Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Tunga sentensi ukitumia yambwa tendwa na yambwa tendewa.

      

Tunga sentensi ukitumia yambwa tendwa na yambwa tendewa.

  

Answers


sharon
Mtoto alinunuliwa baiskeli na baba.
Mtoto - Yambwa tendewa
Baiskeli - Yambwa tendwa.
sharon kalunda answered the question on October 3, 2019 at 09:06


Next: Andika sentensi ifuatayo katika hali ya wastani. Kijumba hiki kilijengwa karibu na kijiji.
Previous: Identify limitation of algorithms?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Andika sentensi ifuatayo katika hali ya wastani. Kijumba hiki kilijengwa karibu na kijiji.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika hali ya wastani.
    Kijumba hiki kilijengwa karibu na kijiji.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha kiima na kiarifa katika sentensi ifuatayo: Kitabu chake kilianguka majini.(Solved)

    Onyesha kiima na kiarifa katika sentensi ifuatayo:
    Kitabu chake kilianguka majini.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa. "Kazi yako itamalizika kesho." Tajiri alimwambia mwajiriwa.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa.
    "Kazi yako itamalizika kesho." Tajiri alimwambia mwajiriwa.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha matumizi ya kiambishi "ni" katika sentensi ifuatayo: Maria ni mpole ndio maana ninapenda kwenda kwao.(Solved)

    Onyesha matumizi ya kiambishi "ni" katika sentensi ifuatayo:
    Maria ni mpole ndio maana ninapenda kwenda kwao.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi hii Ijapokuwa kulikuwa na joto kali niliondoka kwenda sokoni.(Solved)

    Onyesha kishazi huru na kishazi tegemezi katika sentensi hii
    Ijapokuwa kulikuwa na joto kali niliondoka kwenda sokoni.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika vitenzi vifuatavyo katika mnyambuliko uliopewa. i) kunja (tendeka) ii) la (tendesheana)(Solved)

    Andika vitenzi vifuatavyo katika mnyambuliko uliopewa.
    i) kunja (tendeka)
    ii) la (tendesheana)

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali ya kuendelea. Juma anafundisha katika shule hii.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali ya kuendelea.
    Juma anafundisha katika shule hii.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo uliyopewa. Yaya alimpikia mtoto chakula kitamu. Anza : chakula……(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo uliyopewa.
    Yaya alimpikia mtoto chakula kitamu.
    Anza : chakula……

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Uzi iko kwa ngeli gani?(Solved)

    Uzi iko kwa ngeli gani?

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Weka "kiziwi" kwa ngeli yake.(Solved)

    Weka "kiziwi" kwa ngeli yake.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Tumia neno "Nairobi" katika sentensi kama : (Solved)

    Tumia neno "Nairobi" katika sentensi kama :
    i) Nomino
    ii) Kielezi

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentesi moja kutofautisha maana ya: ngoma goma(Solved)

    Tunga sentesi moja kutofautisha maana ya:
    ngoma
    goma

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha viambishi katika kitenzi kifuatacho. Walimtembelea(Solved)

    Ainisha viambishi katika kitenzi kifuatacho.
    Walimtembelea

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya sentensi ya masharti.(Solved)

    Eleza maana ya sentensi ya masharti.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Andika sifa mbili za irabu / u /(Solved)

    Andika sifa mbili za irabu / u /

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • (Solved)

    Andika sauti yenye sifa zifuatazo;
    -Kikwamizo
    -Kaakaa gumu
    -Sighuna

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu la ajali za barabarani bado inaendelea kuwafedhehesha wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Aibu kubwa ya taifa kushindwa kukabiliana na tatizo sugu la ajali za barabarani bado inaendelea kuwafedhehesha wahusika katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano licha ya matumizi ya vidhibiti mwendo na kanda za usalama.
    Ajali za barabarani zinaangamiza idadi kubwa ya watu kila mwaka wakiwemo viongozi na watu mashuhuri. Miongoni mwa sababu ambazo zinaleta maafa barabarani pamoja na uendeshaji kasi kupita inavyotakikana, yaani kukiuka masharti yaliyowekwa na wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano. Madereva wengi hung‘oa vidhibiti mwendo vilivyowekwa, hawarekebishi mikanda ya usalama, wala hawayapeleki magari yao kukaguliwa mara kwa mara kama inavyopaswa. Yale yanayopelekwa kwa ukaguzi, mengi hushindwa kutekeleza kanuni zilizoweka kwa hivyo hutegemea hongo kuwa barabarani. Fauka ya hayo, madereva wa malori na matrela mara nyingi huendesha magari hayo wakiwa walevi. Dawa za kulevya kama miraa na bangi hutumiwa sana na hawa na matokeo yake huwa ajali mbaya.
    Hata hivyo, lawama haiwezi kuelekezewa madereva pekee. Ukiangazia barabara nchini Kenya utapata kuwa barabara haziko katika hali nzuri. Zile za lami zimekuwa na mashimo makubwa ambapo mvua ikinyesha hufanya vidimbwi mithili ya michimbo ya madini yaliyojaa maji baada ya kuachwa wazi. Na zile barabara zisizokuwa na lami zimeharibika kiasi kwamba
    ni vigumu kuzitofautisha na njia za ng‘ombe kwenye maeneo kame. Kinachohitajika ni kuzirudisha katika kiwango ambacho zinaweza kufaa tena.
    Wananchi pia inafaa waelimishwe ili wasikubali kupanda magari ambayo tayari yamejaa. Hili litawasaidia wananchi wenyewe kudumisha usalama wao barabarani. Pia inawafaa watambue ya kwamba wana jukumu la kuwaarifu walinda usalama endapo dereva anaendesha kwa kasi kuliko ile ya kilomita themanini kwa saa iliyokubaliwa. Inafahamika kuwa maafia wa usalama ndio wafisadi zaidi, hivyo basi huchangia katika kuongeza idadi ya vifo barabarani. Katika vita vya ufisadi na ajali za barabarani ni mwanachi mwenyewe ambaye atawezesha kukomesha hali hii. Kwa mfano, afisa wa usalama akipatikana akichukua hongo, yeye pamoja na yule aliyetoa hongo wakamatwe na kupelekwa kwenye vituo vya kukabiliana na ufisadi na kuchukuliwa hatua kali, matatizo haya yataisha. Lakini kabla kufikia hapo, ni muhimu kumhamasisha mwananchi kuhusu haki zake na namna ya kukabiliana na suala hili la ufisadi. Hali hii inatuonyesha kwamba mipango maalum inapaswa kufanywa na serikali ili kuwaelimisha wananchi kama hatua ya kwanza kukabiliana na ufisadi, hatimaye izilainishe sekta zote wala si ya uchukuzi na mawasiliano pekee.
    (a) Kwa kurejelea aya ya pili na ya tatu, eleza mambo yanayochangia ajali za barabarani. (Maneno 45-50)
    (b) Fupisha ujumbe wa aya ya mwisho. (maneno 50-55)
    (c) Mbali na ajali za barabarani, taja, tatizo lingine sugu ambalo linakumba nchi ya Kenya
    (d) Mwandishi anapendekeza hatua zipi zichukuliwe na serikali ili suluhisho la kudumu
    lipatikane?
    (e) Taja hatua ambazo serikali imechukua ili kuimarisha uchukuzi
    (f) Ni kitu gani ambacho kinaonyesha kuwa serikali imeshindwa kukabiliana na ajali
    barabarani?
    (g) Eleza maana ya maneno haya:-
    (i) Tatizo sugu.
    (ii) Vithibiti mwendo.
    (iii) Machimbo.
    (iv) Ukarabati.
    (v) Hongo.
    (vi) Kuhamasisha..

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Zaraa ndio uti wa mgongo wa taifa la Kenya. Viwanda vingi nchini hutegemea kilimo kama malighafi yake na kuwalisha wafanyakazi(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Zaraa ndio uti wa mgongo wa taifa la Kenya. Viwanda vingi nchini hutegemea kilimo kama malighafi yake na kuwalisha wafanyakazi. Licha ya umuhimu wa sekta hii, mkulima ambaye ndiye nguzo za zaraa anaendelea kukabiliwa na matatizo mbalimbali yanavokwamiza juhudi zake.
    Mojawapo ya matatizo yanayomkabili mkulima ni ukosefu wa ushauri wa zaraa. Wataalamu wanaotarajiwa kumshauri mkulima kuhusu njia bora za kuzalisha na kuongeza pato lake ni haba ikilinganishwa na idadi ya wakulima wanaohitaji ushauri. Wachache walioko nao wanakwamizwa na mambo tofauti. Mathalani, utawapata hawaendi nyanjani ili kukutana na wakulima kwa kuwa hawana usafiri. Iwapo usafiri upo, huenda petroli ikawa ni kizungumkuti. Halikadhalika, usisahau kuwa baadhi ya wataalamu hawa ni walazadamu au mafisadi. Kuna wale wanaofika ofisini na kushinda siku nzima wakisoma gazeti huku wakijaza miraba, wakicheza bao au karata. Kuna wale nao ambao hufika ofisini wakaangika koti au sweta kitini ili waonekane kuwa bado wapo na kisha kutokomea kwenda kushughulikia mambo yao ya kibinafsi yasiyohusu ndewe wala sikio kazi waliyoajiriwa kuifanya.
    Ukosefu wa sera mwafaka kuhusu ardhi nalo ni tatizo jingine linalotatiza kilimo nchini. Serikali haijaweka sera mahususi kuhusu matumizi ya ardhi. Wananchi wengi huongozwa na taratibu za utamaduni wa nasaba zao. Taratibu hizi hupendekeza ugawaji wa ardhi kwa minajili ya urithi kulingana na warithi waliopo. Si ajabu kuwa kote nchini, ardhi inayofaa kwa kilimo imekatwakatwa vipande vidogo vidogo ambavyo haviwezi kuwa na faida kwa zaraa.
    Kushindwa kwa mkulima kuongeza virutubishi ardhini ni changamoto nyingine inayokabili kilimo nchini. Ulimaji wa kile kipande cha ardhi mwaka nenda mwaka rudi, bila kukipa nafasi ya kukipumzisha, huufanya mchanga kupoteza virutubishi muhimu vinavyohitajiwa na mimea. Hili nalo huchangia kupunguza uzalishaji wa mazao. Ili kutatua tatizo hili, wakulima wengi hukimbilia mbolea za kisasa ambazo badala ya kumsaidia, humwongezea madhila. Mbolea hizi zinatambulikana kuchangia uchafuzi wa mchanga na ardhi.
    Mabadiliko ya hali ya anga nayo huongeza msururu wa madhila ya mkulima. Mabadiliko haya yamemfanya mkulima kushindwa kupanga wakati anaotakiwa kutayarisha shamba, kupanda, kupalilia, kunyunyizia dawa na kadhalika. Mvua imekuwa adimu. Badala yake panakuwa na vipindi virefu vya kiangazi ambavyo huathiri bidii za mkulima. Maji nayo yanaendelea kupungua na wakulima wengi hawawezi kukimu mahitaji ya unyunyizaji maji mashambani.

    (a) Andika anwani inayofaa kifungu hiki.
    (b) Huku ukirejelea kifungu, fafanua umuhimu wa kilimo hapa nchini.
    (c) Eleza changamoto tatu zinazowakabili wataalamu wa kilimo
    (d) Mbali na matatizo yanayowakumba wataalamu onyesha matatizo mengine matatu yanayokumba sekta ya zaraa. (alama 6)
    (e) Eleza maana za msamiati ufuatao kulingana na taarifa.
    (i) yanayokwamiza
    (ii) sera
    (iii) adimu

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Eleza sifa za lugha ya hotelini.(Solved)

    Eleza sifa za lugha ya hotelini.

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)

  • Pambanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mstari. Naimba huku nafanya kazi(Solved)

    Pambanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mstari.

    Naimba huku nafanya kazi

    Date posted: October 3, 2019.  Answers (1)