Tamaa
-Lucy alikuwa akiota miaka mingi kwenda London kwa sababu ni nchi arnbayo imeendelea sana. kwa mfano barabara pana zilizojaa magari.
-Alitamani muluki ya haraka haraka.
-Uingereza wakimbizi walipewa nyumba au makazi, na starehe nyinginezo
-Lucy alipitapita jijini macho yake yakitazama nyuso za wazungu - vijana na wazee
-Lucy kumkimbilia mzee mmoja wa kizungu mkofu, mbovu.
-Katika ukumbi wa sinema, Lucy hakuona mchezo akifikiria wakati utakapoisha apate zawadi aliyoahidiwa.
-Lucy anatamani kuomba zawadi kubwa ya kuchukuliwa Uingereza.
-Lucy anatamani Crusoe afe.
-Alitaka ifike kesho kutwa akarithishwe ile mali.
Mauti
-Lucy kuolewa na mwanamume mzee asiye na nguvu za aina yoyote.
-Kumtunza mzee mkongwe - kumkanda, kumlisha n.k.
-Anaanza kuchoka kuishi na mzee ambaye hawezi kumchangamsha kwa namna yoyote.
-Lile jumba lilimzidishia hali ya upweke.
-Lucy alianza kumchukia Crusoe
-Awali Lucy alipuuza masomo na hakufaulu vizuri.
-Lucy alipata ajali ya gari na kupoteza uhai wake.
sharon kalunda answered the question on October 3, 2019 at 11:05
- "Uniulie nini na ndoa yetu na wewe inamhusu pia yeye?"(Solved)
Mwana wa Darubini (K. Mwende Mbai)
"Uniulie nini na ndoa yetu na wewe inamhusu pia yeye?"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Eleza sifa zozote nne za msemewa.
c) Jadili madhila yanayomkumba mwanamke katika hadithi hii.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Lazima kwanza mnihakikishie kuwa huyo sumu hapati hata fununu ya jambo hili."(Solved)
Mstahiki Meya
"Lazima kwanza mnihakikishie kuwa huyo sumu hapati hata fununu ya jambo hili."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Taja sifa zozote nne za msemaji.
c) Andika umuhimu wa huyo sumu.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Tayari nimemkabidhi barua ya kujiuzulu ninapohusika."(Solved)
Mstahiki Meya
Tayari nimemkabidhi barua ya kujiuzulu ninapohusika."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Mbali na changamoto inayofanya msemaji kujiuzulu, jadili changamoto nyinginezo zinazowakumba wanacheneo.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Eleza namna mbinu ya Taharuki ilivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.(Solved)
Eleza namna mbinu ya Taharuki ilivyotumiwa na mwandishi wa riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Kwa kufafanua hoja saba thibitisha kwamba kuna haja ya kuwa na Revolution.(Solved)
Kidagaa kimemwozea
Kwa kufafanua hoja saba thibitisha kwamba kuna haja ya kuwa na Revolution.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Lakini bila matumaini hatuwezi kwenda mbele na Revolution."(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Lakini bila matumaini hatuwezi kwenda mbele na Revolution."
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
ii) Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza katika dondoo hili.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Naingia ukumbini, nyote kuwakariria,(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Naingia ukumbini, nyote kuwakariria,
Ushairi niwapeni, hoja nitawaachia,
Mnipe masikioni, shike nachoelezea,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Naanza kwa uzalendo, nchi yetu tuipende,
Yadhihirishe matendo, nchi yetu tuilinde,
Wa kila mtu mwendo, usije kawa mpinde,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili
Wote tuwe na umoja, tuuache ukabila
Kabila lisiwe hoja, mwenza kumnyima hela,
Taifa letu ni moja, Mkenya ndilo kabila,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Linda demokrasia, uongozi tushiriki,
Haki kujielezea, wachotaka na hutaki.
Changu naweza tetea, demokrasia haki,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Tena adili usawa, mgao raslimali,
Bajeti inapogawa, isawazishe ratili.
Idara zilizoundwa, ‗faidi kila mahali,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Tuwe na uadilifu, twache tamaa ya hongo,
Tusiwe na udhaifu, wa kuwa watu waongo,
Tukomeshe uhalifu, kisha tuache maringo,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Ubinafsi si adili, ila ni kusaidia,
Ukiwa nayo mali, asiyenacho patia,
Kama mtu mswahili, ubinafsi achia,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.
Na inavyoelezea, katiba ni kielezi,
Tutii kwa mazoea, hadi kijacho kizazi,
Kwa hayo nitamwachia. hiyo ya ziada kazi,
Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili
a) Eleza mambo yoyote manne ambayo mshairi anashauri taifa lifanye ili kuwa na aadili.
b) Taja tamathali yoyote moja inayojitokeza katika shairi hili.
c) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia kigezo kifuatacho :
Mpangilio wa vina
d) Bainisha nafsineni (mzungumzaji) katika shairi hili.
e) Eleza toni ya shairi hili
f) Eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika ubeti wa nne
g) Andika ubeti wa pili kw lugha nathari
h) Eleza maana ya neon lifuatalo kama ilivyotumiwa katika shairi:
i) hongo
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Vijana wana kumbwa na changamoto kadhaa katika jamii.Jadili baadhi ya changamoto hizi kwa kurejelea hadithi zozote tano kutoka diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine.(Solved)
Vijana wana kumbwa na changamoto kadhaa katika jamii.Jadili baadhi ya changamoto hizi kwa kurejelea hadithi zozote tano kutoka diwani ya Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Mungu akikupa kilema, hukupa na mwendowe"
Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi Mzizi na Matawi.(Solved)
"Mungu akikupa kilema, hukupa na mwendowe"
Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hadithi Mzizi na Matawi.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Hivi vitu lazima viwepo,au kama havipo ni lazima viwe ni vipengee mahususi vya uhalisia wamaisha yetu:(Solved)
Damu Nyeusi Na Hadithi Nyingine-Ken Wal'ibora Na S.Ahmed
"Hivi vitu lazima viwepo,au kama havipo ni lazima viwe ni vipengee mahususi vya uhalisia wa maisha yetu:
(a) Liweke dondoo katika muktadha wake faafu.
(b) Fafanua sifa zozote nne za msemaji wa maneno haya.
(c) Eleza kwa tafsili matatizo yoyote mawili yanayoikumba jamii ya hadithi mlimotolewa nukuu hii.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Wewe,Utazame mlolongo wa(Solved)
SHAIRI A
Wewe,
Utazame mlolongo wa
Waja unaoshika njia likiwapo;
Unaofuata pembe za barabara zisokuwapo,
Kwenda kuisaka auni,
Kuitafuta kazi inayowachenga.
Itazame migongo ya wachapa kazi,
Watokwao na jasho kapakapana,
Wanaotafunwa uhai na jua liso huruma:
Wakiinua vyuma na magunia,
Wakiinua makontena,
Wakichubuka mashambani,
Wakiumia viwandani,
Wakiteseka makazini,
Halafu
Uangalie ule ujira wa kijungu meko,
Mshahara uso kifu haja,
Nguo zisizositiri miili dhaifu,
Kilio chao kisichokuwa na machozi,
Na
Ujiangalie
Mwili wako unaomereta ujana wa ufanisi,
Gari lako la kifahari lililozibwa vioo,
Jumba lako la kujishasha kama uwanja mdogo,
Malaki yapesa unayomiliki,
Ujiitapo mwajiri kwa raha, hunusi usaha wa hali yao?
SHAIRI B
Dunia kitendawili, hakuna ateguaye;
Dunia kama tapeli, hadaa nyingi ujuye;
Dunia mwenye akili, inampiku na yeye;
Dunia ina mizungu, tena yapika majungu.
Dunia na yake hali, hupumbaza hatimaye;
Dunia ina akili, binadamu sichezeye;
Dunia uwe na mali, huiwezi dhorubaye;
Dunia ina mizungu, tena yapika majungu.
Dunia wenye muali, ambao waichezeye;
Dunia kipigo kali, huwakumba hatimaye;
Dunia wakaja kuli, ?menipata nini miye?
Dunia ina mizungu, tena yapika majungu
Maswali
(a) Je, mashairi haya mawili ni ya aina gani? Toa sababu.
(b) Taja dhamira kuu katika kila shairi.
(c) Kwa kutoa hoja zozote tatu linganua mashairi haya kiumbo.
(d) Taja na uelezee nafsi-pokezi katika mashairi haya mawili.
(e) Kwa kutolea mfano mmoja mmoja eleza matumizi ya mbinu hizi
(i) Kweli –kinzani
(ii) Mishata
(f) Tambua idhini ya kishairi iliyo tumika katika neno ?Waichezeye"
Na uelezee dhima yake katika utoshelezi wa kian ldhi.
(g) Dondoa mfano mmoja mmoja wa mbinu ya tashihisi kutoka kwenye Mashairi yote mawili.
(h) Andika ubeti wa tatu katika shairi la A kwa lugha nathari.
(i) Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyotu? nika katika vifungu hivi.
(i) Inampiku.
(ii) Makontena.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Eleza namna mwandishi wa kidagaa Kimemwozea alivyofaulu kutumia fani ya barua kwa kutolea mifano mitano.(Solved)
Eleza namna mwandishi wa kidagaa Kimemwozea alivyofaulu kutumia fani ya barua kwa kutolea mifano mitano.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Tembo itakuua ndugu yangu. Punguza ulevi bwana.Siku hizi naona aibu kukuita ndugu yangu."(Solved)
Kidagaa kimemwozea
"Tembo itakuua ndugu yangu. Punguza ulevi bwana.Siku hizi naona aibu kukuita ndugu yangu."
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili.
(b) Wahusika hawa wawili ni kama shilingi kwa ya pili.Thibitisha.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "...Sote ni wafanyikazi wa baraza. Kile linachochuma Baraza tunagawana sote."(Solved)
Timothy Arege, Mstahiki Meya
"...Sote ni wafanyikazi wa baraza. Kile linachochuma Baraza tunagawana sote."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Fafanua sifa tano za msemaji
(c) Tunagawana sote ni kinyume ejia hali halisi. Thibitisha.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Pana jambo ninatukiya, kwangu hilo ni muhali,
(Solved)
SIPENDI KUCHEKA
Pana jambo ninatukiya, kwangu hilo ni muhali,
Kitenda naona haya, kujishusha yangu hali
Sipendi unipe hidaya, sipendi kutenda hili
Sipendi mimi kucheka
Sipendi mimi kucheka, kuchekea mawi
Sipendi na ya dhihaka, kwangu nyemi hiwi
Sipendi kwa hakika, mwovu kistawika
Halafuye nikacheka!
Masikini akiteswa
Yatima akinyanyaswa
Mnyonge naye akinyonywa
Sipendi hata ikiwa
Unazo nguvu najuwa
Ni hili sitatekezwa
Mbona lakini nicheke, kwayo furaha?
Na wewe ukajiweke, uli na siha?
Na yatima ali pwek.e, wa anahaha?
Amenyimwa haki yake, hanayo raha!
Na moyo wangu ucheke, kwa ha ha, ha!
Kucheka kwa kucheka Mimi katu sitacheka.
MASWALI
a) Shairi hili ni la aina gani? Thibitisha.
b) Taj a sababu zinazomfanya mshairi asitake kucheka.
c) Chambua umbo la shairi hili kwa kuzingatia ubeti wa mwisho.
d) Tambua nafsineni na nafsinenewa katika shairi hili.
e) Tambua toni ya shairi hili.
f) Fafanua uhuru wa mshairi katika shairi hili.
g) Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi.
h) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi
i) Mawi
ii) Nyemi
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Eleza hali ya shaka ya mambo inavyojitokeza katika hadithi ya shaka ya mambo.(Solved)
“Shaka ya Mambo” (Farouk Topan)
Eleza hali ya shaka ya mambo inavyojitokeza katika hadithi ya shaka ya mambo.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Nashangaa vile kwetu tunavyoabudu watu hao wasiotujali."(Solved)
“Damu Nyeusi” (Ken Walibora)
"Nashangaa vile kwetu tunavyoabudu watu hao wasiotujali."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha matumizi ya mbinu ya ishara kwa kurejelea hadithi ya gilasi ya mwisho makaburini.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Eleza jinsi wanacheneo walivyotatua shida zinazowakumba.(Solved)
Mstahiki Meya
Eleza jinsi wanacheneo walivyotatua shida zinazowakumba.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- "Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."(Solved)
Mstahiki Meya
"Mtu huvuna alichopanda, ukipanda pojo huwezi kuvuna kunazi."
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Anayeambiwa alisema nini baada ya kuambiwa haya?
c) Thibitisha kuwa wanacheneo walipanda pojo.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)
- Taja aina nne za hadithi.(Solved)
Taja aina nne za hadithi.
Date posted: October 3, 2019. Answers (1)