Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Ainisha viambishi katika kitenzi kifuatacho. Walimtembelea

      

Ainisha viambishi katika kitenzi kifuatacho.
Walimtembelea

  

Answers


sharon
Wa - nafsi
li - wakati uliopita
m – mtendwa
tembe - mzizi
le - kauli
a - kiishio
sharon kalunda answered the question on October 3, 2019 at 08:20


Next: Explain how high osmotic pressure is reduced back to normal in the human body.
Previous: Discuss the types of Non- Print Media.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Eleza maana ya sentensi ya masharti.(Solved)

    Eleza maana ya sentensi ya masharti.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika sifa mbili za irabu / u /(Solved)

    Andika sifa mbili za irabu / u /

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • (Solved)

    Andika sauti yenye sifa zifuatazo;
    -Kikwamizo
    -Kaakaa gumu
    -Sighuna

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu la ajali za barabarani bado inaendelea kuwafedhehesha wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu la ajali za barabarani bado inaendelea kuwafedhehesha wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya matumizi ya vidhibiti mwendo na kanda za usalama.
    Ajali za barabarani zinaangamiza idadi kubwa ya watu kila mwaka wakiwemo viongozi na watu mashuhuri. Miongoni mwa sababu ambazo zinaleta maafa barabarani pamoja na uendeshaji kasi kupita inavyotakikana, yaani kukiuka masharti yaliyowekwa na wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano. Madereva wengi hung‘oa vidhibiti mwendo vilivyowekwa, hawarekebishi mikanda ya usalama, wala hawayapeleki magari yao kukaguliwa mara kwa mara kama inavyopaswa. Yale yanayopelekwa kwa ukaguzi, mengi hushindwa kutekeleza kanuni zilizoweka kwa hivyo hutegemea hongo kuwa barabarani. Fauka ya hayo, madereva wa malori na matrela mara nyingi huendesha magari hayo wakiwa walevi. Dawa za kulevya kama miraa na bangi hutumiwa sana na hawa na matokeo yake huwa ajali mbaya.
    Hata hivyo, lawama haiwezi kuelekezewa madereva pekee. Ukiangazia barabara nchini Kenya utapata kuwa barabara haziko katika hali nzuri. Zile za lami zimekuwa na mashimo makubwa ambapo mvua ikinyesha hufanya vidimbwi mithili ya michimbo ya madini yaliyojaa maji baada ya kuachwa wazi. Na zile barabara zisizokuwa na lami zimeharibika kiasi kwamba
    ni vigumu kuzitofautisha na njia za ng‘ombe kwenye maeneo kame. Kinachohitajika ni kuzirudisha katika kiwango ambacho zinaweza kufaa tena.
    Wananchi pia inafaa waelimishwe ili wasikubali kupanda magari ambayo tayari yamejaa. Hili litawasaidia wananchi wenyewe kudumisha usalama wao barabarani. Pia inawafaa watambue ya kwamba wana jukumu la kuwaarifu walinda usalama endapo dereva anaendesha kwa kasi kuliko ile ya kilomita themanini kwa saa iliyokubaliwa. Inafahamika kuwa maafia wa usalama ndio wafisadi zaidi, hivyo basi huchangia katika kuongeza idadi ya vifo barabarani. Katika vita vya ufisadi na ajali za barabarani ni mwanachi mwenyewe ambaye atawezesha kukomesha hali hii. Kwa mfano, afisa wa usalama akipatikana akichukua hongo, yeye pamoja na yule aliyetoa hongo wakamatwe na kupelekwa kwenye vituo vya kukabiliana na ufisadi na kuchukuliwa hatua kali, matatizo haya yataisha. Lakini kabla kufikia hapo, ni muhimu kumhamasisha mwananchi kuhusu haki zake na namna ya kukabiliana na suala hili la ufisadi. Hali hii inatuonyesha kwamba mipango maalum inapaswa kufanywa na serikali ili kuwaelimisha wananchi kama hatua ya kwanza kukabiliana na ufisadi, hatimaye izilainishe sekta zote wala si ya uchukuzi na mawasiliano pekee.
    (a) Kwa kurejelea aya ya pili na ya tatu, eleza mambo yanayochangia ajali za barabarani. (Maneno 45-50)
    (b) Fupisha ujumbe wa aya ya mwisho. (maneno 50-55)
    (c) Mbali na ajali za barabarani, taja, tatizo lingine sugu ambalo linakumba nchi ya Kenya
    (d) Mwandishi anapendekeza hatua zipi zichukuliwe na serikali ili suluhisho la kudumu
    lipatikane?
    (e) Taja hatua ambazo serikali imechukua ili kuimarisha uchukuzi
    (f) Ni kitu gani ambacho kinaonyesha kuwa serikali imeshindwa kukabiliana na ajali
    barabarani?
    (g) Eleza maana ya maneno haya:-
    (i) Tatizo sugu.
    (ii) Vithibiti mwendo.
    (iii) Machimbo.
    (iv) Ukarabati.
    (v) Hongo.
    (vi) Kuhamasisha..

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Zaraa ndio uti wa mgongo wa taifa la Kenya. Viwanda vingi nchini hutegemea kilimo kama malighafi yake na kuwalisha wafanyakazi(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Zaraa ndio uti wa mgongo wa taifa la Kenya. Viwanda vingi nchini hutegemea kilimo kama malighafi yake na kuwalisha wafanyakazi. Licha ya umuhimu wa sekta hii, mkulima ambaye ndiye nguzo za zaraa anaendelea kukabiliwa na matatizo mbalimbali yanavokwamiza juhudi zake.
    Mojawapo ya matatizo yanayomkabili mkulima ni ukosefu wa ushauri wa zaraa. Wataalamu wanaotarajiwa kumshauri mkulima kuhusu njia bora za kuzalisha na kuongeza pato lake ni haba ikilinganishwa na idadi ya wakulima wanaohitaji ushauri. Wachache walioko nao wanakwamizwa na mambo tofauti. Mathalani, utawapata hawaendi nyanjani ili kukutana na wakulima kwa kuwa hawana usafiri. Iwapo usafiri upo, huenda petroli ikawa ni kizungumkuti. Halikadhalika, usisahau kuwa baadhi ya wataalamu hawa ni walazadamu au mafisadi. Kuna wale wanaofika ofisini na kushinda siku nzima wakisoma gazeti huku wakijaza miraba, wakicheza bao au karata. Kuna wale nao ambao hufika ofisini wakaangika koti au sweta kitini ili waonekane kuwa bado wapo na kisha kutokomea kwenda kushughulikia mambo yao ya kibinafsi yasiyohusu ndewe wala sikio kazi waliyoajiriwa kuifanya.
    Ukosefu wa sera mwafaka kuhusu ardhi nalo ni tatizo jingine linalotatiza kilimo nchini. Serikali haijaweka sera mahususi kuhusu matumizi ya ardhi. Wananchi wengi huongozwa na taratibu za utamaduni wa nasaba zao. Taratibu hizi hupendekeza ugawaji wa ardhi kwa minajili ya urithi kulingana na warithi waliopo. Si ajabu kuwa kote nchini, ardhi inayofaa kwa kilimo imekatwakatwa vipande vidogo vidogo ambavyo haviwezi kuwa na faida kwa zaraa.
    Kushindwa kwa mkulima kuongeza virutubishi ardhini ni changamoto nyingine inayokabili kilimo nchini. Ulimaji wa kile kipande cha ardhi mwaka nenda mwaka rudi, bila kukipa nafasi ya kukipumzisha, huufanya mchanga kupoteza virutubishi muhimu vinavyohitajiwa na mimea. Hili nalo huchangia kupunguza uzalishaji wa mazao. Ili kutatua tatizo hili, wakulima wengi hukimbilia mbolea za kisasa ambazo badala ya kumsaidia, humwongezea madhila. Mbolea hizi zinatambulikana kuchangia uchafuzi wa mchanga na ardhi.
    Mabadiliko ya hali ya anga nayo huongeza msururu wa madhila ya mkulima. Mabadiliko haya yamemfanya mkulima kushindwa kupanga wakati anaotakiwa kutayarisha shamba, kupanda, kupalilia, kunyunyizia dawa na kadhalika. Mvua imekuwa adimu. Badala yake panakuwa na vipindi virefu vya kiangazi ambavyo huathiri bidii za mkulima. Maji nayo yanaendelea kupungua na wakulima wengi hawawezi kukimu mahitaji ya unyunyizaji maji mashambani.

    (a) Andika anwani inayofaa kifungu hiki.
    (b) Huku ukirejelea kifungu, fafanua umuhimu wa kilimo hapa nchini.
    (c) Eleza changamoto tatu zinazowakabili wataalamu wa kilimo
    (d) Mbali na matatizo yanayowakumba wataalamu onyesha matatizo mengine matatu yanayokumba sekta ya zaraa. (alama 6)
    (e) Eleza maana za msamiati ufuatao kulingana na taarifa.
    (i) yanayokwamiza
    (ii) sera
    (iii) adimu

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Eleza sifa za lugha ya hotelini.(Solved)

    Eleza sifa za lugha ya hotelini.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Pambanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mstari. Naimba huku nafanya kazi(Solved)

    Pambanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mstari.

    Naimba huku nafanya kazi

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume cha maneno yafuatayo. i. Tandika ii. Umba(Solved)

    Andika kinyume cha maneno yafuatayo.

    i. Tandika

    ii. Umba

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Kamilisha methali zifuatazo ? i. Cha kuvunda(Solved)

    Kamilisha methali zifuatazo ?

    i. Cha kuvunda

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi zifuatazo. i. Mimi nilicheza. ii. Wewe huchora(Solved)

    Kanusha sentensi zifuatazo.

    i. Mimi nilicheza.

    ii. Wewe huchora

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Tambua kikundi nomino (KN) na kikundi tenzi (KT) katika sentensi zifuatazo. i. Anatembea kwa madaa kama tausi(Solved)

    Tambua kikundi nomino (KN) na kikundi tenzi (KT) katika sentensi zifuatazo.

    i. Anatembea kwa madaa kama tausi

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendeshana. i. Penda . ii. Endesha.(Solved)

    Andika vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendeshana.

    i. Penda .

    ii. Endesha.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Geuza sentensi zifuatazo katika hali ya usemi halisi. i. Ruhenialishauliwa na kasisiaache tabia mbaya. ii. Mwalimu alimwabiapremjiafanye bidii katika masomo yake.(Solved)

    Geuza sentensi zifuatazo katika hali ya usemi halisi.

    i. Ruhenialishauliwa na kasisiaache tabia mbaya.

    ii. Mwalimu alimwabiapremjiafanye bidii katika masomo yake.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika ukubwa. i. Jiji hili litapanuka upesi ii. Jizee lililokosa adabu limekaripiwa. (Solved)

    Andika katika ukubwa.

    i. Jiji hili litapanuka upesi.

    ii. Jizee lililokosa adabu limekaripiwa.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Fafanua maana ya misemo ifuatayo. i. Kula mate(Solved)

    Fafanua maana ya misemo ifuatayo.

    i. Kula mate

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Fafanua sifa zozote za lugha rasmi.(Solved)

    Fafanua sifa zozote za lugha rasmi.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Jazapengo kwa kiulizi sahihi kisha uandike sentensi kwa wingi Ni mpishi ________________ aliyepika(Solved)

    Jazapengo kwa kiulizi sahihi kisha uandike sentensi kwa wingi

    Ni mpishi ________________ aliyepika

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Tumiavivumishi vya sifa katika mabanokukamilisha sentensi zifuatazo. i. Mtoto Yule ni ______________________ (nene) ii. Bei ya meli ni _____________________ mno (ghali)(Solved)

    Tumiavivumishi vya sifa katika mabanokukamilisha sentensi zifuatazo.

    i. Mtoto Yule ni ______________________ (nene)

    ii. Bei ya meli ni _____________________ mno (ghali)

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya lugha rasmi.(Solved)

    Eleza maana ya lugha rasmi.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha nomino hizi ni za aina gani. i. Sukari. ii. Mapenzi.(Solved)

    Bainisha nomino hizi ni za aina gani.

    i. Sukari.

    ii. Mapenzi.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)