Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,

Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali.

SIKUJUA!
1. Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,
Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama,
Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama.

2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima,
Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama,
Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma.

3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima,
Chakula siyo matata, ni machicha na mtama,
Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima.

4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima,
Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma,
Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma.

Kiitikio
Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida

SHAIRI B
Afrika na Watu Wake

Mimi ninaona mgonjwa
Bado amelala kitandani.
Kama hatutamtoa miiba iliyobaki
Mgonjwa hataweka miguu yake chini
Ili kutembea bila ya kujiegemeza.

Miiba iliyomo ndani mwetu lazima
Pia iondolewe upesi kabla haijaingia
Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi.
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma
Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi.

Lakini kuitoa miiba hii
Tunahitaji macho makali
Mikono isiyotetemeka
Moyo usio na huruma
Na kuona miiba ilipoingilia.

MASWALI
(a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B unavyokatisha tamaa.
(b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B.
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma.
(c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B.
(d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi Mshairi alivyotumia kibali chake.
(e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za aina hii.
(f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A?
(g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B.
(h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari.

Answers


sharon
(a) Shairi A - Mshairi ametambua myama aliyemfuga anamletea hasara kwa kumuumiza (anampiga teke na
kumuuma).
Shairi B - Mshairi analalamikia tatizo (miiba) linalowaathiri. Kulisuluhisha tatizo hilo kunahitaji juhudi na
makini.
(b) Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma watahadhari tatizo hilo lisirejee tena kuwaadhiri.
(c) Shairi A Shairi B
(i) Mishororo ni minne - Mishororo ni mitano
(ii) Ubeti una vina vya kati na vya - Ubeti hauna vina vinavyobainika
mwisho
(iii) Kila mshororo una migao miwili - Mishororo haina migao.
(iv) Kila mshororo una mizani kumi na sita - Idadi ya mizani hailingani.
(d) Kudondosha msamiati/kuacha/kuondoa msamiati (na kondoo kundi zima " na kundi zima la kondoo) neno la limedondoshwa.
(e) Takriri - Neno miiba limerudiwarudiwa.
(f) (i) Majuto - matumizi ya maneno - kama ningefuga
- Kumbe nimefuga punda
(g) (i) Mgonjwa
(ii) Wanasiasa (tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi)
(h) (i) Kusuluhisha tatizo hili
(ii) Tunahitaji makini, ujasiri na kutokuwa na huruma
(iii) Ili kuona tatizo lilipoanzia
sharon kalunda answered the question on October 2, 2019 at 08:41

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia? (Solved)

    SABUNI YA ROHO
    Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
    Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
    Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
    Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
    Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
    Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.
    Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
    Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
    Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
    Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
    Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
    Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
    Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Umevunja usuhuba, familia zazozana,
    Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
    Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
    Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
    Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
    Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
    Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii. (Solved)

    Mstahiki Meya
    Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua. (Solved)

    Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee" (Solved)

    Damu Nveusi na Hadithi nyingine
    "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Thibitisha ufaafu wa anwani ya hadithi hii.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……." (Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."
    (a) Weka dondoo hili katika muktadha wake .
    (b) Eleza tamathali mbili zilizotumika katika dondoo hili.
    (c) Eleza aina za kiu na njaa zilizomkumba mrejelewa wa kwanza.
    (d) Mrejelewa wa pili alishindwa mtihani wa maisha. Jadili.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • "Duniani kuna watu na viatu" (Solved)

    Tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
    "Duniani kuna watu na viatu"
    (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
    (b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao. (Solved)

    Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.
    (i) Diwani wa tatu
    (ii) Bili
    (iii) Mhubiri
    (iv) Diwani I na II

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Kila nikaapo hushika tama. (Solved)

    Kila nikaapo hushika tama
    Na kuwazia hali inayonizunguka.
    Huyawazia madhila
    Huziwazia shida
    Huiwazia dhiki

    Dhiki ya ulezi
    Shida ya kudhalilishwa kazini.
    Madhila ya kufanyiwa dharau
    Kwa sababu ya jinsia ya kike.

    Hukaa na kujidadisi
    Hujidadisi kujua kwa nini
    Jamii haikisikii kilio changu
    Wenzangu hawanishiki mikono
    Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni

    Hukaa na kujiuliza
    I wapi raha yangu uiimwengu huu?
    I wapi jamaa nzima ya wanawake?

    MASWALI
    (a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza
    (b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
    (c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata.
    (d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili.
    (e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili.
    (f) Fafanua toni ya shairi hili.
    (g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili.
    (h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa.
    (i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
    (i) Madhila
    (ii) Kudhalilishwa.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako, (Solved)

    Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
    1. Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,
    Ondoka andama ndiya, nondosheya uso wako,
    Ondoka wanisikiya, ziwate jeuri zako,
    Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani?

    2. Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri,
    Haistahamilikii, uovu umekithiri,
    Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri,
    Sikati yako shari, enda zako wasiwasi.

    3. Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha,
    Viumbe na zao nyoyo, vitina kuwagotanisha,
    Hiino ndio kaziyo, yenye kukufurahisha,
    Ni kazi isiyokuchosha, mno umeizoeya.

    4. Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani,
    Ati mambo si mazuri, mambo yote tatashani,
    Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini,
    Nisononeke moyoni, upate kufurahika.

    5. Au mara hunijiya, na kingine kisahani,
    Kuhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani,
    Huwa husishi nambiya, hali zao taabani,
    Zingawa wakati gani? Ni zako au ni zao?

    6. Na mara kuja mambiya, nitakapotoka humu,
    Na kwamba yaningojea, nde maisha magumu,
    Uliloni kusudiya, ni kunitiya wazimu,
    Kama ndiyo yako hamu, basi unshatahayari.

    (a) Eleza ujumbe uliojitokeza katika shairi hili.
    (b) Fafanua muundo wa ubeti wa tatu.
    (c) Eleza aina ya shairi hili.
    (d) Fafanua arudhi za utunzi alizozingatia mshairi.
    (e) Eleza toni ya mshairi.
    (f) Andika ubeti wa tano katika lugha ya kinathari.
    (g) Eleza mifano mitatu ya uhuru wa mshairi.
    (h) Eleza maana ya misamiati ifuatayokama ilivyotumika katika shairi.
    (i) ndiya
    (ii) kisahani
    (iii) nde

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge, (Solved)

    Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
    1. Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
    Asinywe yalo na vunju,
    Yakampa kigegezi,
    Yakamkibua roho akaona na kinyaa,
    Awali ndio awali, awali mbovu hamna.

    2. Kiwa utalimatia.
    Utayaramba makombo,
    Utadata vitu cheche,
    Kisomo chenye dhamana kikakupa kisogo,
    Inajuzu ujihimu
    Mwanafuu darasani,
    Urauka po mapema,
    Katu hutayaramba makombo,
    Hutakosa kisebeho.

    3. Dereva hata utingo,
    Natija ni asubuhi,
    Wateja utawawahi,
    Wasaa kuzingatia,
    Uwafikishe kazini,
    Kwa wasaa ufaao,
    Wasije wakateteshwa,
    Na bosi wao kazini,
    Nao wakakuapiza.

    4. Na ewe mwanazaraa,
    Mpini uukamate,
    Kabla jua kuwaka sana,
    Majasho kutiririsha mwilini,
    Yang‘oe yote magugu,
    Kutoka kwa lako konde.

    5. Mhadimu mwenye ajizi,
    Yakujuza ujihimu,
    Ununue na maziwa,
    Majogoo uyawahi mapema,
    Usije ukayadata,
    Chai mkandaa ukaandaa,
    Wateja wakuambae mithili ya ibilisi.

    Maswali
    (a) Eleza nasaha yoyote inayotolewa kwa wafanyakazi wowote watatu kwenye shairi.
    (b) Taja sifa zozote za kimuundo zilizotumiwa na mtunzi.
    (c) Eleza toni ya mshairi.
    (d) Nafsi nenewa anahimizwa kufanya nini.
    (e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi.
    (f) Toa mifano miwili ya uhuru wa mshairi.
    (g) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa kwenye shairi.
    (i) Maji maenge
    (ii) Natija
    (iii) Majogoo

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili (Solved)

    Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo. (Solved)

    Onyesha jinsi ukatili unavyojitokeza kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
    (i) Kanda la usufi
    (ii) Shaka ya mambo
    (iii) Mwana wa darubini
    (iv) Ndoa ya Samani.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Thibitisha jinsi anwani "Damu Nyeusi" inaafiki yaliyomo katika hadithi. (Solved)

    Thibitisha jinsi anwani "Damu Nyeusi" inaafiki yaliyomo katika hadithi.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Jadili matatizo KUMI ya kijamii ukirejelea hadithi "Mwana wa Darubini" (Solved)

    Jadili matatizo KUMI ya kijamii ukirejelea hadithi "Mwana wa Darubini"

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Riwaya ya kidagaa kimemwozea inaonyesha jitihada za vijana kujenga jamii mpya. Thibitisha kwa kutoa mifano (Solved)

    Riwaya ya kidagaa kimemwozea inaonyesha jitihada za vijana kujenga jamii mpya. Thibitisha kwa kutoa mifano

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Kwa kurejelea tamthilia ya Mstahiki Meya, fafanua vichocheo vya migogoro katika jamii ya Cheneo. (Solved)

    Kwa kurejelea tamthilia ya Mstahiki Meya, fafanua vichocheo vya migogoro katika jamii ya Cheneo.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Matambiko ni nini? Eleza dhima zake mbili. (Solved)

    Matambiko ni nini? Eleza dhima zake mbili.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana ya maapizo. (Solved)

    Eleza maana ya maapizo.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza maana ya ngoma katika fasihi simulizi kisha utoe dhima zake nne. (Solved)

    Eleza maana ya ngoma katika fasihi simulizi kisha utoe dhima zake nne.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Mtu mmoja alimpa mke wake nambari yake ya simu. (Solved)

    Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.
    Mtu mmoja alimpa mke wake nambari yake ya simu. Kila mara bibi akipigia mumewe simu, ilipokelewa na sauti nyororo "mteja wa nambari uliopiga hapatikani kwa sasa."Alifunga safari kumtembelea mume wake mjini na kukabiliana na huyu kisura.

    MASWALI
    a) Bainisha kipera cha utungo huu.
    b) Onyesha sifa tano za kipera hiki.
    c) Eleza manufaa tano ya kipera hiki.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)