Siwe ulosema jana, ya kuwa u mashuhuri? Ya kuwa wajuwa sana, aidha huna kiburi? Nchini wajulikana, mwanasiasa mahiri, Bungeni tukuajiri?

      

SIWE?

1. Siwe ulosema jana, ya kuwa u mashuhuri?
Ya kuwa wajuwa sana, aidha huna kiburi?
Nchini wajulikana, mwanasiasa mahiri,
Bungeni tukuajiri?

2. Siwe ulotushawishi, kwa chumvi na kwa sukari,
Na matamu matamshi, ukaziteka suduri,
Ukanena penya moshi, moto ndiyo yakwe siri,
Nawe ndiye hiyo nari?

3. Siwe uloji‘ta moto, uwakao biribiri,
Kamba ‗tatia fukuto, Litakalo leta kheri‘,
Utatufunua mato, Maisha yawe mazuri,
Tukupe kura waziri?

4. Siwe ulosema hayo, na mengi ukabashiri,
Ukamba wafata nyayo, nyayo ziso utiriri,
Tusiwe na wayowayo, wa kufikirifikiri,
Tukuachie ujari?

5. Siwe tulokuinua, Mabegani kama mwari,
Tungawa twalemelewa, waume tukajasiri,
Kamba tukikuchaguwa, mema kwetu yatajiri,
Tukakeyi kusubiri?

6. Siwe ulotugeuka, kwamba leo u waziri,
Wajiona melimuka, tena ukawa ayari,
Walaghai ukicheka, ukuu umekughuri,
Leo mekuwa hodari?

7. Siwe ulojawa raha, za hino yetu sayari,
Ukawa ja vile shaha, hatukupati shauri,
kutuona ni karaha, wakatiwo twahasiri,
Ushakiya msitari?

8. Siwe uliyetughura, ukafunga na safari,
Ukaelekea bara, Kwa wenzio matajiri,
Ukatuacha majura, na tama kukithiri,
Kanama Ushaghairi?

9. Siwe uliyetuasi, ukenda pasi kwaheri,
Mbona hutwambii nasi, tukajua yetu shari,
Leo una masidisi, husemi na aso gari,
Ndio mezidi jeuri?

10. Siwe‘lotwaa mgwisho, ukawa wajifakhiri?
Chenye mwanzo kina mwisho, hilo wajuwa dhahiri,
Vyaja kutoka vitisho, kwani hayo sidahari,
Mambo mengimdawari?

11. Siwe utakayeiza, mwishowo ukidhihiri,
Siku itayoteleza, kuja kwetu ansari,
Kuja kutubembeleza, kwa nyunga nalo khamri,
Tauya nazo nadhiri.

MASWALI
a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani?
b) Taja na ueleze bahari tatu za shairi hili?
c) Onyesha jinsi mtunzi alivyotumia idhini ya kishairi.
d) Taja na ufafanue tamahali ya usemi iliyotawala katika shairi hili.
e) Anayerejelewa alibailika vipi? Eleza.
f) Andika ubeti wa tisa kwa lugha ya nathari.
g) Mshairi ana maana gani kwa kusema:
(i) Wakatiwo twahasiri.
(ii) Ukaziteka suduri.

  

Answers


sharon
(a) Kuonyesha jinsi mwanasiasa fulani alivyojipendekeza kwao wakampa kura kisha baadaye akawageuka na kutowajali.
(b)
- Msuko
- Ukaraguni – Vina vya nje vinatiririka vya undani vinabadilika badilika.
- Tarbia – Mishororo minne.
- Mathnawi – vipande viwili.
- Kikwamba – neno siwe kuanzia kila ubeti.
(c)
Inkisari – Mfano: Siwe – si wewe. Ulosema – Uliyesema
Lahaja – Mfano: Mato – Macho
Kuboronga sarufi – Mfano: Vyaja kutoka vitisho – vitisho vyaja kumtoka .
Tukujua yetu shairi – Tukujua shari yetu.
(d) Maswali ya balagha – maswali chochezi yasiyo na majibu.
Mfano: Bungeni tukuajiri?
Nawe ndiyo hiyo nari?
Tukupe kura waziri
(e)
- Alianza ulaghai
- Ukubwa ukampa kiburi
- Aliingilia raha
- Akawa aseme kuwa watu wanamharibia muda.
- Akawaacha na kujiunga na matajiri wenzake.
- Akazidisha tamaa.
- Ana Masidisi na anawadharau wenzio na mafari.
(f) Si wewe uliyetuacha na kuenda bila ya kutuaga mbona usitueleze sisi ili tupate kujua makosa yetu.
Hivi leo umenunua kwa hivyo hujihusishi na wasio na magari umekuwa mjeuri sana.
(g) (i) Wakai tunahariri – Tunaharibu wakati wako.
(ii) Ukaziteka suduri – Ukaziteka nyayo.
sharon kalunda answered the question on October 3, 2019 at 05:38


Next: Andika vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendeshana. i. Penda . ii. Endesha.
Previous: In figure below power dissipated by the 16? resistor is 8w, what is the power dissipated in 200?

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.(Solved)

    Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • "Nimemwita bwana huyu aje huku juu kusudi mumwone."(Solved)

    Damu nyeusi na hadithi zingine
    "Nimemwita bwana huyu aje huku juu kusudi mumwone."
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Eleza sifa tatu za mzungumzaji.
    c) Jadili maudhui ya ubaguzi namna yanavyojitokeza katika hadithi husika

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • "Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"(Solved)

    Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.
    "Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"
    a) Eleza muktadha wa maneno haya.
    b) Eleza umuhimu wa mrejelewa katika dondoo hili kwenye riwaya.
    c) Eleza maisha ya msemaji yalivyokuwa kwa mujibu wa Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • "Kutowajibika kwa viongozi baada ya mkoloni kuondoka ni dhahiri." Jadili kauli hii kwa mujibu wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)

    "Kutowajibika kwa viongozi baada ya mkoloni kuondoka ni dhahiri." Jadili kauli hii kwa mujibu wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • "Nashukuru sasa umeanza kuona mambo yanavyostahili kwenda."(Solved)

    Mstahiki Meya.
    "Nashukuru sasa umeanza kuona mambo yanavyostahili kwenda."
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Eleza sifa zozote nne za msemaji.
    c) Fafanua maudhui ya ufisadi kama yalivyoangaziwa na mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Hadhira e pulikeni, kisa changu mpaeni,(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

    1) Hadhira e pulikeni, kisa changu mpaeni,
    Mpateni mweleweni, mchekeni, mlieni,
    Funzo lake mpateni, uamuzi mfanyeni,
    Kisa hiki asilani, sisahau maishani.

    2) Cha nne niliingiya, mtoto kafurahiya,
    Malkia ungedhaniya, duniani meingiya,
    Mapambo lijipambiya, kung‘ara kikang‘ariya,
    Kisa change chatokeya, mwanzowe nafunguliya.

    3) Darasani lizembea, bidii sikutilia,
    Starehe nakwambia, nilipenda najutia,
    Kimadaha litembea, tausi nilitulia,
    Kisa kilinigonjea, mtume! Ningalijua.

    4) Muhula kutamatika, dafu sikufua, kaka,
    Enda, Ewe, Embe, fika, alama duni, viraka,
    Nilipokea waraka, mzazi kahitajika,
    Kisa kijatambulika, nakuomba makinika.

    5) Muhula wa pili sasa, nikarudia makosa,
    Sikupigeni msasa, makali nikayakosa,
    Kisu sikunoa hasa, sikukata cha darasa,
    Kisa ndicho hicho sasa, ninakupa pasi pesa.

    6) Sasa muhula wa tatu, umetimia wanetu,
    Mtihani kama chatu, nimeuogopa, mtu,
    Sijausomea katu, ningalilindaje utu?
    Kisa mkasa wa chatu, kilinipata wa kwetu.

    7) Mbwa katu hafi maji, kiona ufuko, maji,
    Tajaribu sife maji, hata akiyanywa maji,
    Ilibidi twende jiji, kuwasaka wajuaji,
    Kisa change mfumbaji, sasa dawa lihitaji.

    8) Mpango ulitolewa, mchango ulipangiwa,
    Pesa tele litolewa, na simu kununuliwa,
    Mtandao liwekewa, ‗kunani‘ kupakuliwa,
    Kisa cha simu kujuwa, linifanya kupagawa.

    9) Tulikata dari ona, simu yetu kufichana,
    Usiku tulikutana, maswali kurushiana,
    Majibu tulipeana, "panga‘ kabadilishana,
    Kisa kinajulikana, vile nilivyokazana.

    10) Niliyangoja majibu, nikiwa na hamu, babu,
    Nilikimya kama bubu, nisije toa aibu,
    Nilivichoma vitabu, bila kuwa na sababu.
    Kisa kawa masaibu, kashindwa kuyaharibu.

    11) Kutangazwa matokeo, nakumbuka hadi leo,
    Lilishangaza toleo, sikuamini redio,
    Lipokea matokea, yalinitia kimbio,
    Kisa change mchocheo, haya yangu mapokeo.

    12) Nilifeli mtihani, sababu simu juweni,
    Najuta nisameheni, nijilaumu moyoni,
    Ningalijua mbeleni, ningalisoma jamani,
    Kisa nimemalizeli, wenzangu mzindukeni.

    13) Watahiniwa mlipo, msiwe mithili popo,
    Skuli kwenu kuwepo, nia mpate malipo,
    Bidii hapo mlipo, toa uzembe pasipo,
    Kisa change kingalipo, simu daima siwepo!

    MASWALI
    a) Taja anwani mwafaka ya shairi hili.
    b) Fafanua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili.
    c) Bainisha nafsi lengwa katika shairi hili.
    d) Changanua arudhi zilizotumiwa na mtunzi wa shairi hili.
    e) Andika ubeti wa kumi katika lugha nathari.
    f) Eleza maana ya maneno na vifungu vifuatavyo kwa mujibu wa shairi.
    g) Eleza maana ya maneno na vifungu vifuatavyo kwa mujibu wa shairi.
    (i) Sikukata cha darasa
    (ii) Yalinitia kimbio
    (iii) Kupagawa

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • "Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"(Solved)

    Damu nyeusi na hadithi zingine
    "Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili.
    c) Huku ukitoa mifano, thibitisha maudhui sita ambayo yamejitokeza katika hadithi ya Damu Nyeusi na wanayoyaendeleza.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kutoa mifano kumi,eleza vizingiti walivyokumbana navyo wanacheneo wakati wa kupigania mageuzi.(Solved)

    Mstahiki Meya
    Kwa kutoa mifano kumi,eleza vizingiti walivyokumbana navyo wanacheneo wakati wa kupigania mageuzi.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • "Iwapo umefanya, yapo mengi ambayo hayakunyoka."(Solved)

    Mstahiki Meya
    "Iwapo umefanya, yapo mengi ambayo hayakunyoka."
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Tambua mbinu moja iliyotumika katika muktadha wa dondoo.
    c) Fafanua kauli kwamba"yapo mengi ambayo hayakunyoka".
    d) Eleza jinsi baadhi ya wahusika walivyojaribu kuyanyoosha.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • "Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."(Solved)

    Kidagaa kimemwozea
    "Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."
    a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    b) Ni nini sifa za mvuto zinazowaleta pamoja mzungumzaji na mzungumziwa.
    c) Tambua na ufafanue mbinu inayotumika katika dondoo.
    d) Kwa mifano mwafaka fafanua tanzia hiyo inayorejelewa katika dondoo.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • "Ikamchagiza kama vile kiu ya mtu aliyekuwa akisafiri jangwani".(Solved)

    DAMU NYEUSI
    "Ikamchagiza kama vile kiu ya mtu aliyekuwa akisafiri jangwani".
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili
    (b) Fafanua sifa zozote nne za mrejelewa
    (c) Eleza fani uliotumiwa na mwandishi katika dondoo hili
    (d) Kwa kurejea hadithi zozote tatu,eleza namna wahusika wowote watatu walivyoathiriwa na kiu.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Nonsense! Hivi huyu ana nia gani?(Solved)

    Mstahiki Meya
    Nonsense! Hivi huyu ana nia gani?
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Taja na ueleze mbinu za lugha zinazojitokeza katika dondoo hili.
    (c) Jadili umuhimu wa msemaji katika tamthilia hii.
    (d) Jadili njia za kuondoa uozo katika jamii ukijikita katika tamthilia ya Mstahiki Meya.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.(Solved)

    Jadili mbinu zifuatazo kama zilivyotumika katika Mstahiki Meya.
    (a) Jazanda
    (b) Uzungumzi nafsia
    (c) Majazi
    (d) Methali
    (e) Taharuki

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.(Solved)

    Eleza dhima ya lakabu kwa kurejelea hoja tano.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine (Solved)

    Eleza maudhui ya ukengeushi ukirejea hadithi zifuatazo katika diwani ya Damu nyeusi na hadithi nyingine
    (i) Mke wangu
    (ii) Damu Nyeusi
    (iii) Tazamana na Mauti
    (iv) Mizizi na matawi

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • "Ulimwengu wake ulivurugika akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"(Solved)

    Kanda la usufi
    "Ulimwengu wake ulivurugika akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaenda arijojo"
    (a) Eleza sifa zozote nne za mrejelewa
    (b) Kwa nini mrejelewa amelinganisha na tiara iliyopeperushwa na upepo

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • "Alipofikishwa kwenye zahanati hakushughulikiwa ipasavyo.Ubwete ni ugonjwa mmoja mbaya walioambukizwa madaktari na wauguzi wengi Tomoko"(Solved)

    "Alipofikishwa kwenye zahanati hakushughulikiwa ipasavyo.Ubwete ni ugonjwa mmoja mbaya walioambukizwa madaktari na wauguzi wengi Tomoko"
    a) Eleza Muktadha wa dondoo hili.
    b) Dhihirisha jinsi mtunzi alivyoitumia tamathali yoyote moja inayobainika kifunguni .
    c) Riwaya Ya Kidagaa Kimemwozea ni muhtasari wa maradhi yanayolihujumu Bara Afrika.Tetea rai hii kwa mifano faafu riwayani.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)

    "Wanyonge ndio wanyongwao" ni kauli inayodhihirika vyema kupitia wahusika tofauti katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
    Jadili.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,(Solved)

    Soma mashairi yafuatayo kisha ujibu maswali.

    SIKUJUA!
    1. Kama ningefuga ng‘ombe, mafahali na vindama,
    Zisingenidhuru pembe, ngeu kuniandama,
    Samli ni lembelembe, na minofu ya minyama.

    2. Kama ningefuga mbuzi, na kondoo kundi zima,
    Ningewajengea zizi, na maziwa nikakama,
    Ningewachuna na ngozi, kutengenezea ngoma.

    3. Kama ningefuga bata, nao kuku kwa ujima,
    Chakula siyo matata, ni machicha na mtama,
    Mayai ningeyapata, na kitoweo kizima.

    4. Kumbe nimefuga punda, mashuzi ndio heshima,
    Ni ukaidi na inda, mateke kurusha nyuma,
    Nyama limekuwa nunda, mfugaji humuuma.

    Kiitikio
    Sikujua wa kufuga, mnyama mwenye faida

    SHAIRI B
    Afrika na Watu Wake

    Mimi ninaona mgonjwa
    Bado amelala kitandani.
    Kama hatutamtoa miiba iliyobaki
    Mgonjwa hataweka miguu yake chini
    Ili kutembea bila ya kujiegemeza.

    Miiba iliyomo ndani mwetu lazima
    Pia iondolewe upesi kabla haijaingia
    Kati ya mfupa na kufa pamoja nasi.
    Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma
    Halafu tucheze nao mchezo wa siasa na uchumi.

    Lakini kuitoa miiba hii
    Tunahitaji macho makali
    Mikono isiyotetemeka
    Moyo usio na huruma
    Na kuona miiba ilipoingilia.

    MASWALI
    (a) Onyesha jinsi ujumbe unaopatikana katika ubeti wa nne wa Shairi A na Shairi la B unavyokatisha tamaa.
    (b) Eleza maana ya mshororo huu kama unavyojitokeza kwenye ubeti wa pili wa shairi B.
    Baada ya kuitoa tuvae viatu vya chuma.
    (c) Linganua sifa za kimuundo ukizingatia ubeti wa pili wa Shairi A na Shairi B.
    (d) Ukizingatia Mshororo wa kwanza kwenye ubeti wa pili wa Shairi A, onyesha jinsi Mshairi alivyotumia kibali chake.
    (e) Onyesha sifa moja ambayo inadhihirika kwenye shairi la B na ambayo hutawala tungo za aina hii.
    (f) Nafsi neni amedhihirisha toni gani kwenye shairi A?
    (g) Taja nafsi mbili nenwa kwenye shairi la B.
    (h) Andika ubeti wa mwisho wa shairi B kwa lugha ya nadhari.

    Date posted: October 2, 2019.  Answers (1)

  • Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?(Solved)

    SABUNI YA ROHO
    Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?
    Ndiwe suluhu za zama, waja wakukimbilia,
    Waja wanakutazama, madeni wakalipia,
    Ndiwa sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,
    Utanunua majoho, majumba na nyumbani,
    Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvinja mlima.
    Matajiri wanakujua, wema wako wameonja,
    Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,
    Sura zao ‗mefufua, wanazuru kila njanja,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mvunja mlima, onana na maskini,
    Watazame mayatima, kwao kumekua duni,
    Webebe waliokuwa, wainue walio chini,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Ndiwe mvunja mlima, wapi kapata uwezo,
    Umezua uhasama, waja kupata mizozo,
    Ndiwe chanzo cha zahama, umewatia vikwazo,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Umevunja usuhuba, familia zazozana,
    Waliokuwa mahabuba, kila mara wagombana,
    Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,
    Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,
    Niondoe jahanamu, ya ufukara wa simu,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.
    Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika,
    Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,
    Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,
    Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

    Date posted: October 1, 2019.  Answers (1)