a) - Kisa
- Kisa changu
- Simu
- Matokeo ya uzembe / simu. (yoyote moja 1 x 1 = alama 1)
(b) Tashbihi - Mtihani kama chatu.
- Nilikimya kama bubu.
- Mithili popo.
Misemo - Sikupigeni msasa.
Jazanda / Sitiari - Kunoa kisu
- Tausi
- Sikukata cha darasa
Maswala ya balagha – ningalilindaje utu?
Za kwanza mbili – za mwanafunzi
Kutaja – alama 1, Mfano alama
(c) - Wanafunzi / wasomi / watahiniwa.
(d) - Matumizi ya beti.
- Matumizi ya mishororo (Idadi maalum)
- Matumizi ya vipande.
- Matumizi ya mizani (idadi maalum)
- Matumizi ya vina.
- Utoshelezaji wa beti.
(e) - Msimulizi / mshairi / mtunzi anasema kuwa / anaeleza aliyangoja matokeo (kwa) akiwa na hamu kubwa.
- Anaongezea kuwa ilibidi awe kimya / anyamaze kama bubu ili asije akatoa aibu.
- Anazidi kusema kuwa alivichoma vitabu bila sababu.
- Anamaliza kuwa kisa kilikuwa masaibu / shida hata akashindwa kuyaharibu / kusuluhisha.
(f) Inkisari – ilijipambiya – nilijipambiya.
- Uzembea – nilizembea
- Tajaribu – atajaribu
- Litolewa – zilitolewa
Tabdila - Nilingiya - niliingia
- Kufurahiya – kafurahiya
- Meingiya – meingia
- Kujiwa – kujua
- Lijipambiya – lijipambia
Kuboronga sarufi / sintaksia ngeu
- Dafu sikufua – sikufua dafu
- Tulikata dari ona – ona tulikata dari
- Usiku tulikutana – tulikutana usiku.
Utohozi - Nilifeli.
(g) (i) Sikukata cha darasa – sikufaulu / sikupata chochote darasani.
(ii) Yalinitia kimbio – nilingiwa na wasiwasi sikutulia.
(iii) Kupagawa – kuingiwa na wazimu / kukosa kujielewa.
sharon kalunda answered the question on October 2, 2019 at 11:23
- "Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"(Solved)
Damu nyeusi na hadithi zingine
"Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili.
c) Huku ukitoa mifano, thibitisha maudhui sita ambayo yamejitokeza katika hadithi ya Damu Nyeusi na wanayoyaendeleza.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Kwa kutoa mifano kumi,eleza vizingiti walivyokumbana navyo wanacheneo wakati wa kupigania mageuzi.(Solved)
Mstahiki Meya
Kwa kutoa mifano kumi,eleza vizingiti walivyokumbana navyo wanacheneo wakati wa kupigania mageuzi.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Iwapo umefanya, yapo mengi ambayo hayakunyoka."(Solved)
Mstahiki Meya
"Iwapo umefanya, yapo mengi ambayo hayakunyoka."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Tambua mbinu moja iliyotumika katika muktadha wa dondoo.
c) Fafanua kauli kwamba"yapo mengi ambayo hayakunyoka".
d) Eleza jinsi baadhi ya wahusika walivyojaribu kuyanyoosha.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Ni nini sifa za mvuto zinazowaleta pamoja mzungumzaji na mzungumziwa.
c) Tambua na ufafanue mbinu inayotumika katika dondoo.
d) Kwa mifano mwafaka fafanua tanzia hiyo inayorejelewa katika dondoo.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Ikamchagiza kama vile kiu ya mtu aliyekuwa akisafiri jangwani".(Solved)
DAMU NYEUSI
"Ikamchagiza kama vile kiu ya mtu aliyekuwa akisafiri jangwani".
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili
(b) Fafanua sifa zozote nne za mrejelewa
(c) Eleza fani uliotumiwa na mwandishi katika dondoo hili
(d) Kwa kurejea hadithi zozote tatu,eleza namna wahusika wowote watatu walivyoathiriwa na kiu.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Nonsense! Hivi huyu ana nia gani?(Solved)
Mstahiki Meya
Nonsense! Hivi huyu ana nia gani?
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Taja na ueleze mbinu za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili.
(c) Jadili umuhimu wa msemaji katika tamthilia hii.
(d) Jadili njia za kuondoa uozo katika jamii ukijikita katika tamthilia ya Mstahiki Meya.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.(Solved)
Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.
(a) Jazanda
(b) Uzungumzi nafsia
(c) Majazi
(d) Methali
(e) Taharuki
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.(Solved)
Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine (Solved)
Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine
(i) Mke wangu
(ii) Damu Nyeusi
(iii) Tazamana na Mauti
(iv) Mizizi na matawi
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Ulimwengu wake ulivurugika akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"(Solved)
Kanda la usufi
"Ulimwengu wake ulivurugika akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"
(a) Eleza sifa zozote nne za mrejelewa
(b) Kwa nini mrejelewa amelinganisha na tiara iliyopeperushwa na upepo
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Alipofikishwa kwenye zahanati hakushughulikiwa ipasavyo.Ubwete ni ugonjwa mmoja mbaya walioambukizwa madaktari na wauguzi wengi Tomoko"(Solved)
"Alipofikishwa kwenye zahanati hakushughulikiwa ipasavyo.Ubwete ni ugonjwa mmoja mbaya walioambukizwa madaktari na wauguzi wengi Tomoko"
a) Eleza Muktadha wa dondoo hili.
b) Dhihirisha jinsi mtunzi alivyoitumia tamathali yoyote moja inayobainika kifunguni .
c) Riwaya Ya Kidagaa Kimemwozea ni muhtasari wa maradhi yanayolihujumu Bara Afrika.Tetea rai hii kwa mifano faafu riwayani.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)
"Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Jadili.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,(Solved)
Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali.
SIKUJUA!
1. Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,
Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama,
Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama.
2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima,
Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama,
Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma.
3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima,
Chakula siyo matata, ni machicha na mtama,
Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima.
4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima,
Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma,
Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma.
Kiitikio
Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida
SHAIRI B
Afrika na Watu Wake
Mimi ninaona mgonjwa
Bado amelala kitandani.
Kama hatutamtoa miiba iliyobaki
Mgonjwa hataweka miguu yake chini
Ili kutembea bila ya kujiegemeza.
Miiba iliyomo ndani mwetu lazima
Pia iondolewe upesi kabla haijaingia
Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi.
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma
Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi.
Lakini kuitoa miiba hii
Tunahitaji macho makali
Mikono isiyotetemeka
Moyo usio na huruma
Na kuona miiba ilipoingilia.
MASWALI
(a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B unavyokatisha tamaa.
(b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B.
Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma.
(c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B.
(d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi Mshairi alivyotumia kibali chake.
(e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za aina hii.
(f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A?
(g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B.
(h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?(Solved)
SABUNI YA ROHO
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.
Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Umevunja usuhuba, familia zazozana,
Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Nitafukuzwa mbinguni
Kwa ushairi wangu mbaya
Lakini hata motoni nitaimba:(Solved)
Nitafukuzwa mbinguni
Kwa ushairi wangu mbaya
Lakini hata motoni nitaimba:
Wanasema
Wanasiasa ni kama jizi
Lililosukuma mtoto pembeni
Na kunyonya ziwa la mama
Wakati amelala usingizi usiku.
Wanasema
Mwanasiasa afapo
Tumejikomboa na domo
Moja pana lizibwalo na mchanga
Na kilima cha simenti ngumu
Lisikike tena hadharani.
Wanasema pia
Kusema haki
Kwa kawaida
Wanasiasa hatuwapendi.
Kupiga kura ni hasira za mkizi
Ni basi tu. Ni Ah!
Ah!
Wanamalizia
Nchi mmefiilisi waacheni walimu
Wakajenga taifa jipya.
Top grade predictor publishers Page | 63
Kama hamwezi kuona mbali
Bure kuweka mkono usoni,
Bure hakuna kichwa
Kama hamwezi kufikiri.
Ng‘ombe amekamuliwa na wazungu
Waarabu, wahindi na wao
Sasa anatoa damu
Vilivyobaki ni chai ya rangi
Na madomo mapana zaidi
Yaliyo bado hai.
Kuimba nimeimba
Maswali
(a) Mshairi ana dhamira gani?
(b) Shairi hili ni la kukatisha tama, tetea rai hii.
(c) Onyesha matumizi mawili ya mishata.
(d) Eleza mbinu zozote nne za lugha zilizotumika katika shairi hili.
(e) Andika ubeti wa mwisho katika lugha tutumbi.
(f) Fafanua umbo la shairi hili.
(g) Eleza maana ya mafungu ya maneno ya maneno yafuatayo:
(i) kupiga kura ni hasira ya mkizi
(ii) kuweka mkono usoni
(iii) ng‘ombe amekamuliwa.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.(Solved)
Mstahiki Meya
Jadili matumizi ya mbinu ya ishara katika tamthilia hii.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.(Solved)
MSTAHIKI MEYA: Timothy Arege
Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
Hayawezi kulinganishwa na tendo hili ndogo. Walifanya vizuri kuja.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua nafasi ya wanaorejelewa kuwa ―"walifanya vizuri kuja" katika tamthilia hii.
(c) Migogoro katika tamthilia hii hazikusuluhishwa vyema. Jadili.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.(Solved)
Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea imesheheni hali zinazotukia bila kutarajiwa. Fafanua.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?(Solved)
Kidagaa Kimemwozea:
"Nyamaza boza wewe. Wadhani sisi kazi tunaanza leo? Tumekutana na wauaji wangapi?
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Dondoo hili linadokeza maudhui gani? Kwa kutoa mifano saba kwenye riwaya, bainisha jinsi maudhui hayo yanavyojitokeza.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)
- "Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"(Solved)
Kanda la Usufi
"Hakujua maisha yake yangechukua mkondo upi. Mzo wa majuto ulimwandama. Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Taja na kueleza tamathali ya usemi kwenye dondoo hili.
(c) Kwa kutolea mifano, onyesha jinsi anwani Kanda la Usufi inavyoafiki hadithi husika.
Date posted: October 1, 2019. Answers (1)