Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

"Alipofikishwa kwenye zahanati hakushughulikiwa ipasavyo.Ubwete ni ugonjwa mmoja mbaya walioambukizwa madaktari na wauguzi wengi Tomoko"

      

"Alipofikishwa kwenye zahanati hakushughulikiwa ipasavyo.Ubwete ni ugonjwa mmoja mbaya walioambukizwa madaktari na wauguzi wengi Tomoko"
a) Eleza Muktadha wa dondoo hili.
b) Dhihirisha jinsi mtunzi alivyoitumia tamathali yoyote moja inayobainika kifunguni .
c) Riwaya Ya Kidagaa Kimemwozea ni muhtasari wa maradhi yanayolihujumu Bara Afrika.Tetea rai hii kwa mifano faafu riwayani.

  

Answers


sharon
a) Haya ni maelezo ya mwandishi.
Anamrejelea Bob D.j.
Hii ni baada ya yeye kupelekwa huko baada ya kung‘atwa na mbwa wake Mtemi.
Hata hivyo hapewi huduma ifaavyo kutokana na mazoea ya utepetevu ya wahudumu wa afya pale zahanatini.

b) Istiara- "ubwete ni ugonjwa mmoja walioambukizwa madaktari na wauguzi wengi Tomoko."
Mtunzi amefananisha ubwete /uzembe na ugonjwa moja kwa moja.Kwa kufanya hivi anaukejeli mfumo wa afya ambao umeshindwa kuwajibikia majukumu yake ipaswavyo.

c) Swali hili linamhitaji mwanafunzi kudhihirisha uozo wowote mwengine wa kijamii unaojibainisha riwaya ni mbali na Mapuuza/Kutowajibika. Mifano ni kama:
i. Ukatili.Mtemi anaongoza kwa mabavu na kunyakua mashamba ya baadhi ya Wanatomoko.Kwa mfano anapanga mauaji ya Chichiri Hamadi ilikufaidi shamba lake.
ii. Mifumo duni ya Elimu.Katika Mazungumzo yao,Amani na Madhubuti wanalalamikia mfumo duni wa elimu Tomoko ambao unamwezesha mtu kupita mitihani tu bali haumpi maarifa ya kukabili maisha kikamilifu.
iii. Ufisadi .Mtemi alighushi vyeti vya umiliki ardhihi viakaweza kuwapoka wengi ardhiyao.Pia,kwapa moja na wanakamati walioteuliwa kusimamia ujenzi wa hospitali kwa ufadhili kutoka Uingereza anafuja sehemu kubwa ya fedha zizona kuishia kujenga kijizahanati kibovu.
iv. Utabaka.Jamii imegawika kitabaka huku wachochole wa kidunishwa.Katika sherehe za SikuKuu Ya Wazalendo,wageni wanaketi kwenye mahema ilhali rai wanachwa kusongamana katika jua kali lililowaumiza.
v. Mapendeleo/Ubaguzi wa Kinasaba.Mwandishi anaeleza kwamba Mtemi alipata nafasi yake kutokana na uhusiano wa kinasaba aliokuwa nao na Mudirwa Wilaya.Pia,Majisifu ana bahatika kupata kazi baada ya nyingine kwa kuwa jamaa zake walikuwa uongozini.
vi. Usaliti.Viongozi wa Tomoko baada ya KupatikanaUhuru wanasaliti juhudi za upiganiaji Uhuru huo.Mtemi na wenziwe wanachukulia nyadhifa zao kuwakibali cha kudhulumu,kupokonya na kufaidi binafsi tofauti na malengo ya kujikomboa.
vii. Umasikini.Wahusika wengi riwayani ni masikini wakutupwa.Tukuta naponaa maniamevaa mararu na anaelezwa kubeba kila kilichokuwa chake katika mkoba mdogo mweusi.Imani anaelezwa kuwa nanguo moja pekee.
viii. Ajira ya watoto.Watoto kama D.J wanaajiriwa kuwa chungang‘ombewa matajiri kule Sokomoko.Wanaanza kufanya kazi wangaliwa change jambo linalo wanyima fursa ya kuiendeleza kimasomo na kukua kama wenzao waumriwao.
ix. Ukabila.Madhubuti anakejeli hali anaposema kuwa ingefaa kama angepata shahada katika fani ya uongo,ufisadi na ukabila;ithibati tosha kuwa ukabila ni sehemu ya jamii hii.
x. Tatizo la mihadarati. Mwalimu Majisifu ni mraibu sugu wapombe.Analewa hadi ya kulala mitaroni na kushindwa kutekeleza wajibu wake.Ben Bella ni mvutaji bangia shiki.
xi. Kiburi.Viongozi kama Mtemi wamesawiriwa kuwa waliojaataadi.Mwandishi anadaikuwa Mtemi alijiona kuwa aliyefaa heshima na ikibidi alifaa kushikwa moo na kurambwa unyayo kama nusu Mungu.
xii. Ubinafsi.Mwalimu Majisifu anatawaliwa na ubinafsi mwingi hivi kughushi kazi za waandishi chipukizi akizichapisha kana kwamba ni zake halali.Wazazi wake Fao wanafanya mapango afaidi fedha walizotengewa masikini kwa masomo yao.
xiii. Uasherati.Mtemi anashiriki mapenzi nje ya ndoa na Lowela.Hivi anamwacha mkewe mpweke na mwenye utashiwa mapenzi.
xiv. Ubarakala.Balozi amechorwa kuwa kasuku ambaye anafanya kila jambo kumfurahisha Mtemi tu.
xv. Biashara haramu.Mamaye D.j anauza pombe haramu.Majisifu anamzungumzia Mama Nitilie ambaye alifahamika kwa kuuza gongo kali.Kwamba Ben Bella ni mvutaji bangi ni ushadi kuwa biashara haiipo.
xvi. Kuvunjika kwa familia/jamii.D.j anatenganishwa na familia yake.Wahusika kama Chwechwe Makweche wanawania sifa na hivyo kusahau wajibu wao kwa familia zao.Familia ya Bwana na Bi Maozi inaelekea kusambaratika kwa kuwa Ben Bella ni mhalifu ambaye kwa muda mwingi huwa jela na Lowela nimpenda anasa aliyeyoyomea raha hata asijitambue.
sharon kalunda answered the question on October 2, 2019 at 08:55


Next: In an experiment to determine the half-life of the radioactive element,the following data was obtained.
Previous: You are planning to carry out field study in a forest within your district.

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)

    "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
    Jadili.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,(Solved)

    Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali.

    SIKUJUA!
    1. Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,
    Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama,
    Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama.

    2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima,
    Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama,
    Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma.

    3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima,
    Chakula siyo matata, ni machicha na mtama,
    Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima.

    4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima,
    Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma,
    Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma.

    Kiitikio
    Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida

    SHAIRI B
    Afrika na Watu Wake

    Mimi ninaona mgonjwa
    Bado amelala kitandani.
    Kama hatutamtoa miiba iliyobaki
    Mgonjwa hataweka miguu yake chini
    Ili kutembea bila ya kujiegemeza.

    Miiba iliyomo ndani mwetu lazima
    Pia iondolewe upesi kabla haijaingia
    Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi.
    Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma
    Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi.

    Lakini kuitoa miiba hii
    Tunahitaji macho makali
    Mikono isiyotetemeka
    Moyo usio na huruma
    Na kuona miiba ilipoingilia.

    MASWALI
    (a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B unavyokatisha tamaa.
    (b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B.
    Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma.
    (c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B.
    (d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi Mshairi alivyotumia kibali chake.
    (e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za aina hii.
    (f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A?
    (g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B.
    (h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?(Solved)

    SABUNI YA ROHO
    Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
    Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
    Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
    Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
    Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
    Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.
    Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
    Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
    Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
    Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
    Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
    Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
    Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Umevunja usuhuba, familia zazozana,
    Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
    Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
    Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
    Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
    Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
    Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Nitafukuzwa mbinguni Kwa ushairi wangu mbaya Lakini hata motoni nitaimba:(Solved)

    Nitafukuzwa mbinguni
    Kwa ushairi wangu mbaya
    Lakini hata motoni nitaimba:
    Wanasema
    Wanasiasa ni kama jizi
    Lililosukuma mtoto pembeni
    Na kunyonya ziwa la mama
    Wakati amelala usingizi usiku.
    Wanasema
    Mwanasiasa afapo
    Tumejikomboa na domo
    Moja pana lizibwalo na mchanga
    Na kilima cha simenti ngumu
    Lisikike tena hadharani.
    Wanasema pia
    Kusema haki
    Kwa kawaida
    Wanasiasa hatuwapendi.
    Kupiga kura ni hasira za mkizi
    Ni basi tu. Ni Ah!
    Ah!
    Wanamalizia
    Nchi mmefiilisi waacheni walimu
    Wakajenga taifa jipya.
    Top grade predictor publishers Page | 63
    Kama hamwezi kuona mbali
    Bure kuweka mkono usoni,
    Bure hakuna kichwa
    Kama hamwezi kufikiri.
    Ng‘ombe amekamuliwa na wazungu
    Waarabu, wahindi na wao
    Sasa anatoa damu
    Vilivyobaki ni chai ya rangi
    Na madomo mapana zaidi
    Yaliyo bado hai.
    Kuimba nimeimba

    Maswali
    (a) Mshairi ana dhamira gani?
    (b) Shairi hili ni la kukatisha tama, tetea rai hii.
    (c) Onyesha matumizi mawili ya mishata.
    (d) Eleza mbinu zozote nne za lugha zilizotumika katika shairi hili.
    (e) Andika ubeti wa mwisho katika lugha tutumbi.
    (f) Fafanua umbo la shairi hili.
    (g) Eleza maana ya mafungu ya maneno ya maneno yafuatayo:
    (i) kupiga kura ni hasira ya mkizi
    (ii) kuweka mkono usoni
    (iii) ng‘ombe amekamuliwa.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.(Solved)

    Mstahiki Meya
    Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.(Solved)

    MSTAHIKI MEYA: Timothy Arege
    Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
    Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Fafanua nafasi ya wanaorejelewa kuwa ―"walifanya vizuri kuja" katika tamthilia hii.
    (c) Migogoro katika tamthilia hii hazikusuluhishwa vyema. Jadili.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.(Solved)

    Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?(Solved)

    Kidagaa Kimemwozea:
    "Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Dondoo hili linadokeza maudhui gani? Kwa kutoa mifano saba kwenye riwaya, bainisha jinsi maudhui hayo yanavyojitokeza.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"(Solved)

    Kanda la Usufi
    "Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Taja na kueleza tamathali ya usemi kwenye dondoo hili.
    (c) Kwa kutolea mifano, onyesha jinsi anwani Kanda la Usufi inavyoafiki hadithi husika.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"(Solved)

    Damu Nveusi na Hadithi nyingine
    "………Alimaliza kwa kuandika, "yajayo yapokee"
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Thibitisha ufaafu wa anwani ya hadithi hii.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Elimu imeshindwa kutimiza lengo la kuwapa vijana uwezo wa kukabiliana na maisha ya kisasa. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo.(Solved)

    Elimu imeshindwa kutimiza lengo la kuwapa vijana uwezo wa kukabiliana na maisha ya kisasa. Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo.
    (a) Mke wangu
    (b) Samaki wanchi zajoto
    (c) Damu nyeusi.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."(Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    "Alikuwa na kiu lakini si ya maji, kadhalika alikuwa na njaa lakini si ya chakula Habebeki mwanamume habebeki……."
    (a) Weka dondoo hili katika muktadha wake .
    (b) Eleza tamathali mbili zilizotumika katika dondoo hili.
    (c) Eleza aina za kiu na njaa zilizomkumba mrejelewa wa kwanza.
    (d) Mrejelewa wa pili alishindwa mtihani wa maisha. Jadili.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Kuvunjwa kwa haki na sheria lilikuwa jambo la kawaida chini ya uongozi wa Mtemi Nasaba bora. Thibitisha ukweli wa Kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa...(Solved)

    Kuvunjwa kwa haki na sheria lilikuwa jambo la kawaida chini ya uongozi wa Mtemi Nasaba bora. Thibitisha ukweli wa Kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa kimemwozea.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "Duniani kuna watu na viatu"(Solved)

    Tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.
    "Duniani kuna watu na viatu"
    (a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
    (b) Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea tamthilia nzima ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.(Solved)

    Mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya ametumia wahusika kukuza kazi yake, Thibitisha kauii hili kwa kuwarejelea wahusika wafuatao.
    (i) Diwani wa tatu
    (ii) Bili
    (iii) Mhubiri
    (iv) Diwani I na II

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Kila nikaapo hushika tama.(Solved)

    Kila nikaapo hushika tama
    Na kuwazia hali inayonizunguka.
    Huyawazia madhila
    Huziwazia shida
    Huiwazia dhiki

    Dhiki ya ulezi
    Shida ya kudhalilishwa kazini.
    Madhila ya kufanyiwa dharau
    Kwa sababu ya jinsia ya kike.

    Hukaa na kujidadisi
    Hujidadisi kujua kwa nini
    Jamii haikisikii kilio changu
    Wenzangu hawanishiki mikono
    Bali wananidharau kwa kuukosoa utamaduni

    Hukaa na kujiuliza
    I wapi raha yangu uiimwengu huu?
    I wapi jamaa nzima ya wanawake?

    MASWALI
    (a) Shairi hili ni la aina. gani? Eleza
    (b) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili.
    (c) Kwa kutolea mifano eleza maana ya mistari mishata.
    (d) Taja na ueleze tamathali mbili zilizotumika katika shairi hili.
    (e) Tambulisha nafsi-neni katika shairi hili.
    (f) Fafanua toni ya shairi hili.
    (g) Fafanua maudhui mawili ya shairi hili.
    (h) Onyesha namna nafasi neni anavyosalitiwa.
    (i) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi.
    (i) Madhila
    (ii) Kudhalilishwa.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,(Solved)

    Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
    1. Wasiwasi n‘ondokeya, ondoka enenda zako,
    Ondoka andama ndiya, nondosheya uso wako,
    Ondoka wanisikiya, ziwate jeuri zako,
    Jishughulishe na yako, yangu wayatakiyani?

    2. Wasiwasi siitaki, suhuba yako si nzuri,
    Haistahamilikii, uovu umekithiri,
    Inganyoshwa hainyoki, ikukutene kikiri,
    Sikati yako shari, enda zako wasiwasi.

    3. Huna kazi ufanyayo, ela kuwafitinisha,
    Viumbe na zao nyoyo, vitina kuwagotanisha,
    Hiino ndio kaziyo, yenye kukufurahisha,
    Ni kazi isiyokuchosha, mno umeizoeya.

    4. Mara waja na habari, mambo yalivyo nyumbani,
    Ati mambo si mazuri, mambo yote tatashani,
    Wanitaka nifikiri, usemayo ni yakini,
    Nisononeke moyoni, upate kufurahika.

    5. Au mara hunijiya, na kingine kisahani,
    Kuhusu zao afiya, hao waliyo nyumbani,
    Huwa husishi nambiya, hali zao taabani,
    Zingawa wakati gani? Ni zako au ni zao?

    6. Na mara kuja mambiya, nitakapotoka humu,
    Na kwamba yaningojea, nde maisha magumu,
    Uliloni kusudiya, ni kunitiya wazimu,
    Kama ndiyo yako hamu, basi unshatahayari.

    (a) Eleza ujumbe uliojitokeza katika shairi hili.
    (b) Fafanua muundo wa ubeti wa tatu.
    (c) Eleza aina ya shairi hili.
    (d) Fafanua arudhi za utunzi alizozingatia mshairi.
    (e) Eleza toni ya mshairi.
    (f) Andika ubeti wa tano katika lugha ya kinathari.
    (g) Eleza mifano mitatu ya uhuru wa mshairi.
    (h) Eleza maana ya misamiati ifuatayokama ilivyotumika katika shairi.
    (i) ndiya
    (ii) kisahani
    (iii) nde

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge, (Solved)

    Soma ushairi ufuatao kisha ujibu maswali.
    1. Ajaye kisimani mbele hunywa maji maenge,
    Asinywe yalo na vunju,
    Yakampa kigegezi,
    Yakamkibua roho akaona na kinyaa,
    Awali ndio awali, awali mbovu hamna.

    2. Kiwa utalimatia.
    Utayaramba makombo,
    Utadata vitu cheche,
    Kisomo chenye dhamana kikakupa kisogo,
    Inajuzu ujihimu
    Mwanafuu darasani,
    Urauka po mapema,
    Katu hutayaramba makombo,
    Hutakosa kisebeho.

    3. Dereva hata utingo,
    Natija ni asubuhi,
    Wateja utawawahi,
    Wasaa kuzingatia,
    Uwafikishe kazini,
    Kwa wasaa ufaao,
    Wasije wakateteshwa,
    Na bosi wao kazini,
    Nao wakakuapiza.

    4. Na ewe mwanazaraa,
    Mpini uukamate,
    Kabla jua kuwaka sana,
    Majasho kutiririsha mwilini,
    Yang‘oe yote magugu,
    Kutoka kwa lako konde.

    5. Mhadimu mwenye ajizi,
    Yakujuza ujihimu,
    Ununue na maziwa,
    Majogoo uyawahi mapema,
    Usije ukayadata,
    Chai mkandaa ukaandaa,
    Wateja wakuambae mithili ya ibilisi.

    Maswali
    (a) Eleza nasaha yoyote inayotolewa kwa wafanyakazi wowote watatu kwenye shairi.
    (b) Taja sifa zozote za kimuundo zilizotumiwa na mtunzi.
    (c) Eleza toni ya mshairi.
    (d) Nafsi nenewa anahimizwa kufanya nini.
    (e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha tutumbi.
    (f) Toa mifano miwili ya uhuru wa mshairi.
    (g) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa kwenye shairi.
    (i) Maji maenge
    (ii) Natija
    (iii) Majogoo

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.(Solved)

    Jumuiya ya "Mstahiki Meya" inaafiki kwa kiasi kikubwa jamii ya kisasa. Thibitisha.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)

  • "Huu ni ukoloni mamboleo"(Solved)

    Mstahiki Meya
    "Huu ni ukoloni mamboleo"
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Eleza umuhimu wa msemewa katika tamthilia hii.
    (c) Jadili namna ukoloni mamboleo unavyojitokeza katika tamthilia.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)