MUHTASARISoma kifungu kifuatacho cha habari kisha ujibu maswali yanayofuatia.Watu wengi, wanaamini kwamba kufundisha watoto nyimbo shuleni ni kupoteza wakati unaofaa kwa masomo ya maana....

      

MUHTASARI
Soma kifungu kifuatacho cha habari kisha ujibu maswali yanayofuatia.

Watu wengi, wanaamini kwamba kufundisha watoto nyimbo shuleni ni kupoteza wakati unaofaa kwa masomo ya maana. Lakini muziki nyumbani na shuleni una manufaa mengi.

Muziki ni kitulizo kikubwa sana cha moyo wa binadamu. Muziki una njia ya kipekee ya kuwasiliana. Baadhi ya ujumbe hauwezi kupitishwa kwa njia nyingine ila kwa muziki.

Muziki umetajwa kumsaidia mtoto kwa mambo yafuatayo:
Kuendeza hisia nzuri, za kuburudisha na kuzuzua. Muziki humsaidia mtoto kuweza kukabiliana na tajriba mbaya nazo. Unampa fursa ya kutoa moyoni simanzi na dhiki yake na hivyo kumrejeshea raha tena. Liwazo la muziki ni dhahiri wakati mtoto anapolala pindi anapoimbiwa bembelezi.

Inaaminika pia kwamba muziki unakomaza akili ya mtoto na ni nyenzo muhimu sana katika hafla yake ya kujifanya mambo, hasa kwenye miaka yake ya mapema. Muziki huhitaji umakinifu ili kutambua miondoko na maneno halisi ya wimbo huo na mambo haya humfanya mtoto kuhamisha umakini huu kwenye masomo mengine darasani. Inaaminika pia kwamba kupitia kwa muziki mtoto anaweza kujifunza mbinu ya kukumbuka mambo anayofunzwa masomoni.

Watoto ambao hujifunza muziki mara kwa mara hujipatia mbinu za werevu shuleni haswa kwenye somo la hesabu na werevu wa mambo mengine kwa jumla. Utafiti umeonyesha kwamba watu wazima ambao walijifunza muziki kabla wafikishe umri wa miaka 12 huwa na utumizi mzuri wa maneno magumu na msamiati kuliko wale ambao hawakujifunza kuimba.

Muziki pia husaidia watoto walio na kasoro za kuzungumza au walio na ulimi mzito wa kuzungumza.
Watoto au watu wazima walio na shida ya kigugumizi huweza kujieleza kwa ufasaha kwa kupitia muziki na jambo hili huboresha kujiamini kwao kwa kibinafsi. Watoto kama hao huweza kujifunza na kuelewa mila na tamaduni zao.

MASWALI
a) Bila kupoteza maana iliyokusudiwa na mwandishi, fupisha aya ya kwanza hadi ya tatu.
(maneno 40 – 45)
MATAYARISHO
NAKALA SAFI

b) Dondoa hoja muhimu zinazojitokeza katika aya ya nne na ya tano. (Maneno 45 – 50)
MATAYARISHO
JIBU

  

Answers


Kavungya
A(i) Kupitisha wakati
(ii) Kitulizo cha moyo
(iii) Kuendeleza hisia, kuburudisha na kuzuzua
(iv) Kukubaliana na tajriba mbaya
(v) Unampa fursa ya kutoa moyoni simanzi na dhiki
(vi) Kukomaza akili
(vii) Kuhamasisha umakinifu katika masomo mengine
(viii) Mbinu ya kukumbuka

b)(i) Watoto hujipatia mbinu za werevu shuleni.
(ii) Watu wazima waliojifunza muziki kabla ya miaka 12 huwa na utumizi mzuri wa maneno magumu na msamiati.
(iii) Husaidia watoto walio na kasoro ya kuzungumza/walio na ulimi mzito wa kuzungumza.
(iv) Husaidia watu wazima walio na shida ya kigugumizi.
(v) Watoto huweza kujifunza kuelewa mila na tamaduni.
Kavungya answered the question on October 3, 2019 at 12:47


Next: UFAHAMUSoma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.Mojawapo kati ya misingi na nguzo za maendeleo uliwenguni ni viwanda. Viwanda ni muhimu kwa kuwa ndivyo vinavyoigeuza malighafi inayopatikana...
Previous: Andika sifa mbili mbili bainifu za sauti. i)/e/ ii)/n/

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions