Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu la ajali za barabarani bado inaendelea kuwafedhehesha wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya...

      

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu la ajali za barabarani bado inaendelea kuwafedhehesha wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya matumizi ya vidhibiti mwendo na kanda za usalama.
Ajali za barabarani zinaangamiza idadi kubwa ya watu kila mwaka wakiwemo viongozi na watu mashuhuri. Miongoni mwa sababu ambazo zinaleta maafa barabarani pamoja na uendeshaji kasi kupita inavyotakikana, yaani kukiuka masharti yaliyowekwa na wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano. Madereva wengi hung‘oa vidhibiti mwendo vilivyowekwa, hawarekebishi mikanda ya usalama, wala hawayapeleki magari yao kukaguliwa mara kwa mara kama inavyopaswa. Yale yanayopelekwa kwa ukaguzi, mengi hushindwa kutekeleza kanuni zilizoweka kwa hivyo hutegemea hongo kuwa barabarani. Fauka ya hayo, madereva wa malori na matrela mara nyingi huendesha magari hayo wakiwa walevi. Dawa za kulevya kama miraa na bangi hutumiwa sana na hawa na matokeo yake huwa ajali mbaya.
Hata hivyo, lawama haiwezi kuelekezewa madereva pekee. Ukiangazia barabara nchini Kenya utapata kuwa barabara haziko katika hali nzuri. Zile za lami zimekuwa na mashimo makubwa ambapo mvua ikinyesha hufanya vidimbwi mithili ya michimbo ya madini yaliyojaa maji baada ya kuachwa wazi. Na zile barabara zisizokuwa na lami zimeharibika kiasi kwamba
ni vigumu kuzitofautisha na njia za ng‘ombe kwenye maeneo kame. Kinachohitajika ni kuzirudisha katika kiwango ambacho zinaweza kufaa tena.
Wananchi pia inafaa waelimishwe ili wasikubali kupanda magari ambayo tayari yamejaa. Hili litawasaidia wananchi wenyewe kudumisha usalama wao barabarani. Pia inawafaa watambue ya kwamba wana jukumu la kuwaarifu walinda usalama endapo dereva anaendesha kwa kasi kuliko ile ya kilomita themanini kwa saa iliyokubaliwa. Inafahamika kuwa maafia wa usalama ndio wafisadi zaidi, hivyo basi huchangia katika kuongeza idadi ya vifo barabarani. Katika vita vya ufisadi na ajali za barabarani ni mwanachi mwenyewe ambaye atawezesha kukomesha hali hii. Kwa mfano, afisa wa usalama akipatikana akichukua hongo, yeye pamoja na yule aliyetoa hongo wakamatwe na kupelekwa kwenye vituo vya kukabiliana na ufisadi na kuchukuliwa hatua kali, matatizo haya yataisha. Lakini kabla kufikia hapo, ni muhimu kumhamasisha mwananchi kuhusu haki zake na namna ya kukabiliana na suala hili la ufisadi. Hali hii inatuonyesha kwamba mipango maalum inapaswa kufanywa na serikali ili kuwaelimisha wananchi kama hatua ya kwanza kukabiliana na ufisadi, hatimaye izilainishe sekta zote wala si ya uchukuzi na mawasiliano pekee.
(a) Kwa kurejelea aya ya pili na ya tatu, eleza mambo yanayochangia ajali za barabarani. (Maneno 45-50)
(b) Fupisha ujumbe wa aya ya mwisho. (maneno 50-55)
(c) Mbali na ajali za barabarani, taja, tatizo lingine sugu ambalo linakumba nchi ya Kenya
(d) Mwandishi anapendekeza hatua zipi zichukuliwe na serikali ili suluhisho la kudumu
lipatikane?
(e) Taja hatua ambazo serikali imechukua ili kuimarisha uchukuzi
(f) Ni kitu gani ambacho kinaonyesha kuwa serikali imeshindwa kukabiliana na ajali
barabarani?
(g) Eleza maana ya maneno haya:-
(i) Tatizo sugu.
(ii) Vithibiti mwendo.
(iii) Machimbo.
(iv) Ukarabati.
(v) Hongo.
(vi) Kuhamasisha..

  

Answers


sharon
a)
- Uendashaji kasi kupita inavyotakikana
- Kung‘oa vidhibiti mwendo vilivyowekwa.
- Kutorekebisbwa kwa mikanda ya usalama.
- Kutopelekwa kwa magari kukaguliwa mara kwa mara.
- Magari mengi kushindwa kutekeleza kanuni zilizowekwa.
- Utegemezi wa hongo kuwa barabarani.
- Madereva huendesha magari wakiwa waievi,
- Barabara mbovu.
b)
- Wananchi waelimishwe iii wasikubali kupanda magari ambayo yamejaa.
- Wananchi wana jukumu la kuwaarifu walinda usalama dereva akikiuka kanuni.
- Wananchi waripoti wanaotoa na kuchukua hongo.
- Wafisadi wakamatwe.
- Wachukuliwe hatua kali.
- Kuwahamasisha wananchi kuhusiana na haki zao.
- Serikali iwaelimishe wananchi namna ya kukabiliana na uti sadi.
- Ilainishe sekta zote wala si ya uchukuzi na mawasiliano pekee.


c) Ufisadi


(d) (i) Wananchi wafahamishwe ya kwamba wana jukumu la kuwaeleza walinda usalalam
endapo gari linapelekwa kwa kasi kupita kiasi.
(ii) Wananchi waelimishwe ili wasikubali kuingia kwenye magari ambayo yamejaa
kupita kiasi


(e) (i) Kuwekwa kwa vidhibiti mwendo kwenye magari ya abiria
(ii) Kuwachukulia hatua wale wanaotoa na kuchukua hongo
(iii) Kurekebisha baadhi ya barabara mbovu
(iv) Kuwekwa kwa mikanda ya usalama kwenye magari


(f) (i) Kung’olewa kwa vidhibiti mwendo
(ii) Kutokuweko kwa mikanda ya usalama
(iii) Gari kwenda kwa kasi zaidi kutokana na kurekebishwa kwa vidhibiti mwendo


(g) (i) Shida ambayo imedumu muda mrefu bila suluhisho kuliko kiwango kilichokubaliwa
(ii) Vifaa vya gari kwenda kwa kasi kuliko kiwango kilichokubaliwa
(iii) Mashimo yaliyoachwa baada ya madini kutolewa
(iv) Urekebishaji
(v) Kuchukua au kutoa mlungula/rushwa
(vi) Tia hamu ya kufanya jambo
sharon kalunda answered the question on October 3, 2019 at 08:01


Next: Give the differences between print and non-print media.
Previous: Explain the effect of discharging hot water in an aquatic ecosystem.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions