a).Maneno ya Mtemi Nasaba Bora kwa kakake Mwalimu Majisifu nyumbani kwa Mtemi alipotembelewa na kakake.Anakaribishwa na Bi.Zuhura mkewe Mtemi.Wameketi ukumbini wakiwa wamersyamaziana,Mtemi amnamwuh'za nduguye kwa nini hakuhudhuria sherehe ya Siku Kuu ya Wazalendo.Majisifu anasema kuwa alikuwa amekwenda "ibada" yaani ulevini ambapo Mtemi anaanza kumshauri aache ulevi.
(b)
- Japo ba'ba yao alikuwa kasisi.wote wawiii wanaasi dini.
- Majisifu aSighiri kusomea upadre alipokwenda ng‘ambo.Nasaba Bora alipewa Biblia na babake alipopata ajira ya kwanza lakini hakusoraa hadi alipopata shida-kidagaa kilipomwozea.
- Hawawajibiki kazini.Majisifu kwa sababu ya uievi wake na ufisadi aiipokuwa mhariri;Mtemi alighushi stakabadhi za mashamba ya watu.
- Wote ni wapyaro. Wanawatusi wake zao. Hawawaheshimu.
- Wote wana taasubi za kmme
- Ndoa zao zina mushkili.Majisifu kwa kushinda ulevini na kutomsaidia kazini.Mtemi kugombana na mkewewe,kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa.
- Wote si walezi weza-Majisifu hamsaidii mkewe kuwatunza waioto walemavu.Mtemi baonekani kumsbughulikia bintiye Mashaka anlipowehuka.
- Wote wanabadili mienendo yao miovu.Majisifu alibadilika ma kuanza kuwahurumia watoto wake walemavu,alikiri makosa ya kuibia waandishi miswada na kuchapisba kama yake.Mtemi anakiri maovu aliyowatendea watu wa Sokomoko na njama alizofmfanyia Chichiri Harnadi na Yusufu.
- Wote ni wezi.Mtemi ni mwizi wa mashamba,Majisifu ni mwizi wa kazi za kitaaluma (miswada)
- Wote walipenda sifa. Majisifu kudai kuwa yeye ni mwandishi bora barani Afrika.Mtemi alisambaza jina lake takriban kwa kilataasisi kuitwa kwa jina lake-Nasaba Bora.
sharon kalunda answered the question on October 3, 2019 at 06:58
- "...Sote ni wafanyikazi wa baraza. Kile linachochuma Baraza tunagawana sote."(Solved)
Timothy Arege, Mstahiki Meya
"...Sote ni wafanyikazi wa baraza. Kile linachochuma Baraza tunagawana sote."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua sifa tano za msemaji
(c) Tunagawana sote ni kinyume ejia hali halisi. Thibitisha.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Pana jambo ninatukiya, kwangu hilo ni muhali,
(Solved)
SIPENDI KUCHEKA
Pana jambo ninatukiya, kwangu hilo ni muhali,
Kitenda naona haya, kujishusha yangu hali
Sipendi unipe hidaya, sipendi kutenda hili
Sipendi mimi kucheka
Sipendi mimi kucheka, kuchekea mawi
Sipendi na ya dhihaka, kwangu nyemi hiwi
Sipendi kwa hakika, mwovu kistawika
Halafuye nikacheka!
Masikini akiteswa
Yatima akinyanyaswa
Mnyonge naye akinyonywa
Sipendi hata ikiwa
Unazo nguvu najuwa
Ni hili sitatekezwa
Mbona lakini nicheke, kwayo furaha?
Na wewe ukajiweke, uli na siha?
Na yatima ali pwek.e, wa anahaha?
Amenyimwa haki yake, hanayo raha!
Na moyo wangu ucheke, kwa ha ha, ha!
Kucheka kwa kucheka Mimi katu sitacheka.
MASWALI
a) Shairi hili ni la aina gani? Thibitisha.
b) Taj a sababu zinazomfanya mshairi asitake kucheka.
c) Chambua umbo la shairi hili kwa kuzingatia ubeti wa mwisho.
d) Tambua nafsineni na nafsinenewa katika shairi hili.
e) Tambua toni ya shairi hili.
f) Fafanua uhuru wa mshairi katika shairi hili.
g) Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi.
h) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi
i) Mawi
ii) Nyemi
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Eleza hali ya shaka ya mambo inavyojitokeza katika hadithi ya shaka ya mambo.(Solved)
“Shaka ya Mambo” (Farouk Topan)
Eleza hali ya shaka ya mambo inavyojitokeza katika hadithi ya shaka ya mambo.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Nashangaa vile kwetu tunavyoabudu watu hao wasiotujali."(Solved)
“Damu Nyeusi” (Ken Walibora)
"Nashangaa vile kwetu tunavyoabudu watu hao wasiotujali."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha matumizi ya mbinu ya ishara kwa kurejelea hadithi ya gilasi ya mwisho makaburini.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Eleza jinsi wanacheneo walivyotatua shida zinazowakumba.(Solved)
Mstahiki Meya
Eleza jinsi wanacheneo walivyotatua shida zinazowakumba.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."(Solved)
Mstahiki Meya
"Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Anayeambiwa alisema nini baada ya kuambiwa haya?
c) Thibitisha kuwa wanacheneo walipanda pojo.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Taja aina nne za hadithi.(Solved)
Taja aina nne za hadithi.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii.(Solved)
Kidagaa kimemwozea
Mtemi Nasaba Bora ni kielelezo cha viongozi wa kiafrika wanaondeleza uongozi mbaya. Jadili kauli hii.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Siwe ulosema jana, ya kuwa u mashuhuri?
Ya kuwa wajuwa sana, aidha huna kiburi?
Nchini wajulikana, mwanasiasa mahiri,
Bungeni tukuajiri?(Solved)
SIWE?
1. Siwe ulosema jana, ya kuwa u mashuhuri?
Ya kuwa wajuwa sana, aidha huna kiburi?
Nchini wajulikana, mwanasiasa mahiri,
Bungeni tukuajiri?
2. Siwe ulotushawishi, kwa chumvi na kwa sukari,
Na matamu matamshi, ukaziteka suduri,
Ukanena penya moshi, moto ndiyo yakwe siri,
Nawe ndiye hiyo nari?
3. Siwe uloji‘ta moto, uwakao biribiri,
Kamba ‗tatia fukuto, Litakalo leta kheri‘,
Utatufunua mato, Maisha yawe mazuri,
Tukupe kura waziri?
4. Siwe ulosema hayo, na mengi ukabashiri,
Ukamba wafata nyayo, nyayo ziso utiriri,
Tusiwe na wayowayo, wa kufikirifikiri,
Tukuachie ujari?
5. Siwe tulokuinua, Mabegani kama mwari,
Tungawa twalemelewa, waume tukajasiri,
Kamba tukikuchaguwa, mema kwetu yatajiri,
Tukakeyi kusubiri?
6. Siwe ulotugeuka, kwamba leo u waziri,
Wajiona melimuka, tena ukawa ayari,
Walaghai ukicheka, ukuu umekughuri,
Leo mekuwa hodari?
7. Siwe ulojawa raha, za hino yetu sayari,
Ukawa ja vile shaha, hatukupati shauri,
kutuona ni karaha, wakatiwo twahasiri,
Ushakiya msitari?
8. Siwe uliyetughura, ukafunga na safari,
Ukaelekea bara, Kwa wenzio matajiri,
Ukatuacha majura, na tama kukithiri,
Kanama Ushaghairi?
9. Siwe uliyetuasi, ukenda pasi kwaheri,
Mbona hutwambii nasi, tukajua yetu shari,
Leo una masidisi, husemi na aso gari,
Ndio mezidi jeuri?
10. Siwe‘lotwaa mgwisho, ukawa wajifakhiri?
Chenye mwanzo kina mwisho, hilo wajuwa dhahiri,
Vyaja kutoka vitisho, kwani hayo sidahari,
Mambo mengimdawari?
11. Siwe utakayeiza, mwishowo ukidhihiri,
Siku itayoteleza, kuja kwetu ansari,
Kuja kutubembeleza, kwa nyunga nalo khamri,
Tauya nazo nadhiri.
MASWALI
a) Mtunzi wa shairi hili ana dhamira gani?
b) Taja na ueleze bahari tatu za shairi hili?
c) Onyesha jinsi mtunzi alivyotumia idhini ya kishairi.
d) Taja na ufafanue tamahali ya usemi iliyotawala katika shairi hili.
e) Anayerejelewa alibailika vipi? Eleza.
f) Andika ubeti wa tisa kwa lugha ya nathari.
g) Mshairi ana maana gani kwa kusema:
(i) Wakatiwo twahasiri.
(ii) Ukaziteka suduri.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.(Solved)
Kwa kurejelea hadithi zozote tano katika Diwani Damu Nyeusi, jadili namna ambavyo wahusika wa kike wamesawiriwa.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Nimemwita bwana huyu aje huku juu kusudi mumwone."(Solved)
Damu nyeusi na hadithi zingine
"Nimemwita bwana huyu aje huku juu kusudi mumwone."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Eleza sifa tatu za mzungumzaji.
c) Jadili maudhui ya ubaguzi namna yanavyojitokeza katika hadithi husika
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"(Solved)
Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.
"Hizi kurani zako ndizo zifanyazo nisije huku …"
a) Eleza muktadha wa maneno haya.
b) Eleza umuhimu wa mrejelewa katika dondoo hili kwenye riwaya.
c) Eleza maisha ya msemaji yalivyokuwa kwa mujibu wa Riwaya ya Kidaa Kimemwozea.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Kutowajibika kwa viongozi baada ya mkoloni kuondoka ni dhahiri." Jadili kauli hii kwa mujibu wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)
"Kutowajibika kwa viongozi baada ya mkoloni kuondoka ni dhahiri." Jadili kauli hii kwa mujibu wa Riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Nashukuru sasa umeanza kuona mambo yanavyostahili kwenda."(Solved)
Mstahiki Meya.
"Nashukuru sasa umeanza kuona mambo yanavyostahili kwenda."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Eleza sifa zozote nne za msemaji.
c) Fafanua maudhui ya ufisadi kama yalivyoangaziwa na mwandishi wa tamthilia ya Mstahiki Meya.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Hadhira e pulikeni, kisa changu mpaeni,(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
1) Hadhira e pulikeni, kisa changu mpaeni,
Mpateni mweleweni, mchekeni, mlieni,
Funzo lake mpateni, uamuzi mfanyeni,
Kisa hiki asilani, sisahau maishani.
2) Cha nne niliingiya, mtoto kafurahiya,
Malkia ungedhaniya, duniani meingiya,
Mapambo lijipambiya, kung‘ara kikang‘ariya,
Kisa change chatokeya, mwanzowe nafunguliya.
3) Darasani lizembea, bidii sikutilia,
Starehe nakwambia, nilipenda najutia,
Kimadaha litembea, tausi nilitulia,
Kisa kilinigonjea, mtume! Ningalijua.
4) Muhula kutamatika, dafu sikufua, kaka,
Enda, Ewe, Embe, fika, alama duni, viraka,
Nilipokea waraka, mzazi kahitajika,
Kisa kijatambulika, nakuomba makinika.
5) Muhula wa pili sasa, nikarudia makosa,
Sikupigeni msasa, makali nikayakosa,
Kisu sikunoa hasa, sikukata cha darasa,
Kisa ndicho hicho sasa, ninakupa pasi pesa.
6) Sasa muhula wa tatu, umetimia wanetu,
Mtihani kama chatu, nimeuogopa, mtu,
Sijausomea katu, ningalilindaje utu?
Kisa mkasa wa chatu, kilinipata wa kwetu.
7) Mbwa katu hafi maji, kiona ufuko, maji,
Tajaribu sife maji, hata akiyanywa maji,
Ilibidi twende jiji, kuwasaka wajuaji,
Kisa change mfumbaji, sasa dawa lihitaji.
8) Mpango ulitolewa, mchango ulipangiwa,
Pesa tele litolewa, na simu kununuliwa,
Mtandao liwekewa, ‗kunani‘ kupakuliwa,
Kisa cha simu kujuwa, linifanya kupagawa.
9) Tulikata dari ona, simu yetu kufichana,
Usiku tulikutana, maswali kurushiana,
Majibu tulipeana, "panga‘ kabadilishana,
Kisa kinajulikana, vile nilivyokazana.
10) Niliyangoja majibu, nikiwa na hamu, babu,
Nilikimya kama bubu, nisije toa aibu,
Nilivichoma vitabu, bila kuwa na sababu.
Kisa kawa masaibu, kashindwa kuyaharibu.
11) Kutangazwa matokeo, nakumbuka hadi leo,
Lilishangaza toleo, sikuamini redio,
Lipokea matokea, yalinitia kimbio,
Kisa change mchocheo, haya yangu mapokeo.
12) Nilifeli mtihani, sababu simu juweni,
Najuta nisameheni, nijilaumu moyoni,
Ningalijua mbeleni, ningalisoma jamani,
Kisa nimemalizeli, wenzangu mzindukeni.
13) Watahiniwa mlipo, msiwe mithili popo,
Skuli kwenu kuwepo, nia mpate malipo,
Bidii hapo mlipo, toa uzembe pasipo,
Kisa change kingalipo, simu daima siwepo!
MASWALI
a) Taja anwani mwafaka ya shairi hili.
b) Fafanua mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili.
c) Bainisha nafsi lengwa katika shairi hili.
d) Changanua arudhi zilizotumiwa na mtunzi wa shairi hili.
e) Andika ubeti wa kumi katika lugha nathari.
f) Eleza maana ya maneno na vifungu vifuatavyo kwa mujibu wa shairi.
g) Eleza maana ya maneno na vifungu vifuatavyo kwa mujibu wa shairi.
(i) Sikukata cha darasa
(ii) Yalinitia kimbio
(iii) Kupagawa
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"(Solved)
Damu nyeusi na hadithi zingine
"Leo ni siku, siku ya nyani kufa ambapo miti yote huteleza"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili.
c) Huku ukitoa mifano, thibitisha maudhui sita ambayo yamejitokeza katika hadithi ya Damu Nyeusi na wanayoyaendeleza.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- Kwa kutoa mifano kumi,eleza vizingiti walivyokumbana navyo wanacheneo wakati wa kupigania mageuzi.(Solved)
Mstahiki Meya
Kwa kutoa mifano kumi,eleza vizingiti walivyokumbana navyo wanacheneo wakati wa kupigania mageuzi.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Iwapo umefanya, yapo mengi ambayo hayakunyoka."(Solved)
Mstahiki Meya
"Iwapo umefanya, yapo mengi ambayo hayakunyoka."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Tambua mbinu moja iliyotumika katika muktadha wa dondoo.
c) Fafanua kauli kwamba"yapo mengi ambayo hayakunyoka".
d) Eleza jinsi baadhi ya wahusika walivyojaribu kuyanyoosha.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Umenena ndipo ndugu yangu. Hiyo ndiyo tanzia ya Afrika huru."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Ni nini sifa za mvuto zinazowaleta pamoja mzungumzaji na mzungumziwa.
c) Tambua na ufafanue mbinu inayotumika katika dondoo.
d) Kwa mifano mwafaka fafanua tanzia hiyo inayorejelewa katika dondoo.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)
- "Ikamchagiza kama vile kiu ya mtu aliyekuwa akisafiri jangwani".(Solved)
DAMU NYEUSI
"Ikamchagiza kama vile kiu ya mtu aliyekuwa akisafiri jangwani".
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili
(b) Fafanua sifa zozote nne za mrejelewa
(c) Eleza fani uliotumiwa na mwandishi katika dondoo hili
(d) Kwa kurejea hadithi zozote tatu,eleza namna wahusika wowote watatu walivyoathiriwa na kiu.
Date posted: October 2, 2019. Answers (1)