Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Bainisha aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.

Bainisha aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.
Kuimba kwa Yusufu kunaudhi

Answers


sharon
Nomino ya kitenzi – jina
sharon kalunda answered the question on October 2, 2019 at 07:42

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Akifika sentensi ifuatayo kwa kutumia alama ya kibainishi kisha eleza matumizi yake. Ntakwenda Unguja mwezi wa Disemba (Solved)

    Akifika sentensi ifuatayo kwa kutumia alama ya kibainishi kisha eleza matumizi yake.
    Ntakwenda Unguja mwezi wa Disemba

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika kauli iliyo mabanoni. Paka analamba mchuzi (kutendwa) (Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika kauli iliyo mabanoni.
    Paka analamba mchuzi (kutendwa)

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Inaaminika kuwa majeruhi wengi katika mikasa ya ajali huaga au huathirika vibaya zaidi kutokana na hali mbaya ya uokoaji. (Solved)

    Utoaji wa Huduma ya Kwanza.

    Inaaminika kuwa majeruhi wengi katika mikasa ya ajali huaga au huathirika vibaya zaidi kutokana na hali mbaya ya uokoaji. Watu wengi ambao hujitolea kuokoa majeruhi baada ya ajali kama za barabarani, maporomoko ya ardhi au nyumba huwa hawang‘amui hata chembe jinsi ya kukabiliana na uokoaji. Hatima ya juhudi zao ambazo hulenga kutenda mema ni kuathirika zaidi kwa majeruhi.
    Hali ya ukoaji inaweza kurekebishwa kwa kutoa elimu ya huduma ya kwanza kwa umma. Elimu hii yahitajika na kila Mkenya kwani mikasa ya ajali za barabarani na nyinginezo inaendelea kutokea kila siku.Ajali zinapotokea, si ajabu kuona makundi ya waokoaji yakibeba majeruhi hobelahobela bila kuzingatia madhara yanayoweza kuwaongezea kutokana na ubebaji wao. Kutojua namna ya kumbeba majeruhi kunaweza kumhatarisha na hata kusababisha kifo.
    Kuna mambo mbalimbali ambayo makundi ya waokoaji yanatakiwa kuzingatia wakati yanatoa huduma ya kuokoa. Kwanza, ni muhimu kuchunguza kama kuna hatari yoyote inayoweza ikatokea na kuwatia majeruhi na waokoaji hatarini zaidi. Makundi ya waokoaji yameweza kuhatarisha majeruhi kwa kuliingilia eneo la ajali mbumbumbu kama mzungu wa reli.
    Hatua ya pili ni kutafuta idadi ya majeruhi. Pana uwezekano wa majeruhi kutupwa mbali na eneo la ajali. Vivyo hivyo, kuna majeruhi ambao huweweseka baada ya ajali na kuanza kutembea wasijue wanakoelekea. Wengi wao huanguka karibu na eneo la ajali au wakaenda mbali.
    Hatua ya tatu ni kuchunguza kama majeruhi amezimia, moyo unapiga na jinsi anavyopumua. Ili kuhakikisha kuwa majeruhi anapumua, mwokoaji atazame kama kifua kinapanda na kushuka. Halikadhalika, mwokoaji anaweza kusikiliza au kuguza kifua na kuona kama kuna ishara za kupumua. Iwapo majeruhi anapumua, mwokoaji amweke katika hali ambayo itaimarisha kupumua kwake. Anaweza akamlaza chali au kumgeuza kwa pamoja na kichwa chake ili kufungua mkondo wa hewa. Pia, mwokoaji ahakikishe hamna chochote kinywani kinachoweza kumsakama. Ikiwa hapumui, mwokoaji anaweza kujaribu kumfanya apumue kwa kupuliza hewa mdomoni mwake. Fauka ya hayo, upulizaji wa hewa utahakikisha kuwa damu inazunguka mwilini vizuri.
    Maswali :
    (a) Fupisha aya mbili za kwanza kwa maneno 55 – 65.
    (b) Eleza kwa kutumia maneno 90-100, hatua zinazotakiwa kufuatwa wakati wa uokoaji.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Zitavuma, Zitakoma, Nitakwima, Mti-mle. (Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Zitavuma,
    Zitakoma,
    Nitakwima,
    Mti-mle.

    Na muda nikisimama,
    Nitatongoa nudhuma,
    Kwa tenzi zilizo njema,
    Nilisifu mti – mle.

    Tazipanga tathlitha, tungo zilizo na hekima,
    Za huba na thiatha, za kuburudi mitima,
    Mashairi mabuthutha, musome mnaosoma.

    Mti nishainukia,namea kuwa mzima,
    Mizizi yadidimia, ardhini imeuma,
    Nanena kitarbia, tungo zilizo adhama
    Japo ni tungo za zama, mti-mle hutumia.

    Zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,
    Dharuba kinitikisa, mti-mle huinama,
    Huyumba nikaziasa, matawi yakakingama,
    Gharika ikishapisa, hurudi nikawa wima,
    Na tungo za takhimisa, mti-mle huzipima.

    Maswali
    (1) Shairi hili ni la kimapokea. Toa sababu mbili kuunga kauli hii.
    (2) Taja bahari kuu ya ushairi ambayo imetumiwa na mshairi. Fafanua.
    (3) Fafanua dhamira ya mshairi.
    (4) Kwa kutoa mifano bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili.
    (5) Eleza jinsi mshairi ametumia idhini ya ushairi katika utungo huu.
    (6) Andika ubeti wa nne kwa lugha natharia.
    (7) Mshairi anamaanisha nini anaposema "zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,"
    (8) Eleza toni ya shairi hili.
    (9) Eleza maana ya msamiati ufuatao.
    i) Nitatongoa
    ii) Zitapusa.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza matatizo yanayomkabili mtu anapoitumia lugha yoyote isipokuwa ile ya kwanza. (Solved)

    Eleza matatizo yanayomkabili mtu anapoitumia lugha yoyote isipokuwa ile ya kwanza.

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Fafanua mambo matano yanaosababisha kutokea kwa lahaja. (Solved)

    Fafanua mambo matano yanaosababisha kutokea kwa lahaja.

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Andika kwa wingi. Mimi ndimi shangazi yake. (Solved)

    Andika kwa wingi.
    Mimi ndimi shangazi yake.

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Andika katika hali ya udogo: Mvulana yule alibeba kiti kikubwa (Solved)

    Andika katika hali ya udogo:
    Mvulana yule alibeba kiti kikubwa

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Taja sauti zinazotamkiwa kwenye ufizi. (Solved)

    Taja sauti zinazotamkiwa kwenye ufizi.

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha vishazi tegemezi na vishazi huru katika sentensi ifuatayo. Nilimwona Agwambo nilipofika Mombasa (Solved)

    Onyesha vishazi tegemezi na vishazi huru katika sentensi ifuatayo.
    Nilimwona Agwambo nilipofika Mombasa

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia viunganishi hivi vya kinyume Ingawaje, ila (Solved)

    Tunga sentensi ukitumia viunganishi hivi vya kinyume Ingawaje, ila

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi moja ili kudhihirisha matumizi ya viwakifishi hivi: i)Semi koloni ii)Mshazari (Solved)

    Tunga sentensi moja ili kudhihirisha matumizi ya viwakifishi hivi:
    i)Semi koloni
    ii)Mshazari

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Kanusha katika wingi. Alikuarifu kuhusu yule hajala. (Solved)

    Kanusha katika wingi.
    Alikuarifu kuhusu yule hajala.

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Unganisha sentensi hizi kwa kutumia kirejeshi cha kati. (i) Kalamu imeibwa (ii) Kalamu ni yangu (Solved)

    Unganisha sentensi hizi kwa kutumia kirejeshi cha kati.
    (i) Kalamu imeibwa
    (ii) Kalamu ni yangu

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Unda nomino mbili kutokana na kitenzi arifu. (Solved)

    Unda nomino mbili kutokana na kitenzi arifu.

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Ainisha viambishi katika neno lifuatalo: aliyelima (Solved)

    Ainisha viambishi katika neno lifuatalo: aliyelima

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi yenye kiingizi na kihusishi cha mahali. (Solved)

    Tunga sentensi yenye kiingizi na kihusishi cha mahali.

    Date posted: September 26, 2019 .    Answers (1)

  • Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano. i) twaa (kutendeka) ii) Kosa (Kutendesha) iii) Cha (Kutendwa) (Solved)

    Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano.
    i) twaa (kutendeka)
    ii) Kosa (Kutendesha)
    iii) Cha (Kutendwa)

    Date posted: September 26, 2019 .    Answers (1)

  • Maneno haya yamo katika ngeli gani? i) Fagio ii) Nyigu (Solved)

    Maneno haya yamo katika ngeli gani?
    i) Fagio
    ii) Nyigu

    Date posted: September 26, 2019 .    Answers (1)

  • Ngeli ni nini? (Solved)

    Ngeli ni nini?

    Date posted: September 26, 2019 .    Answers (1)