Nchi nyingi duniani zimetia saini mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto.

      

Soma taarifa ifatayo kwa makini kisha ujibu maswali yanayofuata.
Nchi nyingi duniani zimetia saini mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto.
Haki ni mambo mema ambayo watoto wanastahili kutendewa. Kwa kutia saini, nchi hizizimetangaza kujitolea kwao kuzilinda na kuhahakikisha kuwa hakuna ukiukaji wake nakuwa watoto wote katika himaya zao wananufaika kutokana na haki hizi.
Miongoni mwa haki hizi ni kuwa kila mtoto ana haki ya kuishi na kupata chakula cha kutosha na chenye viinilishe bora. Pili, kila mtoto ana haki ya kupata elimu. Elimu hii inafaa kutolewa bila ada na iwe inayofaa na inayopatikana kwa urahisi.Kisha kila mtoto ana haki ya kutopigwa na kutodunishwa kwa namna yoyote, iwe kitabaka, kirangi, kijinsia na vinginevyo. Mtoto ana haki pia kutolazimishwa kufanya kazi za kiutumwa, nzito na zakushurutishwa. Hali kadhalika, ana haki ya kuishi katika nyumba au makazi bora nasalama, kutunzwa na kulindwa dhidiya hali yoyote inayoweza kumhatarisha. Anatakiwa ashirikishwe katika kufanya maamuzi.Fauka ya haya, ana haki ya kupata huduma za afya,mahitaji maalum,michezo, upendo na habari. Isitoshe,anastahili kuheshimiwa kimawazo na kihisia. Haki hizi zinatakiwa kulindwa na kila mwanajamii, hivyo serikali za mataifa mengi zimeshirikisha haki hizi katika katiba za nchi zao na sheria zao.
Walakini haki hizi bado zinakiukwa.Watoto wengi kote duniani bado wananyimwa haki zao. La kusikitisha na kukera ni kuwa wanaotarajiwa kuwa vigogo vya kuzilinda haki hizi, ndio wanaoongoza kuzikiuka. Kila siku tunasikia na kushuhudia visa vya watoto kupigwa, kunyimwa chakula, kufanyishwa kazi kipunda, kuteswa, kuishi katika mazingira hatari, na hata kuuawa. Kuna watoto wengi wanaolala nje, wengine hawapati chakula licha ya kuwa wanatakiwa kupata chenye lishe bora. Kwao kutarajiwa mlo awamu tatu kwa siku ni njozi kwani hata awamu moja ni adimu kupata.
Watoto wengi katika mataifa yenye fujo na ghasia hutekwa na kutumikishwa vitani. Viongozi katika mataifa haya hawafanyi kitu ila kutazama tu wakati watoto wanaotakiwa kuwalinda wanageuzwa kuwa mibaba ya kuua na kuuana. Watoto hawa huvishwa magwanda ambayo miili yao minyonge haiwezi kuyahimili. Pia, huvalishwa mabuti ya kijeshi ambayo ni mizigo mizito ya kubeba mbali na bunduki zinazokaribia kuwazidi uzani wakati wanatakiwa kuwa wamelindwa majumbani, na shuleni na wazazi wao na serikali.
Jukwaa la vijiji vya mataifa ya ulimwengu wa tatu limesheheni watoto wasioenda shule kwa sababu ya lindi la ufukara uliokithiri. Elimu ya bure inayogusiwa katika haki za watoto haipo. Wanaong‘ang‘ana iwepo ni kana kwamba ni waota ndotomchana. Jiulize watoto wangapi sasa hivi wamo majumbani bila kwenda shuleni kutokana na ukosefu wa karo? Wangapi wamo mitaani wakivuta na kunusa gundi huku wakiombaomba vishilingi?
Hali ilivyo sasa hivi inadai kuwa mimi na wewe tufanye hima na kuungana mikono kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu haki za watoto. Twapasa kuhimiza serikali zetu kufanya kila ziwezavyo kuhakikisha kuwa watoto wote wamo shuleni. Nasi tushirikiane kutoa huduma kwa watoto na kukomesha dhuluma, mateso na dhiki kwao. Haitoshi kupeleka miswada mbungeni kuhusu haki za watoto na kuipitisha kuwa sheria. Twastahili kubadilisha misimamo yetu kuhusu haki hizi na kuzilinda kwa dhati bali si kwa chati.
Maswali
a) Fupisha aya mbili za kwanza. ( maneno 65-70)
b) Eleza ni vipi ukiukaji wa haki za watoto unaweza kuepukwa . ( maneno 30-35)

  

Answers


sharon
a)
- Nchi nyingi duniani zimetia saini mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto
- Kuhakikisha kuwa hakuna ukiukaji wake katika himaya zao.
- Haki hizi ni kupata chakula bora
- Elimu isiyotolewa ada
- Kutopigwa na kutodunishwa
- Kutolazimishwa kufanya kazi za kiutumwa au kushurutishwa
- Kuishi katika nyumba au makazi bora
- Kulindwa dhidi ya madhara yoyote
- Kushirikishwa katika maamuzi
- Kupata huduma za kiafya
- kuheshimiwa kimawazo na kihisia
- Haki hizi zinastahili kulindwa na wanajamii
- Serikali kushirikisha haki hizi katika katiba za nchi zao.
b)
- Serikali kuhakikisha kuwa watoto wote wako shuleni
- Watu wote kushirikiana kukomesha dhuluma
- Miswada kuhusu watoto kupelekwa bungeni na kupitishwa kuwa sheria.
- Kubadilisha misimamo yetu kuhusu haki hizi na kuzilinda upasavyo
sharon kalunda answered the question on October 2, 2019 at 10:00


Next: If the study of a farm, 10 hectares are found to be devoted to coffee growing and the total acreage is 100 hectare. What is...
Previous: A pupil was requested to pick out fourteen numbers randomly from a set of numbers.She picked 20,1,66,42,12,6,15,12,42,100,3,82,42,37

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Alipokuwa akiukemea utamaduni na dhana za kikabila katika nyimbo zake, marehemu Bob Marley aliufananisha ubepari na "wanyama wala watu."(Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali yanayofuata.

    Alipokuwa akiukemea utamaduni na dhana za kikabila katika nyimbo zake, marehemu Bob Marley aliufananisha ubepari na "wanyama wala watu." Katika wimbo "Babylon System" (yaani mfumo wa kibepari), Marley alisema kuwa utamaduni huo ndio mzawa wa matatizo yote ya kiutawala ambayo yalikuwa yakiyakumba mataifa ya Weusi katika karne ya 20, wakati nchi zao zilikuwa zikitawaliwa na nchi za mataifa ya Ulaya.
    Kwa mantiki hiyo, pengine Marley alikuwa na maono kuwa Afrika haingejikomboa kutoka kwa utumwa wa Kizungu, ikiwa ingeendelea kuziabudu na kuzishadidia tamaduni za Kimagharibi.
    Utabiri huo nauoanisha na yanayoendelea nchini, ambapo serikali ya Jubilee imeonekana kushindwa kabisa kuikabili saratani ya ufisadi, ambayo inahatarisha kuliangamiza taifa hili lenye uchumi dhalili.
    Donda hili linazidi kuyatandaza mabawa yake kutoka, tisho kuu likiwa ni uvamizi wa taasisi ―takatifu‖ ambazo tunazitegemea kulikabili donda hilo.
    Ni nani tutategemea kukabiliana na rushwa ikiwa taasisi kama Bunge, Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC) kati ya zingine muhimu zimepakwa tope na saratani hiyo?
    Kimsingi yote tunayopitia ni matunda ya uasi wa tamaduni za Kiafrika na uegemezi wa mifumo ya Kizungu kama mihimili ya jamii na nchi zetu.
    Ndoto za watetezi wa Uafrika na nafasi ya Weusi kama marehemu Malcom X na Martin Luther King, zilikuwa ni kuona kuwa wameungana kabisa kukabiliana na matatizo yaliyowakabili bila kuzingatia mazingara waliyokuwemo.
    Pindi tu baada ya mataifa mengi ya Kiafrika kujinyakulia uhuru wao katika miaka ya hamsini na sitini, viongozi wakuu walioziongoza nchi hizo kama Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Mwalimu Julius Kibarage Nyerere kati ya wengine walianza harakati za kuliunganisha bara hili na kubuni Muungano wa Nchi za Kiafrika (OAU) japo ndoto hiyo haikufikia.
    Kwa msingi huo, mhimili mkuu wa kiutawala ungekuwa ni mfumo wa kisosholisti, ambao ungekuwa nguzo kuu ya kuyaunganisha mataifa hayo.
    Hata hivyo, migawanyiko mikubwa ilianza kushuhudiwa, huku baadhi ya mataifa yakianza kukabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kutaasisika kwa maovu yote tunayoshuhudia sasa: ufisadi na tamaa ya kuogofya kutoka kwa viongozi wetu.

    Maswali
    a. Ipe taarifa hii anwani mwafaka.
    b. Onyesha mambo mawili makuu ambayo msanii aliyapinga .
    c. Kwa nini ubepari umelinganishwa na "wanyama wala watu"?
    d. Kwa mujibu wa taarifa eleza sifa za Bob Marley.
    e. Swala linalozungumziwa limerejelewa kama "Donda".
    i) Eleza mbinu ya lugha iliyotumika..
    ii) Ni kweli kuwa donda hili laelekea kuwa gumu? Thibitisha.
    f. Tatizo hili la "donda" ni kama kujipalia makaa. Fafanua.
    g. Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa taarifa.
    i) Mhimili
    ii). Taasisi

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • …ya leo ni kuwapa pole wanaofuata na kuenzi makala ya Burudani,toleo la kila Ijumaa.Mwanamziki huyu aliteka nyoyo za wapenzi wa mtindo huu wa mziki.Kwa kweli...(Solved)

    …ya leo ni kuwapa pole wanaofuata na kuenzi makala ya Burudani,toleo la kila Ijumaa.Mwanamziki huyu aliteka nyoyo za wapenzi wa mtindo huu wa mziki.Kwa kweli ya Muumba hufumbwa tu!Mnapoyasoma wakumbukeni jamaa na wapenzi wa nyimbo zake.
    (i) Tambua sajili hii na utoe Ushahidi.
    (ii) Fafanua sifa zozote za sajili hii.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Tambua na ueleze virai katika sentensi hii. Kisichana kile kimejirembesha kwa manukato mazuri ajabu(Solved)

    Tambua na ueleze virai katika sentensi hii.
    Kisichana kile kimejirembesha kwa manukato mazuri ajabu

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Andika kwa usemi wa taarifa. "Nitakuja kwenu kesho," Mwalimu alisema.(Solved)

    Andika kwa usemi wa taarifa.
    "Nitakuja kwenu kesho," Mwalimu alisema.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha hali katika sentensi zifuatazo. (i) Huenda mvua isinyeshe msimu huu. (ii) Waislamu huenda msikitini kuomba kila Ijumaa.(Solved)

    Onyesha hali katika sentensi zifuatazo.
    (i) Huenda mvua isinyeshe msimu huu.
    (ii) Waislamu huenda msikitini kuomba kila Ijumaa.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo kulingana na maagizo. Mwanasiasa huyu alishinda kura. (Tumia kiashiria kisistizi)(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo kulingana na maagizo.
    Mwanasiasa huyu alishinda kura. (Tumia kiashiria kisistizi)

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Badilisha sentensi iwe katika hali ya kuamuru. Rutto fagia chumba.(Solved)

    Badilisha sentensi iwe katika hali ya kuamuru.
    Rutto fagia chumba.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Tambua na ueleze aina za vivumishi katika sentensi zifuatazo. (i) Viatu vyangu vimepotea (ii) Viatu vyenyewe vinapendeza(Solved)

    Tambua na ueleze aina za vivumishi katika sentensi zifuatazo.
    (i) Viatu vyangu vimepotea
    (ii) Viatu vyenyewe vinapendeza

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Tambua aina ya chagizo katika sentensi ifuatayo. Walimu wataenda Mombasa Ijumaa ijayo.(Solved)

    Tambua aina ya chagizo katika sentensi ifuatayo.
    Walimu wataenda Mombasa Ijumaa ijayo.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Ikarabati sentensi hii: Mpira yangu amepotea (Solved)

    Ikarabati sentensi hii:
    Mpira yangu amepotea

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Tambua viambishi awali na tamati katika neno ajaye(Solved)

    Tambua viambishi awali na tamati katika neno ajaye

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Maneno yafuatayo yako katika ngeli gani. Kero. Nywele.(Solved)

    Maneno yafuatayo yako katika ngeli gani.
    Kero.
    Nywele.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya ku katika jozi zifuatazo za sentensi.(Solved)

    Eleza matumizi ya ku katika jozi zifuatazo za sentensi.
    (i) Kuchora kwao kulikuwa kwa uangalifu mkubwa
    (ii) Nilikuita lakini hukuitika

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika umoja. Manukato haya yananukia vizuri(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika umoja.
    Manukato haya yananukia vizuri

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.(Solved)

    Bainisha aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.
    Kuimba kwa Yusufu kunaudhi

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Akifika sentensi ifuatayo kwa kutumia alama ya kibainishi kisha eleza matumizi yake. Ntakwenda Unguja mwezi wa Disemba(Solved)

    Akifika sentensi ifuatayo kwa kutumia alama ya kibainishi kisha eleza matumizi yake.
    Ntakwenda Unguja mwezi wa Disemba

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika kauli iliyo mabanoni. Paka analamba mchuzi (kutendwa)(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika kauli iliyo mabanoni.
    Paka analamba mchuzi (kutendwa)

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Inaaminika kuwa majeruhi wengi katika mikasa ya ajali huaga au huathirika vibaya zaidi kutokana na hali mbaya ya uokoaji.(Solved)

    Utoaji wa Huduma ya Kwanza.

    Inaaminika kuwa majeruhi wengi katika mikasa ya ajali huaga au huathirika vibaya zaidi kutokana na hali mbaya ya uokoaji. Watu wengi ambao hujitolea kuokoa majeruhi baada ya ajali kama za barabarani, maporomoko ya ardhi au nyumba huwa hawang‘amui hata chembe jinsi ya kukabiliana na uokoaji. Hatima ya juhudi zao ambazo hulenga kutenda mema ni kuathirika zaidi kwa majeruhi.
    Hali ya ukoaji inaweza kurekebishwa kwa kutoa elimu ya huduma ya kwanza kwa umma. Elimu hii yahitajika na kila Mkenya kwani mikasa ya ajali za barabarani na nyinginezo inaendelea kutokea kila siku.Ajali zinapotokea, si ajabu kuona makundi ya waokoaji yakibeba majeruhi hobelahobela bila kuzingatia madhara yanayoweza kuwaongezea kutokana na ubebaji wao. Kutojua namna ya kumbeba majeruhi kunaweza kumhatarisha na hata kusababisha kifo.
    Kuna mambo mbalimbali ambayo makundi ya waokoaji yanatakiwa kuzingatia wakati yanatoa huduma ya kuokoa. Kwanza, ni muhimu kuchunguza kama kuna hatari yoyote inayoweza ikatokea na kuwatia majeruhi na waokoaji hatarini zaidi. Makundi ya waokoaji yameweza kuhatarisha majeruhi kwa kuliingilia eneo la ajali mbumbumbu kama mzungu wa reli.
    Hatua ya pili ni kutafuta idadi ya majeruhi. Pana uwezekano wa majeruhi kutupwa mbali na eneo la ajali. Vivyo hivyo, kuna majeruhi ambao huweweseka baada ya ajali na kuanza kutembea wasijue wanakoelekea. Wengi wao huanguka karibu na eneo la ajali au wakaenda mbali.
    Hatua ya tatu ni kuchunguza kama majeruhi amezimia, moyo unapiga na jinsi anavyopumua. Ili kuhakikisha kuwa majeruhi anapumua, mwokoaji atazame kama kifua kinapanda na kushuka. Halikadhalika, mwokoaji anaweza kusikiliza au kuguza kifua na kuona kama kuna ishara za kupumua. Iwapo majeruhi anapumua, mwokoaji amweke katika hali ambayo itaimarisha kupumua kwake. Anaweza akamlaza chali au kumgeuza kwa pamoja na kichwa chake ili kufungua mkondo wa hewa. Pia, mwokoaji ahakikishe hamna chochote kinywani kinachoweza kumsakama. Ikiwa hapumui, mwokoaji anaweza kujaribu kumfanya apumue kwa kupuliza hewa mdomoni mwake. Fauka ya hayo, upulizaji wa hewa utahakikisha kuwa damu inazunguka mwilini vizuri.
    Maswali :
    (a) Fupisha aya mbili za kwanza kwa maneno 55 – 65.
    (b) Eleza kwa kutumia maneno 90-100, hatua zinazotakiwa kufuatwa wakati wa uokoaji.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Miaka 15 iliyopita, Umoja wa Mataifa uliitangaza August 12 kila mwaka,(Solved)

    Soma makala yafuatao kisha ujibu maswali yanayofuata.
    Miaka 15 iliyopita, Umoja wa Mataifa uliitangaza August 12 kila mwaka, kuwa Siku ya Vijana Duniani‘ ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Vijana na Afya ya Akili‘. Kwa mujibu wa andiko kutoka Umoja wa Mataifa, asilimia 20 ya vijana duniani kote hupata tatizo linalohusiana na afya ya akili kila mwaka. Hatari zaidi hutokea katika kipindi cha kuhama kutoka utoto kuingia utu uzima. Kutengwa pamoja na aibu mara nyingi huongeza zaidi tatizo kwa kuwa vijana wengine hushindwa kutafuta msaada wanaouhitaji. Hivyo mwaka huu, Umoja wa Mataifa umeazimia kuitumia siku hii kukuza uelewa kuhusu afya ya akili kwa vijana. Wakati tunaadhimisha Siku ya Vijana Duniani 2014, tuwawezeshe vijana wenye matatizo ya afya ya akili kubaini umuhimu wao, na tuoneshe kuwa afya ya akili inatuhusu sote, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Maitafa, Ban Ki Moon kwenye maelezo yake. Miongoni mwa sababu kubwa zinazochangia tatizo la afya ya akili ni umaskini unaochangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa ajira. Asimilia kubwa ya vijana walio chini ya miaka 25 au wale wanaohitimu masomo yao nchini hawana ajira. Wanachuo wengi wameendelea kuzunguka huku na kule kuomba kazi bila mafanikio. Wengi wamekaa zaidi ya miaka mitatu nyumbani tangu wamalize masomo yao bila kuwa na ajira inayowaingizia kipato. Na pia wachache wanaopata kazi, wamekuwa wakilipwa ujira mdogo na hivyo kuendelea kuishi maisha magumu. Ukosefu wa ajira na kukosa fedha za kujikimu, umewafanya vijana wengi kuwa na msongo wa mawazo, tatizo kubwa linalohusiana na afya ya akili. Tatizo ni kubwa zaidi pale ambapo takwimu zinaonesha kuwa kwa wastani soko la ajira nchini lina uwezo wa kuzalisha ajira zipatazo 300,000 kwa mwaka katika sekta rasmi ukilinganisha na wastani wa wahitimu 600,000 hadi 800,000 wanaoingia katika soko la ajira nchini. Kwa kijana ambaye hana mahali pa kuishi, hajui atakula nini kesho, hana fedha za kununua nguo, kukata tamaa na kuamua kufanya lolote si kitu anachoweza kukifikiria mara mbili. Kwa vijana wa kiume wapo wanaoamua kuwa wezi au matapeli huku wengine wakijikuta wakiwa walevi wa kutupwa au kuvuta unga kama njia ya kupunguza msongo wa mawazo unaotokana na maisha magumu.Utumiaji wa vilevi hivyo, umechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza tatizo la afya ya akili kwa vijana wengine. Kwa wasichana, ukosefu wa ajira, huwaingiza wengi katika wimbi la kutumia miili yao kujipatia kipato kutoka kwa wanaume. Wengine hujikuta wakiolewa mapema na hivyo kupoteza ndoto za kujiendeleza kielimu ili kujitegemea. Mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini kwakuwa wasichana wadogo huzalishwa katika umri mdogo na wengine kukumbana na unyanyasaji wa nyumbani kutoka kwa waume zao.Katika maeneo ya vijijini ambako shughuli kubwa ya kiuchumi ni kilimo, ufugaji au uvuvi, baadhi ya wasichana waliolewa, hujikuta wakiachiwa familia zao kwa muda mrefu na waume zao wanaoenda kutafuta maisha. Baadhi ya wanaume hao huondoka kimoja na kuwaachia wake mzigo wa ulezi wa familia. Hivyo, tatizo kubwa la ajira kwa vijana lipo kwa wale ambao hawana elimu ya kutosha kustahili kuajiriwa katika ajira rasmi. Kwa mujibu wa survey iliyofanywa na Restless Development, Tanzania ina takriban watu milioni 25 walio chini ya miaka 25 nchini. Hiyo ina maana kuwa karibu nusu ya watu wote nchini ni vijana.
    Dunia nzima, vijana wamekuwa wakitambulika kwa kuwa na mchango mkubwa kuanzia katika upatikanaji wa uhuru enzi za ukoloni hadi katika kuvumbua teknolojia mpya na kugundua njia mpya za sanaa na muziki. Vijana ndio wanaolisukuma zaidi gurudumu la maendeleo kwa uchapakazi wao kutokana na miili na akili zao kuwa na uchangamfu zaidi. Hata hivyo Tanzania ni nchi iliyo na matabaka yanayotokana na umri na jinsia huku vijana wakioneana kutopewa fursa katika mchakato wa maamuzi katika hatua za kijamii na hata katika serikali. Ili kuwapa nafasi zaidi vijana katika nafasi za juu za maamuzi, vijana wanapaswa kutambua kuwa huu ndio wakati wao na sio kesho. Vijana wanatakiwa kwanza kujiamini wao wenyewe kuwa hakuna nafasi ya baadaye kwakuwa huu ndio wakati unaowaruhusu kuwa wabunifu zaidi kushawishi maendeleo. Mawazo yao mapya na njia zao tofauti za kukabiliana na mambo, yataleta utofauti mkubwa wa sera, maamuzi na muelekeo wa serikali au taasisi mbalimbali. ―Uongozi wa kizazi kipya upo tayari kushika hatamu za uongozi na kuijenga Tanzania mpya, kwa fikra mpya na maarifa mapya. Mabadiliko, kokote yalikotokea, yalidaiwa na kuongozwa na vijana. Vijana wa Tanzania washike usukani wa kuleta mabadiliko wanayoyataka. Ukiona kijana anamwambia kijana mwenzake hana uzoefu, basi kazi ya kuleta mabadiliko ni kubwa zaidi. Kutokuwa na uzoefu ni sifa ya kijana. Tusi kubwa kwa Obama mwaka 2008 lilikuwa ni kukosa uzoefu, kukosa rekodi. Tusi hilo lilikuwa muziki kwa wapiga kura wa Marekani. Tanzania mpya inahitaji viongozi wapya, mazoea mapya, fikra mpya na maarifa mapya. Inahitaji kuthubutu mambo makubwa sio kulinda uzoefu wa nyuma. Tunaweza, aliandika January Makamba kwenye mtandao wa Facebook. Ni kweli muda wa vijana ni sasa na sio kesho tena.

    Maswali
    (a) Ipe makala hii anwani mwafaka.
    (b) Ni wakati gani ambapo vijana huwa hatarini sana kukumbwa na tatizo la afya ya akilini.
    c) Ni nini lengo la Umoja wa Mataifa mwaka huu kuhusu vijana?
    d) Taja changamoto zinazowakumba vijana wenye matatizo ya afya ya akili.
    e) Eleza mambo ambayo huchangia matatizo ya afya ya akili miongoni mwa vijana.
    f) Taja mambo ambayo huchangia kutamauka kwa vijana.
    g) Ukosefu wa ajira umechangia uozo upi miongoni mwa vijana?

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Eleza jinsi mbinu ya kwelikinzani imetumika kwa kurejelea riwaya ya "kidagaa kimemwozea".(Solved)

    Eleza jinsi mbinu ya kwelikinzani imetumika kwa kurejelea riwaya ya "kidagaa kimemwozea".

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)