (Solved)
Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
(i) Kanda la usufi
(ii) Shaka ya mambo
(iii) Mwana wa darubini
(iv) Ndoa ya Samani.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Wafrika hupitia changamoto nyingi sana wakiwa masomoni ughaibuni. Thibitisha kauli hii ukirejelea hadithi "Damu nyeusi"(Solved)
Wafrika hupitia changamoto nyingi sana wakiwa masomoni ughaibuni. Thibitisha kauli hii ukirejelea hadithi "Damu nyeusi"
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Kero hizi na dharau zinamfanya kuthamini zaidi utu wake ....."Ukirejelea hadithi "Damu nyeusi" Eleza muktadha wa dondoo hili.(Solved)
"Kero hizi na dharau zinamfanya kuthamini zaidi utu wake ....."Ukirejelea hadithi "Damu nyeusi" Eleza muktadha wa dondoo hili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Thibitisha jinsi anwani "Damu Nyeusi" inaafiki yaliyomo katika hadithi.(Solved)
Thibitisha jinsi anwani "Damu Nyeusi" inaafiki yaliyomo katika hadithi.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Jadili matatizo KUMI ya kijamii ukirejelea hadithi "Mwana wa Darubini"(Solved)
Jadili matatizo KUMI ya kijamii ukirejelea hadithi "Mwana wa Darubini"
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Sisi kama wazazi...........hukabiliana na mengi...........mara nyingi tabia zao hutupiga chenga........"(Solved)
"Damu nyeusi na hadithi zingine"
"Sisi kama wazazi...........hukabiliana na mengi...........mara nyingi tabia zao hutupiga chenga........"
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake
b) Dhihirisha mbinu NNE za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili
c) Jadili yaliyomsibu mrejelewa.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Riwaya ya kidagaa kimemwozea inaonyesha jitihada za vijana kujenga jamii mpya. Thibitisha kwa kutoa mifano(Solved)
Riwaya ya kidagaa kimemwozea inaonyesha jitihada za vijana kujenga jamii mpya. Thibitisha kwa kutoa mifano
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "...........wanaume wangewastahi wanawake kidogo,.......dunia ingekuwa pahala pema zaidi pa kuishi.(Solved)
kidagaa kimemwozea
"...........wanaume wangewastahi wanawake kidogo,.......dunia ingekuwa pahala pema zaidi pa kuishi.
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.
b) Kwa kurejelea wahusika wanne, onyesha jinsi Mtemi Nasaba Bora anavyochangia kumkandamiza mwanamke.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Kwa kurejelea tamthilia ya Mstahiki Meya, fafanua vichocheo vya migogoro katika jamii ya Cheneo.(Solved)
Kwa kurejelea tamthilia ya Mstahiki Meya, fafanua vichocheo vya migogoro katika jamii ya Cheneo.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Hadi sasa sijaelewa kwa nini hakujitokeza kueleza hali ilivyo........Huenda hii ni dalili za..........."(Solved)
"Mstahiki Meya"
"Hadi sasa sijaelewa kwa nini hakujitokeza kueleza hali ilivyo........Huenda hii ni dalili za..........."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Fafanua masuala matano yanayofaa kuelezewa kuhusu hali inayorejelewa.
c) Eleza umuhimu wa anayerejelewa
d) Bainisha matumizi ya tamathali moja katika dondoo
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Matambiko ni nini? Eleza dhima zake mbili.(Solved)
Matambiko ni nini? Eleza dhima zake mbili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Eleza maana ya maapizo.(Solved)
Eleza maana ya maapizo.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Eleza maana ya ngoma katika fasihi simulizi kisha utoe dhima zake nne.(Solved)
Eleza maana ya ngoma katika fasihi simulizi kisha utoe dhima zake nne.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)