
a) maneno haya ni ya mwandishi
- Anamrejelea Bi Zuhura
- Bi Zuhura amelala kitandani pekee akiwaza ni usiku wa manane
- Mumewe alikuwa na mazoea ya kumwacha mkewe peke yake na kumzidishia upweke. Aliporudi usiku wa manane hujitupa kitandani kama gogo (bila kutekeleza majukumu ya ndoa) zozote 4x1=4
b) sitiari - kiu / njaa
Msisitizo - alikuwa na, si
c) i) Alikuwa na kiu ya mapenzi / ya kupendwa
ii) Alikuwa na kiu ya kuwa pamoja wa mumewe zozote 2x2 = 4
d) Mtemi Nasaba bora alikosa kutimiza majukumu ya ndoa kwa mkewe hadi akatamani (mkewe) kuzini na Amani mwishowe alimtaliki
- Mtemi Nasaba Bora alishindwa kudhibiti familia yake ambapo mtotowe madhubuti alimuasi
- Mtemi Nasaba Bora alijiingiza katika mapenzi na wasichana wadogo marika na binti yake aliishia kupata mtoto wa Lowela kisha akamtupa mtoto na kusababisha kifo cha uhuru
- Mtemi alieleweka kumficha Lowela na kumringa kisa kilichomfanya Benbela kusitisha mapenzi / uchumba na Mashaka - Mashaka akawa mkichaa
- Mtemi aliiba mashamba ya watu alipogundulika alijuta sana na kujitia kitanzi
- Alishindwa kutimiza ahadi alizompa msichana waliokuwa naye katika matwana moja wakati msichana alipoibukia kuwa kiwete
- Alishindwa kupatana na nduguye Majisifu wakawa maasidi
- Alipokosolewa na Matuko Weye kwenye jukwaa la siku ya wazalendo, Mtemi hakuwa na subira ila alimfungia Weye baadaye aliona ujinga wake akamfungulia
- Mtemi alimwacha mwanamke aliyekuwa akijikopolea barabarani. Jambo hili lilionyesha kutowajibika
- Mtemi Nasaba Bora aliwapeleka watoto wake ng‘ambo badala ya kuboresha elimu ya tomoko
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 11:59
-
"Duniani kuna watu na viatu"
(Solved)
Tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
"Duniani kuna watu na viatu"
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.
(Solved)
Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.
(i) Diwani wa tatu
(ii) Bili
(iii) Mhubiri
(iv) Diwani I na II
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Kila nikaapo hushika tama.
(Solved)
Kila nikaapo hushika tama
Na kuwazia hali inayonizunguka.
Huyawazia madhila
Huziwazia shida
Huiwazia dhiki
Dhiki ya ulezi
Shida ya kudhalilishwa kazini.
Madhila ya kufanyiwa dharau
Kwa sababu ya jinsia ya kike.
Hukaa na kujidadisi
Hujidadisi kujua kwa nini
Jamii haikisikii kilio changu
Wenzangu hawanishiki mikono
Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni
Hukaa na kujiuliza
I wapi raha yangu uiimwengu huu?
I wapi jamaa nzima ya wanawake?
MASWALI
(a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza
(b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
(c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata.
(d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili.
(e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili.
(f) Fafanua toni ya shairi hili.
(g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili.
(h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa.
(i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
(i) Madhila
(ii) Kudhalilishwa.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,
(Solved)
Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
1. Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,
Ondoka andama ndiya, nondosheya uso wako,
Ondoka wanisikiya, ziwate jeuri zako,
Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani?
2. Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri,
Haistahamilikii, uovu umekithiri,
Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri,
Sikati yako shari, enda zako wasiwasi.
3. Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha,
Viumbe na zao nyoyo, vitina kuwagotanisha,
Hiino ndio kaziyo, yenye kukufurahisha,
Ni kazi isiyokuchosha, mno umeizoeya.
4. Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani,
Ati mambo si mazuri, mambo yote tatashani,
Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini,
Nisononeke moyoni, upate kufurahika.
5. Au mara hunijiya, na kingine kisahani,
Kuhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani,
Huwa husishi nambiya, hali zao taabani,
Zingawa wakati gani? Ni zako au ni zao?
6. Na mara kuja mambiya, nitakapotoka humu,
Na kwamba yaningojea, nde maisha magumu,
Uliloni kusudiya, ni kunitiya wazimu,
Kama ndiyo yako hamu, basi unshatahayari.
(a) Eleza ujumbe uliojitokeza katika shairi hili.
(b) Fafanua muundo wa ubeti wa tatu.
(c) Eleza aina ya shairi hili.
(d) Fafanua arudhi za utunzi alizozingatia mshairi.
(e) Eleza toni ya mshairi.
(f) Andika ubeti wa tano katika lugha ya kinathari.
(g) Eleza mifano mitatu ya uhuru wa mshairi.
(h) Eleza maana ya misamiati ifuatayokama ilivyotumika katika shairi.
(i) ndiya
(ii) kisahani
(iii) nde
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
(Solved)
Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
1. Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
Asinywe yalo na vunju,
Yakampa kigegezi,
Yakamkibua roho akaona na kinyaa,
Awali ndio awali, awali mbovu hamna.
2. Kiwa utalimatia.
Utayaramba makombo,
Utadata vitu cheche,
Kisomo chenye dhamana kikakupa kisogo,
Inajuzu ujihimu
Mwanafuu darasani,
Urauka po mapema,
Katu hutayaramba makombo,
Hutakosa kisebeho.
3. Dereva hata utingo,
Natija ni asubuhi,
Wateja utawawahi,
Wasaa kuzingatia,
Uwafikishe kazini,
Kwa wasaa ufaao,
Wasije wakateteshwa,
Na bosi wao kazini,
Nao wakakuapiza.
4. Na ewe mwanazaraa,
Mpini uukamate,
Kabla jua kuwaka sana,
Majasho kutiririsha mwilini,
Yang‘oe yote magugu,
Kutoka kwa lako konde.
5. Mhadimu mwenye ajizi,
Yakujuza ujihimu,
Ununue na maziwa,
Majogoo uyawahi mapema,
Usije ukayadata,
Chai mkandaa ukaandaa,
Wateja wakuambae mithili ya ibilisi.
Maswali
(a) Eleza nasaha yoyote inayotolewa kwa wafanyakazi wowote watatu kwenye shairi.
(b) Taja sifa zozote za kimuundo zilizotumiwa na mtunzi.
(c) Eleza toni ya mshairi.
(d) Nafsi nenewa anahimizwa kufanya nini.
(e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi.
(f) Toa mifano miwili ya uhuru wa mshairi.
(g) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa kwenye shairi.
(i) Maji maenge
(ii) Natija
(iii) Majogoo
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili
(Solved)
Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
(Solved)
Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
(i) Kanda la usufi
(ii) Shaka ya mambo
(iii) Mwana wa darubini
(iv) Ndoa ya Samani.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Thibitisha jinsi anwani "Damu Nyeusi" inaafiki yaliyomo katika hadithi.
(Solved)
Thibitisha jinsi anwani "Damu Nyeusi" inaafiki yaliyomo katika hadithi.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Jadili matatizo KUMI ya kijamii ukirejelea hadithi "Mwana wa Darubini"
(Solved)
Jadili matatizo KUMI ya kijamii ukirejelea hadithi "Mwana wa Darubini"
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Riwaya ya kidagaa kimemwozea inaonyesha jitihada za vijana kujenga jamii mpya. Thibitisha kwa kutoa mifano
(Solved)
Riwaya ya kidagaa kimemwozea inaonyesha jitihada za vijana kujenga jamii mpya. Thibitisha kwa kutoa mifano
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Kwa kurejelea tamthilia ya Mstahiki Meya, fafanua vichocheo vya migogoro katika jamii ya Cheneo.
(Solved)
Kwa kurejelea tamthilia ya Mstahiki Meya, fafanua vichocheo vya migogoro katika jamii ya Cheneo.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Matambiko ni nini? Eleza dhima zake mbili.
(Solved)
Matambiko ni nini? Eleza dhima zake mbili.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Eleza maana ya maapizo.
(Solved)
Eleza maana ya maapizo.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Eleza maana ya ngoma katika fasihi simulizi kisha utoe dhima zake nne.
(Solved)
Eleza maana ya ngoma katika fasihi simulizi kisha utoe dhima zake nne.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Mtu mmoja alimpa mke wake nambari yake ya simu.
(Solved)
Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.
Mtu mmoja alimpa mke wake nambari yake ya simu. Kila mara bibi akipigia mumewe simu, ilipokelewa na sauti nyororo "mteja wa nambari uliopiga hapatikani kwa sasa."Alifunga safari kumtembelea mume wake mjini na kukabiliana na huyu kisura.
MASWALI
a) Bainisha kipera cha utungo huu.
b) Onyesha sifa tano za kipera hiki.
c) Eleza manufaa tano ya kipera hiki.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
a) Kanda la usufi ni anwani mwafaka.
Fafanua kwa kutolea mifano.
(b) Lini angepata nafasi ya kupenya kwenye chungio…"
Fafanua jinsi msemewa angepata nafasi na changamoto zake.
(Solved)
Kanda la Usufi - (R. Nyaga)
(a) Kanda la usufi ni anwani mwafaka.
Fafanua kwa kutolea mifano.
(b) Lini angepata nafasi ya kupenya kwenye chungio…"
Fafanua jinsi msemewa angepata nafasi na changamoto zake.
Date posted:
October 1, 2019
.
Answers (1)
-
Assumpta Matei: Chozi la Heri
Alijiona kama mfa maji ambaye anakabiliwa na mtutumo wa mawimbi ya misiba, mmoja baada ya mwingine.
(a) Bainisha muktadha wa dondoo hili....
(Solved)
Assumpta Matei: Chozi la Heri
Alijiona kama mfa maji ambaye anakabiliwa na mtutumo wa mawimbi ya misiba, mmoja baada ya mwingine.
(a) Bainisha muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza sifa tatu za anayerejelewa katika dondoo hili.
(c) Eleza tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili.
(d) Fafanua masaibu yaliyomkumba mrejelewa.
(e) Huku ukitolea mifano riwayani, jadili matatizo yanayowakumba wanajamii katika ndoa.
Date posted:
September 24, 2019
.
Answers (1)
-
Alifa chokocho na Dumu Kayanda: Tumbo Lisiloshiba
'Doa ndio kawaida inayobainisha maisha ya mwanadamu.'Onyesha ukweli wa kauli hii kwa mujibu wa hadithi za: Shogake Dada ana...
(Solved)
Alifa chokocho na Dumu Kayanda: Tumbo Lisiloshiba
'Doa ndio kawaida inayobainisha maisha ya mwanadamu.'Onyesha ukweli wa kauli hii kwa mujibu wa hadithi za: Shogake Dada ana Ndevu, Mame Bakari, Shibe Inatumaliza na Mtihani wa Maisha.
Date posted:
September 24, 2019
.
Answers (1)
-
Taja baadhi ya maudhui yanayojitokeza katika hadithi ya tumbo lisiloshiba?
(Solved)
Taja baadhi ya maudhui yanayojitokeza katika hadithi ya tumbo lisiloshiba?
Date posted:
September 18, 2019
.
Answers (1)
-
Taja mifano ya taswira katika hadithi ya tumbo lisiloshiba?
(Solved)
Taja mifano ya taswira katika hadithi ya tumbo lisiloshiba?
Date posted:
September 18, 2019
.
Answers (1)