Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
(a)
(i) Lugha ni mfumo wa mawasiliano .
(ii) Imeanza tangu chanzo / kuwepo kwa binadamu.
(b)
(i) Lugha ya taifa ni lugha inayoteuliwa kutumika katika shughuli zote za taifa.
(ii) Hueneza umoja na uelewano miongoni mwa jamii nyingi tofauti.
(iii) Lugha ya kikazi ni lugha inayotumiwa kuendesha shughuli rasmi za taifa.
(c)
(i) Ili kuenezea maongozi ya taifa.
(ii) Ili kuleta ufahamikiano kote nchini.
(iii) Ili kukomesha hisia za kibinafsi na kikabila.
(iv) Ili kuunda moyo wa uaminifu.
(d)
(i) Kuendeshea elimu.
(ii) Katika maandishi
(iii) Katika siasa.
(iv) Katika biashara.
(v) Kuenezea maongozi.
(e)
(i) Matendo na hulka za binadamu / watu.
(ii) Mazingira ya watu / mazingira wanamoishi binadamu.
(iii) Haiwezekani / Haitawezekana.
(f)
(i) Ni chombo cha mawasiliano.
(ii) Ni kielelezo cha fikra na hisia za binadamu
sharon kalunda answered the question on October 2, 2019 at 11:09
- Taja madhumuni ya kusanifisha lugha ya Kiswahili nchini(Solved)
Taja madhumuni ya kusanifisha lugha ya Kiswahili nchini
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali(Solved)
Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali
Mwanafunzi aliyeondoka jana alishindwa kumwona
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Kanusha
Akimaliza kucheza mwite(Solved)
Kanusha
Akimaliza kucheza mwite
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Bainisha matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mistari katika sentensi(Solved)
Bainisha matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mistari katika sentensi
i)Yego ana ujuzi mwingi
ii) Yule mfanyibiashara aliyejidanganya amepata hasara
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi sahihi kuonyesha wakati uliopo usiodhihirika(Solved)
Tunga sentensi sahihi kuonyesha wakati uliopo usiodhihirika
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Akifisha sentensi:
lo unaweza kuubeba mzigo huo pekeyo mzee alishangaa(Solved)
Akifisha sentensi:
lo unaweza kuubeba mzigo huo pekeyo mzee alishangaa
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli kwenye mabano(Solved)
Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli kwenye mabano
1. Oa (kufanyiza)
2. -la- (kufanyana )
3. Dhuru (fanyika)
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Andika upya sentensi zifuatazo kwa kutumia jina jingine lililo na maana sawa na lililopigiwa mstari(Solved)
Andika upya sentensi zifuatazo kwa kutumia jina jingine lililo na maana sawa na lililopigiwa mstari
i. Ni nadra sana kumpata msichana asiyetoga masikio siku hizi
ii. Zahama ilizuka wafanyikazi walipogoma
iii. Lengo la kila mwanafunzi ni kupasi mtihani
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Tumia neno vizuri kama:(Solved)
Tumia neno vizuri kama:
i) Kielezi
ii)Kiwakilishi
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Weka shadda kwa neno WALAKINI ili kuonyesha maana mbili(Solved)
Weka shadda kwa neno WALAKINI ili kuonyesha maana mbili
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Tumia ‘po’ kutunga sentensi ya kuleta dhana ya wakati maalum(Solved)
Tumia ‘po’ kutunga sentensi ya kuleta dhana ya wakati maalum
i) Wakati maalum
ii) Wakati usiodhihirika
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi yenye maneno N + V + E + E + T + N(Solved)
Tunga sentensi yenye maneno N + V + E + E + T + N
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Toa mifano miwili ya aina za nomino zifuatazo(Solved)
Toa mifano miwili ya aina za nomino zifuatazo
i)nomino mseto
ii) nomino za wingi
iii) nomino za fikra
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Tumia kivumishi cha a- unganifu pamoja na nomino katika ngeli ya I-I kutunga sentensi(Solved)
Tumia kivumishi cha a- unganifu pamoja na nomino katika ngeli ya I-I kutunga sentensi
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.(Solved)
Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
“Mimi nitawakaribisha wageni leo jioni. Kisha nitaondoka kwenda kwangu kesho.” Fatuma alimwambia juma.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Ainisha viambishi katika neno HAKUJULIKANA(Solved)
Ainisha viambishi katika neno HAKUJULIKANA
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Eleza maana ya kiambishi(Solved)
Eleza maana ya kiambishi
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii, na kwa dhati ya mioyo yetu tuweze kupata ufanisi, na uwezekano wa kuinua nchi yetu...(Solved)
Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii, na kwa dhati ya mioyo yetu tuweze kupata ufanisi, na uwezekano wa kuinua nchi yetu changa katika kiwango cha juu. Tukumbuke, “Ajizi ni nyumba ya njaa” Kwa hivyo basi haifai kulaza damu ikiwa matatizo nchini mwetu yametuzonga. Lazima tufanye kazi kwa busara, adabu njema na jitihada kwa moyo mmoja. Sharti tutilie maanani zaidi elimu ya vijana na watu wazima,kilimo,uchumi na amani katika nchi yetu vigumu sana kuweza kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Tupende tusipende lazima tizidishe mazao kilimo, uchumi na amani katika nchi yetu. Tunahitaji taifa lenye watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kuweza kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Tupende tusipende lazima tuzidishe mazao mashambani kwani kila kukicha idadi ya watu inaongezeka, Ni sharti tuweze kujitosheleza katika vyakula. Zaidi ya haya pia lazima tujishughulishe na biashara ambapo kwa sasa ni Wakenya wachache sana ambao wanatambua umuhimu wa biashara. Wengi ni wale wenye mawazo ya kwamba, lazima kila mmoja aajiriwe maishani. Yatupasa tujitahidi kuleta uchumi katika mikono ya wananchi wa Kenya badala ya kuwaachia wengine ambao hawahusiki.
Mafunzo tunayopata majumbani, shuleni na hata katika jamii, lazima yatuwezeshe kutambua mbinu za kupitia. Tunahitaji elimu tambuzi ambayo itamfanya Mwanakena kujua wajibu wake katika jamii. Tumesinywa na elimu pumbao; inayotupumbaza na kutufanya tusione mbele. Sisi vijana tukiwa viongozi wa ‘utengano ni uvundo’, lugha ya taifa ndicho chombo cha pekee ambacho kinatuunganisha na kuweza kutuwasilishia mapendekeza, mawaidha ni hisia zetu. Kukosa ndiko binadamu, wakati tunapokosea, lazima tukubali tumekosea na kufanya masahihisho mara moja. “Kwani usipoziba ufa, utajenga ukuta”. Tusikasirike kwa sababu tumesahihishwa makosa yetu tukiwa wazalendo halisi.
Sisi tukiwa vijana sharti tujishughukishe na kuyaangalia matatizo ya nchi, pia kutafuta njia za kutatua matatizo hayo. Siku zote tutekeleze nidhamu.Ni jambo la kusikitisha kwamba sisi vijana twashutumiwa mara kwa mara kwa kutokuwa na nidhamu shuileni na majumbani mwetu.Utamaduni wa assili unanakariri sana kuwa tuwe na nidhamu shuleni na majumbani mwetu.Ili watu waweze kuishi maisha bora na kuwa na maendeleo,amani na upendo lazima tuwe na bidii,ushirikiano mwema na kuchagua viongozi wenye mioyo ya maendeleo.Tukiwa viongozi ambao hawajishughulishi na maendeleo,basi tutabaki nyuma kama mkia kila siku zote.Bahati mbaya ni kwamba wananchi wengi siku hizi huchagua viongozi wao kwa kufuata ukoo ama kama kwa utajiri wake.Kwa hivyo basi tuchagueni viongozi ambao watatuletea ufanisi badala ya viongozi wanaotokana na sababu kubwa au ya utajiri.
a) Ni nini dhamira ya mwandishi?
b) Katika aya ya kwanza, mwandishi anawahimiza vijana kufanya nini ili kuleta maendeleo nchini?
c) Ni mambo gani yaliyochangia, kuzorota kwa maendeleo nchini Kenya kwa mujibu wa taarifa?
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Siku ya kuzungumza gharama za serikali katika bunge hungojewa kwa pashau kubwa.(Solved)
Siku ya kuzungumza gharama za serikali katika bunge hungojewa kwa pashau kubwa. Maana kwa hakika siku hiyo ndiyo inayomuathiri kila mtu kwani ndipo serikali inapomchakuria mifuko na vibindo vyake. Wiki nzima kabla ya hapo huwa Waziri wa Hazina na Maendeleo ya Uchumi amekwisha onyesha kiasi kadha wa kadha kitahitajiwa katika mwaka kuikuza elimu ya wananchi – kwa idadi ya skuli zilioko mpaka sasa, vifaa na ala zihitajiwazo, waalimu watakiwao, shule gani mpya za aina gani zataka kujengwa na zitagharimu Serikali kiasi gani, na kadhalika. Wizara ya Afya itahitajia milioni kadha wa kadha kuongeza mavuno ya konde na mazao ya nyanyangu. Basi hivyo Waziri anaendelea kudondoa makisio ya kila wizara kinaganaga na viwango vya fedha zinazodhamiriwa kutumiwa kutosheleza kila kinacholazimu.
Basi juma hilo lote huwa wafanyibiashara wanavuna kwa wanunuzi; namna biashara inayokwenda ni ajabu maana wanunuzi huwa wananunua kila kitu ambacho wanachelea kitabandikwa ushuru. Wafanyi biashara ndio wanaowatia hofu kuwa bidhaa zitapanda bei.Wachuuzi wa magari huwa wanatangaza kuwa wamepata fununu ‘mwaka huu ushuru wa magari utapandishwa mpaka thalathini katika mia. Basi patilizeni kabla siku hiyo maana baada ya hapo bei itakuwa haishikiki.’
Wauzaji mapombe nao huwa na vishindo vyao: “Kodi ya forodha ya kila aina ya mvinyo itokayo ugenini itaongezwa ishirini kila mia, na pombe za kienyeji zitapandishwa peni kila chupa.’ Sigara nazo pia zaambiwa zitapanda: Fulani amedokezwa kuwa kila pakiti itazidishwa bei kwa mapeni mawili.
Mradi, mlolongo wa bidhaa hupandishwa ushuru mkubwa kabla ya siku yenyewe haijafika.Basi angalia kufundika huko! Kande za vyakula na vifaa aina aina hununuliwa vikawekwa kwa kuchelea kuwa vitaongezwa bei au pengine vitakuwa adimu. Wafanyi biashara nao huwa wamekwisha ‘piga pua’ kuwa vitu fulani vitaekewa ushuru. Basi huvinunua kwa wingi wakavitutiza maghalani mwao kwa bei ya tahafifu kabla ya kuongezwa ushuru na baada ya kupandishwa kodi, huviuza kwa bei mpya.
Ikifikia hiyo siku kila mtu mwenye hamu ya mambo ya kilimwengu huwa amechachawa kukimbilia penye redio kusikiliza hotuba ya waziri wa Fedha.Ikishamalizika huwa kila mtu akishusha pumzi,maana huwa mbichi na mbivu ishajulikana na kwa upande wake anaona hakuelemewa sana.
a) Toa anwani mwafaka kwa taarifa uliyoisoma
b) Taja wizara ambazo zimetajwa kwenye taarifa
c) Ni mambo gani huzingatiwa katika makisio ya masomo
d) Unadhani ni sababu zipi zichangiazo mavuno ya wafanya biashara kabla ya kusomwa makadirio ya fedha
e) Wafanyi biashara hutumia mbinu gani ili kujipa faida zaidi
f) Kuvumbika bidhaa maghalani si ufanyaji biashara halali. Toa maoni yako
g) Eleza maana ya vifungu hivi kama vilivyotumiwa katika muktadha wa habari hii
i. Fununu
ii. Siha
iii. Mbichi na mbivu
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Uhifadhi wa mazingira una manufaa mengi kwa binadamu .Thibitisha(Solved)
Uhifadhi wa mazingira una manufaa mengi kwa binadamu .Thibitisha
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)