UFAHAMUSoma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.Mojawapo kati ya misingi na nguzo za maendeleo uliwenguni ni viwanda. Viwanda ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyoigeuza malighafi inayopatikana...

      

UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

Mojawapo kati ya misingi na nguzo za maendeleo uliwenguni ni viwanda. Viwanda ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyoigeuza malighafi inayopatikana na kuwa bidhaa zinazoweza kutumiwa na watu. Katika nchi zinazoendelea, ambazo hazina uwezo mkubwa wa mitaji viwanda vinavyoimarika ni vile vidogo. Hivi ni viwanda ambavyo huhusisha amali za mikono. Kuimarika kwa viwanda hivi vidogo kunatokana na sababu mbalimbali.

Nchi zinazoendelea huwa na masoko finyu sana kwa kuzingatia uwezo wa ununuzi wa wanaolengwa na bidhaa za viwanda . Katika msingi huu viwanda vikubwa vitawiwa ugumu kufanya biashara katika mazingira ambako masoko yake ni finyu au utashi wa bidhaa zake sio mkubwa. Viwanda vidogo pia vinao uwezo wa kuwaajiri wafanyikazi wengi hasa kwa kuwa havina uwezo wa kugharamia mashine. Uajiri huu wa wafanyikazi wengi ni muhimu katika maeneo mengi ambako tatizo la ajira ni mojawapo wa matatizo sugu. Tofauti na mataifa ya kitasmia (yenye viwanda vingi) mataifa mengi yanayoendelea hayana mifumo imara ya kuwakimu watu wasiokuwa na kazi. Utegemezi wa jamaa wanaofanya kazi kwa hivyo unakuwa nyenzo ya pekee ya kuyamudu maisha.

Kuanzisha viwanda vidogo vidogo hakuhitaji mtaji mkubwa tofauti na viwanda vikubwa. Hali hii inasahilisha uwezekano wa watu wengi kujasurisha shughuli yoyote ile. Sambamba na suala hili ni kuwa ni rahisi kujarisha bidhaa mpya kwa kiwango kidogo cha kiwanda kidogo. Ikiwa mzalishaji yeyote atazalisha bidhaa mpya kwa mapanu, kwa mfano kama ilivyo kwa viwanda vikubwa, pana uwezekano wa kupata hasara kubwa. Huenda utashi wa bidhaa hiyo uwe mdogo ukilinganishwa na ugavi wa bidhaa yenyewe. Majaribio mazuri huwa ni kwa kiwango kidogo.

Kuwepo kwa viwanda vidogo huwa chocheo kubwa la usambazaji wa viwanda hadi maeneo ya mashambani. Hali hii inahakikisha kuwa nafasi za ajira zimezambazwa nchini hali ambayo inasaidia kuhakikisha kuwa pana mweneo mzuri wa kimapato nchini. Mweneo huo wa mapato unachangia katika kuboresha uwezo wa kiununuzi wa umma. Huu ni msingi muhimu wa maendeleo. Upanuzi na ueneaji wa viwanda vidogo vidogo ni msingi mkubwa wa kujitegemea kiuchumi. Aghalabu viwanda vikubwa huegemea kwenye mitaji ya mashirika ya kimataifa na huwa msingi wa kuendelezwa kwa utegemezi wa kiuchumi.

Maswali
a)Kwa nini viwanda ni muhimu?
b)Ni nini kiini cha matatizo ya uuzaji wa bidhaa katika nchi zinazoendelea?
c)Eleza faida zinazotokana na kuwepo kwa viwanda vidogo vidogo.
d)Usambazaji wa viwanda katika maeneo ya mashambani una faida gani?
e)Fafanua maana ya msamiati huu kama ulivyotumika katika kifungu.
i)Kujasurisha
ii)Amali
iii)Utashi

  

Answers


Kavungya
a)Hugeuza malighafi inayopatikana kuwa bidhaa za kutumiwa na watu.

b)Masoko finyu kutokana na uwezo wa wanunuzi.

c)(i) Vina uwezo wa kuwaajiri wafanyakazi wengi.
(ii) Hakuhitaji mtaji mkubwa.
(iii) Ni rahisi kujaribisha bidhaa mpya kwa kiwango kidogo cha kiwanda kidogo.
(iv) Huwa chocheo kubwa la usambazaji wa viwanda hadi maeneo ya mashambani.
(v) Watu wengi wanaweza kuanzisha viwanda hivyo.

d)(i) Nafasi za ajira zimesambazwa.
(ii) Hutoa mweneo mzuri wa kimapato
(iii) Huboresha uwezo wa kiununuzi wa umma.
(iv) Ni msingi mkubwa wa kujitegemea kiuchumi.

e)(i) Kuanzisha
(ii) Kazi
(iii) Hamu
Kavungya answered the question on October 3, 2019 at 12:42


Next: The table below illustrates the relationship between land in hectares , inputs (DAP) fertilizers and total maize production in 90kg bags , and the marginal production...
Previous: MUHTASARISoma kifungu kifuatacho cha habari kisha ujibu maswali yanayofuatia.Watu wengi, wanaamini kwamba kufundisha watoto nyimbo shuleni ni kupoteza wakati unaofaa kwa masomo ya maana....

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions