Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Uhifadhi wa mazingira una manufaa mengi kwa binadamu .Thibitisha

Uhifadhi wa mazingira una manufaa mengi kwa binadamu .Thibitisha

Answers


Wilfred
- Kuwepo kwa miti - Ivutayo mvua,Ipayo chakula ,dawa.n.k.
- Hutupa mbao za ujenzi.
- Tabaka la Ozoni likihifadhiwa tutakingwa dhidi ya miale ya jua isababishayo kansa ya ngozi.n.k.
- Binadamu atakuwa na afya nzuri kutokana na hewa safi yenye oksjeni.
- Uhifadhi wa misitu utazuia maporomoko ya ardhi yasababishayo vifo na uharibifu mkubwa.
- Misitu pia itasaidia kuzuia gharika iletayo maafa.
- Wanyama na mimea itakua bila matatizo yatokanayo na kemikali hatari na takataka nyingine.
- Mito na maziwa na maji safi.
Wilfykil answered the question on October 2, 2019 at 10:01

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Nchi nyingi duniani zimetia saini mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto. (Solved)

    Soma taarifa ifatayo kwa makini kisha ujibu maswali yanayofuata.
    Nchi nyingi duniani zimetia saini mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto.
    Haki ni mambo mema ambayo watoto wanastahili kutendewa. Kwa kutia saini, nchi hizizimetangaza kujitolea kwao kuzilinda na kuhahakikisha kuwa hakuna ukiukaji wake nakuwa watoto wote katika himaya zao wananufaika kutokana na haki hizi.
    Miongoni mwa haki hizi ni kuwa kila mtoto ana haki ya kuishi na kupata chakula cha kutosha na chenye viinilishe bora. Pili, kila mtoto ana haki ya kupata elimu. Elimu hii inafaa kutolewa bila ada na iwe inayofaa na inayopatikana kwa urahisi.Kisha kila mtoto ana haki ya kutopigwa na kutodunishwa kwa namna yoyote, iwe kitabaka, kirangi, kijinsia na vinginevyo. Mtoto ana haki pia kutolazimishwa kufanya kazi za kiutumwa, nzito na zakushurutishwa. Hali kadhalika, ana haki ya kuishi katika nyumba au makazi bora nasalama, kutunzwa na kulindwa dhidiya hali yoyote inayoweza kumhatarisha. Anatakiwa ashirikishwe katika kufanya maamuzi.Fauka ya haya, ana haki ya kupata huduma za afya,mahitaji maalum,michezo, upendo na habari. Isitoshe,anastahili kuheshimiwa kimawazo na kihisia. Haki hizi zinatakiwa kulindwa na kila mwanajamii, hivyo serikali za mataifa mengi zimeshirikisha haki hizi katika katiba za nchi zao na sheria zao.
    Walakini haki hizi bado zinakiukwa.Watoto wengi kote duniani bado wananyimwa haki zao. La kusikitisha na kukera ni kuwa wanaotarajiwa kuwa vigogo vya kuzilinda haki hizi, ndio wanaoongoza kuzikiuka. Kila siku tunasikia na kushuhudia visa vya watoto kupigwa, kunyimwa chakula, kufanyishwa kazi kipunda, kuteswa, kuishi katika mazingira hatari, na hata kuuawa. Kuna watoto wengi wanaolala nje, wengine hawapati chakula licha ya kuwa wanatakiwa kupata chenye lishe bora. Kwao kutarajiwa mlo awamu tatu kwa siku ni njozi kwani hata awamu moja ni adimu kupata.
    Watoto wengi katika mataifa yenye fujo na ghasia hutekwa na kutumikishwa vitani. Viongozi katika mataifa haya hawafanyi kitu ila kutazama tu wakati watoto wanaotakiwa kuwalinda wanageuzwa kuwa mibaba ya kuua na kuuana. Watoto hawa huvishwa magwanda ambayo miili yao minyonge haiwezi kuyahimili. Pia, huvalishwa mabuti ya kijeshi ambayo ni mizigo mizito ya kubeba mbali na bunduki zinazokaribia kuwazidi uzani wakati wanatakiwa kuwa wamelindwa majumbani, na shuleni na wazazi wao na serikali.
    Jukwaa la vijiji vya mataifa ya ulimwengu wa tatu limesheheni watoto wasioenda shule kwa sababu ya lindi la ufukara uliokithiri. Elimu ya bure inayogusiwa katika haki za watoto haipo. Wanaong‘ang‘ana iwepo ni kana kwamba ni waota ndotomchana. Jiulize watoto wangapi sasa hivi wamo majumbani bila kwenda shuleni kutokana na ukosefu wa karo? Wangapi wamo mitaani wakivuta na kunusa gundi huku wakiombaomba vishilingi?
    Hali ilivyo sasa hivi inadai kuwa mimi na wewe tufanye hima na kuungana mikono kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu haki za watoto. Twapasa kuhimiza serikali zetu kufanya kila ziwezavyo kuhakikisha kuwa watoto wote wamo shuleni. Nasi tushirikiane kutoa huduma kwa watoto na kukomesha dhuluma, mateso na dhiki kwao. Haitoshi kupeleka miswada mbungeni kuhusu haki za watoto na kuipitisha kuwa sheria. Twastahili kubadilisha misimamo yetu kuhusu haki hizi na kuzilinda kwa dhati bali si kwa chati.
    Maswali
    a) Fupisha aya mbili za kwanza. ( maneno 65-70)
    b) Eleza ni vipi ukiukaji wa haki za watoto unaweza kuepukwa . ( maneno 30-35)

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Alipokuwa akiukemea utamaduni na dhana za kikabila katika nyimbo zake, marehemu Bob Marley aliufananisha ubepari na "wanyama wala watu." (Solved)

    Soma taarifa hii kisha ujibu maswali yanayofuata.

    Alipokuwa akiukemea utamaduni na dhana za kikabila katika nyimbo zake, marehemu Bob Marley aliufananisha ubepari na "wanyama wala watu." Katika wimbo "Babylon System" (yaani mfumo wa kibepari), Marley alisema kuwa utamaduni huo ndio mzawa wa matatizo yote ya kiutawala ambayo yalikuwa yakiyakumba mataifa ya Weusi katika karne ya 20, wakati nchi zao zilikuwa zikitawaliwa na nchi za mataifa ya Ulaya.
    Kwa mantiki hiyo, pengine Marley alikuwa na maono kuwa Afrika haingejikomboa kutoka kwa utumwa wa Kizungu, ikiwa ingeendelea kuziabudu na kuzishadidia tamaduni za Kimagharibi.
    Utabiri huo nauoanisha na yanayoendelea nchini, ambapo serikali ya Jubilee imeonekana kushindwa kabisa kuikabili saratani ya ufisadi, ambayo inahatarisha kuliangamiza taifa hili lenye uchumi dhalili.
    Donda hili linazidi kuyatandaza mabawa yake kutoka, tisho kuu likiwa ni uvamizi wa taasisi ―takatifu‖ ambazo tunazitegemea kulikabili donda hilo.
    Ni nani tutategemea kukabiliana na rushwa ikiwa taasisi kama Bunge, Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC) kati ya zingine muhimu zimepakwa tope na saratani hiyo?
    Kimsingi yote tunayopitia ni matunda ya uasi wa tamaduni za Kiafrika na uegemezi wa mifumo ya Kizungu kama mihimili ya jamii na nchi zetu.
    Ndoto za watetezi wa Uafrika na nafasi ya Weusi kama marehemu Malcom X na Martin Luther King, zilikuwa ni kuona kuwa wameungana kabisa kukabiliana na matatizo yaliyowakabili bila kuzingatia mazingara waliyokuwemo.
    Pindi tu baada ya mataifa mengi ya Kiafrika kujinyakulia uhuru wao katika miaka ya hamsini na sitini, viongozi wakuu walioziongoza nchi hizo kama Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Mwalimu Julius Kibarage Nyerere kati ya wengine walianza harakati za kuliunganisha bara hili na kubuni Muungano wa Nchi za Kiafrika (OAU) japo ndoto hiyo haikufikia.
    Kwa msingi huo, mhimili mkuu wa kiutawala ungekuwa ni mfumo wa kisosholisti, ambao ungekuwa nguzo kuu ya kuyaunganisha mataifa hayo.
    Hata hivyo, migawanyiko mikubwa ilianza kushuhudiwa, huku baadhi ya mataifa yakianza kukabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kutaasisika kwa maovu yote tunayoshuhudia sasa: ufisadi na tamaa ya kuogofya kutoka kwa viongozi wetu.

    Maswali
    a. Ipe taarifa hii anwani mwafaka.
    b. Onyesha mambo mawili makuu ambayo msanii aliyapinga .
    c. Kwa nini ubepari umelinganishwa na "wanyama wala watu"?
    d. Kwa mujibu wa taarifa eleza sifa za Bob Marley.
    e. Swala linalozungumziwa limerejelewa kama "Donda".
    i) Eleza mbinu ya lugha iliyotumika..
    ii) Ni kweli kuwa donda hili laelekea kuwa gumu? Thibitisha.
    f. Tatizo hili la "donda" ni kama kujipalia makaa. Fafanua.
    g. Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa taarifa.
    i) Mhimili
    ii). Taasisi

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • …ya leo ni kuwapa pole wanaofuata na kuenzi makala ya Burudani,toleo la kila Ijumaa.Mwanamziki huyu aliteka nyoyo za wapenzi wa mtindo huu wa mziki.Kwa kweli... (Solved)

    …ya leo ni kuwapa pole wanaofuata na kuenzi makala ya Burudani,toleo la kila Ijumaa.Mwanamziki huyu aliteka nyoyo za wapenzi wa mtindo huu wa mziki.Kwa kweli ya Muumba hufumbwa tu!Mnapoyasoma wakumbukeni jamaa na wapenzi wa nyimbo zake.
    (i) Tambua sajili hii na utoe Ushahidi.
    (ii) Fafanua sifa zozote za sajili hii.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Andika kwa usemi wa taarifa. "Nitakuja kwenu kesho," Mwalimu alisema. (Solved)

    Andika kwa usemi wa taarifa.
    "Nitakuja kwenu kesho," Mwalimu alisema.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha hali katika sentensi zifuatazo. (i) Huenda mvua isinyeshe msimu huu. (ii) Waislamu huenda msikitini kuomba kila Ijumaa. (Solved)

    Onyesha hali katika sentensi zifuatazo.
    (i) Huenda mvua isinyeshe msimu huu.
    (ii) Waislamu huenda msikitini kuomba kila Ijumaa.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Tambua viambishi awali na tamati katika neno ajaye (Solved)

    Tambua viambishi awali na tamati katika neno ajaye

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Maneno yafuatayo yako katika ngeli gani. Kero. Nywele. (Solved)

    Maneno yafuatayo yako katika ngeli gani.
    Kero.
    Nywele.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza matumizi ya ku katika jozi zifuatazo za sentensi. (Solved)

    Eleza matumizi ya ku katika jozi zifuatazo za sentensi.
    (i) Kuchora kwao kulikuwa kwa uangalifu mkubwa
    (ii) Nilikuita lakini hukuitika

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika umoja. Manukato haya yananukia vizuri (Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika umoja.
    Manukato haya yananukia vizuri

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Bainisha aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo. (Solved)

    Bainisha aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo.
    Kuimba kwa Yusufu kunaudhi

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Akifika sentensi ifuatayo kwa kutumia alama ya kibainishi kisha eleza matumizi yake. Ntakwenda Unguja mwezi wa Disemba (Solved)

    Akifika sentensi ifuatayo kwa kutumia alama ya kibainishi kisha eleza matumizi yake.
    Ntakwenda Unguja mwezi wa Disemba

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika kauli iliyo mabanoni. Paka analamba mchuzi (kutendwa) (Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika kauli iliyo mabanoni.
    Paka analamba mchuzi (kutendwa)

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Inaaminika kuwa majeruhi wengi katika mikasa ya ajali huaga au huathirika vibaya zaidi kutokana na hali mbaya ya uokoaji. (Solved)

    Utoaji wa Huduma ya Kwanza.

    Inaaminika kuwa majeruhi wengi katika mikasa ya ajali huaga au huathirika vibaya zaidi kutokana na hali mbaya ya uokoaji. Watu wengi ambao hujitolea kuokoa majeruhi baada ya ajali kama za barabarani, maporomoko ya ardhi au nyumba huwa hawang‘amui hata chembe jinsi ya kukabiliana na uokoaji. Hatima ya juhudi zao ambazo hulenga kutenda mema ni kuathirika zaidi kwa majeruhi.
    Hali ya ukoaji inaweza kurekebishwa kwa kutoa elimu ya huduma ya kwanza kwa umma. Elimu hii yahitajika na kila Mkenya kwani mikasa ya ajali za barabarani na nyinginezo inaendelea kutokea kila siku.Ajali zinapotokea, si ajabu kuona makundi ya waokoaji yakibeba majeruhi hobelahobela bila kuzingatia madhara yanayoweza kuwaongezea kutokana na ubebaji wao. Kutojua namna ya kumbeba majeruhi kunaweza kumhatarisha na hata kusababisha kifo.
    Kuna mambo mbalimbali ambayo makundi ya waokoaji yanatakiwa kuzingatia wakati yanatoa huduma ya kuokoa. Kwanza, ni muhimu kuchunguza kama kuna hatari yoyote inayoweza ikatokea na kuwatia majeruhi na waokoaji hatarini zaidi. Makundi ya waokoaji yameweza kuhatarisha majeruhi kwa kuliingilia eneo la ajali mbumbumbu kama mzungu wa reli.
    Hatua ya pili ni kutafuta idadi ya majeruhi. Pana uwezekano wa majeruhi kutupwa mbali na eneo la ajali. Vivyo hivyo, kuna majeruhi ambao huweweseka baada ya ajali na kuanza kutembea wasijue wanakoelekea. Wengi wao huanguka karibu na eneo la ajali au wakaenda mbali.
    Hatua ya tatu ni kuchunguza kama majeruhi amezimia, moyo unapiga na jinsi anavyopumua. Ili kuhakikisha kuwa majeruhi anapumua, mwokoaji atazame kama kifua kinapanda na kushuka. Halikadhalika, mwokoaji anaweza kusikiliza au kuguza kifua na kuona kama kuna ishara za kupumua. Iwapo majeruhi anapumua, mwokoaji amweke katika hali ambayo itaimarisha kupumua kwake. Anaweza akamlaza chali au kumgeuza kwa pamoja na kichwa chake ili kufungua mkondo wa hewa. Pia, mwokoaji ahakikishe hamna chochote kinywani kinachoweza kumsakama. Ikiwa hapumui, mwokoaji anaweza kujaribu kumfanya apumue kwa kupuliza hewa mdomoni mwake. Fauka ya hayo, upulizaji wa hewa utahakikisha kuwa damu inazunguka mwilini vizuri.
    Maswali :
    (a) Fupisha aya mbili za kwanza kwa maneno 55 – 65.
    (b) Eleza kwa kutumia maneno 90-100, hatua zinazotakiwa kufuatwa wakati wa uokoaji.

    Date posted: October 2, 2019 .    Answers (1)

  • Zitavuma, Zitakoma, Nitakwima, Mti-mle. (Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Zitavuma,
    Zitakoma,
    Nitakwima,
    Mti-mle.

    Na muda nikisimama,
    Nitatongoa nudhuma,
    Kwa tenzi zilizo njema,
    Nilisifu mti – mle.

    Tazipanga tathlitha, tungo zilizo na hekima,
    Za huba na thiatha, za kuburudi mitima,
    Mashairi mabuthutha, musome mnaosoma.

    Mti nishainukia,namea kuwa mzima,
    Mizizi yadidimia, ardhini imeuma,
    Nanena kitarbia, tungo zilizo adhama
    Japo ni tungo za zama, mti-mle hutumia.

    Zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,
    Dharuba kinitikisa, mti-mle huinama,
    Huyumba nikaziasa, matawi yakakingama,
    Gharika ikishapisa, hurudi nikawa wima,
    Na tungo za takhimisa, mti-mle huzipima.

    Maswali
    (1) Shairi hili ni la kimapokea. Toa sababu mbili kuunga kauli hii.
    (2) Taja bahari kuu ya ushairi ambayo imetumiwa na mshairi. Fafanua.
    (3) Fafanua dhamira ya mshairi.
    (4) Kwa kutoa mifano bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili.
    (5) Eleza jinsi mshairi ametumia idhini ya ushairi katika utungo huu.
    (6) Andika ubeti wa nne kwa lugha natharia.
    (7) Mshairi anamaanisha nini anaposema "zingavuma zitapusa, pepo kali zitakoma,"
    (8) Eleza toni ya shairi hili.
    (9) Eleza maana ya msamiati ufuatao.
    i) Nitatongoa
    ii) Zitapusa.

    Date posted: October 1, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza matatizo yanayomkabili mtu anapoitumia lugha yoyote isipokuwa ile ya kwanza. (Solved)

    Eleza matatizo yanayomkabili mtu anapoitumia lugha yoyote isipokuwa ile ya kwanza.

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Fafanua mambo matano yanaosababisha kutokea kwa lahaja. (Solved)

    Fafanua mambo matano yanaosababisha kutokea kwa lahaja.

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Andika kwa wingi. Mimi ndimi shangazi yake. (Solved)

    Andika kwa wingi.
    Mimi ndimi shangazi yake.

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Andika katika hali ya udogo: Mvulana yule alibeba kiti kikubwa (Solved)

    Andika katika hali ya udogo:
    Mvulana yule alibeba kiti kikubwa

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Taja sauti zinazotamkiwa kwenye ufizi. (Solved)

    Taja sauti zinazotamkiwa kwenye ufizi.

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)

  • Onyesha vishazi tegemezi na vishazi huru katika sentensi ifuatayo. Nilimwona Agwambo nilipofika Mombasa (Solved)

    Onyesha vishazi tegemezi na vishazi huru katika sentensi ifuatayo.
    Nilimwona Agwambo nilipofika Mombasa

    Date posted: September 28, 2019 .    Answers (1)