Miaka 15 iliyopita, Umoja wa Mataifa uliitangaza August 12 kila mwaka,

      

Soma makala yafuatao kisha ujibu maswali yanayofuata.
Miaka 15 iliyopita, Umoja wa Mataifa uliitangaza August 12 kila mwaka, kuwa Siku ya Vijana Duniani‘ ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Vijana na Afya ya Akili‘. Kwa mujibu wa andiko kutoka Umoja wa Mataifa, asilimia 20 ya vijana duniani kote hupata tatizo linalohusiana na afya ya akili kila mwaka. Hatari zaidi hutokea katika kipindi cha kuhama kutoka utoto kuingia utu uzima. Kutengwa pamoja na aibu mara nyingi huongeza zaidi tatizo kwa kuwa vijana wengine hushindwa kutafuta msaada wanaouhitaji. Hivyo mwaka huu, Umoja wa Mataifa umeazimia kuitumia siku hii kukuza uelewa kuhusu afya ya akili kwa vijana. Wakati tunaadhimisha Siku ya Vijana Duniani 2014, tuwawezeshe vijana wenye matatizo ya afya ya akili kubaini umuhimu wao, na tuoneshe kuwa afya ya akili inatuhusu sote, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Maitafa, Ban Ki Moon kwenye maelezo yake. Miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia tatizo la afya ya akili ni umaskini unaochangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa ajira. Asimilia kubwa ya vijana walio chini ya miaka 25 au wale wanaohitimu masomo yao nchini hawana ajira. Wanachuo wengi wameendelea kuzunguka huku na kule kuomba kazi bila mafanikio. Wengi wamekaa zaidi ya miaka mitatu nyumbani tangu wamalize masomo yao bila kuwa na ajira inayowaingizia kipato. Na pia wachache wanaopata kazi, wamekuwa wakilipwa ujira mdogo na hivyo kuendelea kuishi maisha magumu. Ukosefu wa ajira na kukosa fedha za kujikimu, umewafanya vijana wengi kuwa na msongo wa mawazo, tatizo kubwa linalohusiana na afya ya akili. Tatizo ni kubwa zaidi pale ambapo takwimu zinaonesha kuwa kwa wastani soko la ajira nchini lina uwezo wa kuzalisha ajira zipatazo 300,000 kwa mwaka katika sekta rasmi ukilinganisha na wastani wa wahitimu 600,000 hadi 800,000 wanaoingia katika soko la ajira nchini. Kwa kijana ambaye hana mahali pa kuishi, hajui atakula nini kesho, hana fedha za kununua nguo, kukata tamaa na kuamua kufanya lolote si kitu anachoweza kukifikiria mara mbili. Kwa vijana wa kiume wapo wanaoamua kuwa wezi au matapeli huku wengine wakijikuta wakiwa walevi wa kutupwa au kuvuta unga kama njia ya kupunguza msongo wa mawazo unaotokana na maisha magumu.Utumiaji wa vilevi hivyo, umechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza tatizo la afya ya akili kwa vijana wengine. Kwa wasichana, ukosefu wa ajira, huwaingiza wengi katika wimbi la kutumia miili yao kujipatia kipato kutoka kwa wanaume. Wengine hujikuta wakiolewa mapema na hivyo kupoteza ndoto za kujiendeleza kielimu ili kujitegemea. Mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini kwakuwa wasichana wadogo huzalishwa katika umri mdogo na wengine kukumbana na unyanyasaji wa nyumbani kutoka kwa waume zao.Katika maeneo ya vijijini ambako shughuli kubwa ya kiuchumi ni kilimo, ufugaji au uvuvi, baadhi ya wasichana waliolewa, hujikuta wakiachiwa familia zao kwa muda mrefu na waume zao wanaoenda kutafuta maisha. Baadhi ya wanaume hao huondoka kimoja na kuwaachia wake mzigo wa ulezi wa familia. Hivyo, tatizo kubwa la ajira kwa vijana lipo kwa wale ambao hawana elimu ya kutosha kustahili kuajiriwa katika ajira rasmi. Kwa mujibu wa survey iliyofanywa na Restless Development, Tanzania ina takriban watu milioni 25 walio chini ya miaka 25 nchini. Hiyo ina maana kuwa karibu nusu ya watu wote nchini ni vijana.
Dunia nzima, vijana wamekuwa wakitambulika kwa kuwa na mchango mkubwa kuanzia katika upatikanaji wa uhuru enzi za ukoloni hadi katika kuvumbua teknolojia mpya na kugundua njia mpya za sanaa na muziki. Vijana ndio wanaolisukuma zaidi gurudumu la maendeleo kwa uchapakazi wao kutokana na miili na akili zao kuwa na uchangamfu zaidi. Hata hivyo Tanzania ni nchi iliyo na matabaka yanayotokana na umri na jinsia huku vijana wakioneana kutopewa fursa katika mchakato wa maamuzi katika hatua za kijamii na hata katika serikali. Ili kuwapa nafasi zaidi vijana katika nafasi za juu za maamuzi, vijana wanapaswa kutambua kuwa huu ndio wakati wao na sio kesho. Vijana wanatakiwa kwanza kujiamini wao wenyewe kuwa hakuna nafasi ya baadaye kwakuwa huu ndio wakati unaowaruhusu kuwa wabunifu zaidi kushawishi maendeleo. Mawazo yao mapya na njia zao tofauti za kukabiliana na mambo, yataleta utofauti mkubwa wa sera, maamuzi na muelekeo wa serikali au taasisi mbalimbali. ―Uongozi wa kizazi kipya upo tayari kushika hatamu za uongozi na kuijenga Tanzania mpya, kwa fikra mpya na maarifa mapya. Mabadiliko, kokote yalikotokea, yalidaiwa na kuongozwa na vijana. Vijana wa Tanzania washike usukani wa kuleta mabadiliko wanayoyataka. Ukiona kijana anamwambia kijana mwenzake hana uzoefu, basi kazi ya kuleta mabadiliko ni kubwa zaidi. Kutokuwa na uzoefu ni sifa ya kijana. Tusi kubwa kwa Obama mwaka 2008 lilikuwa ni kukosa uzoefu, kukosa rekodi. Tusi hilo lilikuwa muziki kwa wapiga kura wa Marekani. Tanzania mpya inahitaji viongozi wapya, mazoea mapya, fikra mpya na maarifa mapya. Inahitaji kuthubutu mambo makubwa sio kulinda uzoefu wa nyuma. Tunaweza, aliandika January Makamba kwenye mtandao wa Facebook. Ni kweli muda wa vijana ni sasa na sio kesho tena.

Maswali
(a) Ipe makala hii anwani mwafaka.
(b) Ni wakati gani ambapo vijana huwa hatarini sana kukumbwa na tatizo la afya ya akilini.
c) Ni nini lengo la Umoja wa Mataifa mwaka huu kuhusu vijana?
d) Taja changamoto zinazowakumba vijana wenye matatizo ya afya ya akili.
e) Eleza mambo ambayo huchangia matatizo ya afya ya akili miongoni mwa vijana.
f) Taja mambo ambayo huchangia kutamauka kwa vijana.
g) Ukosefu wa ajira umechangia uozo upi miongoni mwa vijana?

  

Answers


sharon
a)
Vijana na afya ya jamii.
b)
Kipindi cha kuhama kutoka utoto kuingia utu uzima.
c)
Kukuza uelewa kuhusu afya ya akili ya vijana.
d)
Kutengwa
Aibu
e)
Ukosefu wa ajira.
Mshahara mdogo.
Umaskini.
Dawa za kulevya.
f)
Kukosa mahali pa kuishi.
Kukosa chakula.
Ukosefu wa mavazi.
g)
Wasichana kutumia miili yao kujipatia mapato.
Vijana wa kiume kuwa wezi.
Kushiriki ulevi.
sharon kalunda answered the question on October 2, 2019 at 07:25


Next: What are the reasons that made Jewish leaders to rise against Jesus?.
Previous: Explain Traditional African use of beer.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions