Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
Maana: Mbinu hii hujitokeza wakati ambapo dalili Fulani hutokea kabla ya tukio Fulani.
Mifano:
- Tunamwona Meya akiwa ameinama chini akiwa ameshika tama. Hii inaweza kuashiria kusambaratika kwa uongozi wake/ pingamizi zinazomkabil kama kiongozi
- Tunamwona Meya akipanga mafaili yake pamoja ofisini. Hii inaweza kuashiri kule kujaribu kutafuta ufuasi kwa kuunda kamati barazani kuwatuza marrafikiye.
- Ndege zinazowabeba mameya wageni zinaelekezwa uwanje wan chi jirani. Inaashiria kule kuharibika kwa hali Cheneo- kuzorota kwa taasisi muhimu kama vile sekta ya mafuta, usafi nk.
- Propaganda na hila hazikubaiki tena ma umma kwa mfano kupitia nyimbo bandia za ?kizalendo?. Hii ni dalili za mwanzo wa mapinduzi.
- Harufu mbaya inayotokana uchafu mjini ni ishara ya mambo kwenda mrama. Hakuna mshahara, mafuta hakuna , kuna njaa.
- Meya anashindwa kunywa maji. Hii inashiria kushindwa kutekeleza wajibu wake. Kwa mfano kulipa mshahara, kusitisha ufisadi nk.
- Mayai madogo pia yanaweza kuashiria udunifu wa hali kama vile: umaskini umeenea, njaa, kiwango cha elimu kimeenda shule.
- Sauti za wafanyakazi ni ishara tosha ya kuwa wafanyakazi wamezinduka na wako tayari kutetea maslahi yao barabara.
- Kuwacha kazi kwa Waridi kunaweza kuashiria kuchoshwa na uongozi dhalimu wa Cheneo.
- Vifo vya wagonjwa vinaweza kuashiria ubovu au kusambaratika kwa taasisi muhimu za serikali kwa mfano sekta ya afya, elimu nk.
sharon kalunda answered the question on October 1, 2019 at 13:28
- Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.(Solved)
MSTAHIKI MEYA: Timothy Arege
Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua nafasi ya wanaorejelewa kuwa ―"walifanya vizuri kuja" katika tamthilia hii.
(c) Migogoro katika tamthilia hii hazikusuluhishwa vyema. Jadili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.(Solved)
Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?(Solved)
Kidagaa Kimemwozea:
"Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Dondoo hili linadokeza maudhui gani? Kwa kutoa mifano saba kwenye riwaya, bainisha jinsi maudhui hayo yanavyojitokeza.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"(Solved)
Kanda la Usufi
"Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Taja na kueleza tamathali ya usemi kwenye dondoo hili.
(c) Kwa kutolea mifano, onyesha jinsi anwani Kanda la Usufi inavyoafiki hadithi husika.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"(Solved)
Damu Nveusi na Hadithi nyingine
"………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Thibitisha ufaafu wa anwani ya hadithi hii.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Elimu imeshindwa kutimiza lengo la kuwapa vijana uwezo wa kukabiliana na maisha ya kisasa. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo.(Solved)
Elimu imeshindwa kutimiza lengo la kuwapa vijana uwezo wa kukabiliana na maisha ya kisasa. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
(a) Mke wangu
(b) Samaki wanchi zajoto
(c) Damu nyeusi.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake .
(b) Eleza tamathali mbili zilizotumika katika dondoo hili.
(c) Eleza aina za kiu na njaa zilizomkumba mrejelewa wa kwanza.
(d) Mrejelewa wa pili alishindwa mtihani wa maisha. Jadili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Kuvunjwa kwa haki na sheria lilikuwa jambo la kawaida chini ya uongozi wa Mtemi Nasaba bora. Thibitisha ukweli wa Kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa...(Solved)
Kuvunjwa kwa haki na sheria lilikuwa jambo la kawaida chini ya uongozi wa Mtemi Nasaba bora. Thibitisha ukweli wa Kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa kimemwozea.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Duniani kuna watu na viatu"(Solved)
Tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
"Duniani kuna watu na viatu"
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.(Solved)
Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.
(i) Diwani wa tatu
(ii) Bili
(iii) Mhubiri
(iv) Diwani I na II
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Kila nikaapo hushika tama.(Solved)
Kila nikaapo hushika tama
Na kuwazia hali inayonizunguka.
Huyawazia madhila
Huziwazia shida
Huiwazia dhiki
Dhiki ya ulezi
Shida ya kudhalilishwa kazini.
Madhila ya kufanyiwa dharau
Kwa sababu ya jinsia ya kike.
Hukaa na kujidadisi
Hujidadisi kujua kwa nini
Jamii haikisikii kilio changu
Wenzangu hawanishiki mikono
Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni
Hukaa na kujiuliza
I wapi raha yangu uiimwengu huu?
I wapi jamaa nzima ya wanawake?
MASWALI
(a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza
(b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
(c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata.
(d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili.
(e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili.
(f) Fafanua toni ya shairi hili.
(g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili.
(h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa.
(i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
(i) Madhila
(ii) Kudhalilishwa.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,(Solved)
Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
1. Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,
Ondoka andama ndiya, nondosheya uso wako,
Ondoka wanisikiya, ziwate jeuri zako,
Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani?
2. Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri,
Haistahamilikii, uovu umekithiri,
Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri,
Sikati yako shari, enda zako wasiwasi.
3. Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha,
Viumbe na zao nyoyo, vitina kuwagotanisha,
Hiino ndio kaziyo, yenye kukufurahisha,
Ni kazi isiyokuchosha, mno umeizoeya.
4. Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani,
Ati mambo si mazuri, mambo yote tatashani,
Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini,
Nisononeke moyoni, upate kufurahika.
5. Au mara hunijiya, na kingine kisahani,
Kuhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani,
Huwa husishi nambiya, hali zao taabani,
Zingawa wakati gani? Ni zako au ni zao?
6. Na mara kuja mambiya, nitakapotoka humu,
Na kwamba yaningojea, nde maisha magumu,
Uliloni kusudiya, ni kunitiya wazimu,
Kama ndiyo yako hamu, basi unshatahayari.
(a) Eleza ujumbe uliojitokeza katika shairi hili.
(b) Fafanua muundo wa ubeti wa tatu.
(c) Eleza aina ya shairi hili.
(d) Fafanua arudhi za utunzi alizozingatia mshairi.
(e) Eleza toni ya mshairi.
(f) Andika ubeti wa tano katika lugha ya kinathari.
(g) Eleza mifano mitatu ya uhuru wa mshairi.
(h) Eleza maana ya misamiati ifuatayokama ilivyotumika katika shairi.
(i) ndiya
(ii) kisahani
(iii) nde
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
(Solved)
Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
1. Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
Asinywe yalo na vunju,
Yakampa kigegezi,
Yakamkibua roho akaona na kinyaa,
Awali ndio awali, awali mbovu hamna.
2. Kiwa utalimatia.
Utayaramba makombo,
Utadata vitu cheche,
Kisomo chenye dhamana kikakupa kisogo,
Inajuzu ujihimu
Mwanafuu darasani,
Urauka po mapema,
Katu hutayaramba makombo,
Hutakosa kisebeho.
3. Dereva hata utingo,
Natija ni asubuhi,
Wateja utawawahi,
Wasaa kuzingatia,
Uwafikishe kazini,
Kwa wasaa ufaao,
Wasije wakateteshwa,
Na bosi wao kazini,
Nao wakakuapiza.
4. Na ewe mwanazaraa,
Mpini uukamate,
Kabla jua kuwaka sana,
Majasho kutiririsha mwilini,
Yang‘oe yote magugu,
Kutoka kwa lako konde.
5. Mhadimu mwenye ajizi,
Yakujuza ujihimu,
Ununue na maziwa,
Majogoo uyawahi mapema,
Usije ukayadata,
Chai mkandaa ukaandaa,
Wateja wakuambae mithili ya ibilisi.
Maswali
(a) Eleza nasaha yoyote inayotolewa kwa wafanyakazi wowote watatu kwenye shairi.
(b) Taja sifa zozote za kimuundo zilizotumiwa na mtunzi.
(c) Eleza toni ya mshairi.
(d) Nafsi nenewa anahimizwa kufanya nini.
(e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi.
(f) Toa mifano miwili ya uhuru wa mshairi.
(g) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa kwenye shairi.
(i) Maji maenge
(ii) Natija
(iii) Majogoo
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.(Solved)
Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Huu ni ukoloni mamboleo"(Solved)
Mstahiki Meya
"Huu ni ukoloni mamboleo"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza umuhimu wa msemewa katika tamthilia hii.
(c) Jadili namna ukoloni mamboleo unavyojitokeza katika tamthilia.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili(Solved)
Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Kwa nini mnaifunga mnyororo ile doggy mgonjwa? Mbona msiiwache free".(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Kwa nini mnaifunga mnyororo ile doggy mgonjwa? Mbona msiiwache free".
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Onyesha jinsi wahusika riwayani wamefungwa minyororo.
(c) Minyororo inayorejelewa katika (b) hapo juu ilifunguliwaje?
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo. (Solved)
Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
(i) Kanda la usufi
(ii) Shaka ya mambo
(iii) Mwana wa darubini
(iv) Ndoa ya Samani.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Wafrika hupitia changamoto nyingi sana wakiwa masomoni ughaibuni. Thibitisha kauli hii ukirejelea hadithi "Damu nyeusi"(Solved)
Wafrika hupitia changamoto nyingi sana wakiwa masomoni ughaibuni. Thibitisha kauli hii ukirejelea hadithi "Damu nyeusi"
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Kero hizi na dharau zinamfanya kuthamini zaidi utu wake ....."Ukirejelea hadithi "Damu nyeusi" Eleza muktadha wa dondoo hili.(Solved)
"Kero hizi na dharau zinamfanya kuthamini zaidi utu wake ....."Ukirejelea hadithi "Damu nyeusi" Eleza muktadha wa dondoo hili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)