Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
-Vyangu ni kivumishi kimililishi.
-Vyenyewe ni kivumishi cha pekee.
sharon kalunda answered the question on October 2, 2019 at 08:08
- Tambua aina ya chagizo katika sentensi ifuatayo.
Walimu wataenda Mombasa Ijumaa ijayo.(Solved)
Tambua aina ya chagizo katika sentensi ifuatayo.
Walimu wataenda Mombasa Ijumaa ijayo.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Ikarabati sentensi hii:
Mpira yangu amepotea (Solved)
Ikarabati sentensi hii:
Mpira yangu amepotea
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Tambua viambishi awali na tamati katika neno ajaye(Solved)
Tambua viambishi awali na tamati katika neno ajaye
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Maneno yafuatayo yako katika ngeli gani.
Kero.
Nywele.(Solved)
Maneno yafuatayo yako katika ngeli gani.
Kero.
Nywele.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Eleza matumizi ya ku katika jozi zifuatazo za sentensi.(Solved)
Eleza matumizi ya ku katika jozi zifuatazo za sentensi.
(i) Kuchora kwao kulikuwa kwa uangalifu mkubwa
(ii) Nilikuita lakini hukuitika
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi ifuatayo katika umoja.
Manukato haya yananukia vizuri(Solved)
Andika sentensi ifuatayo katika umoja.
Manukato haya yananukia vizuri
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Bainisha aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.(Solved)
Bainisha aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.
Kuimba kwa Yusufu kunaudhi
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Akifika sentensi ifuatayo kwa kutumia alama ya kibainishi kisha eleza matumizi yake.
Ntakwenda Unguja mwezi wa Disemba(Solved)
Akifika sentensi ifuatayo kwa kutumia alama ya kibainishi kisha eleza matumizi yake.
Ntakwenda Unguja mwezi wa Disemba
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi ifuatayo katika kauli iliyo mabanoni.
Paka analamba mchuzi (kutendwa)(Solved)
Andika sentensi ifuatayo katika kauli iliyo mabanoni.
Paka analamba mchuzi (kutendwa)
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Inaaminika kuwa majeruhi wengi katika mikasa ya ajali huaga au huathirika vibaya zaidi kutokana na hali mbaya ya uokoaji.(Solved)
Utoaji wa Huduma ya Kwanza.
Inaaminika kuwa majeruhi wengi katika mikasa ya ajali huaga au huathirika vibaya zaidi kutokana na hali mbaya ya uokoaji. Watu wengi ambao hujitolea kuokoa majeruhi baada ya ajali kama za barabarani, maporomoko ya ardhi au nyumba huwa hawang‘amui hata chembe jinsi ya kukabiliana na uokoaji. Hatima ya juhudi zao ambazo hulenga kutenda mema ni kuathirika zaidi kwa majeruhi.
Hali ya ukoaji inaweza kurekebishwa kwa kutoa elimu ya huduma ya kwanza kwa umma. Elimu hii yahitajika na kila Mkenya kwani mikasa ya ajali za barabarani na nyinginezo inaendelea kutokea kila siku.Ajali zinapotokea, si ajabu kuona makundi ya waokoaji yakibeba majeruhi hobelahobela bila kuzingatia madhara yanayoweza kuwaongezea kutokana na ubebaji wao. Kutojua namna ya kumbeba majeruhi kunaweza kumhatarisha na hata kusababisha kifo.
Kuna mambo mbalimbali ambayo makundi ya waokoaji yanatakiwa kuzingatia wakati yanatoa huduma ya kuokoa. Kwanza, ni muhimu kuchunguza kama kuna hatari yoyote inayoweza ikatokea na kuwatia majeruhi na waokoaji hatarini zaidi. Makundi ya waokoaji yameweza kuhatarisha majeruhi kwa kuliingilia eneo la ajali mbumbumbu kama mzungu wa reli.
Hatua ya pili ni kutafuta idadi ya majeruhi. Pana uwezekano wa majeruhi kutupwa mbali na eneo la ajali. Vivyo hivyo, kuna majeruhi ambao huweweseka baada ya ajali na kuanza kutembea wasijue wanakoelekea. Wengi wao huanguka karibu na eneo la ajali au wakaenda mbali.
Hatua ya tatu ni kuchunguza kama majeruhi amezimia, moyo unapiga na jinsi anavyopumua. Ili kuhakikisha kuwa majeruhi anapumua, mwokoaji atazame kama kifua kinapanda na kushuka. Halikadhalika, mwokoaji anaweza kusikiliza au kuguza kifua na kuona kama kuna ishara za kupumua. Iwapo majeruhi anapumua, mwokoaji amweke katika hali ambayo itaimarisha kupumua kwake. Anaweza akamlaza chali au kumgeuza kwa pamoja na kichwa chake ili kufungua mkondo wa hewa. Pia, mwokoaji ahakikishe hamna chochote kinywani kinachoweza kumsakama. Ikiwa hapumui, mwokoaji anaweza kujaribu kumfanya apumue kwa kupuliza hewa mdomoni mwake. Fauka ya hayo, upulizaji wa hewa utahakikisha kuwa damu inazunguka mwilini vizuri.
Maswali :
(a) Fupisha aya mbili za kwanza kwa maneno 55 – 65.
(b) Eleza kwa kutumia maneno 90-100, hatua zinazotakiwa kufuatwa wakati wa uokoaji.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Miaka 15 iliyopita, Umoja wa Mataifa uliitangaza August 12 kila mwaka,(Solved)
Soma makala yafuatao kisha ujibu maswali yanayofuata.
Miaka 15 iliyopita, Umoja wa Mataifa uliitangaza August 12 kila mwaka, kuwa Siku ya Vijana Duniani‘ ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Vijana na Afya ya Akili‘. Kwa mujibu wa andiko kutoka Umoja wa Mataifa, asilimia 20 ya vijana duniani kote hupata tatizo linalohusiana na afya ya akili kila mwaka. Hatari zaidi hutokea katika kipindi cha kuhama kutoka utoto kuingia utu uzima. Kutengwa pamoja na aibu mara nyingi huongeza zaidi tatizo kwa kuwa vijana wengine hushindwa kutafuta msaada wanaouhitaji. Hivyo mwaka huu, Umoja wa Mataifa umeazimia kuitumia siku hii kukuza uelewa kuhusu afya ya akili kwa vijana. Wakati tunaadhimisha Siku ya Vijana Duniani 2014, tuwawezeshe vijana wenye matatizo ya afya ya akili kubaini umuhimu wao, na tuoneshe kuwa afya ya akili inatuhusu sote, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Maitafa, Ban Ki Moon kwenye maelezo yake. Miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia tatizo la afya ya akili ni umaskini unaochangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa ajira. Asimilia kubwa ya vijana walio chini ya miaka 25 au wale wanaohitimu masomo yao nchini hawana ajira. Wanachuo wengi wameendelea kuzunguka huku na kule kuomba kazi bila mafanikio. Wengi wamekaa zaidi ya miaka mitatu nyumbani tangu wamalize masomo yao bila kuwa na ajira inayowaingizia kipato. Na pia wachache wanaopata kazi, wamekuwa wakilipwa ujira mdogo na hivyo kuendelea kuishi maisha magumu. Ukosefu wa ajira na kukosa fedha za kujikimu, umewafanya vijana wengi kuwa na msongo wa mawazo, tatizo kubwa linalohusiana na afya ya akili. Tatizo ni kubwa zaidi pale ambapo takwimu zinaonesha kuwa kwa wastani soko la ajira nchini lina uwezo wa kuzalisha ajira zipatazo 300,000 kwa mwaka katika sekta rasmi ukilinganisha na wastani wa wahitimu 600,000 hadi 800,000 wanaoingia katika soko la ajira nchini. Kwa kijana ambaye hana mahali pa kuishi, hajui atakula nini kesho, hana fedha za kununua nguo, kukata tamaa na kuamua kufanya lolote si kitu anachoweza kukifikiria mara mbili. Kwa vijana wa kiume wapo wanaoamua kuwa wezi au matapeli huku wengine wakijikuta wakiwa walevi wa kutupwa au kuvuta unga kama njia ya kupunguza msongo wa mawazo unaotokana na maisha magumu.Utumiaji wa vilevi hivyo, umechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza tatizo la afya ya akili kwa vijana wengine. Kwa wasichana, ukosefu wa ajira, huwaingiza wengi katika wimbi la kutumia miili yao kujipatia kipato kutoka kwa wanaume. Wengine hujikuta wakiolewa mapema na hivyo kupoteza ndoto za kujiendeleza kielimu ili kujitegemea. Mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini kwakuwa wasichana wadogo huzalishwa katika umri mdogo na wengine kukumbana na unyanyasaji wa nyumbani kutoka kwa waume zao.Katika maeneo ya vijijini ambako shughuli kubwa ya kiuchumi ni kilimo, ufugaji au uvuvi, baadhi ya wasichana waliolewa, hujikuta wakiachiwa familia zao kwa muda mrefu na waume zao wanaoenda kutafuta maisha. Baadhi ya wanaume hao huondoka kimoja na kuwaachia wake mzigo wa ulezi wa familia. Hivyo, tatizo kubwa la ajira kwa vijana lipo kwa wale ambao hawana elimu ya kutosha kustahili kuajiriwa katika ajira rasmi. Kwa mujibu wa survey iliyofanywa na Restless Development, Tanzania ina takriban watu milioni 25 walio chini ya miaka 25 nchini. Hiyo ina maana kuwa karibu nusu ya watu wote nchini ni vijana.
Dunia nzima, vijana wamekuwa wakitambulika kwa kuwa na mchango mkubwa kuanzia katika upatikanaji wa uhuru enzi za ukoloni hadi katika kuvumbua teknolojia mpya na kugundua njia mpya za sanaa na muziki. Vijana ndio wanaolisukuma zaidi gurudumu la maendeleo kwa uchapakazi wao kutokana na miili na akili zao kuwa na uchangamfu zaidi. Hata hivyo Tanzania ni nchi iliyo na matabaka yanayotokana na umri na jinsia huku vijana wakioneana kutopewa fursa katika mchakato wa maamuzi katika hatua za kijamii na hata katika serikali. Ili kuwapa nafasi zaidi vijana katika nafasi za juu za maamuzi, vijana wanapaswa kutambua kuwa huu ndio wakati wao na sio kesho. Vijana wanatakiwa kwanza kujiamini wao wenyewe kuwa hakuna nafasi ya baadaye kwakuwa huu ndio wakati unaowaruhusu kuwa wabunifu zaidi kushawishi maendeleo. Mawazo yao mapya na njia zao tofauti za kukabiliana na mambo, yataleta utofauti mkubwa wa sera, maamuzi na muelekeo wa serikali au taasisi mbalimbali. ―Uongozi wa kizazi kipya upo tayari kushika hatamu za uongozi na kuijenga Tanzania mpya, kwa fikra mpya na maarifa mapya. Mabadiliko, kokote yalikotokea, yalidaiwa na kuongozwa na vijana. Vijana wa Tanzania washike usukani wa kuleta mabadiliko wanayoyataka. Ukiona kijana anamwambia kijana mwenzake hana uzoefu, basi kazi ya kuleta mabadiliko ni kubwa zaidi. Kutokuwa na uzoefu ni sifa ya kijana. Tusi kubwa kwa Obama mwaka 2008 lilikuwa ni kukosa uzoefu, kukosa rekodi. Tusi hilo lilikuwa muziki kwa wapiga kura wa Marekani. Tanzania mpya inahitaji viongozi wapya, mazoea mapya, fikra mpya na maarifa mapya. Inahitaji kuthubutu mambo makubwa sio kulinda uzoefu wa nyuma. Tunaweza, aliandika January Makamba kwenye mtandao wa Facebook. Ni kweli muda wa vijana ni sasa na sio kesho tena.
Maswali
(a) Ipe makala hii anwani mwafaka.
(b) Ni wakati gani ambapo vijana huwa hatarini sana kukumbwa na tatizo la afya ya akilini.
c) Ni nini lengo la Umoja wa Mataifa mwaka huu kuhusu vijana?
d) Taja changamoto zinazowakumba vijana wenye matatizo ya afya ya akili.
e) Eleza mambo ambayo huchangia matatizo ya afya ya akili miongoni mwa vijana.
f) Taja mambo ambayo huchangia kutamauka kwa vijana.
g) Ukosefu wa ajira umechangia uozo upi miongoni mwa vijana?
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Eleza jinsi mbinu ya kwelikinzani imetumika kwa kurejelea riwaya ya "kidagaa kimemwozea".(Solved)
Eleza jinsi mbinu ya kwelikinzani imetumika kwa kurejelea riwaya ya "kidagaa kimemwozea".
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Mwafulani 1: Nilikusahau lini ndiyo sasa nije kukusahau?......
Mwafulani II: …..tusikie.(Solved)
Tamthilia "Mstahiki Meya"
Mwafulani 1: Nilikusahau lini ndiyo sasa nije kukusahau?......
Mwafulani II: …..tusikie.
(a) Eleza muktahda wa dondoo hili.
(b) Bainisha mbinu ya lugha inayojitokeza katika dondoo hili.
(c) Fafanua mambo yoyote manne yanayo zungumziwa na mwafulani wa pili kulingana na muktadha wa dondoo.
(d) Fafanua maudhui yoyote matano yanayojitokeza kulingana na muktadha wa dondoo hili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Huyo Meya wetu ana washauri ambao huwasikiliza zaidi hata kama wanampotosha.Fafanua ukirejelea tamthilia "Mstahiki Meya".(Solved)
Huyo Meya wetu ana washauri ambao huwasikiliza zaidi hata kama wanampotosha.Fafanua ukirejelea tamthilia "Mstahiki Meya".
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Zitavuma,
Zitakoma,
Nitakwima,
Mti-mle.(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Zitavuma,
Zitakoma,
Nitakwima,
Mti-mle.
Na muda nikisimama,
Nitatongoa nudhuma,
Kwa tenzi zilizo njema,
Nilisifu mti – mle.
Tazipanga tathlitha, tungo zilizo na hekima,
Za huba na thiatha, za kuburudi mitima,
Mashairi mabuthutha, musome mnaosoma.
Mti nishainukia,namea kuwa mzima,
Mizizi yadidimia, ardhini imeuma,
Nanena kitarbia, tungo zilizo adhama
Japo ni tungo za zama, mti-mle hutumia.
Zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,
Dharuba kinitikisa, mti-mle huinama,
Huyumba nikaziasa, matawi yakakingama,
Gharika ikishapisa, hurudi nikawa wima,
Na tungo za takhimisa, mti-mle huzipima.
Maswali
(1) Shairi hili ni la kimapokea. Toa sababu mbili kuunga kauli hii.
(2) Taja bahari kuu ya ushairi ambayo imetumiwa na mshairi. Fafanua.
(3) Fafanua dhamira ya mshairi.
(4) Kwa kutoa mifano bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili.
(5) Eleza jinsi mshairi ametumia idhini ya ushairi katika utungo huu.
(6) Andika ubeti wa nne kwa lugha natharia.
(7) Mshairi anamaanisha nini anaposema "zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,"
(8) Eleza toni ya shairi hili.
(9) Eleza maana ya msamiati ufuatao.
i) Nitatongoa
ii) Zitapusa.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Eleza matatizo yanayomkabili mtu anapoitumia lugha yoyote isipokuwa ile ya kwanza.(Solved)
Eleza matatizo yanayomkabili mtu anapoitumia lugha yoyote isipokuwa ile ya kwanza.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Fafanua mambo matano yanaosababisha kutokea kwa lahaja.(Solved)
Fafanua mambo matano yanaosababisha kutokea kwa lahaja.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Andika kwa wingi.
Mimi ndimi shangazi yake.(Solved)
Andika kwa wingi.
Mimi ndimi shangazi yake.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Fafanua matumizi ya po, ki na kwa katika sentensi ifuatayo.
Walipokuwa wakilima waliimba kwa furaha.
(Solved)
Fafanua matumizi ya po, ki na kwa katika sentensi ifuatayo.
Walipokuwa wakilima waliimba kwa furaha.
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)
- Andika katika hali ya udogo:
Mvulana yule alibeba kiti kikubwa (Solved)
Andika katika hali ya udogo:
Mvulana yule alibeba kiti kikubwa
Date posted: September 28, 2019. Answers (1)