"Wanyonge ndio wanyongwao nikauli inayodhihirka vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.Jadili.
- Amani kupagazwa kitoto Uhuru licha ya kukosa uwezo wa kukilea
- Mtemi Nasaba Bora kukataa kumsaidia mama mja mzito aliyekuwa anajifungua kando ya barabara
- Ben Bella kukibaka kitoto kidogo
- Mwalimu Majisifu kumwibia Amani mswada wake
- Mtemi kujihusisha kimapenzi na kumringa Lowela,msichana warika la bintiye
- Fao kumringa mwanafunzi wake
- Yusufu kusingiziwa mauaji ya Chichiri Hamadi na kufungwa gerezani
- Mtemi na Lowela kukitupa kitoto Uhuru nje ya kibanda cha Amani kwenye baridi shadidi
- Askari wa Mtemi kutishia kumpokonya shamba lake,kumpiga na kishaakafa
- Imani kufurushwa kwa nyumba yao kutiwa moto baada ya kifo cha mamake na kugurakwa Oscar Kambona
- Serikali kumpuuza Chwechwe Mkweche baada ya kuvunjika fupaja licha ya kuiletea taifa na timu yake ushindi
- Matuko Weye kupuuzwa na serikali licha ya kuwehuka baada ya kushirikishwa katika vita vya dunia anatupwa gerezani anapojaribu kuzindua wananchi kuhusu uongozi mbaya wa Mtemi
- Bi.Zuhura licha ya kuisha katika upweke akiwa mkewe Mtemi anaishilia kutalikiwa baada ya kufumaniwa na Mtemi akiwa na Amani katika chumba chake
- Amani kama mchungaji katika boma la Mtemi alichapwa kinyama na Mtemi na kutupwa kando ya Mto Kiberenge
- Wauguzi zahanati ni walikataa kukiuuguza kitoto Uhuru licha ya kuwa katika hali mahututi-kikafia njiani
- Majisifu kukosa kuhudhuria vipindi shuleni ni dhuluma kwa wanafunzi kwa vile walihitaji kufunzwa
- Mtemi kuagiza Imani na Amani kufungwa gerezani pasi kosa la kukiua kitoto Uhuru ni kunyongwa kwa wanyonge
- Majisifu kuwadharau na kutaka kuwaua kwa kuwatupa wanawe walemavu majinini kunyogwa kwa wanyonge
- Mtemi kukataa kumpeleka DJ hospitalini baada ya kungatwa na jibwa lake Jimmy ni dhuluma kwa mnyonge licha ya kufahamu kuwa halikuchanjwa
- Mtemi,Maozi wanopowaajiri watoto ni dhuluma kwa wanyonge..wanajukumishwa ajira wakiwa wadogo na kwa mishahara midogo
sharon kalunda answered the question on October 2, 2019 at 08:46
- Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,(Solved)
Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali.
SIKUJUA!
1. Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,
Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama,
Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama.
2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima,
Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama,
Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma.
3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima,
Chakula siyo matata, ni machicha na mtama,
Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima.
4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima,
Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma,
Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma.
Kiitikio
Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida
SHAIRI B
Afrika na Watu Wake
Mimi ninaona mgonjwa
Bado amelala kitandani.
Kama hatutamtoa miiba iliyobaki
Mgonjwa hataweka miguu yake chini
Ili kutembea bila ya kujiegemeza.
Miiba iliyomo ndani mwetu lazima
Pia iondolewe upesi kabla haijaingia
Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi.
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma
Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi.
Lakini kuitoa miiba hii
Tunahitaji macho makali
Mikono isiyotetemeka
Moyo usio na huruma
Na kuona miiba ilipoingilia.
MASWALI
(a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B unavyokatisha tamaa.
(b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B.
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma.
(c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B.
(d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi Mshairi alivyotumia kibali chake.
(e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za aina hii.
(f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A?
(g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B.
(h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?(Solved)
SABUNI YA ROHO
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.
Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Umevunja usuhuba, familia zazozana,
Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Nitafukuzwa mbinguni
Kwa ushairi wangu mbaya
Lakini hata motoni nitaimba:(Solved)
Nitafukuzwa mbinguni
Kwa ushairi wangu mbaya
Lakini hata motoni nitaimba:
Wanasema
Wanasiasa ni kama jizi
Lililosukuma mtoto pembeni
Na kunyonya ziwa la mama
Wakati amelala usingizi usiku.
Wanasema
Mwanasiasa afapo
Tumejikomboa na domo
Moja pana lizibwalo na mchanga
Na kilima cha simenti ngumu
Lisikike tena hadharani.
Wanasema pia
Kusema haki
Kwa kawaida
Wanasiasa hatuwapendi.
Kupiga kura ni hasira za mkizi
Ni basi tu. Ni Ah!
Ah!
Wanamalizia
Nchi mmefiilisi waacheni walimu
Wakajenga taifa jipya.
Top grade predictor publishers Page | 63
Kama hamwezi kuona mbali
Bure kuweka mkono usoni,
Bure hakuna kichwa
Kama hamwezi kufikiri.
Ng‘ombe amekamuliwa na wazungu
Waarabu, wahindi na wao
Sasa anatoa damu
Vilivyobaki ni chai ya rangi
Na madomo mapana zaidi
Yaliyo bado hai.
Kuimba nimeimba
Maswali
(a) Mshairi ana dhamira gani?
(b) Shairi hili ni la kukatisha tama, tetea rai hii.
(c) Onyesha matumizi mawili ya mishata.
(d) Eleza mbinu zozote nne za lugha zilizotumika katika shairi hili.
(e) Andika ubeti wa mwisho katika lugha tutumbi.
(f) Fafanua umbo la shairi hili.
(g) Eleza maana ya mafungu ya maneno ya maneno yafuatayo:
(i) kupiga kura ni hasira ya mkizi
(ii) kuweka mkono usoni
(iii) ng‘ombe amekamuliwa.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.(Solved)
Mstahiki Meya
Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.(Solved)
MSTAHIKI MEYA: Timothy Arege
Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua nafasi ya wanaorejelewa kuwa ―"walifanya vizuri kuja" katika tamthilia hii.
(c) Migogoro katika tamthilia hii hazikusuluhishwa vyema. Jadili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.(Solved)
Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?(Solved)
Kidagaa Kimemwozea:
"Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Dondoo hili linadokeza maudhui gani? Kwa kutoa mifano saba kwenye riwaya, bainisha jinsi maudhui hayo yanavyojitokeza.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"(Solved)
Kanda la Usufi
"Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Taja na kueleza tamathali ya usemi kwenye dondoo hili.
(c) Kwa kutolea mifano, onyesha jinsi anwani Kanda la Usufi inavyoafiki hadithi husika.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"(Solved)
Damu Nveusi na Hadithi nyingine
"………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Thibitisha ufaafu wa anwani ya hadithi hii.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Elimu imeshindwa kutimiza lengo la kuwapa vijana uwezo wa kukabiliana na maisha ya kisasa. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo.(Solved)
Elimu imeshindwa kutimiza lengo la kuwapa vijana uwezo wa kukabiliana na maisha ya kisasa. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
(a) Mke wangu
(b) Samaki wanchi zajoto
(c) Damu nyeusi.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake .
(b) Eleza tamathali mbili zilizotumika katika dondoo hili.
(c) Eleza aina za kiu na njaa zilizomkumba mrejelewa wa kwanza.
(d) Mrejelewa wa pili alishindwa mtihani wa maisha. Jadili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Kuvunjwa kwa haki na sheria lilikuwa jambo la kawaida chini ya uongozi wa Mtemi Nasaba bora. Thibitisha ukweli wa Kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa...(Solved)
Kuvunjwa kwa haki na sheria lilikuwa jambo la kawaida chini ya uongozi wa Mtemi Nasaba bora. Thibitisha ukweli wa Kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa kimemwozea.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Duniani kuna watu na viatu"(Solved)
Tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
"Duniani kuna watu na viatu"
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.(Solved)
Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.
(i) Diwani wa tatu
(ii) Bili
(iii) Mhubiri
(iv) Diwani I na II
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Kila nikaapo hushika tama.(Solved)
Kila nikaapo hushika tama
Na kuwazia hali inayonizunguka.
Huyawazia madhila
Huziwazia shida
Huiwazia dhiki
Dhiki ya ulezi
Shida ya kudhalilishwa kazini.
Madhila ya kufanyiwa dharau
Kwa sababu ya jinsia ya kike.
Hukaa na kujidadisi
Hujidadisi kujua kwa nini
Jamii haikisikii kilio changu
Wenzangu hawanishiki mikono
Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni
Hukaa na kujiuliza
I wapi raha yangu uiimwengu huu?
I wapi jamaa nzima ya wanawake?
MASWALI
(a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza
(b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
(c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata.
(d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili.
(e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili.
(f) Fafanua toni ya shairi hili.
(g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili.
(h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa.
(i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
(i) Madhila
(ii) Kudhalilishwa.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,(Solved)
Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
1. Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,
Ondoka andama ndiya, nondosheya uso wako,
Ondoka wanisikiya, ziwate jeuri zako,
Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani?
2. Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri,
Haistahamilikii, uovu umekithiri,
Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri,
Sikati yako shari, enda zako wasiwasi.
3. Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha,
Viumbe na zao nyoyo, vitina kuwagotanisha,
Hiino ndio kaziyo, yenye kukufurahisha,
Ni kazi isiyokuchosha, mno umeizoeya.
4. Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani,
Ati mambo si mazuri, mambo yote tatashani,
Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini,
Nisononeke moyoni, upate kufurahika.
5. Au mara hunijiya, na kingine kisahani,
Kuhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani,
Huwa husishi nambiya, hali zao taabani,
Zingawa wakati gani? Ni zako au ni zao?
6. Na mara kuja mambiya, nitakapotoka humu,
Na kwamba yaningojea, nde maisha magumu,
Uliloni kusudiya, ni kunitiya wazimu,
Kama ndiyo yako hamu, basi unshatahayari.
(a) Eleza ujumbe uliojitokeza katika shairi hili.
(b) Fafanua muundo wa ubeti wa tatu.
(c) Eleza aina ya shairi hili.
(d) Fafanua arudhi za utunzi alizozingatia mshairi.
(e) Eleza toni ya mshairi.
(f) Andika ubeti wa tano katika lugha ya kinathari.
(g) Eleza mifano mitatu ya uhuru wa mshairi.
(h) Eleza maana ya misamiati ifuatayokama ilivyotumika katika shairi.
(i) ndiya
(ii) kisahani
(iii) nde
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
(Solved)
Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
1. Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
Asinywe yalo na vunju,
Yakampa kigegezi,
Yakamkibua roho akaona na kinyaa,
Awali ndio awali, awali mbovu hamna.
2. Kiwa utalimatia.
Utayaramba makombo,
Utadata vitu cheche,
Kisomo chenye dhamana kikakupa kisogo,
Inajuzu ujihimu
Mwanafuu darasani,
Urauka po mapema,
Katu hutayaramba makombo,
Hutakosa kisebeho.
3. Dereva hata utingo,
Natija ni asubuhi,
Wateja utawawahi,
Wasaa kuzingatia,
Uwafikishe kazini,
Kwa wasaa ufaao,
Wasije wakateteshwa,
Na bosi wao kazini,
Nao wakakuapiza.
4. Na ewe mwanazaraa,
Mpini uukamate,
Kabla jua kuwaka sana,
Majasho kutiririsha mwilini,
Yang‘oe yote magugu,
Kutoka kwa lako konde.
5. Mhadimu mwenye ajizi,
Yakujuza ujihimu,
Ununue na maziwa,
Majogoo uyawahi mapema,
Usije ukayadata,
Chai mkandaa ukaandaa,
Wateja wakuambae mithili ya ibilisi.
Maswali
(a) Eleza nasaha yoyote inayotolewa kwa wafanyakazi wowote watatu kwenye shairi.
(b) Taja sifa zozote za kimuundo zilizotumiwa na mtunzi.
(c) Eleza toni ya mshairi.
(d) Nafsi nenewa anahimizwa kufanya nini.
(e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi.
(f) Toa mifano miwili ya uhuru wa mshairi.
(g) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa kwenye shairi.
(i) Maji maenge
(ii) Natija
(iii) Majogoo
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.(Solved)
Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Huu ni ukoloni mamboleo"(Solved)
Mstahiki Meya
"Huu ni ukoloni mamboleo"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Eleza umuhimu wa msemewa katika tamthilia hii.
(c) Jadili namna ukoloni mamboleo unavyojitokeza katika tamthilia.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili(Solved)
Kufariki kwa kitoto Uhuru ni jazanda inayoashiria hali halisi ya mambo riwayani "kidagaa kimemwozea". Jadili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)