Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Bainisha nomino hizi ni za aina gani. i. Sukari. ii. Mapenzi.

      

Bainisha nomino hizi ni za aina gani.

i. Sukari.

ii. Mapenzi.

  

Answers


Martin
i. Sukari.- wingi

ii. Mapenzi – dhahania
marto answered the question on October 3, 2019 at 05:29


Next: Andika kwa wingi sentensi hizi. i. Goti la mtoto liliumia. ii. Ukwato wa ngamia ni mpana
Previous: Eleza maana ya lugha rasmi.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Andika kwa wingi sentensi hizi. i. Goti la mtoto liliumia. ii. Ukwato wa ngamia ni mpana(Solved)

    Andika kwa wingi sentensi hizi.

    i. Goti la mtoto liliumia.

    ii. Ukwato wa ngamia ni mpana

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya msemo ufuatao : Kula kitana.(Solved)

    Eleza maana ya msemo ufuatao :
    Kula kitana.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo. MAVAZI REKEBISHENI(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.
    MAVAZI REKEBISHENI

    vazi.png
    heri.png

    MASWALI YA USHAIRI

    (a) Shairi hili ni la aina gani?

    (b) Eleza vina vya beti za kwanza mbili

    (c) Toa kibwagizo cha shairi hili kisha ufafanue maana yake

    (d) Eleza maana ya misamiati hii kama ilivyotumika katika ushairi

    Staha –
    Dhahiri –
    Shani –
    Duni

    (e) Shairi hili liko katika bahari zipi?

    f) Uhuru wa mshairiunadhihirikavipi katika shairi hili?

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika usemi wa taarifa: "Nataka ufikirie sana juu ya maisha yako ya ndoa. Sitaki uishi maisha yasiyo na mweleko." Babu alinishauri.(Solved)

    Andika katika usemi wa taarifa:
    "Nataka ufikirie sana juu ya maisha yako ya ndoa. Sitaki uishi maisha yasiyo na mweleko." Babu alinishauri.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha yambwa katika sentensi ifuatayo.(Solved)

    Onyesha yambwa katika sentensi ifuatayo.
    Mwamburi alitumia ufunguo kumfungulia Rashid mlango.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Eleza tofauti iliopo katika kauli zifuatazo. Kutendeana na kutendana.(Solved)

    Eleza tofauti iliopo katika kauli zifuatazo.
    Kutendeana na kutendana.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi kubainisha matumizi ya vivumishi vya nomino katika ngeli ya U – I; katika umoja na wingi.(Solved)

    Tunga sentensi kubainisha matumizi ya vivumishi vya nomino katika ngeli ya U – I; katika umoja na wingi.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Ukitungia sentensi, onyesha matumizi ya vivumishi vya nomino.(Solved)

    Ukitungia sentensi, onyesha matumizi ya vivumishi vya nomino.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Fafanua njia zozote tatu zinazotumiwa katika uundaji wa maneno.(Solved)

    Fafanua njia zozote tatu zinazotumiwa katika uundaji wa maneno.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika udogo. Jijipu lilipasuka lenyewe.(Solved)

    Andika katika udogo.
    Jijipu lilipasuka lenyewe.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Yakinisha katika umoja: Msingalivumilia nyakati ile msingalipata zawadi kubwa.(Solved)

    Yakinisha katika umoja:
    Msingalivumilia nyakati ile msingalipata zawadi kubwa.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Tofautisha kwa mifano thabiti mbinu za litifati na tadmini kama zilivyotumika katika tamthilia ya kigogo.(Solved)

    Tofautisha kwa mifano thabiti mbinu za litifati na tadmini kama zilivyotumika katika tamthilia ya kigogo.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • ukombozi wa jamii yoyote unahitaji uvumilivu kupiga moyo konde .Thibitisha kauli hii ukirejelea tamthilia ya kigogo(Solved)

    ukombozi wa jamii yoyote unahitaji uvumilivu kupiga moyo konde .Thibitisha kauli hii ukirejelea tamthilia ya kigogo

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • CHOZI LA HERI Eleza jinsi mbinu ya majazi imetawala kazi ya kisanaa ya mwandishi wa chozi la heri.(Solved)

    CHOZI LA HERI

    Eleza jinsi mbinu ya majazi imetawala kazi ya kisanaa ya mwandishi wa chozi la heri.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata.(Solved)

    Soma shairi hili kasha ujibu maswali yanayofuata.

    SABUNI YA ROHO
    Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
    Ndiwe suluhu la zama, waja wa kukimbilia,
    Waja wana kutazama, madeni wakalipia,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
    Utanunua majoho, majumba na nyumbani
    Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Matajiri wakujua, wema wako wameonja,

    Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
    Sura zao mefufua,wanazuru kila Nyanja,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
    Watazame mayatima, kwao kumekua wa duni,
    Wabebe waliokwama, wainue waliochini,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Ndiwe mvunja mlima, wapi kupata uwezo?
    Umezua uhasama, waja kupata mizozo
    Ndiwe chanzo cha zahama, umewaitia vikwamizo,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Umevunja usuhuba, familia zazozana,
    Walokuwama habuba, kila mara wagombana,
    Roho zao umekaba, majumbani wa chinjana,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
    Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,

    Niondoe jehanamu, ya ufukara wa sumu,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
    Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
    Nichekeshe kibogoyo, name nipate kuwika,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima

    Maswali

    a) Mshairi anaongea na nani katika shairi hili?
    .
    b) Taja majina mengine matatu aliyopewa huyu anayesemeshwa

    c) Anayezungumziwa katika shairi hili anasababisha balaa gani?

    d) Mshairi anatoa mwito gani kwa mwenziwe?

    e) Fafanua maudhui ya ubeti wa sita.

    f) Mbinu kadha za uandishi zimetumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe wake. Taja mbinu zozote tatu na uzitolee mifano katika shairi.

    g) Fafanua maana ya : sura zao ’mefufua, wanazuru kila nyanja’

    h) Andika ubeti wa saba katika lugha nathari.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Lugha inaweza kuelezwa kwa jumla kuwa ni mfumo wa mawasiliano.(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Lugha inaweza kuelezwa kwa jumla kuwa ni mfumo wa mawasiliano.Haiyamkiniki kwa mtu yeyote kueleza chanzo au kiini cha lugha na sote tunakubalina kuwa matumizi yake yameanza tangu kuumbwa kwa binadamu kwani ni vigumu kukisia kuwepo kwa jamii ya watu bila lugha ya mawasiliano yoyote ile.
    Katika taifa lolote,huwapo na lugha moja au hata zaidi ya moja ambayo huwa ndicho chombo zatika cha mawasiliano ya taifa katika nyanja za:elimu maandishi,siasa na biashara.Kwa mfano mataifa ya Kanada hutumia lugha mbili kwa usawa kama lugha za taifa na za kikazi.Maana ya lugha ya taifa ni lugha moja ambayo huteuliwa kutumika katika shughuli zote za taifa hasa katika nchi yenye lugha nyingi za kikabila.Lugha ya taifa ni muhimu sana kwa maisha na maendeleo ya taifa lolote lile.Lugha hii huwa ndiyo kiungo cha kueneza umoja na uelewano miongoni mwa jamii nyingi tofauti na huwa kama kitambulisho kwao kwa kuwa wao ni ndugu wa jamii moja kubwa,yaani taifa lao.
    Kenya ni mfano mzuri wa taifa lenye lugha nyingi zinazozidi 40 za vikundi vidogo vidogo vya kikabila.Hapo kabla ya miaka mia moja hivi iliyopita kila kimojawapo cha vikundi hivi kilijitambulisha kama kabila huru.Baada ya kuja kwa serikali ya kikoloni na hasa baada ya Kenya kujinyakulia uhuru,haja ya kuunganisha raia wote chini ya taifa moja lenye uongozi na shabaha moja ilikuwa ndilo jambo lililozingatiwa sana.Kwa hivyo utamaduni wa taifa Kenya ni mchanganyiko wa tamaduni za watu wengi wenye mila,desturi,imani na itikadi tofauti.Utamaduni humaanisha jumla ya amali na tabia za watu wa jamii fulani.Amali hizi zinafungamanisha fikira,ustaarabu,mila,taasisi na sanaa za aina zote za jamii inayohusika.
    Ili kujieneza na kujiimarisha,taifa huhitaji chombo hicho kuwasiliana na kuwaunganisha watu wake wenye asili mbalimbali. Chombo hicho huwa ni lugha ambayo siyo tu kwamba ni sehemu ya utamaduni wa jamii bali pia ni njia muhimu sana ya kutawanyia na kustawishia ule utamaduni.
    Katika taifa lenye lugha nyingi kama Kenya kwa mfano,lugha ya taifa inayozungumzwa na kueleweka na baadhi kubwa ya raia ambayo imekiuka mipaka na tofauti za kikabila ni njia muhimu sana ya kueneza maongozi ya taifa na kuleta ufahamikiano bora kote nchini.Kama
    zilivyo taasisi kama wimbo wa taifa,bendera ya taifa au bunge la taifa, lugha ya taifa ndicho kielelezo cha taifa lolote lile.Lugha kama hiyo huvunja na hukomesha hisia za kibinafsi na kikabila na badala yake kuunda moyo wa uaminifu wa kitaifa.
    Zaidi ya kuwa chombo cha mawasiliano,lugha ni kielelezo cha fikira na hisia za binadamu.Lugha ya watu fulani haituelezi tu ujuzi au maarifa yao bali pia mtazamo wao kimaisha,falsafa na mawazo yao.Kwa ufupi lugha hutufahamisha namna akili za watu waizungumzayo ile lugha zinavyofikiri na kufanya maazimio.Lugha ni sehemu ya utamaduni wa taifa tulimozaliwa na lazima lugha hiyo ifunzwe katika muktadha wa maisha ya jamii ihusikayo.Utamaduni wa jamii havitenganiki na lugha yake.

    Maswali
    (a) Huku ukirejelea kifungu, eleza fasiri na chanzo cha lugha.
    (b) Tofautisha baina ya lugha ya taifa na lugha ya kikazi.
    (c) Kwa nini lugha ya taifa huhitajika sana katika nchi kama Kenya.
    (d) Eleza kazi nne kuu zinazotekelezwa na lugha ya taifa.
    (e) Eleza maana ya mafungu yafuatayo kama yalivyotumiwa katika taarifa:
    (i) Amali na tabia za watu:
    (ii) Muktadha wa maisha ya jamii:
    (iii) Haiyamkiniki:
    (f)Eleza majukumu mawili ya lugha kwa ujumla

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Taja madhumuni ya kusanifisha lugha ya Kiswahili nchini(Solved)

    Taja madhumuni ya kusanifisha lugha ya Kiswahili nchini

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali

    Mwanafunzi aliyeondoka jana alishindwa kumwona

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha Akimaliza kucheza mwite(Solved)

    Kanusha
    Akimaliza kucheza mwite

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mistari katika sentensi(Solved)

    Bainisha matumizi ya viambishi vilivyopigiwa mistari katika sentensi

    i)Yego ana ujuzi mwingi
    ii) Yule mfanyibiashara aliyejidanganya amepata hasara

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)