
Mbinu ya majazi
Majina mengi ya wahusika yamejengwa kimajazi ambapo majina hayo yamebeba tabia za mhusika mwenyewe.
Ridhaa;
jina hili linabeba maana ya hali ya kukubali au kutosheka na jambo Fulani. Mhusika Ridhaa anakubaliana na hali ya upweke uliomkuta baada ya kufiwa mkewe Terry,mwanawe Tila,mkaza mwana wake Lily na mjukuu wake Beky. Katika kukubaliana na hali hiyo,Ridhaa anaacha kundoa majivu ya miili hiyo iliyotekea kwa moto ili kukubaliana na hali hiyo Tenge; jina hili linarejelea kwenda kombo. Kitendo cha Bwana huyu hususan kitendo kitendo cha kuigiza wanawake ndani na kushiriki nao ufuska wakati mkewe ameenda kazini kinasawiri kabisajina lake.
Wahafidhina;
hili nalo ni jina la kimajazi likiirejelea jamii isiyotaka kubadili mtazamo wa mambo .Mwandishi ametumia jinahilo kwa kuwakatika jamii bado kuna watu wameshikilia msimamo kwamba mwanamke hawezi kupewa madaraka ya juu ya kiuongozi.
Msitu wa Heri;
hii ni ardhi iliyokuwans rutuba.Bwana Lunga-Kiriri Kangata aliweka makazi yake hapa akajikuta heri imemwangujia kutokana na kufaidi mazo ya kilimo. Hata hivyo,kitumbua kiliingia mchanga walipofurushwa na dola kwamba wanaishi hapo kiharamu.
Mwekevu Tendakazi;
jina Mwekevu limetokana na nenola Kiswahili “wekeza” lenye maana ya kufanya jambo Fulani kwa lengo la kuzalisha Zaidi baadaye.Jina Tendakazi ni mwambatano wa manen “tenda” na “kazi” kwa maana ya kufanya shughuli. Mwekevu Tendakazi aliweka juhudi nyingi katika kuwainua raia alipokuwa mkurugenzi wa Shirika la Chemchemi ambazobaadaye zlizaa matunda kwa wnanchi kumwamini na kumchagua
Majina mengine ya kimajazi ni kama vile Dhahabu,Mwenge,Chandachema,Hazina,Waridi,Subira,Neema,Nyangumi,Kipanga,Tindi na kadhalika
marto answered the question on October 2, 2019 at 11:49
-
Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata.
(Solved)
Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata.
SABUNI YA ROHO
Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
Ndiwe suluhu la zama, waja wa kukimbilia,
Waja wana kutazama, madeni wakalipia,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
Utanunua majoho, majumba na nyumbani
Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Matajiri wakujua, wema wako wameonja,
Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
Sura zao mefufua,wanazuru kila Nyanja,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
Watazame mayatima, kwao kumekua wa duni,
Wabebe waliokwama, wainue waliochini,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Ndiwe mvunja mlima, wapi kupata uwezo?
Umezua uhasama, waja kupata mizozo
Ndiwe chanzo cha zahama, umewaitia vikwamizo,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Umevunja usuhuba, familia zazozana,
Walokuwama habuba, kila mara wagombana,
Roho zao umekaba, majumbani wa chinjana,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
Niondoe jehanamu, ya ufukara wa sumu,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
Nichekeshe kibogoyo, name nipate kuwika,
Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima
Maswali
a) Mshairi anaongea na nani katika shairi hili?
.
b) Taja majina mengine matatu aliyopewa huyu anayesemeshwa
c) Anayezungumziwa katika shairi hili anasababisha balaa gani?
d) Mshairi anatoa mwito gani kwa mwenziwe?
e) Fafanua maudhui ya ubeti wa sita.
f) Mbinu kadha za uandishi zimetumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe wake. Taja mbinu zozote tatu na uzitolee mifano katika shairi.
g) Fafanua maana ya : sura zao ’mefufua, wanazuru kila nyanja’
h) Andika ubeti wa saba katika lugha nathari.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Lugha inaweza kuelezwa kwa jumla kuwa ni mfumo wa mawasiliano.
(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Lugha inaweza kuelezwa kwa jumla kuwa ni mfumo wa mawasiliano.Haiyamkiniki kwa mtu yeyote kueleza chanzo au kiini cha lugha na sote tunakubalina kuwa matumizi yake yameanza tangu kuumbwa kwa binadamu kwani ni vigumu kukisia kuwepo kwa jamii ya watu bila lugha ya mawasiliano yoyote ile.
Katika taifa lolote,huwapo na lugha moja au hata zaidi ya moja ambayo huwa ndicho chombo zatika cha mawasiliano ya taifa katika nyanja za:elimu maandishi,siasa na biashara.Kwa mfano mataifa ya Kanada hutumia lugha mbili kwa usawa kama lugha za taifa na za kikazi.Maana ya lugha ya taifa ni lugha moja ambayo huteuliwa kutumika katika shughuli zote za taifa hasa katika nchi yenye lugha nyingi za kikabila.Lugha ya taifa ni muhimu sana kwa maisha na maendeleo ya taifa lolote lile.Lugha hii huwa ndiyo kiungo cha kueneza umoja na uelewano miongoni mwa jamii nyingi tofauti na huwa kama kitambulisho kwao kwa kuwa wao ni ndugu wa jamii moja kubwa,yaani taifa lao.
Kenya ni mfano mzuri wa taifa lenye lugha nyingi zinazozidi 40 za vikundi vidogo vidogo vya kikabila.Hapo kabla ya miaka mia moja hivi iliyopita kila kimojawapo cha vikundi hivi kilijitambulisha kama kabila huru.Baada ya kuja kwa serikali ya kikoloni na hasa baada ya Kenya kujinyakulia uhuru,haja ya kuunganisha raia wote chini ya taifa moja lenye uongozi na shabaha moja ilikuwa ndilo jambo lililozingatiwa sana.Kwa hivyo utamaduni wa taifa Kenya ni mchanganyiko wa tamaduni za watu wengi wenye mila,desturi,imani na itikadi tofauti.Utamaduni humaanisha jumla ya amali na tabia za watu wa jamii fulani.Amali hizi zinafungamanisha fikira,ustaarabu,mila,taasisi na sanaa za aina zote za jamii inayohusika.
Ili kujieneza na kujiimarisha,taifa huhitaji chombo hicho kuwasiliana na kuwaunganisha watu wake wenye asili mbalimbali. Chombo hicho huwa ni lugha ambayo siyo tu kwamba ni sehemu ya utamaduni wa jamii bali pia ni njia muhimu sana ya kutawanyia na kustawishia ule utamaduni.
Katika taifa lenye lugha nyingi kama Kenya kwa mfano,lugha ya taifa inayozungumzwa na kueleweka na baadhi kubwa ya raia ambayo imekiuka mipaka na tofauti za kikabila ni njia muhimu sana ya kueneza maongozi ya taifa na kuleta ufahamikiano bora kote nchini.Kama
zilivyo taasisi kama wimbo wa taifa,bendera ya taifa au bunge la taifa, lugha ya taifa ndicho kielelezo cha taifa lolote lile.Lugha kama hiyo huvunja na hukomesha hisia za kibinafsi na kikabila na badala yake kuunda moyo wa uaminifu wa kitaifa.
Zaidi ya kuwa chombo cha mawasiliano,lugha ni kielelezo cha fikira na hisia za binadamu.Lugha ya watu fulani haituelezi tu ujuzi au maarifa yao bali pia mtazamo wao kimaisha,falsafa na mawazo yao.Kwa ufupi lugha hutufahamisha namna akili za watu waizungumzayo ile lugha zinavyofikiri na kufanya maazimio.Lugha ni sehemu ya utamaduni wa taifa tulimozaliwa na lazima lugha hiyo ifunzwe katika muktadha wa maisha ya jamii ihusikayo.Utamaduni wa jamii havitenganiki na lugha yake.
Maswali
(a) Huku ukirejelea kifungu, eleza fasiri na chanzo cha lugha.
(b) Tofautisha baina ya lugha ya taifa na lugha ya kikazi.
(c) Kwa nini lugha ya taifa huhitajika sana katika nchi kama Kenya.
(d) Eleza kazi nne kuu zinazotekelezwa na lugha ya taifa.
(e) Eleza maana ya mafungu yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa:
(i) Amali na tabia za watu:
(ii) Muktadha wa maisha ya jamii:
(iii) Haiyamkiniki:
(f)Eleza majukumu mawili ya lugha kwa ujumla
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Taja madhumuni ya kusanifisha lugha ya Kiswahili nchini
(Solved)
Taja madhumuni ya kusanifisha lugha ya Kiswahili nchini
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali
(Solved)
Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali
Mwanafunzi aliyeondoka jana alishindwa kumwona
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Bainisha matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mistari katika sentensi
(Solved)
Bainisha matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mistari katika sentensi
i)Yego ana ujuzi mwingi
ii) Yule mfanyibiashara aliyejidanganya amepata hasara
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Tunga sentensi sahihi kuonyesha wakati uliopo usiodhihirika
(Solved)
Tunga sentensi sahihi kuonyesha wakati uliopo usiodhihirika
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli kwenye mabano
(Solved)
Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli kwenye mabano
1. Oa (kufanyiza)
2. -la- (kufanyana )
3. Dhuru (fanyika)
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Andika upya sentensi zifuatazo kwa kutumia jina jingine lililo na maana sawa na lililopigiwa mstari
(Solved)
Andika upya sentensi zifuatazo kwa kutumia jina jingine lililo na maana sawa na lililopigiwa mstari
i. Ni nadra sana kumpata msichana asiyetoga masikio siku hizi
ii. Zahama ilizuka wafanyikazi walipogoma
iii. Lengo la kila mwanafunzi ni kupasi mtihani
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Tumia neno vizuri kama:
(Solved)
Tumia neno vizuri kama:
i) Kielezi
ii)Kiwakilishi
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Weka shadda kwa neno WALAKINI ili kuonyesha maana mbili
(Solved)
Weka shadda kwa neno WALAKINI ili kuonyesha maana mbili
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Tumia ‘po’ kutunga sentensi ya kuleta dhana ya wakati maalum
(Solved)
Tumia ‘po’ kutunga sentensi ya kuleta dhana ya wakati maalum
i) Wakati maalum
ii) Wakati usiodhihirika
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Tunga sentensi yenye maneno N + V + E + E + T + N
(Solved)
Tunga sentensi yenye maneno N + V + E + E + T + N
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Toa mifano miwili ya aina za nomino zifuatazo
(Solved)
Toa mifano miwili ya aina za nomino zifuatazo
i)nomino mseto
ii) nomino za wingi
iii) nomino za fikra
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Tumia kivumishi cha a- unganifu pamoja na nomino katika ngeli ya I-I kutunga sentensi
(Solved)
Tumia kivumishi cha a- unganifu pamoja na nomino katika ngeli ya I-I kutunga sentensi
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
(Solved)
Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
“Mimi nitawakaribisha wageni leo jioni. Kisha nitaondoka kwenda kwangu kesho.” Fatuma alimwambia juma.
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Ainisha viambishi katika neno HAKUJULIKANA
(Solved)
Ainisha viambishi katika neno HAKUJULIKANA
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Eleza maana ya kiambishi
(Solved)
Eleza maana ya kiambishi
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii, na kwa dhati ya mioyo yetu tuweze kupata ufanisi, na uwezekano wa kuinua nchi yetu...
(Solved)
Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii, na kwa dhati ya mioyo yetu tuweze kupata ufanisi, na uwezekano wa kuinua nchi yetu changa katika kiwango cha juu. Tukumbuke, “Ajizi ni nyumba ya njaa” Kwa hivyo basi haifai kulaza damu ikiwa matatizo nchini mwetu yametuzonga. Lazima tufanye kazi kwa busara, adabu njema na jitihada kwa moyo mmoja. Sharti tutilie maanani zaidi elimu ya vijana na watu wazima,kilimo,uchumi na amani katika nchi yetu vigumu sana kuweza kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Tupende tusipende lazima tizidishe mazao kilimo, uchumi na amani katika nchi yetu. Tunahitaji taifa lenye watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kuweza kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Tupende tusipende lazima tuzidishe mazao mashambani kwani kila kukicha idadi ya watu inaongezeka, Ni sharti tuweze kujitosheleza katika vyakula. Zaidi ya haya pia lazima tujishughulishe na biashara ambapo kwa sasa ni Wakenya wachache sana ambao wanatambua umuhimu wa biashara. Wengi ni wale wenye mawazo ya kwamba, lazima kila mmoja aajiriwe maishani. Yatupasa tujitahidi kuleta uchumi katika mikono ya wananchi wa Kenya badala ya kuwaachia wengine ambao hawahusiki.
Mafunzo tunayopata majumbani, shuleni na hata katika jamii, lazima yatuwezeshe kutambua mbinu za kupitia. Tunahitaji elimu tambuzi ambayo itamfanya Mwanakena kujua wajibu wake katika jamii. Tumesinywa na elimu pumbao; inayotupumbaza na kutufanya tusione mbele. Sisi vijana tukiwa viongozi wa ‘utengano ni uvundo’, lugha ya taifa ndicho chombo cha pekee ambacho kinatuunganisha na kuweza kutuwasilishia mapendekeza, mawaidha ni hisia zetu. Kukosa ndiko binadamu, wakati tunapokosea, lazima tukubali tumekosea na kufanya masahihisho mara moja. “Kwani usipoziba ufa, utajenga ukuta”. Tusikasirike kwa sababu tumesahihishwa makosa yetu tukiwa wazalendo halisi.
Sisi tukiwa vijana sharti tujishughukishe na kuyaangalia matatizo ya nchi, pia kutafuta njia za kutatua matatizo hayo. Siku zote tutekeleze nidhamu.Ni jambo la kusikitisha kwamba sisi vijana twashutumiwa mara kwa mara kwa kutokuwa na nidhamu shuileni na majumbani mwetu.Utamaduni wa assili unanakariri sana kuwa tuwe na nidhamu shuleni na majumbani mwetu.Ili watu waweze kuishi maisha bora na kuwa na maendeleo,amani na upendo lazima tuwe na bidii,ushirikiano mwema na kuchagua viongozi wenye mioyo ya maendeleo.Tukiwa viongozi ambao hawajishughulishi na maendeleo,basi tutabaki nyuma kama mkia kila siku zote.Bahati mbaya ni kwamba wananchi wengi siku hizi huchagua viongozi wao kwa kufuata ukoo ama kama kwa utajiri wake.Kwa hivyo basi tuchagueni viongozi ambao watatuletea ufanisi badala ya viongozi wanaotokana na sababu kubwa au ya utajiri.
a) Ni nini dhamira ya mwandishi?
b) Katika aya ya kwanza, mwandishi anawahimiza vijana kufanya nini ili kuleta maendeleo nchini?
c) Ni mambo gani yaliyochangia, kuzorota kwa maendeleo nchini Kenya kwa mujibu wa taarifa?
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Uhifadhi wa mazingira una manufaa mengi kwa binadamu .Thibitisha
(Solved)
Uhifadhi wa mazingira una manufaa mengi kwa binadamu .Thibitisha
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)
-
Nchi nyingi duniani zimetia saini mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto.
(Solved)
Soma taarifa ifatayo kwa makini kisha ujibu maswali yanayofuata.
Nchi nyingi duniani zimetia saini mkataba wa umoja wa mataifa kuhusu haki za watoto.
Haki ni mambo mema ambayo watoto wanastahili kutendewa. Kwa kutia saini, nchi hizizimetangaza kujitolea kwao kuzilinda na kuhahakikisha kuwa hakuna ukiukaji wake nakuwa watoto wote katika himaya zao wananufaika kutokana na haki hizi.
Miongoni mwa haki hizi ni kuwa kila mtoto ana haki ya kuishi na kupata chakula cha kutosha na chenye viinilishe bora. Pili, kila mtoto ana haki ya kupata elimu. Elimu hii inafaa kutolewa bila ada na iwe inayofaa na inayopatikana kwa urahisi.Kisha kila mtoto ana haki ya kutopigwa na kutodunishwa kwa namna yoyote, iwe kitabaka, kirangi, kijinsia na vinginevyo. Mtoto ana haki pia kutolazimishwa kufanya kazi za kiutumwa, nzito na zakushurutishwa. Hali kadhalika, ana haki ya kuishi katika nyumba au makazi bora nasalama, kutunzwa na kulindwa dhidiya hali yoyote inayoweza kumhatarisha. Anatakiwa ashirikishwe katika kufanya maamuzi.Fauka ya haya, ana haki ya kupata huduma za afya,mahitaji maalum,michezo, upendo na habari. Isitoshe,anastahili kuheshimiwa kimawazo na kihisia. Haki hizi zinatakiwa kulindwa na kila mwanajamii, hivyo serikali za mataifa mengi zimeshirikisha haki hizi katika katiba za nchi zao na sheria zao.
Walakini haki hizi bado zinakiukwa.Watoto wengi kote duniani bado wananyimwa haki zao. La kusikitisha na kukera ni kuwa wanaotarajiwa kuwa vigogo vya kuzilinda haki hizi, ndio wanaoongoza kuzikiuka. Kila siku tunasikia na kushuhudia visa vya watoto kupigwa, kunyimwa chakula, kufanyishwa kazi kipunda, kuteswa, kuishi katika mazingira hatari, na hata kuuawa. Kuna watoto wengi wanaolala nje, wengine hawapati chakula licha ya kuwa wanatakiwa kupata chenye lishe bora. Kwao kutarajiwa mlo awamu tatu kwa siku ni njozi kwani hata awamu moja ni adimu kupata.
Watoto wengi katika mataifa yenye fujo na ghasia hutekwa na kutumikishwa vitani. Viongozi katika mataifa haya hawafanyi kitu ila kutazama tu wakati watoto wanaotakiwa kuwalinda wanageuzwa kuwa mibaba ya kuua na kuuana. Watoto hawa huvishwa magwanda ambayo miili yao minyonge haiwezi kuyahimili. Pia, huvalishwa mabuti ya kijeshi ambayo ni mizigo mizito ya kubeba mbali na bunduki zinazokaribia kuwazidi uzani wakati wanatakiwa kuwa wamelindwa majumbani, na shuleni na wazazi wao na serikali.
Jukwaa la vijiji vya mataifa ya ulimwengu wa tatu limesheheni watoto wasioenda shule kwa sababu ya lindi la ufukara uliokithiri. Elimu ya bure inayogusiwa katika haki za watoto haipo. Wanaong‘ang‘ana iwepo ni kana kwamba ni waota ndotomchana. Jiulize watoto wangapi sasa hivi wamo majumbani bila kwenda shuleni kutokana na ukosefu wa karo? Wangapi wamo mitaani wakivuta na kunusa gundi huku wakiombaomba vishilingi?
Hali ilivyo sasa hivi inadai kuwa mimi na wewe tufanye hima na kuungana mikono kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu haki za watoto. Twapasa kuhimiza serikali zetu kufanya kila ziwezavyo kuhakikisha kuwa watoto wote wamo shuleni. Nasi tushirikiane kutoa huduma kwa watoto na kukomesha dhuluma, mateso na dhiki kwao. Haitoshi kupeleka miswada mbungeni kuhusu haki za watoto na kuipitisha kuwa sheria. Twastahili kubadilisha misimamo yetu kuhusu haki hizi na kuzilinda kwa dhati bali si kwa chati.
Maswali
a) Fupisha aya mbili za kwanza. ( maneno 65-70)
b) Eleza ni vipi ukiukaji wa haki za watoto unaweza kuepukwa . ( maneno 30-35)
Date posted:
October 2, 2019
.
Answers (1)